Alhamisi, 09 Rajab 1446 | 2025/01/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Bila Mfumo wa Elimu ya Kiislamu, Haramu inakuwa ni Sharti la Kusoma

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 16 Novemba, gazeti la Times la India liliripoti kwamba Chuo Kikuu cha Uttarakhand Sanskrit huko Haridwar kimeanzisha hatua za kutekeleza uamuzi wa Mahakama ya Upeo juu ya mavazi ya wanafunzi ndani ya chuo kikuu na madarasani, Makamu wa Chansela wa Chuo Kikuu Dinesh Chandra Shastri aliiambia TOI mnamo Alhamisi. Hatua hiyo imekuja baada ya malalamiko kuwa “wanafunzi kadhaa wa Kiislamu wa kike wanaendelea kuvaa burka au hijabu wakiwa chuo hicho kikuu.”

Dkt. Ajai Parmar, Mkuu wa Idara ya Historia ambayo ina idadi kubwa ya wanafunzi wa kike Waislamu alisema, “Kuna wanafunzi wa Kiislamu wapatao 500 katika kozi tofauti katika chuo hicho kikuu. Kati ya hawa, takriban 24 wako wanafanya Historia shahada ya pili. Katika ya hao 16 ni wasichana, na 4 au 5 pekee kati yao huvaa burqa wakati wa masomo. Kufuatia pingamizi za hivi karibuni, chumba cha kubadilishia nguo kimetolewa karibu na lango kuu ambapo wanafunzi hawa wanaweza kubadili mavazi ya kawaida wanapoingia chuoni humo.

Maoni:

Wazo la kwamba haramu hurahisishwa ili wasichana wa Kiislamu wapate haki zao za kimsingi za Kiislamu za kupata elimu halikubaliki kabisa kwa Ummah huu kulistahimilia.

Kamwe haiwezi kuwa hivyo kwamba tunaruhusu kujieleza Kiislamu kivipande.Kuwa na Hijabu nje ya Chuo Kikuu na kulazimishwa kuivua ili kupata taaluma au maendeleo ya kijamii sio jambo la kulisherehekea. Baadhi ya wanafikra wa kisekula wanaweza kusema kwamba “angalau wanaweza kuivaa barabarani”. Huu sio msimamo halali wa kuchukua.

Mwenyezi Mungu (swt) ndiye mwamuzi wa vipimo vya sawa na makosa.

[مَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ]

“Hawakumuadhimisha Mwenyezi Mungu anavyo stahiki kuadhimishwa. Hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mwenye kushinda.” [Al-Hajj:74].

Imeripotiwa kwamba “wengi wa wasichana hao wanatoka katika malezi ya hali ya chini, hufanya vyema katika mtihani, na wana uwezekano mdogo wa kuvunja nidhamu ya chuo kikuu.” Hii ni kutokana na kuwa katika hali ya haja na kuonesha jinsi gani ukosefu wa mamlaka ya kulinda heshima ya wanawake wa Kiislamu ulivyo.  Maisha yao, utu na mustakabali wao havina usalama bila ya Khilafah Je! tunapoingia 2025 mipango hii ya kilimwengu itakoma lini?

Lazima tutambue kwamba inaweza tu kuisha pale faradhi ya Khalifah muongofu (Khalifa Rashid) itakaposimamishwa duniani kama mamlaka ya kweli ya kulinda, sio tu haki za Ummah, bali wale wote wanaokandamizwa na ushawishi wa shetani na wanaofanya kazi naye.

Wanawake wa Ummah wanasimama kidete na mapambano ya dada zetu nchini India, ambao lazima pia wavumilie ukatili uliokithiri dhidi yao, watoto wao na walezi wao wa kiume. Tunawaombea malipo na subira, Amin.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu