Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Epuka Fujo Kumbatia Uislamu

Habari:

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari na tume mbalimbali zinazofuatilia masuala ya uchaguzi nchini kenya; ni kuwa Wakenya hivi sasa wametaharuki na kuingiwa na wasiwasi usokuwa kifani.juu ya uwezekano wa kuibuka kwa ghasia. Hii ikiwa inatokamana na matamshi, mizozo na vitisho kutoka kambi za wanasiasa na taasisi za kitaifa kuhusu namna uchaguzi wa Agosti 8 utakavyoendeshwa au kusimamiwa. Kila upande ukijipigia upatu na kushawishi ngome yake kuwa macho na kuwa tayari kulinda maslahi yao kwa hali yoyote ile.

Maoni:

Yasikitisha kuona kuwa kila baada ya miaka mitano Wakenya wanaingia katika uchaguzi ambao wakihaidiwa makubwa na wanasiasa waongo na wasiokuwa na maadili. Ambao lengo lao ni kuwafanya kama ngazi ili kufikia utawala na hatimaye kujilimbikizia utajiri na mali huku raia wakizama ndani ya umasikini, afya mbaya na miundo mbinu mibovu nk.

Wakati kampeni zimechacha ni muhimu sana kuzingatia mambo yafuatayo:

Kwanza:Uchaguzi huu na mingine iliyotangulia kamwe haitoleta natija kwa Wakenya kwa kuwa asili uchaguzi chini ya nidhamu ya kidemokrasia umemakinishwa juu ya kumpa mwanadamu jukumu la kwenda kutunga sheria kinyume na alizoweka Muumba wa wanadamu.

Pili:Kushiriki au kutoshiriki kamwe hakuna mafungamano na kufaulu au kutofaulu kwako katika maisha haya maanake kimsingi kufaulu ni kuishi ukiwa unatekeleza sheria za Mola wako na huku ukitarajia kuingizwa peponi.

Tatu:kutokubali kutumiwa na wanasiasa katika kuleta fujo na kuhangaisha wenzako kwa misingi ya uchama, ukabila n.k. Mfano tukiangalia Uchaguzi wa 1997 na 2007 ambao ulipelekea kufurushwa na wengine kuuwawa kwa baadhi ya makabila fulani katika maeneo fulani. Walionufaika baadaye ni wanasiasa

Nne: Uchaguzi sio mwisho wa maisha wala sio lengo la kuishi kiasi kwamba tufikie kiwango cha kutaharuki na kuingia wasiwasi kama inavyoshuhudiwa hivi sasa tunapoona watu wanahama majumba yao, wawekezaji wanakimbia, wafanyi biashara wanahamisha bidhaa zao n.k

Enyi Waislamu;

Kufaulu kwenu ni kushikamana na njia ya Allah (swt) na Mtume (saw) nayo ni njia iliyoonyoka ambayo ni kujifunga na maamrisho yakiwa ni pamoja na kulingania kurudi tena kwa maisha ya Uislamu kupitia kuisimamisha tena Serikali ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Utume. Kujiepusha na makatazo ikiwemo pamoja na kushiriki chaguzi za kidemokrasia ambazo hatima yake ni kumkufurisha Allah (swt) kwa kuenda kinyume na hukm zake. (إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ)Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu.” [Yusuf:40]

Uislamu umeharamisha kumwaga damu ya Muislamu, kupora mali yake na kumkosea heshima yake. Na pia umeharamisha Waislamu kujifunga na Uaswabia; عَنْ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَيْسَ مِنَّا مَنْ دَعَا إِلَى عَصَبِيَّةٍ، وَلَيْسَ مِنَّا مَنْ قَاتَلَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ، وَلَيْسَ مِنَّا مَنْ مَاتَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ» Kutoka kwa Jubeir bin Mut'im kwamba Rasul (saw) Asema: Sio katika Sisi Anayelingania Katika Uaswabia, Na Sio Katika Sisi Anayepigania Uaswabia, Na Sio Katika Sisi Anayekufa Kwa Ajili Ya Uaswabia." (Uaswabia– Ukabila, Uzalendo, Utaifa, Uchama, Urangi n.k)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 27 Juni 2020 15:40

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu