Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Silsila ya Majibu ya Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Amiri wa Hizb ut Tahrir "Juu ya Maswali ya Wanaozuru Ukurasa Wake wa Facebook wa "Kifiqhi"

Jibu la Swali

Ukusanyaji wa Qur’an Zama za Abubkar As-Swidiq Radhi za Mwenyezi Mungu Zimwendee

Kwa: Sawt Al-Tahrir

Swali:

Assalamu alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuhu

Swali kuhusu ukusanyaji wa Qur’an tukufu zama za Abubakar As-Swidiq radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee.

Niko na swali linalohusiana na ukusanyaji wa Qur’an tukufu wa Abubakar As-Swidiq, Je ilikuwa ni kunakili au ukusanyaji wa vibao ambavyo viliandikwa Qur’an? Najua kuwa tabanni katika kitabu cha Shakhsiya na Jibu la Amir Mwenyezi Mungu amhifadhi kuhusu haya maudhui, na kitabu cha Taysirul wusul ilal usul, vyote vinasema kwamba ukusanyaji wa Abubakar wa Qur’an yamaanisha ni ukusanyaji wa vijibao ambavyo vimeandikwa na sio kunukuu, lakini nimesoma baadhi ya Nusus ambazo zinatambulisha kuwa makusudio ya ukusanyaji ni kunuu vijibao na sio kuviweka pamoja, Na hizi nusus ni kama yanayofuata:

Imetajwa katika kitabu cha Al Murshid ul-Wajiz ilaa Uluumin Tataa'llaqu bil Kitabil Aziz" miongoni mwa utunzi wa Shihabu Din Abdulrahman bin Ismail bin Ibrahim maarufu kwa jina la Abi Shaybah Al Maqdisiy aliyekufa mwaka 665 Hijri nukuu kadhaa zinazojulisha kuwa ukusanyaji ulikuwa ni kunukuu na kuandika kutoka katika nyaraka zilizoandikwa mbele ya Mtume (saw) katika kitabu kimoja na sio ukusanyaji wa hizo nyaraka katika kitabu kimoja...hadi mwisho na yadhihiri kwangu mgongano huu na kilichokuja katika kitabu cha Shakhsiya, na kilichokuja katika Jibu la Swali, sisi twakataa nukuu moja kwa moja na twazingatia ukusanyaji kuwa ni ukusanyaji wa hivyo vijibao ambavyo viliandikwa mbele ya Mtume (saw) wakati hizi dalili zinathibtisha hayo.

Vipi tunaweza kulinganisha? Na Mwenyezi Mungu awabariki.

Jibu:

Waalaykum Salam Warahmatullahi Wabarakaatuh,

1- Kuhusiana na ukusanyaji wa Qur’an, hayo tumeyafafanua katika vitabu vyetu kwa sura ya wazi, na kwamba katika zama za Abubakar radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee  kulikuwa na ukusanyaji wa nyaraka zilizoandikwa mbele ya Mtume (saw) juu ya vipande vya nguo (viraka) au ngozi au mawe, na vikabakia hivyo kwa Abubakar radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee mpaka kufa kwake, Kisha kwa Umar radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee mpaka kufa kwake, kisha kwa Hafswa Radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee... Na katika zama za Uthman radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee ikawa kuna haja ya kunukuu kutoka kwa hivi viguo (viraka) vilivyokusanywa. Akatuma Ujumbe kwa Hafswa radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee na vikaletwa hivyo viguo vilivyokusanywa Qur’an na akanukuu kutoka hapo kwa Misahafu kadhaa, akatuma kwa maeneo na kubakia na moja na ndio msahafu wa "Al Imam"... na hili jambo tumelifafanua ufafanuzi wa wazi na wenye kutosheleza.

2- Naam zimekuja riwaya zengine tofauti zinazofanya kuwa kunukuliwa kulitukia katika zama za Abubakar radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee, na kwamba kunukuliwa huku ilikuwa ni kutoka kwa vijitambaa vilivyoandikwa na Maswahaba... Na kuna riwaya zengine zinasema kuwa kunukuliwa ilikuwa ni sehemu ya Qur’an na sio Qur’an yote na hayo yalikuwa katika zama za Abubakar ... na mfano wake.

3- Lakini kile kinachotegemewa katika hali hii na mfano wake ni kuchukuliwa riwaya zilizonukuliwa kutoka kwa Bukhari, na kisha kuangaliwa katika riwaya zengine zikiafikiana na kilichoandikwa katika riwaya ya Bukhari zitachukuliwa, na zikigongana hazichukuliwi.

Na kwa kuyasoma haya Masuala kama yalivyokuja katika Bukhari yanabainika yanayofuata:

A- Imekuja katika Sahih Bukhari:

(4311-  Ametuhadhia Abul Yamani ametuelezea Shua'yb kutoka kwa Zuhriy asema amenieleza ibnu Sabbaaq kwamba Zayd bin Thaabit Al Answaariy radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee, na alikuwa miongoni mwa wanaoandika Wahyi asema: Alituma kwangu Abubakar mauwaji ya watu wa Yamama akiwa na Umar akasema Abubakar: Hakika Umar alinijia akasema: Hakika mauwaji yamezidi kwa watu siku ya Yamama na mimi nahofia mauwaji yasizidi kwa wasomaji wa Qur’an katika maeneo ipotee Qur’an nyingi kama hamjaikusanya, Na mie naona ukusanye Qur’an. Akasema Abubakar: Nikamwambia Umar: Vipi nitafanya kitu ambacho hakukifanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)? Akasema Umar: Wallahi ni kheri. Hakuwacha Umar kunikinaisha juu ya hilo hadi Mwenyezi Mungu akakifungua kifua changu nikaona kile alichokiona Umar. Akasema Zayd bin Thabit na Umar yuko hapo amekaa hazungumzi: Akasema Abubakar: Hakika wewe ni Barobaro mwenye akili na wala hatukutuhumu ulikuwa ukiandika Wahyi kwa Mtume (saw) ifuatilie Qur’an na ukusanye. Wallahi lau angenikalifisha kuliondosha Jabali miongoni mwa majabali lisingekuwa zito kwangu kuliko lile aliloniamrisha la kukusanya Qur’an. Nikasema: Vipi mtafanya jambo ambalo hakulifanya Mtume (saw)? Akasema Abubakar: Wallahi hilo jambo ni la kheri. Sikuwacha kukuuliza mpaka Mwenyezi Mungu akakifungua kifua changu kwa lile alilokifungua kifua cha Abubakar na Umar, Nikasimama nikafuatilia Qur’an na kuikusanya kutoka katika vipande vya nguo (viraka), mifupa, ngozi na kutoka kwa vifua vyao waja (waliohifqdhi) mpaka nikapata katika Suratu Tawbah aya mbili kwa Khuzaymah Al Answaariy sikuzipata kwa mwengine asokuwa yeye.

((لَقَدۡ جَاۤءَكُمۡ رَسُولࣱ مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ عَزِیزٌ عَلَیۡهِ مَا عَنِتُّمۡ حَرِیصٌ عَلَیۡكُم ))

"Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana." [At-Tawba: 128] hadi mwisho wake, na nyaraka ambazo zimekusanywa kwayo Qur’an zikawa kwa Abubakar mpaka Mwenyezi Mungu akamfisha kisha zikawa kwa Umar mpaka Mwenyezi Mungu akamfisha kisha zikawa kwa Hafswa Binti Umar...) mwisho

B- Na katika Sahih Bukhari pia:

(6654-  Ametuhadithia Muhammad bin Ubaydillah Abu Thabit ametuhadithia Ibrahim bin Saa'd kutoka kwa ibnu Shihab kutoka kwa Ubayd bin Sabbaaq kutoka kwa Zayd bin Thabit asema: Abubakar aliniita kwa  mauwaji ya watu wa Yamama akiwa pamoja na Umar akasema Abubakar: Hakika Umar amenijia akasema: Hakika mauwaji yamezidi kwa wasomaji wa Qur’an na mimi nachelea mauwaji yasizidi kwa wasomaji wa Qur’an katika maeneo yote ipotee Qur’an nyingi, na mimi naona uamrishe ikusanywe Qur’an. Nikasema: Vipi nitafanya kitu ambacho hakukifanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)? Akasema Umar: Wallahi ni kheri. Basi hakuwacha Umar yuwanikinaisha juu ya hilo hadi Mwenyezi Mungu akakifungua kifua changu kwa lile alilofungua kifua cha Umar nikaona juu ya hayo rai ya Umar, Akasema Zayd: Akasema Abubakar: Hakika wewe ni Barobaro mwenye akili na wala hatukutuhumu ulikuwa ukiandika Wahyi kwa Mtume (saw) ifuatilie Qur’an na uikusanye. Akasema Zayd: Wallahi lau angenikalifisha kuliondosha Jabali miongoni mwa majabali lisingekuwa zito kwangu kuliko lile alilonikalifisha la kukusanya Qur’an. Nikasema: Vipi mtafanya jambo ambalo hakulifanya Mtume (saw)? Akasema Abubakar: Wallahi hilo jambo ni la kheri. Basi hakuwacha kunisisitiza na kunihimiza hadi Mwenyezi Mungu akakifungua kifua changu kwa lile alilofungua kifua cha Abubakar na Umar na nikawa na rai juu ya hilo. Nikafuatilia Qur’an na kuikusanya kutoka mifupa na vipande vya nguo (nguo) na ngozi na kutoka kwa vifua vya wanaume (waliohifadhi Qur’an) nikapata katika mwisho wa Suratu Tawbah:

(لقد جاءكم رسول من أنفسكم)

"Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe" [At-Tawba: 128] mpaka mwisho wake pamoja na Khuzaymah au Abi Khuzaymah nikaiunganisha na Sura yake na nyaraka (suhuf) zilikuwa kwa Abubakar katika uhai wake mpaka Mwenyezi Mungu akamfisha kisha zikawa kwa Umar katika uhai wake mpaka Mwenyezi Mungu akamfisha kisha zikawa kwa Hafsa Binti Umar... Asema Muhammad bin Ubaydillah; Al-likhaaf ni viungo) mwisho

C- Na zimepokewa mara kadhaa riwaya za Bukhari kutoka kwa Zayd bin Thabit radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee na kila riwaya kuna kauli ya Abubakar kumwambia Zayd: (Akasema Abubakar: Hakika wewe ni Barobaro mwenye akili na wala hatukutuhumu ulikuwa ukiandika Wahyi kwa Mtume (saw) ifuatilie Qur’an na uikusanye).

D- Na kutokana nayo yabainika kuwa Abubakar radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee alitaka kwa Zayd afuatilie Qur’an na aikusanye, na sio kuiandika, yamaanisha jukumu la Zayd radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee lilikuwa ni kuzifuatilia nyaraka (Suhuf) zilizoandikwa mbele ya Mtume (saw) sawa iwe vipande vya nguo au mifupa au mawe, akusanye na sio kuandika upya...

E- Na yatilia uzito lile la kwamba Zayd alipokuwa hakupata kuandika mwisho wa Suratu Tawbah ila kwa Khuzaymah Al Answaariy na ilikuwa haikuandikwa na mwengine, alisita ili athibitishe hilo, pamoja na kwamba wao walikuwa wameihifadhi kwa njia ya wengi zaidi ya mmoja (Tawatur), Lakini wao walizilazimu nafsi zao kwamba wasichukue ukurasa (Swahifa) ila wanaposhuhudilia wawili kwamba iliandikwa mbele ya Mtume (saw) na walipokuwa hawakupata aya hii imeandikwa ila na Khuzaymah walisita ili wapate mashahidi wawili, kwani Khuzaymah ni mmoja na wao wanataka shahidi mwengine... Na hawakuiandika aya kwa hifadhi yao pamoja na kwamba wao wameihifadhi kwa njia ya Tawatur... Kisha ikaja faraja kutoka kwa Mwenyezi Mungu wakishuhudia kundi katika maswahaba kwamba Mtume (saw) alifanya ushahidi wa Khuzayma ni sawa na ushahidi wa watu wawili, na juu ya hilo wakachukua ukurasa huu kutoka kwa Khuzaymah kwani ushahidi wake ni sawa na ushahidi wa watu wawili.

F- Ama ushahidi wa Khuzaymah kwamba unalingana na ushahidi wa wawili amepokea Ahmad katika Musnad yake na Abu Daud katika Sunan yake na tamshi ni la Ahmad: (Ametuhadithia Abul Yamaan ametuhadithia Shuaib kutoka kwa Zuhriy amenihadhia Umaratu bin Khuzaymah Al Answaariy, kwamba ami yake amemuhadithia, naye ni katika maswahaba wa Mtume (saw), kwamba Mtume (saw) alinunua farasi kutoka kwa mbedui, Mtume (saw) akamtaka amfuate ili amlipe thamani ya farasi wake, Mtume (saw) ikawa anaenda upesi mbedui akapunguza mwendo, ikawa watu wanamzuia mbedui na kujadiliana naye bei ya farasi hawajui kuwa Mtume (saw) ashamnunua, mpaka baadhi yao wakazidisha thamani ya farasi aliyenunuliwa na katika majadiliano ya bei Kwa thamani ya Farasi ambaye amemnunua Mtume (saw), Mbedui akamuita Mtume (saw) akasema: ikiwa ni wa kumnunua huyu Farasi mnunue au nitamuuza. Akasimama Mtume aliposikia mwito wa mbedui akasema: Je si nimemnunua  kutoka kwako? Mbedui akasema: Laa Wallahi sijakuuzia. Mtume (saw) akasema: bali nimemnunua kutoka kwako. Ikiwa watu wanampitia Mtume (saw) na mbedui wakijadiliana, ikawa mbedui anasema: Mlete shahidi ambaye atashuhudia kwamba mimi nimekuuzia, anayekuja katika Waislamu anamwambia mbedui: Ole wako Mtume (saw) hakuwa ila ni mwenye kusema haki, mpaka akaja Khuzaymah akisikiliza majadiliano ya Mtume (saw) na mbedui, ikawa mbedui anasema: Mlete shahidi atakayeshuhudia kuwa nimekuuzia. Khuzaymah akasema: Mimi nashuhudia kuwa umemuuzia, Mtume (saw) akamuelekea Khuzaymah akasema: Una ushahidi gani? Akasema: kwa kukusadikisha wewe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mtume (saw) akaufanya ushahidi wa Khuzaymah ni ushahidi wa watu wawili). Kadhalika Hakim Ameipokea katika Mustadrak kwa sahih mbili akasema: (... Hii hadith ni Sahih isnad yake na watu wake kwa maafikiano ya mashekh wawili ni waaminifu thiqah" na hawakuipokea mashekh wawili).

G- Yote haya yanathibitisha kuwa Swahaba ambaye kilipatikana kwake kipande kilichoandikwa aya mbili za Tawbah na hakikupatikana kwa mwengine ni Khuzaymah na sio Abu Khuzaymah kama ilivyo katika baadhi ya Riwaya kwamba Aya imetegemewa kwa kuzingatia ushahidi wa mbebaji wake kuwa ni ushahidi wa watu wawili, na hii inatabikika kwa Khuzayma na sio kwa Abu Khuzaymah... na yaonyesha jina liliwachanganya wapokezi baina ya Khuzaymah na Abu Khuzaymah na hili hutokea kawaida... juu ya yote ni Khuzaymah bin Thabit Al Answaariy kama tulivyobainisha hapo juu.

H- Na hivyo Zayd hakusimama kukusanya alichokipata kimeandikwa na Khuzaymah ila baada ya kushuhudia mashahidi kwamba ushahidi wa Khuzaymah ni ushahidi wa watu wawili kwa mujibu wa Hadith ambayo tumeitaja karibuni kuhusu Mtume (saw), na juu ya hayo Moyo wa Zayd ukapata utulivu na kukusanya hiki kipande kilichopatikana kwa Khuzaymah na kukichanganya na vipande vingine vilivyoandikwa.

I- Yote haya yanatilia nguvu kuwa jukumu la Zayd ambalo alimkalifisha nalo Abubakar ni kukusanya Qur’an na sio kuiandika, Zayd alikusanya nyaraka zilizoandikwa mbele ya Mtume (saw) na kuvipanga hivi vipande katika sura zake na sehemu zake katika mahala pamoja, na kila kipande alichokuwa anakikusanya kwa uchache watu wawili walikuwa wakitoa ushahidi kwamba kiliandikwa mbele ya Mtume (saw) isipokuwa mwisho wa Tawbah hakikuwa kinapatikana ila kwa Khuzaymah, na ndiye ambaye Mtume (saw) alifanya ushahidi wake kuwa ushahidi wa watu wawili. Na Mwenyezi Mungu amesema kweli aliposema:

(إِنَّا نَحۡنُ نَزَّلۡنَا ٱلذِّكۡرَ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَـٰفِظُونَ)

"Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda." [Al-Hijr: 9]

I- Na hivyo riwaya ambazo umezitaja katika swali kwamba alichosimama nacho Zaid katika zama za Abubakar ni kunukuu aya za Qur’an na sio kukusanya kama zilivyokuwa katika mbao, vipande vya nguo na mawe, hizi riwaya zinagongana na riwaya Sahih zilizotajwa katika Bukhari kama tulivyobainisha hapo juu. Kwa hiyo inatabikishwa juu yake tulichokitaja na kurudishwa (Diraya) ikiwa Sanad yake imewahi, au hazitachukuliwa kwa udhaifu wake ikiwa Sanad yake ni Dhaifu.

6- Na mwisho ni wazi katika swali lako kwamba wewe ushaipitia Shakhsiya Islamiyah juzuu ya kwanza, na Taysiirul Wusul ilal Usul katika maudhui ya kukusanya Qur’an kwa hiyo haina haja ni kunukulie kilichokuja katika vitabu hivi viwili kuhusu ukusanyaji wa Qur’an...

- Lakini tu nitakata kutoka katika Shakhsia yanayofuata:

)Na juu ya hayo haikuwa amri ya Abubakar katika kukusanya Qur’an ni amri ya kuandikwa kwake katika msahafu mmoja bali ni amri ya kukusanya nyaraka (Suhuf) ambazo ziliandikwa mbele ya Mtume (saw) na ziwe zimeandikwa na maswahaba na zimehifadhiwa na wao. Na zikawa hizi Suhuf zimehifadhiwa kwa Abubakar katika uhai wake, kisha kwa Umar katika uhai wake, kisha kwa Hafsa Binti Umar ummul muuminina kwa mujibu wa wasia wa Umar...

... Kwa hivyo kazi ya Uthman haikuwa ni ukusanyaji wa Qur’an, Bali ni kunakili na kunukuu yale yaliyonukuliwa kutoka kwa Mtume (saw) kama yalivyo.

Kwa hivyo hakufanya lolote isipokuwa ni kunukuu nakala saba kutokana na nakala zilizohifadhiwa kwa Hafsa mama wa waumini, na akawakusanya watu katika maandishi haya pekee na kuzuia maandishi yoyote au mjazo wowote usokuwa hayo.

Na yakamakinika mambo juu ya nakala hii kimaandishi na kiimlai, na hayo ni maandishi yale yale ambayo yaliandikwa misahafu ambayo iliandikwa mbele ya Mtume (saw) wahyi ilipoteremka nayo.

Na ndizo nakala ambazo alizikusanya Abubakar, kisha Waislamu wakawa wanatoa nakala kutokana na nakala hizi na sio zengine, na hukukubakia isipokuwa msahafu wa Uthman kwa maandishi yake. Na zilipopatikana mashini za uchapishaji ikawa msahafu huchapishwa kutokana na nakala hii kwa maandishi yale yale…)

Na nakata kipande katika kitabu cha Taysiir yanayofuata:

(Mwenyezi Mungu amechukua ahadi ya kuihifadhi Qur’an kwa hiyo hazipitiki batili mbele yake wala nyuma yake wala hawezi yeyote kubadilisha katika Qur’an harufu yoyote ila atagundulika:-

(إِنَّا نَحۡنُ نَزَّلۡنَا ٱلذِّكۡرَ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَـٰفِظُونَ)

"Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda." [Al-Hijr: 9]

 (إِنَّ عَلَیۡنَا جَمۡعَهُۥ وَقُرۡءَانَهُۥ)

"Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha." [Qiyama: 17]

(..وَلَوۡ كَانَ مِنۡ عِندِ غَیۡرِ ٱللَّهِ لَوَجَدُوا۟ فِیهِ ٱخۡتِلَـٰفࣰا كَثِیرࣰا)

"Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi." [An-Nisaa: 82]

(لَّا یَأۡتِیهِ ٱلۡبَـٰطِلُ مِنۢ بَیۡنِ یَدَیۡهِ وَلَا مِنۡ خَلۡفِهِۦۖ تَنزِیلࣱ مِّنۡ حَكِیمٍ حَمِیدࣲ)

"Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima, Msifiwa." [Fussilat: 42]

Hakika Mwenyezi Mungu ameihifadhi Qur’an tukufu na akaiwekea wale watakaoikusanya na kuihifadhi isibadilishwe na kutolewa mahala pake mpaka ikatufikia kwa njia ya kunukuliwa kutoka kwa wengi ambao haimkiniki kwao kusema uongo "Mutawatir". Kwani maswahaba- radhi za Mwenyezi Mungu ziwaendee- Walinukuu kile kile kilichoteremka na wahyi, na alichoamrisha Mtume (saw) kuandikwa, nayo itabakia imehifadhiwa mpaka hapo Mwenyezi Mungu atakapoirithi ardhi na walio juu yake na mpaka atakapo Mwenyezi Mungu).

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Rashtah

30 Rabi 'ul Awwal 1442 H

15/12/2020 M

Link ya jibu hili kutoka kwa ukurasa wa Amiri wa Facebook.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu