Ijumaa, 01 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mwito wa Mabadiliko: Uislamu Mfumo pekee Usiocheza Shere na Kuhujumu Maisha ya Watu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kenya, imekumbwa na maandamano makubwa katika masiku ya hivi majuzi baada ya bunge kupitisha mswada wa kuongeza ushuru – ikiwa ni pamoja na mahitaji ya kila siku kama vile mafuta ya kupikia, nepi, na mkate – kwa idadi ya watu ambao tayari wanakabiliwa na mfumko wa bei na viwango vya juu vya ukosefu wa ajira. Rais Ruto alikataa kutia saini mswada huo baada ya maandamano makubwa ambayo kufikia sasa watu 39 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa.

Maoni:

Maandamano ya (Gen Z) yalichochewa na kuwasilishwa kwa mswada mpya wa fedha ambao ungetoza ushuru wa kuadhibu kwa mahitaji ya kila siku, ikiwa ni pamoja na sukari, mkate na mafuta ya kupikia – sera ambayo ingeendeleza athari kubwa ya kiuchumi kwa wakenya wengi masikini. Mswada huo huo ulitenga kando kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya ukarabati wa makaazi ya rais na matumizi mengine makubwa.

Mapema mwezi Juni, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ulifikia makubaliano ya awali juu ya utoaji wa mikopo ambayo uliitaka serikali ya Kenya kuongeza mapato yake; Kenya ikawa na lengo la kupata dolari bilioni 2.7 za ziada. Kwa hivyo Nairobi haikuwa na njia nyengine ila tu kupeleka maumivu kwa raia wake kupitia sera za ushuru kandamizi ambazo zingeendeleza kuathiri zaidi maskini. Wala si Kenya pekee: Zaidi ya watu bilioni 3 kote ulimwenguni wanaishi katika nchi ambazo zinatumia zaidi mapato yake kulipa madeni yao kuliko matumizi ya umma katika sekta ya elimu au afya.

Ingawa kichocheo cha maandamano haya ni sera mbovu za kifedha na tabaka la kisiasa lenye uchu, vyombo vya habari vinaendelea kuonesha kwamba waandamanaji wanawakilisha hisia za vijana wa Kenya, lakini vinashindwa kuona mfumo mbovu wa kiuchumi wa Ubepari. Kwa upande wa vijana, ambao wanaonekana matarajio yao yako gizani, na kukatishwa tamaa na tabaka la kisiasa lenye ulafi lisilojali maslahi yao—vijana wanaonekana dhahiri kutokuwa na viongozi bali wafanyibiashara, na wamejipanga wenyewe mtandaoni, wakifanya mikutano mikubwa ya mtandaoni, na wameingia mitaani bila uoga. Maandamano ambayo hayajawahi kushuhudiwa nchini Kenya, ni dalili  wazi ya kushindwa kabisa kwa wanasiasa wa Kidemokrasia pamoja na mfumo wao wa kibepari – mfumo wa kiuchumi ambao unasukuma ukatili wa wanasiasa na ulafi, hivyo basi kuwanyima raia wa kawaida kukidhi mahitaji ya kimsingi.

Ukoloni wa Magharibi uliunda dhana inayofunga mipaka ya mabadiliko kwenye chaguzi, mageuzi ya katiba na hatua za kiuchumi, kwa maana hii waandamanaji wataingia katika mtego huo huo wa Magharibi yaani kuiga Magharibi wanaojiona kuwa wao ndio wanaomiliki hatima ya ‘mabadiliko’ yoyote.

Mabadiliko ya kweli ambayo vijana sio tu nchini Kenya bali ulimwengu mzima wanapaswa kuyataka ni mfumo ulio na suluhisho la wazi la matatizo yanayowakabili wanadamu. Mfumo huu ni Uislamu ambao haukuacha maisha ya watu kuchezewa na kutumiwa kirahisi na tabaka la wanasiasa walafi wanaohubiri Demokrasia kama njia ya kuhadaa watu kwa lengo la kutimiza ubinafsi wao. Mwenyezi Mungu (swt) alimtuma Mtume wake wa mwisho (saw) akilingania watu maisha ya kweli ya Kiislamu wala sio maisha ya hadaa yaliyosheheni uwajibikaji wa kirongo na kushiriki katika siasa za domokaya.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu