- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Tutakoma Lini Kutazamia Magharibi na UN kwa ajili ya Ukombozi wetu?!
(Imetafsiriwa)
Habari:
“Marekani mnamo Alhamisi ilisitisha kwa ufanisi Umoja wa Mataifa kutokana na kuitambua dola ya Palestina kwa kupiga kura ya turufu katika Baraza la Usalama kuwanyima Wapalestina uanachama kamili wa shirika hilo la ulimwengu:” (Reuters, Aprili 19, 2024).
Maoni Comment:
Naibu Balozi wa Marekani wa U.N., Robert Wood alielezea msimamo wa Marekani kwa maneno yafuatayo: "Marekani inaendelea kuunga mkono sana suluhisho la dola mbili. Kura hii ya turufu haionyeshi kupinga dola ya Palestina, lakini badala yake ni kukiri kwamba itakuja tu kutoka kwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande husika," ambayo inamaanisha kuzuia haki ya watu waliokandamizwa na kufukuzwa hadi mnyakuzi akubali!
Siku tatu kabla Bunge la Wawakilishi liliamua (kura 377 za kuunga mkono, na kura 44 tu dhidi yake) kwamba kauli mbiu, ''kutoka mto hadi baharini, Palestina itakuwa huru '' ni dhidi ya mayahudi na matumizi yake lazima yashutumiwe. Kukataa huku kwa utaifa wa Palestina na wito unaovutia kwa utaifa wa Palestina kuwa kama kimsingi ni dhidi ya Mayahudi kunatokea wakati Marekani inaunga mkono Dola ya Kizayuni katika maangamizi yake wa mauaji ya halaiki wa aina zote za maisha ya Palestina huko Gaza. Haraka, kutambua kikamilifu dola ya Palestina inaweza kuonekana kuwa muhimu, kwani hiyo ingeweka vizuizi vya kisheria katika njia ya Dola ya Kizayuni katika kampeni zake za mauaji ya kikatili huko Gaza na Ukingo wa Magharibi. Walakini, ulinzi wowote wa kisheria wa dola hiyo ungetoa ulinzi mdogo kwa wale walio katika Ukingo wa Magharibi na Gaza, kwani Dola ya Kizayuni ni ya thamani sana kwa nchi za kirasilimali, zikiongozwa na Marekani, na itazifanya zile sheria zinazoitwa kimataifa kwa sura yao wenyewe na kujiona juu ya sheria wakati wowote wanapochagua.
Ama kuhusu kauli mbiu, ''kutoka mto hadi baharini, Palestina itakuwa huru:'' Inapaswa kukataliwa na Waislamu pia, kwa sababu ni ndoto ya udanganyifu na inazidisha ukiukwaji mbaya uliofanywa na dola za kikoloni juu ya ulimwengu wa Kiislamu Baada ya kuvunjwa Khilafah Uthmani.
Ndoto ni ile ya uhuru. Uhuru uko wapi katika ulimwengu wa Kiislamu leo? Marekani, au mamluki wake, kama vile Dola ya Kizayuni, wana uhuru wa kushambulia kijeshi katika sehemu yoyote ya ulimwengu wa Kiislamu wanayotaka. Wanaunda mitaala ya kielimu, sheria, sera za uchumi na serikali za nchi za Waislamu ambazo ni kubwa na tajiri zaidi katika rasilimali kuliko ardhi iliyo koloniwa vikali ambayo inaotwa kuwa Dola ya Palestina. Ikiwa kamwe kunaweza kuwa na kitu kama hicho, ingeshikwa mateka kwa matakwa ya wakoloni kama zilivyo dola zilizofeli zinazoizunguka.
Dola inayozungumziwa kuihusu katika UN ni ile iliyo ndani ya mfumo wa makubaliano ya Sykes-Picot kati ya wakoloni kutumikia madhumuni yao wenyewe na kukandamiza fahamu ya Khilafah. Ikiwa Waislamu hawatasimama kudai ukombozi kutoka kwa ukoloni katika nchi zote za Waislamu na kufutwa kwa mipaka iliyochorwa baina ya Waislamu na wakoloni, basi hakuna Palestina wala ardhi nyingine yoyote ya Waislamu itakayokuwa huru.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin