Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

  Vichwa vya habari 15/04/2020

Vichwa vya habari:

Muonekano wa uchumi unakatisha tamaa

Trump amesema anasitisha ufadhili wake kwa Shirika la Afya Duniani kwa kushindwa kupambana na virusi vya korona

Maelezo:

Muonekano wa uchumi unakatisha tamaa

Siku ya Jumanne Shirika la Fedha Duniani lilichapisha utabiri wake wa muelekeo wa uchumi wa kiulimwengu. Shirika hilo la IMF limeonyesha namna virusi vya korona vilivyo athiri vibaya mno uchumi kuliko hata ilivyo kuwa wakati wa Mporomoko Mkubwa wa kiuchumi, kwa nchi  zilizo endelea kiuchumi inatarajiwa uchumi kushuka kwa asilimia 6.1 katika mwaka wa 2020 na kwa nchi zinazoinukia kiuchumi utasinyaa kwa asilimia 1. Uchumi wa Amerika utashuka kwa asilimia 6, na ukosefu wa ajira utabakia juu ya asilimia 9 hadi mwaka wa 2021. Uingereza itakua kwa kati ya asilimia 6.5 na 24 katika mwaka wa 2020, huku kanda ya Ulaya inatarajiwa kushuka kwa asilimia 7.5. Mataifa mengi yatakayo salia na zuio la shughuli za kijamii, uchumi zao zitayumba kwa muda na kadri hali hiyo itakavyo endelea basi mgogoro wa kiuchumi utazidi kuwa mbaya. Nchi nyingi za Kimagharibi kamwe hazija regesha hali zao kutokana na mgogoro wa kiuchumi uliopita wa mnamo 2008 na kwa hali inavyo onekana janga hili lililopo sasa litafanya mambo kuwa mabaya zaidi.

Trump amesema anasitisha msaada wake kwa Shirika la afya duniani kufatia kushindwa kupambana na virusi vya korona

Siku ya Jumanne tarehe 14 Aprili, Raisi wa Amerika Donald Trump alisema, ameuagiza utawala wake kusitisha kwa muda ufadhili wake kwa Shirika la Afya Duniani kwa kushindwa kwake kupambana na janga la virusi vya korona. Trump, akiwa katika mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya White house, alisema, “Shirika la Afya Duniani limeshindwa kutekeleza jukumu lake la kimsingi na hivyo ni lazima liwajibishwe.” Alisema shirika hilo liliunga mkono China katika "upotoshaji" wake kuhusu virusi na hivyo kupelekea mkurupuko huo kuwa mkubwa zaidi kuliko vile ambavyo ungekuwa. Amerika ni mfadhili mkubwa katika shirika hilo lenye makazi yake jijini Geneva, ilichangia zaidi ya dolari milioni 400 mnamo 2019, ambayo ni takriban asilimia 15 ya bajeti nzima ya shirika hilo. Lakini Trump ameendelea kulishambulia shirika hilo la afya wakati ambapo janga la kiafya linaendelea, amekuwa akilishutumu shirika hilo kwa kuiunga mkono China katika masiku ya mwanzo ya janga la virusi vya korona, na kusababisha vifo visivyo stahili. Trump amekuwa akiutumia utawala wake kuonyesha kutoridhishwa na shirika hilo huku ikizingatiwa kuwa hivi sasa Amerika ndio inayo ongoza kwa idadi ya vifo kutokana na virusi hivyo, inavyo onekana mkakati ya kizamani wa ukwepaji lawama upo imara kwa Trump.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 30 Aprili 2020 06:07

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu