Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari na Maoni  

Virusi vya Korona na Mfumo wa Kirasilimali

Habari

Mkurupuko wa Covid-19 umeukamata uchumi wa dunia katika hali ngumu yenye kuyumbisha. Benki kuu zinazo ongoza duniani, hasa Benki Kuu ya Amerika (FED), zimechukua uamuzi wa kukata kiwango cha riba na kupanua mzunguko wa fedha kama ilivyo kuwa katika mgogoro wa mwaka 2008 .Mgogoro wa kipekee . Kwa mujibu wa wataalamu, mkurupuko wa Korona hauna mfano wake katika historia ya uchumi jumla wa dunia na athari ya mkurupuko huu itaweka maafa ya kudumu katika uchumi wa dunia. (Chanzo: DW, 17.03.2020).

Maoni

Siku za mwishoni mwa mwezi Disemba, virusi vya Korona, ndio mwanzo wa kugunduliwa kwake katika jiji la Wuhan nchini China, na kusambaa kote ulimwenguni. Kuanzia siku za kwanza, kujitokeza virusi hivi, vyombo vya habari vya kiulimwengu vimeibeba kadhia hii katika mitazamo tofauti tofauti. Huku baadhi yao wakisema kwamba hiki ni kirusi kilicho tengezwa katika maabara na Amerika ili kuidhoofisha China, baadhi ya wanasayansi wamesema kwamba Muundo wa RNA wa vurusi hivi sio wa aina ya kutengezwa katika Maabara na daima vinabadilika badilika kimaumbile.

Bila ya kuzingatia ni kutoka kwa nani au ni vipi virusi hivi vimejitokeza, kufikia Machi 21, 2020, kwa mujibu wa takwimu rasmi “idadi ya kesi za maambukizi ya virusi vya Korona ilifikia 244,523. Na huku kiasi cha watu walio poteza maisha ikifikia 10,031, na walio pona kupitia kupokea matibabu 86,000 (Hurriyet.com)”. Katika mkutano na waandishi wa Habari ulio fanyika jijini Geneva mnamo Machi 12,Tedros, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya la Duniani (WHO), alitangaza kwamba walivipa jina virusi vya Korona,  vilivyo onekana katika zaidi ya nchi 100 ulimwengu mzima, PANDEMIA, yaani, mkurupuko wa kiulimwengu.  Katika hatua hii, Amerika na Ulimwengu mzima, hasa nchi za Ulaya, zimeathirika vibaya na virusi hivi. Kabla ya kuzama ndani ya mada hii, ningependa kufafanua baadhi ya nukta.

Wakati virusi hivi vilipo jitokeza mwanzo nchini China, Amerika iliviongoza vyombo vya habari vya kiulimwengu ikitaka kuligeuza janga hili na kuwa fursa kwao. Kando na vipi virusi hivi vilivyo jitokeza au vipi vilivyo zaliwa, wakabuni mchezo, lakini mchezo huu walio ubuni ukawageukia  kama mdundo wa mpira na kuwapiga wenyewe, pia. Na hii inakuwaje!!!

Virusi vya Korona hakika vimetikisa serikali zote, hasa ulimwengu wa kirasilimali wa Kimagharibi. Vimeshusha viwango vya riba na bei ya mafuta iliyo wekwa juu ya dolari hamsini na Amerika. Kwani vimekuwa na athari ya kushtua mno kwa uchumi wa dunia, athari yake bado inaendelea kuongezeka. 

Virusi vya Korona vimeonyesha kwamba mfumo wa urasilimali  ni dhaifu mno na usio imara. Kihakika, kutokana na virusi vya Korona, nchini Amerika, ambayo ndiyo inayo kadiriwa kuwa yenye uchumi wenye nguvu zaidi duniani, akiwa amesimama zaidi ya nusu saa akiwa pamoja na wasaidizi wake, Trump alilazimika kuwashawishi raia kupitia kusema urongo. Kwa sababu, bila shaka, mfumo wao ni kama utandu wa buibui kama vile alivyo twambia Mola wetu.

 (مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنكَبُوتِ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ)

Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni kama mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui , laiti kuwa wanajua. [Al-‘Ankabut 41].

Virusi vya Korona vimeonyesha kwamba mitego iliyo tegwa na makafiri wote, bila ya kuzingatia pande zao, itashindwa kweli kweli mbele ya nguvu na uweza wa Mwenyezi Mungu Azza wa Jalla ambaye ndiye mmiliki wa Kiti cha Enzi. Kwa sababu Mwenyezi Mungu ana majeshi yanayo onekana na yasiyo onekana ardhini na mbinguni. 

(وَلِلَّـهِ جُنُودُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَكَانَ اللَّـهُ عَزِيزًا حَكِيمًا)

“Na Mwenyezi Mungu ana Majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima”. [Al-Ankabut 41]

Wale ambao wana jenga hofu na kukatisha tamaa katika mioyo ya Waislamu na na kuwaegemezea kwa makafiri, hasa kwa Amerika, kwa kuwa wana nguvu, wanaweza kudhibiti kila kitu angani na wana silaha nyepesi na nzito lazima watazame sasa nani mmiliki wa kweli wa nguvu. Kwa sababu hiki kirusi kimeuwacha ulimwengu mzima pasi na msaada  wowote ingawa wamepangilia na kuendeleza aina zote za ushirikiano na kuwa na teknolojia ya hali ya juu na hiki kirusi kimegeuka na kuwa ni nguvu isiyo weza kudhibitiwa.

Virusi hivi lazima vitambulike kama ni fursa kubwa na onyo kwa Waislamu kote ulimwenguni. Lazima ichukuliwe kama ni fursa kubwa kwa sababu virusi hivi, ambavyo haiwezekani kuviona, vimevunja uti wa mgongo wa mfumo huu muovu na kuonyesha ni wanyonge na madhaifu kiasi gani kana kwamba umetengeza kutokana na maboksi. Kwa hiyo, Waislamu wanalazimika kufanya kazi kwa nguvu zao zote ili kuirudisha dini ya Mwenyezi Mungu, Khilafah iliyo anguka miaka 99 iliyopita, bila ya kuhofia lawama ya yeyoye mwenye kulaumu isipo kuwa Mwenyezi Mungu Azza wa Jalla. Bila shaka kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli na tunatarajia kwamba hali tuliyo nayo sasa ndio wakati wake haswa.

Mwisho, katika hadithi sahihi iliyo simuliwa na Muslim katika kitabu cha Al-Imara, Rasulullah (saw) amesema:

«إِنَّهُ لَمْ يَكُنْ نَبِيٌّ قَبْلِي إِلَّا كَانَ حَقًّا عَلَيْهِ أَنْ يَدُلَّ أُمَّتَهُ عَلَى خَيْرِ مَا يَعْلَمُهُ لَهُمْ وَيُنْذِرَهُمْ شَرَّ مَا يَعْلَمُهُ لَهُمْ وَإِنَّ أُمَّتَكُمْ هَذِهِ جُعِلَ عَافِيَتُهَا فِي أَوَّلِهَا وَسَيُصِيبُ آخِرَهَا بَلَاءٌ وَأُمُورٌ تُنْكِرُونَهَا وَتَجِيءُ فِتْنَةٌ فَيُرَقِّقُ بَعْضُهَا بَعْضًا وَتَجِيءُ الْفِتْنَةُ فَيَقُولُ الْمُؤْمِنُ هَذِهِ مُهْلِكَتِي ثُمَّ تَنْكَشِفُ وَتَجِيءُ الْفِتْنَةُ فَيَقُولُ الْمُؤْمِنُ هَذِهِ هَذِهِ فَمَنْ أَحَبَّ أَنْ يُزَحْزَحَ عَنْ النَّارِ وَيُدْخَلَ الْجَنَّةَ فَلْتَأْتِهِ مَنِيَّتُهُ وَهُوَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلْيَأْتِ إِلَى النَّاسِ الَّذِي يُحِبُّ أَنْ يُؤْتَى إِلَيْهِ وَمَنْ بَايَعَ إِمَامًا فَأَعْطَاهُ صَفْقَةَ يَدِهِ وَثَمَرَةَ قَلْبِهِ فَلْيُطِعْهُ إِنْ اسْتَطَاعَ فَإِنْ جَاءَ آخَرُ يُنَازِعُهُ فَاضْرِبُوا عُنُقَ الْآخَرِ»

Hakika hakuna mtume aliyekuwa kabla yangu isipokuwa ilikuwa ni wajibu juu yake kuongoza umma wake kwa lile analolijua kuwa ni kheri kwao na kuwaonya kwa lile alilolijua kwamba ni shari kwao; na hakika Ummah wenu huu umejaaliwa afiya yake ni kwa wale wa mwanzo wake, na katika awamu ya mwisho ya kuwepo kwake itakuwa yenye kujaribiwa kwa misukosuko  na pamoja na vitu ambavyo sio vyenye kukubalika kwenu. (Katika kipindi hicho) kutakuwa na majaribu makubwa yatakayo tokea moja baada ya jengine, na kila janga litakalofuatia litazidi  lililo tangulia kwa uzito. Wakati watakapo kuwa wakijaribiwa kwa misukosuko, muumini atasema: Haya ndio mauti yangu. Na wakati janga litakapo koma, watakuwa wenye kujaribiwa kwa misukosuko tena kwa janga jengine, na muumini atasema: Hii ni hakika sasa itakuwa ndio mwisho wangu. Yeyote mwenye kutarajia kuepukana na moto na kuingia peponi anatakiwa kufa akiwa na imani juu ya Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na awatendee watu mambo ambayo na yeye angetaraji kutendewa na watu. Yule atakaye kumpa bay'ah (kiapo cha utiifu) Khalifah kwa kiganja cha mkono wake na dhati ya moyo wake (yaani hufanyiwa utiifu kwa dhahiri na kwa siri). Basi na amtii kwa kadri anavyo weza. Na pindi atakapo kuja mtu mwengine na kuzozana naye (akiwa mwenye kudai ukhalifah), kateni shingo ya huyo mwengine.  

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Muhammed Hanefi Yagmur

  #Covid19   #Korona  كورونا#

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 16 Aprili 2020 19:37

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu