Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wale Waliotazama Moto wa Gaza Wamehukumiwa Udhalilifu!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Wakati wa mkutano wake na Barzani, Rais Erdogan alijadili maendeleo ya kikanda na kimataifa na kusema, Kuna hatari kwamba uvamizi wa ‘Israel’ utaligeuza eneo hilo kuwa eneo la vita la kila upande. (Mashirika 16.10.2024)

Maoni:

Rais Erdogan amekuwa akifanya kazi kwa ufahamu wa kujitanua ndani ya mfumo wa ardhi iliyoahidiwa ya uwepo wa Mayahudi kukabiliana na uwepo wa uvamizi wa Mayahudi katika vyombo vya habari tofauti tofauti kwa wiki kadhaa. Alikuwa ametoa tamko la kuathirika kwa jamii kwa kusema kwamba Uturuki pia ilikua katika maeneo haya. Sasa, ingawa inakubalika kama lugha ya kisiasa kwamba alitaja hatari ya kuugeuza uvamizi wa uwepo wa Mayahudi kuwa uwanja wa vita katika mkutano wake na Barzani, sawa na kauli hizi, inapaswa kujulikana kwamba hakika ni madhihirisho ya aibu.

Watawala wetu, ambao hawajachukua hatua hata moja madhubuti dhidi ya uwepo wa Mayahudi ambao wamekuwa wakifanya mauaji ya halaiki mjini Gaza kwa mwaka mzima na aibu zaidi katika historia na wasiwasi wa viongozi wetu kuhusu Gaza ni udanganyifu wa kisiasa tu. Hebu fikiria wana wa Umma miili yao inachanwa kwa mabomu, wanachomwa moto wakiwa hai, vilio vyao vinapanda hadi kwenye arshi, lakini pamoja na jeshi kubwa na nyenzo walizo nazo, viongozi ambao hawawezi kuonyesha ujasiri wa kuwakomesha magaidi wachache wa Kiyahudi wanazungumzia hatari ya vita katika eneo! Wakati Gaza ilipokuwa sehemu ya jiografia ya ummah, moto huko haukukuamsha. Licha ya ukweli kwamba mamia ya maelfu ya watoto na wanawake wasio na hatia walichinjwa, mulibandikwa alama ya udhalilifu kwa kukwama kwenu. Ninapata ugumu kuelewa ni aina gani ya hatari ya uwepo wa Mayahudi kwa hakika ina maanisha kutambua muundo munaouita dola ya kigaidi kama dola, kujihusisha na mahusiano ya kidiplomasia, kuendelea kufanya biashara, ingawa kwa njia za hila. Sisi ndio walengwa wa mashambulizi ya jamii ya Mayahudi, kwa hivyo ikiwa huoni aibu na neno hili unaposema Uturuki, tunaaibika kwa niaba yako. Maana hata hutambui kuwa kauli zako mbele ya kuvamiwa kulia na kushoto na magenge machache ambayo yamekuwa yakiikalia kimabavu jiografia ya Palestina kwa miaka 70 yanahujumu watu wako, historia yako, jiografia yako, nguvu yako na imani yako. Kwa hakika, huku uwepo wa Kiyahudi ukipanuka uvamizi wake kwa kupata ujasiri kutoka kwa woga, uzembe, na ushirikiano wa viongozi wetu, kulalamikia jambo hilo ni mtazamo ulio mbali na kufafanuliwa na akili.

Ikiwa Bw. Erdogan angekuwa mkweli, angejibu uwepo huu wa kigaidi kwa nguvu za kijeshi, mateso haya yasingetokea Gaza. Ikiwa kweli wewe ni mkweli, hutanyamaza tena kuhusu mauaji yanayofanywa na magenge ya Kiyahudi huko Gaza na Lebanon, bali utahamasisha jeshi. Kwa hivyo, kanda na jiografia iliyo chini ya moto itakomesha ukatili huu, na utafanya kile kinachohitajika hata ikiwa kimechelewa.

Lakini fahamu kwamba maadamu unayarushia mpira mashirika kama vile Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Waarabu, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu ili kukomesha mateso haya, neno lako halitakuwa na thamani, halina ukweli. Maadamu bado unaendelea kufanya biashara na kafiri huyu, hakuna kiasi cha maneno yako matupu ya Hamas yatakayomzuia kafiri wa Kiyahudi kutokana na mauaji yake. Isipokuwa uyakusanye majeshi, hutaweza kwenda zaidi ya mazungumzo matupu. Watawala wa kweli, viongozi hawawaogopeshi watu wao kwa vitisho, badala yake, wanafanya kile kinachohitajika kuzuia ukafiri huo muovu kwa nguvu zilizo mikononi mwao.

Ukumbusho, Bw. Erdogan. Maadamu unalitambua umbile hili kama dola, eneo hili tayari liko hatarini, na maadamu unaendelea na uhusiano huo, wataendelea kupata nguvu kutokana na kutochukua hatua kwao kwa mauaji ya halaiki wanayofanya dhidi ya ummah.

Dua yetu kwa Mola wetu Mlezi ni kwamba awasilishe mara moja Khilafah itakayomuondoa kafiri huyu wa Kiyahudi na wasaidizi wake chini ya uongozi wa watawala, viongozi, na makamanda wasio waoga.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ahmet SAPA

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu