Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Suala la Utekaji Nyara na Upotezaji nchini Tanzania

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 09 Agosti, 2024, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu utekaji nyara na upotezaji wa watu unaoendelea nchini. Shirika hilo liliorodhesha takriban watu 83 walioripotiwa kutekwa nyara na kutoweka tangu 2016.

Maoni:

Tunakemea vikali vitendo hivi ambavyo vimekuwa vikiongezeka hivi karibuni bila vyombo husika vya serikali kuwajibika ipasavyo.

TLS iliripoti zaidi ya kesi 20 za utekaji nyara/kutoweka mwaka 2024 pekee. Watu waliotekwa nyara/kutoweka ni pamoja na wakosoaji wa serikali, wanasiasa, wafanyibiashara, watu wa kawaida wakiwemo watoto wa kawaida na wenye zeruzeru (albino).

Habari za kupotea watoto zimeripotiwa zaidi katika siku za hivi majuzi na hivyo kuzua hofu miongoni mwa wazazi kwani wengi wao ni watoto wa shule.

Inaaminika kuwa kuna sababu kadhaa za kutekwa nyara na kupotea kwa watu zikiwemo imani za uchawi zinazochochewa zaidi na ajenda za kisiasa zinazohusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka huu na uchaguzi mkuu ujao wa 2025.

Ikumbukwe kwamba mwaka 2015 Bw. Zeid Ra'ad Al Hussein, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, alionya kwamba kuongezeka kwa mauaji ya kinyama ya albino nchini Tanzania kunaweza kuwa na uhusiano na kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazokaribia.

Inasemekana kuwa baadhi ya wanasiasa wanaamini kuwa kuwa na viungo vya albino kwa ajili ya uchawi kungewafanya washinde uchaguzi.

Ukosoaji wa serikali, ulanguzi wa binadamu, biashara ya viungo vya binadamu, uhuni, uasherati na ubakaji pia zinaweza kuwa sababu za kutekwa nyara na kutoweka.

Matukio haya ya kikatili yanafichua ukweli kwamba serikali za kidemokrasia za kibepari hazijali ustawi wa watu wengi, ikiwa ni pamoja na masuala muhimu kama vile usalama wa watu. Ni aibu kwamba licha ya kurudiwa kwa matukio haya kila mwaka au ndani ya miezi kadhaa, bado hayajafanywa ya kutosha kupambana na kuzuia.

Zaidi ya hayo, inaashiria kwa uwazi uovu wa mfumo wa kibepari, miongoni mwao ni fikra yake ya ‘manufaa ya kibinafsi’ ambayo imewafanya watu wawe na ulafi wa kujali tu maslahi ya kibinafsi na faida bila kujali madhara ya matendo yao yanayoweza kuleta kwa watu.

Ingawa tunaitaka serikali kama mchungaji kuingilia kati kwa njia zote zinazowezekana ili kukomesha vitendo hivi visivyo vya utu, vya kishenzi na vya kinyama, inabidi ieleweke wazi kwamba ni chini ya Dola ya Kiislamu tu (Khilafah) ambapo usalama wa kweli  wa watu utapatikana kupitia utekelezaji wa hukmu za Mwenyezi Mungu zinazosimamia haki bila kuzingatia manufaa.

Imeandikwa kwa Ahili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Said Bitomwa

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu