Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Shirika la Ushirikiano la Shanghai ni Sehemu ya Mfumo wa Dunia wa Amerika

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 17 Oktoba 2024, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Mathew Miller alitoa maoni yake kuhusu mkutano wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai, akisema, “Kwa hiyo Marekani inaheshimu haki ya kila nchi ya kujumuika katika makundi ya chaguo lake yenyewe. Tungehimiza kila nchi kuhakikisha kwamba ushiriki wake katika mikutano ya kimataifa unazingatia na kuheshimu sheria za kimataifa, na kuthibitisha tena ubwana, uadilifu wa kieneo, na uhuru wa mataifa yote.” [state.gov]

Maoni:

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje alikuwa sahihi kwa kusema kwamba “kushiriki katika mikutano ya kimataifa kunashikilia na kuheshimu sheria za kimataifa.” Mashirika yote ya kimataifa, mikataba na mijumuiko ya leo iko chini ya mfumo wa kimataifa wa Marekani na sheria zake za kimataifa. Washington hairuhusu shirika lolote kuwepo nje ya ushawishi wake. Ingawa Umoja wa Mataifa ni chombo madhubuti cha sera za kigeni za Marekani, Washington iliunda mashirika ya ziada ili kuendeleza maslahi yake. Kwa mfano, kupitia Mazungumzo ya Usalama ya ‘Quadrilateral Security Dialogue’ (QUAD), Marekani iliizunguka China kutoka Bahari Hindi na Pasifiki. Kwa mfano, Washington inatumia Shirika la Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini (NATO) kudumisha utawala wake juu ya Ulaya, na kuishinikiza Urusi. Mbinu hii inazuia dola zengine zinazotumia kura ya turufu kufanya ukaguzi wa nguvu za Marekani. Shirika la Ushirikiano la Shanghai (SCO) pia liko ndani ya mfumo wa Marekani, na hufanya kazi kwa mujibu wa sheria zake.

Hapo awali Urusi ilianzisha Shirika la Ushirikiano la Shanghai na China ili kujilinda dhidi ya uvamizi wa Amerika katika eneo la Asia ya Kati, ambalo Moscow inalizingatia kuwa duara lake la ushawishi. Baada ya watu wa Urusi kupoteza imani katika fikra potofu ya ujamaa, walibaki kunyimwa msingi wa fikra thabiti kama msingi kwa jamii. Dola ya Urusi inataka kutambuliwa kama dola kuu ya kisiasa ya kijiografia, iliyo sambamba na Marekani. Hata hivyo, kwa kiasi kikubwa inajifunga kwenye vizuizi vya mfumo uliopo wa kimataifa. Kwa upande wa China, kufuatia mkakati wa Marekani wa kuoanisha uchumi wa China katika muundo wa uchumi wa Magharibi, sera yake ya mambo ya nje sasa inazingatia maslahi yake ya kiuchumi. Ndiyo maana China ilitanguliza maslahi yake ya kiuchumi katika uhusiano wake na Urusi, wakati wa mzozo unaoendelea wa Urusi na Ukraine. Matokeo yake ni kwamba Shirika la Ushirikiano la Shanghai halina uzito, licha ya uwezo wake. Sababu ni kwamba Urusi na China zilianzisha SCO ili kuunda duara la ushawishi kwao wenyewe, huku zikisalia chini ya mfumo wa Amerika na sheria za kimataifa.

Ama Pakistan, ni chombo cha sera za kigeni za Marekani kwa sababu watawala wake ni vibaraka wa Amerika. Watawala wa Pakistan wanashiriki katika Shirika la Ushirikiano la Shanghai kama vile Washington inavyowaruhusu. Hivi sasa, wana jukumu la kuhakikisha kuwa Pakistan haileti changamoto yoyote kwa mpango wa kikanda wa Amerika, ambao ni utawala wa India ili kutoa changamoto kwa China na Waislamu wa eneo hilo. Pia wanajifunga kwenye shirika la kanda upande wa mashariki ambalo limejengwa juu ya utaifa, na fahamu ya mataifa ya kitaifa, kama vile watawala wa Waarabu wanavyojifunga kwenye Jumuiya ya Waarabu upande wa Magharibi. Fahamu ya dola za kitaifa inazuia kuunganishwa kwa Waislamu kama dola moja yenye nguvu ya Khilafah, huku ikihakikisha kukaliwa kimabavu kwa ardhi za Waislamu na maadui wa Ummah.

Hizb ut Tahrir imeeleza kwa kina katika “Utangulizi wake wa Katiba,” kwa nini Waislamu hawaruhusiwi kusalimu amri kwa mfumo wa dunia wa Marekani. Inasema, “Umoja wa Mataifa umeanzishwa kwa misingi ya mfumo wa Kibepari, ambao ni mfumo wa Kikafiri, na zaidi ya hayo ni chombo kilicho mikononi mwa dola kubwa, hasa Marekani, ambayo inakitumia kwa ajili ya kulazimisha ushawishi wake juu ya mataifa madogo, ambayo dola za sasa katika Ulimwengu wa Kiislamu ni sehemu yake.”

Katika chapisho hilo hilo, Hizb ut Tahrir pia ilieleza kwa nini Waislamu hawaruhusiwi kuwa sehemu ya mashirika ya kikanda, kama vile Shirika la Ushirikiano la Shanghai na Jumuiya ya Waarabu, ambayo yamejengwa juu ya dola za kitaifa, ikisema, “Jumuiya ya Kiarabu imeanzishwa juu ya msingi wa mfumo wa Ubepari, na inataja kwa uwazi katika katiba yake kwamba ni kwa ajili ya kulinda uhuru wa dola za Kiarabu, kwa maana nyengine, kulinda mtengano na mgawanyiko wa ardhi za Kiislamu, ambao umeharamishwa.”

Pakistan yenyewe ikiwa kama dola ya nyuklia, inayomiliki jeshi lenye nguvu na uwezo na idadi kubwa ya watu wanaopenda Uislamu, ina uwezo wa kuwaunganisha Waislamu wa Asia ya Kusini na Kati. Hii ndiyo njia ya kuelekea mbele ambayo itaregesha hadhi na fahari ya Umma wa Kiislamu. Kitu chengine chochote ni utiishaji mwingine. Watu wenye nguvu nchini Pakistani lazima wakatae zana zote na miundo yote inayoufanya Ummah kugawanyika, na kukimbilia kusimamisha Khilafah ambayo itaunganisha Umma wa Kiislamu. Muundo wa usalama ambao Marekani imeuunda ni kulinda maslahi yake kupitia mfumo wa kimataifa. Dola ya Khilafah Rashida itakayoanzishwa hivi karibuni itatoa msingi wa mfumo mpya na adilifu wa kimataifa. Mwenyezi Mungu (swt) ameonya,

[مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنكَبُوتِ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ]

“Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua.” [Surah Al-Ankabut 29:41].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhannad Mujtaba – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu