Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 17/12/2022

Vichwa vya Habari:

Macron Atangaza Kondomu za Bure kwa Watu wenye Umri wa miaka 18 hadi 25 nchini Ufaransa

David Cameron Achukua Kazi ya Ualimu katika Chuo Kikuu cha New York Abu Dhabi

Tatizo la Taliban la Pakistan ni la Amerika Pia

Maelezo:

Macron Atangaza Kondomu za Bure kwa Watu wenye Umri wa miaka 18 hadi 25 nchini Ufaransa

Rais wa Ufaransa amesema kondomu zitatolewa bure katika maduka ya dawa kwa watu wenye umri wa miaka 18 hadi 25 katika jaribio la kupunguza mimba zisizohitajika miongoni mwa vijana. "Ni mapinduzi madogo ya uzazi wa mpango," Emmanuel Macron alitangaza wakati wa mjadala wa afya na vijana huko Fontaine-le-Comte, kitongoji cha Poitiers magharibi mwa Ufaransa. Hatua hiyo imekuja baada ya serikali kuanza kutoa huduma ya uzazi wa mpango bure kwa wanawake wote walio chini ya umri wa miaka 25 mwaka huu, na kupanua mpango unaolenga watoto chini ya miaka 18 ili kuhakikisha vijana wa kike hawaachi kutumia uzazi wa mpango kwa sababu hawana uwezo wa kuumudu. Kondomu tayari zinafidiwa na mfumo wa huduma ya afya ya kitaifa ikiwa itaagizwa na daktari au mkunga, hatua inayokusudiwa kupambana na kuenea kwa Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa. Kuhusu elimu ya jimai kwa ujumla, rais alisema: “Hatuko vizuri sana katika somo hili. Uhalisia ni tofauti sana na nadharia. Ni eneo ambalo tunahitaji kuwaelimisha walimu wetu vyema zaidi.” Macron alivaa barakoa usoni kwenye mkutano huo, akisema alikuwa akifuata miongozo ya wizara ya afya, huku serikali ikipima majibu yake kwa kuongezeka kwa kesi za Covid katika kipindi cha kabla ya Krismasi, ingawa hadi sasa hakuna maagizo ya barakoa ambayo yalikuwa yameletwa tena. "Tukikabiliwa na kuenea kwa janga hili ... Nadhani ni vyema kuweka mfano kwa sababu hatutaki kurudi kwenye majukumu ya jumla," alisema. Viongozi wanawasihi watu kuvaa barakoa katika kumbi zilizo na watu wengi na kupata nyongeza za chanjo ya Covid wakati msimu wa baridi unakaribia. [Chanzo: The Guardian]

Maadamu Wafaransa wanalishwa mlo wa kila siku wa uhuru wa kibinafsi, kondomu za bure au elimu ya ngono haitakomesha kamwe mimba za utotoni. Uhuru wa kibinafsi pia unachochea kuongezeka kwa familia za mzazi mmoja, baba na mama wasiowajibika, mgogoro wa uzee, na kupungua kwa idadi ya watu. Lakini mwathirika mkubwa zaidi wa uhuru wa kibinafsi ni familia zilizovunjika ambazo huongeza mzigo wa walipa kodi.

David Cameron Achukua Kazi ya Ualimu katika Chuo Kikuu cha New York Abu Dhabi

David Cameron, waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, amekubali nafasi ya ualimu katika Chuo Kikuu cha New York Abu Dhabi. Atawafundisha wanafunzi kuhusu siasa katika enzi ya usumbufu wakati wa kozi ya wiki tatu mnamo Januari, NYUAD ilithibitisha kwa The National. Kozi hiyo itapatikana kwa wanafunzi wote wa NYUAD, pamoja na wahitimu wa muda wote wa NYU katika maeneo mengine. Mada itajumuisha uhamiaji na uvamizi wa Ukraine. "David Cameron atakuwa akifundisha kozi ya wiki tatu kama sehemu ya J-Term mnamo Januari inayoitwa Kufanya Siasa na Serikali katika Enzi ya Machafuko," taarifa kutoka chuo kikuu hicho ilisema. "NYU Abu Dhabi inatoa kozi za J-Term katika maeneo mengi duniani kote. Madarasa mengi yako wazi si kwa wanafunzi wa NYU Abu Dhabi pekee bali pia wahitimu wa muda wote wa NYU kutoka maeneo mengine katika mwaka wao wa pili, wa chini, au wa juu. Kozi hizi zinawapa wanafunzi fursa ya kusoma pamoja na kupata uzoefu wa aina nyingi za Mtandao wa Kimataifa wa NYU. "Mbali na kitivo, kozi za J-Term zinafundishwa na wasomi mashuhuri, waandishi, wasanii, waandishi wa habari, wataalamu, na wachambuzi wa sera ambao hufundisha tu wakati wa muhula wa masomo wa Januari." Bw Cameron alionekana kwenye Tamasha la Mawazo la Abu Dhabi mwaka wa 2018, hafla ya NYUAD, na alizungumza katika kikao chenye kichwa Ubaguzi: Kuziba Mapengo na Saratani: Mwisho wa Maoni. Hapo alitoa maoni kuhusu mojawapo ya mada atakazozifunza mnamo Januari. "Kwa hakika nchini Uingereza, tunapaswa kufanya vizuri zaidi katika kudhibiti uhamiaji ... [ni] suala la kwanza la kisiasa mwaka baada ya mwaka," alisema. Usumbufu wa kisiasa ni mada Bw. Cameron anayoijua sana kuihusu. Alikuwa waziri mkuu kati ya 2010 na 2016, alipokubali kuwapa Waingereza chaguo la kusalia EU au la. Wakati kura ya kuondoka ilipoingia, alijiuzulu, na kusababisha jukwa la viongozi wa taifa lililogawanyika. [Chanzo: The National]

Cameron anaendelea kufuata nyayo za Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza na ametumia nafasi yake ya zamani kupata pesa katika elimu. Katika nchi za Magharibi, ni kawaida kwa wanasiasa kuondoka serikalini na kisha kuchukua dori za faida kubwa katika sekta ya kibinafsi. Kwa kufanya hivyo, fahamu ya "mlango unaozunguka" hubakishwa hai yaani, mamlaka na viunganishi huhamia kwenye duara maalum kwa gharama ya uharibifu wa umma. Madhara ya jumla kwa jamii ni kuongezeka kwa ufisadi na mapendeleo katika duru za kipote cha mabwenyenye ambayo yanalindwa na sheria, huku ufisadi wa maskini ukishtakiwa kikamilifu.

Tatizo la Taliban la Pakistan ni la Amerika Pia

Wakati Marekani ilipoondoa majeshi yake kutoka Afghanistan baada ya miaka 20 nchini humo, ilifanya hivyo kwa ahadi kwamba Taliban mara moja watakaporegea serikalini hawatatoa mazingira salama kwa makundi ya kigaidi. Ahadi ya Taliban ilihusu sio tu al Qaeda - kundi la kigaidi ambalo uwepo wake nchini ulisababisha uvamizi wa Marekani mwaka 2001 - lakini pia pacha jirani wa kimfumo wa Taliban, Taliban ya Pakistan au TTP (Tehrik-i-Taliban Pakistan). Lakini kuvunjika kwa hivi karibuni kwa usitishaji mapigano uliodumu kwa mwaka mzima katika nchi jirani ya Pakistan kati ya TTP na Islamabad kunazua maswali ya kutatanisha kama ahadi hiyo itatekelezwa. Kumalizika kwa usitishaji mapigano nchini Pakistan kunatishia sio tu kuongezeka kwa ghasia katika nchi hiyo lakini uwezekano wa kuongezeka kwa mvutano wa mpaka kati ya serikali ya Afghanistan na Pakistan. Na tayari inaweka uhusiano kati ya Taliban ya Afghanistan na mwenzake ya Pakistan chini ya uangalizi. Hivi majuzi mnamo majira ya mchipuo mwaka jana kiongozi wa Taliban ya Pakistan Noor Wali Mehsud aliiambia CNN kwamba kwa ajili ya kusaidia kuiondoa Marekani kutoka Kabul kundi lake lingetarajia kuungwa mkono na kundi la Taliban la Afghanistan katika mapambano yake yenyewe.

Mithili ya ndugu zao wa zamani waliokuwa na silaha nchini Afghanistan, Taliban ya Pakistan wanataka kupindua serikali ya nchi yao na kuweka kanuni zao kali za Kiislamu. Katika mahojiano ya kipekee na CNN wiki hii, Mehsud alilaumu kuvunjika kwa usitishaji vita kwa Islamabad, akisema "ilikiuka usitishaji mapigano na kuua makumi ya wenzetu na kuwakamata makumi yao." Lakini alilindwa zaidi alipoulizwa moja kwa moja kama Taliban wa Afghanistan sasa wanasaidia kundi lake kama alivyokuwa akitarajia.

Jibu lake: “Tunapigana vita vya Pakistan kutoka ndani ya eneo la Pakistan; kwa kutumia udongo wa Pakistan. Tuna uwezo wa kupigana kwa miongo mingi zaidi na silaha na ari ya ukombozi iliyopo katika ardhi ya Pakistan. Maneno hayo yanapaswa kutia wasiwasi sio tu kwa Islamabad, lakini pia Washington.

FBI imekuwa ikifuatilia TTP kwa angalau muongo mmoja na nusu, muda mrefu kabla ya kumbadilisha na kumfundisha Faisal Shazad kwa shambulizi lake la kuchoma moto gari katika Times Square jijini New York mnamo 2010.

Kufuatia mashambulizi ya Times Square TTP iliorodheshwa kuwa shirika la kigaidi na bado inachukuliwa kuwa tishio kwa maslahi ya Marekani. Na huku Islamabad ikiwa na nia ya kupunguza tishio kutoka kwa kundi hilo - Waziri wa Mambo ya Ndani Rana Sanaullah anasema Pakistan inaweza "kikamilifu" kudhibiti mzozo na TTP na anayaelezea mazungumzo na TTP wakati wa usitishaji wa mapigano kama mazungumzo "ambayo yanafanyika katika hali ya vita" – udhibiti wake wa hali unaegemea kwenye TTP iliyobaki ndani ya mipaka ya Pakistan. [Chanzo: CNN]

Tangu kuwasili kwa Amerika katika eneo hilo mapema miaka ya 80, usalama wa Pakistan na hadhi ya eneo yanaendelea kuhujumiwa. Kupigana vita vya kimataifa vya Marekani dhidi ya ugaidi (GWOT) au kabla ya hapo kufanya kazi na Marekani ili kukabiliana na Wasovieti nchini Afghanistan kumesababisha hasara kubwa kwa mujtamaa wa Pakistan. Matokeo ya kuwa na sera ya kigeni inayounga mkono Marekani ni kwamba Pakistan inakabiliwa tena na kuenea kwa uasi wa kutumia silaha unaotokana na GWOT. Amerika haiko tena kukabiliana na pigo, na uongozi wa Pakistan unatarajiwa kikamilifu na Biden kukabiliana na tishio hili linalozidi. Ndio licha ya kutelekezwa na Amerika, uongozi wa Pakistan unaendelea kuweka maslahi ya Amerika mbele ya Pakistan.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu