Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Msimamo Unaokinzana wa Indonesia juu ya umbile la Kiyahudi: Maneno Makali Lakini Ingali Inadumisha Mahusiano Mazuri

(Imetafsiriwa)

Habari:

Indonesia imeyataka mataifa ya Kiislamu na Kiarabu kukata uhusiano wa kibiashara na kiuchumi na ‘Israel’ ili kukomesha ghasia mjini Gaza. Katika kikao cha Riyadh cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na OIC, Makamu wa Waziri wa Mambo ya Nje Anis Matta alisisitiza ulazima wa kukata vitega uchumi vinavyohusiana na taasisi za Kizayuni na kuimarisha biashara ndani ya uchumi wa nchi za Kiislamu. Licha ya wito huu, biashara ya Indonesia na ‘Israel’ ilifikia dolari milioni 173 kuanzia Januari hadi Septemba 2024, ongezeko la 24.6% kutoka mwaka uliopita. Rais Prabowo Subianto, aliyejitolea kupigania uhuru wa Palestina, anakabiliwa na uungwaji mkono wa ndani kwa kususia bidhaa zinazoiunga mkono Israel. Indonesia haina uhusiano rasmi wa kidiplomasia na 'Israel'. Chanzo: jakartaglobe.id

Maoni:

Msimamo wa Indonesia kuhusu umbile la Kiyahudi unafichua kutowiana kabisa baina ya uungaji mkono wake wa kimatamshi kwa Palestina na matendo yake halisi. Huku serikali ikilaani hadharani uvamizi wa ‘Israel’ na kujiweka kama mtetezi shupavu wa uhuru wa Palestina, mahusiano ya kiuchumi na kijamii na ‘Israel’ yanaendelea. Kwa mfano, biashara ya Indonesia na ‘Israel’ ilifikia dolari milioni 173 katika miezi tisa ya kwanza ya 2024, na kuashiria ongezeko la 24.6% kutoka kipindi kama hicho mnamo 2023. Mahuruji ya Indonesia kwenda umbile la Kiyahudi, haswa katika sekta kama vile mafuta ya mawese na nguo, ulifikia. hadi dolari milioni 130.6 katika kipindi hiki. Takwimu hizi zinaonyesha uhusiano changamfu wa kibiashara, licha ya Indonesia kupinga sera za Israeli.

Zaidi ya shughuli za kibiashara, kitamaduni na kijamii pia inaakisi kusita kwa Indonesia kuchukua hatua madhubuti. Makumi ya maelfu ya watalii wa Kiindonesia, hasa mahujaji Wakristo, huzuru umbile la Kiyahudi kila mwaka, wakiimarisha mafungamano kati ya watu kwa watu. Vile vile, wanariadha na wajumbe wa ‘Israel’ wameshiriki katika hafla zilizoandaliwa na Indonesia, kama vile mashindano ya badminton na michuano ya kupanda miamba. Shughuli hizi zinaunga mkono juhudi za diplomasia ya umma ya umbile la Kiyahudi kuunda upya sura yake ndani ya Indonesia, taifa lenye Waislamu wengi zaidi duniani.

Ukinzani kama huo unaufanya uungaji mkono wa Indonesia kwa Palestina kuwa wa kisanii. Huku Makamu wa Waziri wa Mambo ya Nje Anis Matta hivi majuzi akitoa wito wa kukata mafungamano ya kibiashara na uwekezaji na umbile la Kiyahudi wakati wa mkutano wa OIC, matamshi haya yanasalia kuwa ishara tu bila kuchukuliwa hatua madhubuti.

Hizb ut Tahrir, kama sehemu ya Jumuiya ya Waislamu Ulimwenguni, imeyasihi mara kwa mara mataifa ya Kiislamu kuchukua hatua kali, ikiwemo jihad na vikwazo vya kiuchumi, kama majibu muhimu kwa uvamizi wa ‘Israel’. Licha ya wito huu, ukosefu wa ufuatiliaji kutoka Indonesia na mataifa mengine yenye Waislamu wengi unaashiria kuyapa kipaumbele maslahi ya kiuchumi na kisiasa kuliko mshikamano wa kweli pamoja na Palestina.

Hali mjini Gaza, inayoakisiwa na ghasia za kimfumo na watu kuhama, inasisitiza haja ya uingiliaji kati zaidi. Vikwazo vya kiuchumi na vikwazo vya kibiashara, ingawa vina athari, huenda visitoshe kusitisha uvamizi unaoendelea. Uingiliaji kati wa kijeshi unaweza kutumika kama jibu thabiti zaidi. Iwapo Indonesia na mataifa mengine ya Waislamu yamejitolea kwa dhati kukomesha ukoloni wa umbile la Kiyahudi, lazima wasonge mbele zaidi ya matamshi ya kejeli. Hatua madhubuti, zikiwemo kutengwa kiuchumi, kutengwa kisiasa kwa umbile la Kiyahudi, na mikakati ya kijeshi. Kwa kufanya hivyo, wanaweza kuonyesha uongozi na mshikamano wa kweli, wakihakikisha kwamba matendo yao yanawiana na maneno yao katika kupigania haki ya Palestina.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdullah Aswar

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu