Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari 15/03/2023

Benki za Amerika Zaporomoka

Wadhibiti wa Marekani walifunga Benki ya Silicon Valley (SVB) yenye makao yake California, ambayo ilibobea katika kutoa mikopo kwa makampuni ya teknolojia. Sasa ndio benki kubwa zaidi ya Marekani iliyofeli tangu 2008. Tangu kuporomoka kwake benki mbili zaidi pia zimeporomoka. Maafisa wa Marekani wametoa hakikisho kwamba wawekaji amana wa SVB watalipwa kikamilifu ili kuhakikisha mambo hayawi mabaya zaidi. Benki ya Silicon Valley ilikuwa imenunua mabilioni ya dolari katika bondi katika miaka ya hivi majuzi, kwa kutumia amana za wateja. Hata hivyo, thamani ya bondi hizo ilishuka huku Hifadhi ya Shirikisho ikioongeza viwango vya riba kwa fujo. Wateja wa SVB walikuwa malimbukeni na makampuni mengine ya teknolojia ambayo yalikuwa yamepungukiwa na pesa katika mwaka uliopita. Matokeo yake, wateja wa SVB walianza kutoa amana zao. Kadiri uondoaji ulivyoongezeka ukubwa ndivyo benki ilivyohitaji kuuza mali zake ili kukidhi maombi ya wateja wake. Uvumi ulipoenea kuhusu benki hiyo kuhitaji kuuza mali, biashara na wafanyikazi matajiri wa teknolojia walianza kuwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa kufeli kwa benki. Huku wakikimbilia kutoa pesa na kusababisha kukimbiwa kwa benki hiyo. Wadhibiti waliichukua benki hii ili kulinda mali yake iliyobaki na amana. Mfumo wa benki wa Kimagharibi umejengwa juu ya madhaniwa na kutengeneza asali vizuri zaidi ya ile iliyopo kwenye amana. Hii inasababisha kuanguka kwa mabenki mara kwa mara lakini muhimu zaidi kushuka kwa uchumi na kuporomoka kwa uchumi. Inasalia kuonekana kuenea huku duniani kote.

China Yasimamia Makubaliano kati ya Iran na Saudia

Saudi Arabia na Iran zilikubaliana kuregesha uhusiano wa nchi hizo mbili na kufungua tena afisi za balozi ndani ya miezi miwili ijayo, na kumaliza mpasuko wa miaka saba. Taarifa ya pamoja ya pande tatu ilitolewa jijini Beijing na kutiwa saini na mwanadiplomasia mkuu wa China Wang Yi, mshauri wa usalama wa taifa wa Saudi Musaad bin Mohammed al-Aiban na mkuu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran, Ali Shamkhani. Makubaliano hayo yanathibitisha kanuni zikiwemo “kutoingilia masuala ya ndani ya nchi” na “ubwana wa dola”, na kuregelea kwamba Iran na Saudi Arabia zinataka kutekeleza tena makubaliano ya ushirikiano wa kiusalama waliotia saini mwaka 2001. Kwa kuanzisha upya mafungamano na Iran, Saudi Arabia inatarajia kupunguza uwezekano wake wa mashambulizi ya moja kwa moja ya Iran, pamoja na uharibifu wa dhamana kutokana na kuzorota kwa uhusiano kati ya Marekani na Iran. Iran, kwa upande wake, inatumai makubaliano hayo yatazuia Saudi Arabia kuzidisha mahusiano na mpinzani mkuu wa kikanda wa Tehran, 'Israel'. Makubaliano hayo huenda yakasaidia kupunguza mivutano badala ya kutatua tofauti kubwa kati ya mataifa yote mawili. Lakini ukweli kwamba yalisimamiwa na China unaonyesha ushawishi unaoongezeka wa Beijing.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu