Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 07/09/2022

Vichwa vya Habari:

• Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje kuwa Waziri Mkuu Mpya wa Uingereza

• Washirika wa Marekani Watayarisha Kiwango cha Juu cha Bei ya Mafuta

• Mapigano ya Umwagaji Damu jijini Baghdad

Maelezo:

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje kuwa Waziri Mkuu Mpya wa Uingereza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Liz Truss amechukua nafasi ya Boris Johnson kama waziri mkuu wa Uingereza baada ya Chama cha Conservative cha Uingereza kupiga kura ya kumfanya kiongozi wa serikali. Alimshinda Waziri wa Fedha wa zamani Rishi Sunak, kwa kuungwa mkono na 57% ya wanachama wa Conservative. Liz Truss hakika ni mwendelezo wa Boris Johnson na ushindi huo mdogo unaweza kumletea Truss shida kwa upinzani bungeni. Akitikisa kichwa kwa kambi yake, yeye binafsi alimshukuru Johnson, "kiongozi anayeondoka" na "rafiki yangu". Alisema alivutiwa "kutoka Kyiv hadi Carlisle." Wakati akifanya kampeni ya kuwa waziri mkuu, Truss alisema ikiwa atachukua wadhifa huo, atafuata nyayo za Johnson na kuwa "rafiki mkubwa zaidi" wa Ukraine ili kuhakikisha kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin "anashindwa nchini Ukraine na kupata pigo la kimkakati." Liz Truss sasa ndiye Waziri Mkuu wa nne wa Uingereza katika kipindi cha miaka 6 na kwa migawanyiko katika chama cha tory na changamoto kubwa za Uingereza tangu kujiondoa kutoka Muungano wa Ulaya (Brexit) siyo pepo iliyoahidiwa, Inasalia kuonekana iwapo Liz Truss anaweza kubaki kiongozi hadi uchaguzi mkuu ujao mnamo Mei 2024.

Washirika wa Marekani Watayarisha Kiwango cha Juu cha Bei ya Mafuta

Mawaziri wa fedha kutoka G7 wametangaza kuwa wanapanga kutekeleza kiwango cha juu cha bei ya mafuta ya Urusi. Wazo la kiwango hicho cha juu cha bei ni kudhibiti faida za Urusi kutokana na mauzo ya mafuta, ambayo yako juu sasa kuliko kabla ya vita huku mafuta yakiwekwa kwenye soko la kimataifa ili bei zisipande. Mpango huo unategemea utekelezaji kutoka China na India, ambazo zimekuwa wanunuzi wakuu wa mafuta ya Urusi kutokana na kampeni ya vikwazo vya Magharibi. China na India tayari zinanunua mafuta ya Urusi kwa punguzo, na zina sababu ndogo ya kuharibu hali hiyo na Moscow. Urusi ilijibu kwa onyo kwamba italipiza kisasi dhidi ya mpango wowote wa kuweka kiwango cha juu cha bei ya mafuta ya Urusi. "Kunaweza tu kuwepo na hatua za kulipiza kisasi," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari, kulingana na Reuters. Endapo Urusi italipiza kisasi kwa kupunguza uzalishaji wa mafuta, bei za kimataifa zinaweza kupanda hadi viwango vya juu kupita kiasi, wataalamu na wachambuzi wamesema. Wachambuzi wa JP Morgan Chase walisema kwamba ikiwa Urusi itapunguza uzalishaji wa mafuta kwa mapipa milioni 3 kwa siku, itapandisha bei hadi $190 kwa pipa.

Mapigano ya Umwagaji Damu jijini Baghdad

Takriban watu 30 waliuawa na 700 kujeruhiwa katika mapigano yaliyotokea hivi karibuni jijini Baghdad, yakiashiria tukio la umwagaji damu mkubwa zaidi lililowahi kushuhudiwa katika mji mkuu wa Iraq katika miaka ya hivi karibuni. Ghasia hizo zilizuka baada ya mwanachuoni wa Kishi’ah Muqtada al-Sadr kutangaza bila kutarajiwa kwamba anaachana na siasa, jambo lililozua mkanganyiko na hasira miongoni mwa mamilioni ya wafuasi wake. Jijini Baghdad, wafuasi wa al-Sadr waliingia mabarabarani, ambapo walipambana na wafuasi wa makundi hasimu. Mapigano hayo yanajiri huku kukiwa na mvutano kati ya wafuasi wa al-Sadr na Mfumo wa Uratibu wa Shia unaounga mkono Iran (SCF) kuhusu juhudi za kuunda serikali kufuatia uchaguzi wa Oktoba 2021. WanaSadri walishinda viti vingi, lakini sio vya kutosha vya kuunda serikali ya upande mmoja. Wapinzani wao ndani ya SCF walishinda idadi ya pili kwa ukubwa ya viti katika uchaguzi huo, ambavyo wamevitumia tangu wakati huo kuzuia uundwaji wa serikali ya WanaSadri - na kuiacha Iraq ikiwa katika mgogoro wa kisiasa kwa karibu mwaka mmoja.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu