Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah katika Ukurasa Wake wa Kifikra wa Facebook
Jibu la Swali
Aina za Kufikiri
Kwa: Abu Abdullah Suleiman
(Imetafsiriwa)

Swali:

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Katika kitabu, "Shakhsiya ya Kiislamu – Juzuu I," imetajwa katika mada ya haja ya Ummah leo kuwa wafasiri, katika mstari wa tisa na wa kumi (mithili ya kitabu cha fikra angavu ya kina). Je, neno "angavu" ni sahihi?

Jibu:

Wa Alaikum Assalam wa Rahmatullah wa Barakatahu

Neno "angavu" (mustanirah) ni sahihi kwa sababu kufikiri kuna aina tatu: kwa juu juu, kwa kina, na kwa angavu. Unaweza kupata maelezo katika kitabu "Kufikiri (At-Tafkir)" ukurasa 86 hadi 92, (75-80 cha Kiingereza) na nitakufikishia kutoka huko.

(kufikiri kunaweza kuwa finyo, kwa kina au angavu. Kufikiri finyo ni kufikiri kwa watu wa kawaida. Kufikiri kwa kina ni kwa wasomi. Ama kufikiri kwa angavu, mara nyingi ni kufikiri kwa viongozi, na walioangazwa miongoni mwa wasomi na watu wa kawaida. Kufikiri duni ni kuhamisha uhalisia hadi kwenye ubongo tu pekee, bila kujadili kitu chengine chochote, na bila kujaribu kuhisi kile kinachohusiana na uhalisia; kisha kuunganisha hisia hii na maalumati yanayohusiana na uhalisia huo. bila ya kujaribu kutafuta maalumati mengine yanayofungamana nayo, kisha kutoka na hukmu ya finyo. Haya ndiyo yanayotawala katika makundi, na yanayotawala katika wale wenye fikra finyo, na yanayotawala katika watu wasio na elimu na kwa watu wenye akili ambao hawana thaqafa ...

Kuhusu kufikiri kwa kina ni kujaribu kuingia kina katika kufikiri, yaani kuingia kina katika kuuhisi  uhalisia, na katika maalumati yanayohusishwa na hisia hii ili kuufahamu uhalisia huu. Mwenye kufikiri kwa kina hataridhika na hisia tu na maalumati ya awali ya kuunganisha pamoja na hisia hii, kama ilivyo katika kufikiri finyo. Bali anarudia kuuhisi uhalisia, na anajaribu kuongeza hisia zake kwake, iwe ni kupitia kwa majaribio au kupitia kurudia kuhisi. Pia anarudia utafutaji wa maalumati  mengine kando na maalumati ya awali. Pia anarudia uunganisho wa maalumati na uhalisia zaidi kuliko alivyofanya hapo awali, ima kwa uchunguzi unaorudiwa au kwa kurudia tena uunganisho: kwa hivyo anatoka katika aina hii ya hisia na aina hii ya muunganisho na aina hii ya maalumati, kwa fikra za kina, iwe ni za ukweli au la. Kupitia kukaririwa kwa njia hii na kuizoea, fikira za kina huanzia. Kwa hivyo kufikiri kwa kina hakuridhiki na hisia ya awali, hakuridhiki na maalumati ya awali na hakuridhiki na muunganisho wa awali. Ni hatua ya pili baada ya kufikiri finyo. Huku ni kufikiri kwa wasomi na wanafikra, ingawa si lazima kuwe ni kufikiri kwa watu wenye elimu. Hivyo kufikiri kwa kina ni kuingia kina katika hisia, maalumati na muunganisho.

Ama kuhusu fikra angavu, ni kufikiri kwa kina pamoja na kufikiria juu ya kile kinachozunguka uhalisia na kile kinachohusiana nao, ili kuja na matokeo ya kweli. Kwa maana nyengine, kufikiri kina ni kuzama ndani ya fikra yenyewe, huku fikra angavu ni kuongeza kina katika kufikiri na kufikiri katika yale yanayoizunguka na yanahusiana nayo, kwa ajili ya lengo lililokusudiwa, yaani kufikia matokeo ya kweli. Kwa hivyo kila fikra anagvu ni kufikiri kwa kina. Haiwezekani kufikiri angavu kutokane na fikra finyo. Walakini, kila kufikiri kwa kina sio fikra angavu. Kwa mfano, mwanasayansi mwenye atomi; anapotafiti katika mgawanyiko wa atomi; na mwanasayansi katika kemia anapotafiti uundaji wa vitu; na faqihi anapotafiti uvuaji hukmu na kuweka sheria; wanasayansi hawa na mfano wao, wanapojadili mambo kama haya, wanafanya kina hicho, ambacho bila ya kufikiri kwa kina, wasingeweza kutoka na matokeo hayo adhimu. Hata hivyo, hawakufikiri kwa uangavu, wala kufikiri kwao hakuzingatiwi kuwa ni kufikiri angavu. Kwa hiyo, hupaswi kushangaa unapopata mwanasayansi ambaye anatafiti katika atomi, akiabudu kipande cha mbao, yaani msalaba. Ingawa uangavu mdogo unaonyesha kwamba kipande hiki cha mbao hakinufaishi wala hakidhuru, na si kitu ambacho kingeweza kuabudiwa. Usishangae pia kumkuta mtunzi wa sheria stadi akiamini mbele ya makasisi; na anajisalimisha kwa mtu kama yeye ili amsamehe dhambi zake. Hii ni kwa sababu mwanasayansi na mwanasheria na kama wao, wanafikiri kwa kina lakini si kwa uangavu. Lau wangefikiri

kwa uangavu, wasingeabudu kipande cha mbao, wala wasingaliamini kuwepo kwa makasisi, au kuomba msamaha kutoka kwa watu kama wao. Ni kweli kwamba anayefikiri kwa kina yuko ndani ya yale aliyoyawaza na sio mengine zaidi yake. Kwa hiyo anaweza kuwa na kina anapofikiria kugawanya atomi au kuweka sheria, lakini yeye ni mjinga katika mambo mengine anapofikiria kuyahusu. Walakini, mtu anayefikiria, akiwa amezoea kufikiria kwa kina huingia ndani zaidi ya kile anachofikiria, haswa mambo yanayohusiana na ugumu mkubwa, au mtazamo wa maisha. Hata hivyo, kukosekana kwa uangavu katika kufikiri kwake kunamfanya azoee kufikiri kwa kina na kufikiri kwa kina na hata kufikiri kijinga. Kwa hiyo, kufikiri kwa kina hakutoshi tu kumwamsha mwanadamu na kuinua kiwango chake cha kifikra. Badala yake ni muhimu kuwa na uangavu katika fikra ili mwinuko wa fikra utokee na ili mwanadamu aamke.) MWISHO.

Ikiwa unataka maalumati zaidi, regelea kitabu kilichotajwa. Mwenyezi Mungu awe pamoja nawe.

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

5 Sha'ban 1445 H

sawia na 15 Februari, 2024 M

Link ya jibu hili kutoka ukurasa wa Amiri wa Facebook

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu