Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uhakiki wa Habari 23/08/2023

Kongamano la BRICS

Viongozi na maafisa wakuu kutoka mataifa matano yenye uchumi unaoinukia duniani walikutana jijini Johannesburg kwa mkutano wa siku tatu wa BRICS. Jumuiya hiyo—ambayo wanachama wake ni Brazil, Urusi, India, China, na Afrika Kusini—inawakilisha asilimia 40 ya watu wote duniani na robo ya Pato lake la Taifa. Masuala mawili makuu kwenye ajenda yalikuwa upanuzi wa kundi hilo na kuachana na matumizi ya dolari. Huku mkutano huo ukionyesha jinsi China na Urusi zinavyosukuma BRICS kushirikiana na Global South, kwa jicho la kumaliza ushawishi wa Magharibi, malengo ya wanachama wengine wa BRICS bado hayaeleweki. Afrika Kusini ilidai zaidi ya nchi 40 zilionyesha nia ya kujiunga na umoja huo, na karibu dazeni mbili zilituma maombi rasmi ya kujiunga na umoja huo. Nchi zinazojulikana kuwa na nia ni pamoja na Algeria, Argentina, Misri, Indonesia, Iran, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu. Lakini pamoja na nia hii, mikutano ya kilele ya BRICS imeshindwa kuendeleza ushirikiano kwa kiasi kikubwa kwa sababu Brazil na India zimeelezea wasiwasi wao kuhusu malengo ya Beijing na Moscow ya kutumia BRICS kukabiliana na G-7. Brazil na India zina mafungamano ya kina na Marekani na Ulaya na hazina mvutano wa kijiografia na nchi za Magharibi kama vile China na Urusi zilivyo. Kongamano hilo lilimalizika bila maelezo yoyote ya kina kuhusu jinsi kundi hilo litakavyoipiku dolari. Kutabanni sarafu mpya inaonekana kuwa ndio njia pekee ya wanachama wanaweza kuchukua nafasi ya dolari. Ingawa uwezekano huo umejadiliwa sana kwenye vyombo vya habari, hakuna dalili ya maendeleo yoyote kufanywa.

Misheni ya UN nchini Afghanistan Yanakili Mauaji ya Kinyume cha Sheria

Zaidi ya wanajeshi na maafisa 200 wa zamani wa Afghanistan wameuawa kinyume cha sheria tangu Agosti 2021 licha ya msamaha wa jumla uliotangazwa na Taliban mara tu baada ya kuchukua mamlaka. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Misaada nchini Afghanistan (UNAMA) - katika ripoti yake ya kwanza tangu uchukuaji mamlaka wa Taliban miaka miwili iliyopita - uliandika matukio 800 ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwemo kukamatwa kiholela na kuwekwa kizuizini, kuteswa na kupotezwa kwa watu kwa nguvu. UNAMA ilirekodi karibu nusu ya mauaji ya kiholela ya maafisa wa zamani wa serikali na vikosi vya usalama vya Afghanistan katika miezi minne ya kwanza ya utawala wa Taliban. Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Volker Turk, alisema katika taarifa yake iliyoambatana na kutolewa kwa ripoti hiyo mnamo Jumanne. Tangu Taliban wachukue madaraka mwaka 2022, kwa ujumla wamewasamehe maafisa wa zamani wa serikali na wafanyikazi, lakini walisema wazi wale ambao walikuwa sehemu ya huduma ya siri, ambao walifanya mauaji makubwa dhidi ya Taliban hawatasamehewa na hii ilikuwa muhimu ili kuimarisha utawala wao. Wakati Marekani ilipoweka Muungano wa Kaskazini madarakani mwaka 2001 wanajeshi wa Marekani na wababe wa kivita ambao Marekani ilishirikiana nao walifanya mauaji ya kila aina ili kuimarisha nafasi yao. Huku ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa ikijaribu kuchora picha ya Taliban wakiwa na damu mikononi mwao, uvamizi wa Marekani wa miongo miwili umesababisha mikono yao kuchuruzika damu.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu