Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah katika Ukurasa Wake wa Facebook

Jibu la Swali
Usahihi wa Hadith “سيأتي أقوام يوم القيامة يكون إيمانهم عجباً...”: Watakuja Watu Siku ya Kiyama, Imani yao itakuwa ya Kustaajabisha...”
Kwa: Azzam Abu Fara
(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalamu alaikum wa Rahmatullah wa Barakatahu

Mwenyezi Mungu akubali utiifu wako na heri ya mwaka mpya, Sheikh.

Nilikuwa nikitafuta usahihi wa Hadith hii, lakini sikuweza kupata usahihi ulio kwa maneno haya, kwa hivyo tafadhali nisaidie.

(Siku ya Kiyama, watakuja watu imani yao itakuwa ya kustaajabisha, nuru yao itatoka mikononi mwao na mikononi mwao ya kulia, na itasemwa: Leo mnafurahi, na amani iwe juu yenu ingieni humo milele, Malaika na Manabii watawaonea wivu kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwao. Basi, maswahaba wakauliza ni kina nani hao ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: si katika sisi wala si katika nyinyi, kwani nyinyi ni maswahaba zangu na hao ni vipenzi vyangu. Watakuja baada yenu na kukuta kitabu ambacho watu wameacha kukifuata na Sunnah waliyoiua, basi watakigeukia Kitabu na Sunnah na kuzihuisha na kuzisoma na kuzifundisha kwa watu, na watakumbana katika njia yake na adhabu kali zaidi kuliko mliyoyakabili. Imani ya mmoja wao ni kama arobaini katika nyinyi, na kuuawa shahidi mmoja wao ni kama arobaini katika mashahidi wenu. Mtapata wakuinusuru haki, lakini hao hawatapata wa kuwanusuru, wamezungukwa na wadhalimu kutoka kila mahali, na wako katika maeneo ya Bayt Al-Maqdis.” Na Mwenyezi Mungu akubariki.

Jibu:

Wa Alaikum Assalam wa Rahmatullah wa Barakatahu

1- Kuhusu andiko (hadith) ambalo unauliza kulihusu, hatukulipata kwa maneno haya katika kitabu chochote cha Hadith, na inaonekana kwamba baadhi ya maneno yake yamechukuliwa kutoka katika Hadith kadhaa zilizounganishwa pamoja, kwa hivyo yeyote aliyefanya hivyo alizifanya zionekane kama Hadith moja:

     1. Hadith zinazokusudiwa ni Hadith katika sura nyingi, na sio riwaya nyingi kwa Hadith moja.

      2. Pia, baadhi ya Hadith zina maneno yanayokaribiana na yale yaliyotajwa katika matni (andiko) na sio maneno yale yale.

     3. Katika andiko lililotajwa, pia kuna baadhi ya maana zilizotajwa katika baadhi ya Hadith ingawa maneno ni tofauti.

     4. Zaidi ya hayo, miongoni mwa Hadith ambazo baadhi ya maumbo na maneno yalichukuliwa matni (andiko) husika, baadhi ni Hadith zinazokubalika ambazo hutumika, na baadhi si sahihi na hazitumiki kama dalili.

2- Nitataja baadhi ya zile Hadith zilizokubaliwa ambazo hutumika kama dalili:

- Ahmad amepokea katika Musnad yake kutoka kwa Abu Malik Al-Ash’ari kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipomaliza swala yake, aliwageukia watu kwa uso wake na kusema:

«يَا أَيُّهَا النَّاسُ اسْمَعُوا وَاعْقِلُوا وَاعْلَمُوا أَنَّ لِلَّهِ عَزَّ وَجَلَّ عِبَاداً لَيْسُوا بِأَنْبِيَاءَ وَلَا شُهَدَاءَ يَغْبِطُهُمْ الْأَنْبِيَاءُ وَالشُّهَدَاءُ عَلَى مَجَالِسِهِمْ وَقُرْبِهِمْ مِنْ اللَّهِ»

Enyi watu, sikilizeni, mutafakari, na mujue kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ana waja ambao si manabii, wala mashahidi, manabii na mashahidi wanawaonea wivu kwa ajili ya mikusanyiko yao na kujikurubisha kwao kwa Mwenyezi Mungu”. Basi akaja mtu mmoja katika wapokezi wa Mabedui na akampungia mkono Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kusema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, watu ambao si katika manabii, wala mashahidi wa manabii, na manabii na mashahidi wanawaonea wivu kwa ajili ya mikusanyiko yao na kujikurubisha kwao kwa Mwenyezi Mungu, basi tusifie kuhusu wao. Basi, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akafurahishwa na swali la Bedui, hivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema:

«هُمْ نَاسٌ مِنْ أَفْنَاءِ النَّاسِ وَنَوَازِعِ الْقَبَائِلِ لَمْ تَصِلْ بَيْنَهُمْ أَرْحَامٌ مُتَقَارِبَةٌ تَحَابُّوا فِي اللَّهِ وَتَصَافَوْا يَضَعُ اللَّهُ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَنَابِرَ مِنْ نُورٍ فَيُجْلِسُهُمْ عَلَيْهَا فَيَجْعَلُ وُجُوهَهُمْ نُوراً وَثِيَابَهُمْ نُوراً يَفْزَعُ النَّاسُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يَفْزَعُونَ وَهُمْ أَوْلِيَاءُ اللَّهِ الَّذِينَ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ»

Hao ni watu kutoka katika maangamizo ya watu na fitina za makabila, wasio na mafungamano ya karibu ya kizazi baina yao, na waliopendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atawawekea mimbari za nuru, na atawaketisha juu yake, na atazifanya nyuso zao kuwa nuru, na nguo zao kuwa nuru. Watu watakuwa na hofu Siku ya Kiyama, wala wao hawatatishika, na wao ni wandani wa Mwenyezi Mungu, ambao hawatakuwa na hofu, wala hawatahuzunika.”

- Muslim amepokea katika Sahih yake kutoka kwa Abu Hurairah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alikuja makaburini na kusema: «السَّلَامُ عَلَيْكُمْ دَارَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ وَإِنَّا إِنْ شَاءَ اللَّهُ بِكُمْ لَاحِقُونَ وَدِدْتُ أَنَّا قَدْ رَأَيْنَا إِخْوَانَنَا» “Amani iwe juu yenu enyi nyumba ya waumini, na hakika sisi inshaAllah tutajiunga nanyi. Tunatamani lau tungewaona ndugu zetu”. Wao (wasikilizaji) wakasema: Je, sisi si ndugu zako, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema:«أَنْتُمْ أَصْحَابِي وَإِخْوَانُنَا الَّذِينَ لَمْ يَأْتُوا بَعْدُ»  “Nyinyi ni maswahaba zangu, na ndugu zetu ni wale ambao, bado hawaja duniani.” Wakasema: Wajuaje yule ambaye bado hajaja kutoka kwa Umma wako, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu,? Akasema: «أَرَأَيْتَ لَوْ أَنَّ رَجُلًا لَهُ خَيْلٌ غُرٌّ مُحَجَّلَةٌ بَيْنَ ظَهْرَيْ خَيْلٍ دُهْمٍ بُهْمٍ  أَلَا يَعْرِفُ خَيْلَهُ» “Waonaje; lau mtu ana farasi ambao mgongoni mwao kuna mapaku meupe na meusi, je ataweza kuwatambua farasi wake?”. Wakasema: Ndio, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema:

«فَإِنَّهُمْ يَأْتُونَ غُرّاً مُحَجَّلِينَ مِنَ الْوُضُوءِ وَأَنَا فَرَطُهُمْ عَلَى الْحَوْضِ أَلَا لَيُذَادَنَّ رِجَالٌ عَنْ حَوْضِي كَمَا يُذَادُ الْبَعِيرُ الضَّالُّ أُنَادِيهِمْ أَلَا هَلُمَّ فَيُقَالُ إِنَّهُمْ قَدْ بَدَّلُوا بَعْدَكَ فَأَقُولُ سُحْقاً سُحْقاً»

“Hakika wao watakuja Siku ya Kiyama wakiwa na nyuso, mikono, na miguu yao inang’aa, kwa sababu ya udhu.” Kisha akasema: “Nami nitafika kwenye birika (al-hawdh) mbele yenu.” Kisha akasema: “Watu watafurushwa kutoka kwa birika hilo, kama wanavyofurushwa ngamia waliopotea. Na nitawaita: “Njooni hapa!” lakini itasemwa: walibadilisha baada yako.” Basi nitasema: “ondokeni ondokeni!”

- Muslim amepokea katika Sahih yake kutoka kwa Uqbah aliyesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema: «لَا تَزَالُ عِصَابَةٌ مِنْ أُمَّتِي يُقَاتِلُونَ عَلَى أَمْرِ اللَّهِ قَاهِرِينَ لِعَدُوِّهِمْ لَا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَالَفَهُمْ حَتَّى تَأْتِيَهُمُ السَّاعَةُ وَهُمْ عَلَى ذَلِكَ» “Kundi la umma wangu litaendelea kupigana kwa ajili ya amri ya Mwenyezi Mungu kwa kumtiisha adui yao, na wale wanaowapinga hawatawadhuru mpaka iwafikie Saa ya Kiyama wakiwa katika hali hiyo”.

- Ahmad amepokea katika Musnad yake kutoka kwa Al-Baraa bin Azib kwamba Mtume (saw) alimpiga mawe Yahudi mmoja (kwa kuzini) na akasema: «اللَّهُمَّ إِنِّي أُشْهِدُكَ أَنِّي أَوَّلُ مَنْ أَحْيَا سُنَّةً قَدْ أَمَاتُوهَا» “Ewe Mwenyezi Mungu, nashuhudia kwako kwamba mimi ndiye mtu wa kwanza kuhuisha Sunnah ambayo walikuwa wameiua”.

- Ahmad amepokea katika Musnad kutoka kwa Abu Umamah aliyesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«لَا تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي عَلَى الْحَقِّ ظَاهِرِينَ لَعَدُوِّهِمْ قَاهِرِينَ لَا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَالَفَهُمْ إِلَّا مَا أَصَابَهُمْ مِنْ لَأْوَاءَ حَتَّى يَأْتِيَهُمْ أَمْرُ اللَّهِ وَهُمْ كَذَلِكَ قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَأَيْنَ هُمْ؟ قَالَ: بِبَيْتِ الْمَقْدِسِ وَأَكْنَافِ بَيْتِ الْمَقْدِسِ»

“Bado lingalipo kundi la Ummah wangu juu ya haki, linaloonekana kumshinda adui yao, na hawatadhurika na walio nyuma yao isipokuwa msiba utakapowafikia, mpaka iwafikie amri ya Mwenyezi Mungu hali wao wako hivyo. Wakasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, na wako wapi? Akasema: Katika Bayt Al-Maqdis na viunga vya Bayt Al-Maqdis”.

- Al-Tirmidhi amepokea katika kwa Sunan yake kutoka kwa Abu Umayyah al-Sha`bani ambaye amesema: Nilikwenda kwa Abu Tha'labah al-Khushni na kumwambia: unaamiliana vipi na Ayah hii? Akauliza: Aya ipi? Nikasema: Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنْفُسَكُمْ لَا يَضُرُّكُمْ مَنْ ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ]

“Enyi mlio amini! Kilicho lazima juu yenu ni nafsi zenu. Hawakudhuruni walio potoka ikiwa nyinyi mmeongoka.” [Al-Ma’idah: 5-105] Akasema: Wallahi, Nilimuuliza mjuzi mmoja kuihusu. Nilimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na akasema:

«بَلِ ائْتَمِرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَتَنَاهَوْا عَنِ الْمُنْكَرِ حَتَّى إِذَا رَأَيْتَ شُحّاً مُطَاعاً وَهَوًى مُتَّبَعاً وَدُنْيَا مُؤْثَرَةً وَإِعْجَابَ كُلِّ ذِي رَأْيٍ بِرَأْيِهِ فَعَلَيْكَ بِخَاصَّةِ نَفْسِكَ وَدَعِ الْعَوَامَّ فَإِنَّ مِنْ وَرَائِكُمْ أَيَّاماً الصَّبْرُ فِيهِنَّ مِثْلُ الْقَبْضِ عَلَى الْجَمْرِ لِلْعَامِلِ فِيهِنَّ مِثْلُ أَجْرِ خَمْسِينَ رَجُلاً يَعْمَلُونَ مِثْلَ عَمَلِكُمْ»

Amrisheni mema na katazeni maovu, hata mukiona ubakhili wa mtiifu na matamanio yanayofuatwa, na dunia yenye taathira na ajabu ya kila mwenye rai yake, huna budi kuwaacha watu wa kawaida. Kwani hakika nyuma yenu ni siku za subira, ndani yake ni kama kushika makaa ya moto, kwa yule afanyaye kazi ndani yazo ujira wake ni mithili ya ujira wa watu hamsini wafanyao kazi mithili ya kazi yenu”. Abdullah bin Al-Mubarak amesema: “Mbali na Utbah kuniongezea kwamba ilisemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ujira wa watu hamsini miongoni wetu au wao? Akasema: «بَلْ أَجْرُ خَمْسِينَ مِنْكُمْ» “Bali ujira wa watu hamsini miongoni mwenu”. Abu Issa amesema hii ni hasan lakini gharib.

3- Hadith zilizotajwa hapo juu ni Hadith zinazokubalika zinazumika. Lakini pia kulikuwa na Hadith ambazo ndani yake kulikuwa na ikhtilafu juu yake na zilikuwa na maneno na maumbo yanayofanana na matni inayozungumziwa, na nitataja baadhi yake ili kuonyesha kuwa matni inayozungumzwa imeundwa kwa Hadith kadhaa sahihi na zisizo sahihi.

Imekuja katika al-Ibana al-Kubra ya Ibn Battah kwamba Mtume (saw) amesema: «رحمة الله على  خلفائي»  “Mwenyezi Mungu awarehemu watakaokuja baada yangu”, wakasema: Wataokuja baada yako ni kina nani? Akasema: «الذين يحيون سنتي، ويعلمونها عباد الله»  “Wale ambao wanaihuisha Sunnah yangu na wanaifundisha kwa waja wa Mwenyezi Mungu, na imekuja katika Musnad ya Al-Shihab Al-Quda’i ya Katheer bin Abdullah Al-Muzni, kutoka kwa babake, kutoka kwa babu yake, aliyesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «إن الدين بدأ غريبا، وسيعود كما بدأ غريبا، فطوبى للغرباء» “Dini ilianza ikiwa ngeni, itarudi iwe ngeni kama ilivyo anza, basi bishara njema ni kwa wageni”, Ikasemwa: ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao wageni ni kina nani? Akasema: «الذين يحيون سنتي ويعلمونها عباد الله»  Wale ambao wanaihuisha sunnah yangu na wanaifundisha kwa waja wa Mwenyezi Mungu.” Imeelezwa katika mkusanyiko wa hadith: اللهم ارحم خلفائي الذين يأتون من بعدي يروون أحاديثي وسنتي ويعلمونها الناس... “Ewe Mwenyezi Mungu, warehemu watakaokuja baada yangu, watakaopokea hadith zangu na sunnah zangu na wakazifundisha kwa watu”  (Al-Tabarani katika Al-Awsat, Al-Ramhurmi katika Al-Muhaddith Al-Fasal, Al-Khatib katika Sharaf Al-Hadith, na Ibn Al-Najjar kutoka kwa Ibn Abbas kutoka kwa Ali Al-Tabarani amesema: Ahmad bin Issa Abu Taher Al-Alawi wakipekee. Amesema katika Al-Mizan: Al-Daraqutni amesema: msema urongo, na hivyo hadith hii ni batili. Ibn Abi Hatim, hakitaja jeraha au uzushi ndani yake), Al-Tabarani ameinakili katika Al-Awsat (6/77, Na. 5846). Al-Haythami (1/126) amesema: Inajumuisha Ahmad bin Issa Al-Hashimi.

Al-Daraqutni amesema: Yeye ni msema urongo. Na Al-Ramhorzi katika Al-Muhaddith Al-Fasal (1/163). Imesahihishwa pia na: Al-Dailami (1/479, Na. 1960). Al-Dhahabi amesema katika Al-Mizan (1/270, tafsiri 508) na Al-Hafiz amekuafikiana naye katika Al-Lisan (1/241, tafsiri 756) zote katika tafsiri ya Ahmed bin Isa Al-Hashimi. Daraqutni amesema: Msema urongo[.

- Imekuja katika Kanz al-Ummal ya Anas, ambaye amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), amesema: «متى ألقى أصحابي؟ متى ألقى أحبابي؟» “Lini nitakutana na maswahaba zangu? Lini nitakutana na vipenzi vyangu?, Baadhi ya Maswahaba wakauliza: Je, sisi si vipenzi vyako? Akasema: «أنتم أصحابي، ولكن أحبابي قوم لم يروني وآمنوا بي أنا إليهم بالأشواق»  Nyinyi ni maswahaba zangu, lakini vipenzi vyangu ni watu ambao hawakuniona lakini wameniamini, natamani kuwa nao (Abu Sheikh katika ujira). Na imekuja katika Al-Firdaws kwa kauli ya Al-Khattab ya Al-Daylami kutoka kwa Anas bin Malik: «مَتى ألْقى أَصْحَابِي مَتى ألْقى أحبابي» “Lini nitakutana na maswahaba zangu? Lini nitakutana na vipenzi vyangu.” Baadhi ya maswahaba wakauliza: Je, sisi si vipenzi vyako? Akasema: «أَنْتُم أَصْحَابِي غير أَن أحبابي قوم لم يروني وآمنوا بِي أَنا إِلَيْهِم بالأشواق» “Nyinyi ni maswahaba zangu, lakini vipenzi vyangu ni watu ambao hawakuniona lakini wameniamini, natamani kuwa nao”. Na Al-Qushayri ametaja katika barua kwa silsila ya wapokezi: Ali bin Ahmed Al-Ahwazi, Mwenyezi Mungu amrehemu, alitwambia: amesema: Ahmed bin Ubaid Al-Basri alitwambia, amesema: Yahya bin Muhammad Al-Jiani alitwambia, amesema: Othman bin Abdullah Al-Qurashi alitwambia , kutoka kwa Naim bin Salem, kutoka kwa Anas bin Malik, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «متى ألقى أحبابي؟» “Lini nitakutana na vipenzi vyangu?” Maswahaba zake wakauliza: Kwa jina la baba yetu na mama yetu, je sisi si vipenzi vyako? Akasema: «أنتم أصحابي، أحبابي: قوم لم يروني، وآمنوا بي، وأنا إليهم بالأشواق أكثر» “Nyinyi ni maswahaba zangu, vipenzi vyangu: ni watu ambao hawakuniona lakini wameniamini, natamani sana kuwa nao”. Hadith hii ina wapokezi wasio tegemewa, na baadhi ya watafiti wamesema kuwa ni hadith ya kukataliwa na ya urongo, ikimaanisha kwamba hadith hii si miongoni mwa hadith zinazokubaliwa zinazotumiwa kama dalili.

4- Hivyo, inakuwa wazi kuwa matni husika si Hadith ya Mtume (saw) bali ni matni changamano, iliyo undwa kwa dhahiri na mtu asiyejulikana na ambamo aliunganisha maneno na maumbo yaliyokuja katika hadith tofauti, ambazo baadhi yake zinakubalika kama dalili, na nyengine ambazo hazikubaliki na hazitumiwi, na kwa hivyo sio sahihi kusimulia. Hivyo basi, si sahihi kusimulia matni inayozungumziwa kuwa ni Hadith kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Mwenyezi Mungu ni Mwenye hekima zaidi.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

20 Rabi' al-Awwal 1444 H

Sawia na Oktoba 16, 2022 M

Link ya jibu hili kutoka ukurasa wa Amiri wa Facebook.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu