Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uhakiki wa Habari 27/09/2023

Marekani Yaahidi Msaada Zaidi kwa Visiwa vya Pasifiki

Marekani imewaahidi wanachama wa Jukwaa la Visiwa vya Pasifiki (PIF) maendeleo makubwa na vifurushi vya misaada ya miundombinu vyenye thamani ya dolari milioni 200 katika mkutano wao wa pili wa kila mwaka jijini Washington. Waziri Mkuu wa Visiwa vya Solomon Manase Sogavare aliuruka mkutano huo kwa kupuuza dhahiri. Wakati kukosekana kwa Sogavare kunaonyesha mapendeleo ya serikali yake kwa China licha ya Marekani kuingia (kama vile kufungua upya ubalozi), muamala wa Marekani na Visiwa vya Pasifiki ni muhimu ili kuidhibiti China. Marekani ilitumia muda mwingi wa karne ya 20 kupanuka kutoka bara la Amerika Kaskazini ili kujilinda katika nusu ya ulimwengu wake. Huko Pasifiki Amerika ilifanya miungano anuwai ya usalama na visiwa vidogo vya Pasifiki ambapo ilikuja kuiona kama msaada dhidi ya  mtu yeyote aliyetaka kupambana na Marekani. Marekani ilitumia hatua za Kijapani wakati wa WW2 kukamilisha utawala wake wa Pasifiki. Lakini wakati Vita Baridi vilipoanza Marekani ilipuuza Pasifiki kwani ililenga Eurasia na Atlantiki. Katika muongo mmoja uliopita wakati Marekani iliposhughulika katika ulimwengu wa Kiislamu na China ikatumia uzito wake wa kiuchumi kukuza mahusiano ya kiuchumi na kisiwa hicho na sasa inakubali mikataba ya ulinzi, na Visiwa vya Soloman vinakubaliana na uwepo wa jeshi la China. Bahari ya Pasifiki itakuwa uwanja muhimu wa vita kati ya dola hizo mbili.

Uchaguzi wa Urais wa Misri Wapangwa Disemba

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kitaifa ya Uchaguzi ya Misri alisema uchaguzi wa urais utafanyika mnamo tarehe 10-12 Disemba 2023 na uwezekano wa raundi ya pili mnamo tarehe 8-10 Januari 2024 iwapo hakutakuwa na mgombeaji atakayepata 50%, katika raundi ya kwanza ya uchaguzi wa kitaifa tangu 2018. Al-Sisi huenda asishinde raundi ya kwanza ya uchaguzi moja kwa moja kwa sababu ya kutoridhiwa kwa hali ya uchumi kuliko enea, lakini udhibiti wake wa vyombo vya habari, mfumo wa kisiasa na vikosi vya usalama inahakikisha kwamba atashinda raundi ya pili. Hata hivyo, mvutano wa kiuchumi unaoendelea wa Misri na matarajio ya uongozi unaoendelea wa Al-Sisi yanaweza kusababisha harakati nzuri za upinzaji na hata ghasia ambazo zinalenga kurudia mapinduzi ya 2011 yaliyofanikiwa. Ingawa watu kadhaa wa upinzaji tayari wametangaza kuwa wanagombea, wote wamelalamika juu ya unyanyasaji wa vikosi vya usalama, na wachunguzi wachache wanawatarajia kuwa na uwezo wa kufanya kampeni kwa uhuru au kwa haki. Mnamo mwaka wa 2019, mihula ya urais ya Misri ilirefushwa kutoka miaka minne hadi miaka sita, ikimaanisha kuwa muhula unaofuata utaisha mnamo 2030.

‘Israel’ Yalegeza Kamba juu ya Urutubishaji wa Nyuklia wa Saudia

Maafisa wa Marekani na 'Israel' wanaufanyia kazi mpango wa mradi wa nyuklia wa Saudia ambao utaruhusu Saudi Arabia kurutubisha urani kwenye ardhi yake, ambalo ni takwa kuu la Saudi Arabia huku kukiwa na mazungumzo juu ya uhalalishaji mahusiano kati ya 'Israeli' na Saudia. Waziri wa Mambo ya nje wa umbile la Kiyahudi Eli Cohen pia alidokeza kwamba mfumo wa uhalalishaji mahusiano unaweza kuwa tayari mapema mwanzoni mwa 2024. Lakini, Knesset na Congress zinabaki kuwa na shaka, kwani haijulikani ni usalama juu ya urutubishaji wa nyuklia wa Saudia utakuwa kiasi gani. Kwa kuongezea, vikosi vyengine katika Congress na Knesset vinaendelea kupinga makubaliano mengine kwa Saudi Arabia yanayohusishwa na uhalalishaji mahusiano, ikiwemo makubaliano ya usalama wa Marekani kwa Riyadh na makubaliano kwa Wapalestina. Kiongozi wa upinzaji wa 'Israel' Yair Lapid alisema 'Israel' inapaswa kupinga mpango wowote wa urutubishaji wa nyuklia wa Saudia, kwani Saudi Arabia mwishowe inaweza kutumia uwezo huu kutengeza silaha za nyuklia. Mnamo Septemba 20, Mfalme Mtarajiwa wa Saudia Mohammed bin Salman kwa mara nyengine tena alitishia kupata silaha za nyuklia ikiwa Iran itapata, ingawa alisema Saudi Arabia haikupendelea nchi kuwa na silaha kama hizo.

Pakistan Kufurusha zaidi ya Wakimbizi 1 milioni wa Afghanistan

Pakistan imeamua kuwarudisha wakimbizi wote haramu wa Afghanistan katika uamuzi mkubwa wa sera, ambao unaonekana katika muktadha wa mvutano unaoendelea kati ya nchi hizo mbili. Duru rasmi zilisema kwamba baraza la mpito la mawaziri la federali, kupitia mukhtasari wa ilani, liliidhinisha uamuzi wa kuwarudisha wakimbizi wengi kama milioni 1.1 wa Afghanistan wanaoishi nchini Pakistan kinyume cha sheria. Duru hizo zinasema watu wengi kama 400,000 waliingia Pakistan kinyume cha sheria tangu kurudi kwa Taliban ya Afghanistan nchini Afghanistan mnamo Agosti 2021, na kuongeza kuwa kumekuwa na Waafghani wengine 700,000 waliotambuliwa ambao wamekuwa wakiishi nchini kinyume cha sheria. Baraza la Mawaziri lilizipana mamlaka idhini ya kufanya mipango ya kuwarudisha Waafghani wote katika nchi yao. Msako dhidi ya wakimbizi haramu wa Afghanistan umejiri dhidi ya mazingira ya mvutano kati ya Pakistan na Afghanistan juu ya Tehreek-e-Taliban Pakistan (TTP) iliyopigwa marufuku na kulegeza kamba kwa Afghanistan kuanzisha msako dhidi ya TTP. Pakistan inafadhaishwa kwamba licha ya matakwa ya mara kwa mara Taliban ya Afghanistan wanasita kuchukua hatua dhidi ya TTP. Wiki iliyopita, ujumbe wa Pakistan ulioongozwa na mjumbe maalum wa Balozi wa Afghanistan Asif Durrani ulitembelea Kabul kuishinikiza serikali ya Taliban kuchukua hatua dhidi ya TTP.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu