Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Silsila ya Majibu ya Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Amiri wa Hizb ut Tahrir "Juu ya Maswali ya Wanaozuru Ukurasa Wake wa Facebook wa "Kifiqhi"

Jibu la Swali

Falsafa ya Kiislamu

Kwa: Asad Al-Zahiriyah

Swali:

Katika Kitabu cha Mafahim ya Hizb ut Tahrir uk.35 (nakala ya Kiarabu) (uk 29-30 nakala ya Kiingereza), mstari wa 7 na 9, kimetaja “Falsafa ya Kiislamu”, lakini kinachojulikana kwetu katika chama ni kwamba hakuna wanafalsafa wala falsafa katika Uislamu.

Mungu awalipe kila la kheri


Jibu:

Yafuatayo yameelezwa katika Kitabu cha Mafahim uk.35 (nakala ya Kiarabu) (uk 29-30 nakala ya Kiingereza) kwamba:

(Kwa mukhtarasi, kitendo cha mwanadamu ni cha kimada ambacho mtu anakifanya kimada, isipokuwa kwamba anapokifanya, anatambua uhusiano wake na Mwenyezi Mungu, iwe kazi hii inaruhusiwa (halali) au imeharamishwa (haramu), hivyo anaifanya au anajiepusha nayo kwa msingi huu. Na ufahamu wa mwanadamu juu ya uhusiano wake na Mwenyezi Mungu ni roho, na ndio inayomlazimisha mwanadamu aijue sheria ya Mwenyezi Mungu ili kutofautisha matendo yake, ili apate kufahamu mema na mabaya wakati anajua ni matendo gani yanayomridhisha Mwenyezi Mungu na yanayomkasirisha, na kutofautisha ubaya na uovu. Pale sheria inapombainishia matendo mema na mabaya, na kuona maadili ambayo ni ya lazima kwa maisha ya Kiislamu katika jamii ya Kiislamu kwa mujibu wa sharia ilivyofafanua. Na kwa haya yamkinika kwake anapoifanya kazi hiyo na kutambua uhusiano wake na Mwenyezi Mungu. Kufanya kitendo au kujiepushe nacho kwa mujibu wa utambuzi huu, kwa sababu anajua aina ya kazi, maelezo yake na thamani yake. Hivyo falsafa ya Uislamu ilikuwa ni kuchanganya Mada na Roho, yaani kufanya vitendo viende sawasawa na amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu. Na falsafa hii imekuwa ya daima kwa kila kitendo cha mwanadamu kiwe kingi au kichache zaidi au kidogo. Na hii ndio taswira ya maisha. Na kwa vile aqida ya Kiislamu ndiyo msingi wa maisha, na ndio msingi wa falsafa, na msingi wa mifumo, ikawa Hadhara ya Kiislamu - ambayo ni jumla ya fahamu kuhusu maisha kutoka kwa mtazamo wa Uislamu - imejengwa juu ya msingi mmoja wa kiroho, ambayo ni itikadi (aqidah), na taswira yake juu ya maisha ni kuchanganya mada na roho, na ikawa maana ya furaha katika mtazamo wake ni kupata radhi ya Mwenyezi Mungu.)

Naam hii ndiyo falsafa katika maana ya Kiislamu (kuchanganya mada na roho), yaani kutambua uhusiano na Muumba, kwani ni neno (istilahi) sahihi katika maana hii...

Ama matumizi yake katika istilahi ya Kigiriki au kitu kinachofanana na hayo, yaani (kutafuta zaidi ya uwepo au zaidi ya mada), jambo hili linakanushwa na Uislamu. Imekuja katika utangulizi wa kitabu cha 'Al-Tafkeer' (Kufikiri) katika uk (4) (nakala ya Kiarabu) (uk 5-6 nakala ya Kiingereza), yaani, kabla ya yaliyotajwa hapo juu:

(Wanadamu wamepiga hatua kubwa katika maisha na kutoka enzi ya wakati huku wakishughulishwa zaidi na zao la akili na zao la kufikiria bila kujishughulisha na uhalisia wa akili na uhalisia wa kufikiria. Ni kweli walipatikana waliojaribu kudiriki uhalisia wa akili katika wanazuoni wa Kiislamu, na wanazuoni wasiokuwa Waislamu, zamani na sasa, lakini walishindwa kutambua uhalisia huu, na wapo ambao walijaribu kuchora njia ya kufikiri, lakini walifanikiwa katika baadhi ya vipengele vya matunda ya njia hii kwa mafanikio ya kisayansi, lakini walipotoshwa na kujua kufikiri katika suala la kufikiri, na wakawapoteza wengine waliowafuata walioshangazwa na mafanikio haya ya kisayansi. Na nyuma, tangu zama za Wayunani na wale waliofuata baada yao, walikimbilia kufikia fikra na kufikia kile kiitwacho mantiki, na wakafaulu kufikia baadhi ya fikra, lakini wakaharibu elimu kama ilivyo elimu. Kwa hivyo mantiki ilikuwa ni balaa kwa elimu badala ya kuwa – kama vile inavyotakikana kuwa – njia ya kufikia elimu na kipimo cha usahihi wake. Vilevile hawa waliokimbilia katika kufikiri pia wamefikia kile kinachoitwa falsafa, au kile kinachojulikana kama kupenda hekima, na ufikiriaji wa kina wa kile kilicho nyuma ya uhai, yaani zaidi ya mada, hivyo wakaunda utafiti ambao ulikuwa wa maarifa yenye matokeo matamu na ya kupendeza, lakini yalikuwa mbali na uhakika na yalikuwa mbali zaidi na uhalisia, na kwa hivyo ilipotosha wengi, na kupotoka kutoka kwa ufikiriaji kutoka kwa njia ya sawa.

Kusoma yale yaliyotajwa katika kitabu 'Al-Tafkeer ni uchunguzi tulivu, makini na tafakari ambayo itadhihirisha, Mwenyezi Mungu akipenda, ukweli katika maudhui ya falsafa...

Natumaini kwamba hii itatosheleza, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi na ni Mwenye hekima.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

 03 Jumada II 1443 H

06/01/2022 M

Link ya Jibu hili katika ukurasa wa Amiri wa Facebook

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu