Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari 12/07/2023

Erdogan wa Uturuki Akubali Kuunga Mkono Uanachama wa NATO wa Sweden

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekubali kuunga mkono uanachama wa NATO wa Sweden katika mkesha wa kuamkia mkutano wa siku mbili wa NATO nchini Lithuania. Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema kuwa Erdogan amekubali kuwasilisha itifaki za kujiunga kwa Sweden kwa Bunge la Uturuki, Bunge Kuu la Kitaifa, ambalo linahitaji kuidhinisha uanachama wa NATO wa Stockholm. Tangazo hilo lilikuja baada ya Erdogan na Stoltenberg kukutana na Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kristersson. Katika taarifa yao ya pamoja, viongozi hao wamebainisha juhudi ambazo Sweden imechukua ili kuikomboa Uturuki tangu mkutano wa NATO wa mwaka jana jijini Madrid. Mgogoro mkubwa wa Uturuki na Sweden ni madai ya kuunga mkono PKK. Taarifa hiyo ilisema Sweden "imeifanyia marekebisho katiba yake, imebadilisha sheria zake, na kupanua kwa kiasi kikubwa ushirikiano wake wa kukabiliana na ugaidi dhidi ya PKK." Kwa kuomba kujiunga na NATO, Sweden iliachana na sera yake ya muda mrefu ya kutounga mkono upande wowote, ambayo iliizuia nchi hiyo kutoshiriki vita viwili vya dunia.

Mirziyoyev Ashinda Uchaguzi wa Urais wa Uzbekistan

Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev alishinda uchaguzi wa urais wa 2023 dhidi ya upinzani wowote, na kumwezesha kusalia madarakani hadi angalau 2030. Mirziyoyev alipata 87% ya kura dhidi ya wagombea watatu wa upinzani ambao hawakujulikana. Uchaguzi huo wa haraka unakuja baada ya Uzbekistan kupitisha kura ya maoni ya kikatiba ya kuongeza ukomo wa mihula ya urais kutoka mihula miwili ya miaka mitano hadi miwili ya miaka saba, ambayo pia inaweka upya hesabu ya mihula ya Mirziyoyev. Ushindi wa Mirziyoyev unahakikisha kuendelea kwa utawala wake wa mkono wa chuma. Zaidi ya hayo, kuna uwezekano ataendelea kukuza msimamo wa Uzbekistan wa kutoegemea upande wowote kwenye vita vya Urusi na Ukraine ili kupata mikataba ya nishati na Urusi na kuzidi kuagiza bidhaa za Urusi kama nishati. Ushindi wa Mirziyoyev pia unamaanisha Uzbekistan itaendelea kushirikiana kwa tija na serikali ya Taliban ya Afghanistan na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ili kuhakikisha utulivu wa Afghanistan. Kuna uwezekano mkubwa atawania kuchaguliwa tena mwaka 2030, na kuendeleza utawala wake hadi 2037.

Putin Aripotiwa Kukutana na Prigozhin kufuatia Uasi wa Wagner

Waziri wa vyombo vya habari wa Urusi Dmitry Peskov alitangaza katika taarifa yake ya kila siku kwamba Rais Vladimir Putin alikutana na Yevgeny Prigozhin, kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner, na maafisa wakuu wa Wagner jijini Moscow, Urusi, mnamo Juni 29. Katika mkutano huo, Putin na Prigozhin walijadili kuhusu mpango wa kuondoa mashtaka dhidi ya Prigozhin juu ya uongozi wake wa uasi wa Wagner wa Juni 23-4 dhidi ya Wizara ya Ulinzi, na pia walishughulikia mustakabali wa operesheni za Wagner nje ya nchi na Ukraine. Katika mkutano huo, Prigozhin aliimarisha uaminifu wake kwa Putin, licha ya Putin (hadi sasa) kukataa kumfukuza Shoigu au Gerasimov. Tangazo la hadhara la mkutano huo linakuja siku nne baada ya Rais wa Belarus Alexander Lukashenko kudai kuwa Prigozhin hayuko Belarusi. Inaweza kuonekana kuwa tangazo hilo lilikuwa kuonyesha udhibiti wa Putin kwa Wagner, kwani aliweza kufikia maelewano ya amani na viongozi wa Wagner bila kukubaliana na matakwa ya Prigozhin kwamba Putin awaweke kando mkuu wa Majeshi Valery Gerasimov na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu. Tangazo hilo pia linapendekeza kwa umma kwamba Putin hakumuona Prigozhin kama tishio la halisi na kwamba serikali ina umoja, na hivyo kuimarisha hadharani nguvu ya utawala wa rais.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu