Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari 14/06/2023

Pakistan Yanunua Mafuta ya Urusi kwa Idhini ya Marekani

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif alitangaza mnamo Juni 11 kwamba shehena ya kwanza ya mafuta ghafi ya Urusi iliyopunguzwa bei ilikuwa imewasili Karachi. Huku bei kamili ambayo Pakistan ililipa kwa mafuta hayo ikiwa bado haijafahamika, shirika la habari la Reuters liliripoti kuwa Pakistan ililipia usafirishaji kwa kutumia Yuan ya China. Usafirishaji huo pengine utaleta afueni kwa Pakistan huku kukiwa na hali mbaya ya kiuchumi na mgogoro wa mizani ya biashara za ndani na nje ya dola, kwani malipo mengi ya nje ya nchi ni ya uagizaji wa kawi kutoka nje. Ingawa kwa juu juu makubaliano haya yanaweza kuonekana kwenda kinyume na uhusiano wa Pakistan na Marekani, Masood Khan, balozi wa Pakistan alithibitisha katika kongamano moja jijini Washington lililoandaliwa na Taasisi ya Wilson Center ya Asia Kusini juu ya mustakabali wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili. “Tumetoa agizo la kwanza la mafuta ya Urusi, na hii imefanywa kwa kushauriana na serikali ya Marekani. Hakuna sintofahamu kati ya Washington na Islamabad kuhusu hesabu hii. Wamependekeza kuwa muko huru kununua chochote chini au hadi kikomo cha bei, na tumetii makubaliano hayo. Nadhani Washington iko sawa na hilo.” Mazungumzo kuhusu mpango wa bei ya mafuta ghafi ya Kirusi iliyopunguzwa yaliripotiwa kuanza mnamo Februari 2022, wakati Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan alipotembelea Urusi katika siku za mwanzo za uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Juhudi za kupata makubaliano ziliendelea kwa miezi kadhaa, na hatimaye kukamilika kwa ununuzi ulioripotiwa mnamo Aprili 2023 kwa shehena mbili za jumla ya tani 100,000 za mafuta, zilizowasili wiki hii.

Wazayuni Waunda Kitengo Kipya cha Kijasusi cha Kijeshi Kujitayarisha kwa Vita na Iran

Jeshi la 'Israel' limeunda kitengo kipya cha kijasusi kujiandaa kwa vita na Iran huku kukiwa na mvutano kati ya mataifa hayo mawili. Umbile la Kiyahudi limekuwa likiendesha vita vya siri dhidi ya Iran kwa muda mrefu, lakini katika miaka ya hivi karibuni, maafisa wa 'Israel' wamekuwa wakizungumza kwa uwazi zaidi juu ya ukweli kwamba wanajiandaa kwa mzozo wa kijeshi na Jamhuri hiyo ya Kiislamu. Ripoti ya Ynet ilisema tawi la ujasusi la Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) liliunda kitengo hicho kipya kujiandaa mahsusi kwa mapambano na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC). Mkuu wa utafiti wa kitengo kipya cha kijasusi, kinachojulikana kama Tawi 54, aliiambia Ynet kwamba maandalizi ya mzozo na Iran ni tofauti sana na vita vya 'Israel' ambavyo vimeanzisha nchini Lebanon na Gaza. “Haya ni mabadiliko muhimu ya kifikra ambayo IDF inahitajika kufanya. Hayafanani na vita dhidi ya Hezbollah au operesheni huko Gaza dhidi ya kundi la Hamas au Jihad ya Kiislamu,” alisema afisa huyo aliyefahamika kwa jina la Luteni Kanali T. Habari za maandalizi mapya ya 'Israel' kwa vita na Iran zinajiri huku kukiwa na ripoti kwamba Marekani na Iran zimekuwa katika mazungumzo mapya kuhusiana na mpango wa nyuklia wa kiraia wa Iran, ingawa pande zote mbili zimepuuzilia mbali wazo kwamba makubaliano yanakaribia. Kutokana na ripoti hizo, Waziri Mkuu wa ‘Israel’ Benjamin Netanyahu alimwambia Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken kwamba hakuna makubaliano kati ya Marekani na Iran yatakayozuia ‘Israel’ kuishambulia Jamhuri hiyo ya Kiislamu.

Iran Yathibitisha Kufanya Mazungumzo Yasiyo ya Moja kwa Moja na Marekani

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilithibitisha mnamo Jumatatu tarehe 12 Juni ilisema kuwa maafisa wa Iran walifanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani nchini Oman mwezi uliopita lakini ikatupilia mbali wazo kwamba makubaliano ya muda ya nyuklia yapo mezani. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Nasser Kanaani alionekana kuthibitisha ripoti kutoka kwa Axios iliyosema kuwa mazungumzo hayo yalifanyika Oman Mei 8, wakati afisa mkuu wa Rais Biden wa Marekani katika Mashariki ya Kati kwenye Baraza la Usalama la Taifa, Brett McGurk, alipokuwa jijini Muscat. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, maafisa wa Marekani na Iran hawakukutana moja kwa moja, na maafisa wa Oman walifanya kama wasuluhishi. Vyanzo vya habari vimeiambia Axios kuwa ujumbe mkuu ambao Marekani iliwasilisha kwa Iran ni tishio kwamba kutakuwa na madhara makubwa iwapo Iran itarutubisha uranium kwa asilimia 90, ambayo inahitajika kutengeneza bomu la nyuklia. Lakini hakuna dalili kwamba Tehran itachukua hatua hiyo. Huku kukiwa na ripoti za ushirikiano wa Marekani na Iran, Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alisema Jumapili kwamba “hakuna chochote kibaya” kwa Iran kufikia makubaliano juu ya mpango wake wa nyuklia mradi tu miundombinu inabakia imara. Khamenei pia alisisitiza msimamo wa Iran kwamba haitafuti silaha za nyuklia.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu