Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Jibu la Swali

Hatua ya Rais wa Tunisia Kusimamisha Bunge na Kumfukuza Waziri Mkuu!

(Imetafsiriwa)

Swali:

(Reda Gharslawi alikula kiapo cha kikatiba mbele ya Rais Kais Saied kuendesha Wizara ya Mambo ya Ndani, baada ya kushika nafasi ya mshauri, kama ilivyo kwenye ripoti ya Al-Jazeera mnamo 30/7/2021), na Rais wa Tunisia Kais Saeed alikuwa ametangaza katika hotuba iliyopeperushwa kwenye runinga ya serikali mnamo Jumapili jioni, 25/7/2021, kufuatia mkutano wa dharura na viongozi wa jeshi na usalama, kusimamishwa kwa shughuli za Bunge na kufukuzwa kwa Waziri Mkuu Hisham Al-Mashishi kutoka majukumu yake kulingana na kifungu cha 80 cha Katiba ya Tunisia , kuondoa kinga ya wabunge, na kutangaza kuwafuta kazi Mawaziri wa Ulinzi na Sheria, na kuchukua kwake mamlaka ya kiutendaji kwa usaidizi wa Waziri Mkuu aliyemteuwa yeye mwenyewe ... Kwa nini rais wa Tunisia alichukua hatua hii? Je! Majibu ya kimataifa ni yapi? Je! Hii inamaanisha kuwa mzozo wa kimataifa umehamia sana Tunisia?

Jibu:

Ili kufafanua maoni yanayowezekana juu ya maswala haya, tunakagua yafuatayo:

1- Mgogoro kati ya Rais wa Tunisia Kais Saied na serikali na bunge ulianza mwanzoni mwa mwaka huu, wakati Waziri Mkuu Hisham Al-Mashishi alipotangaza mnamo tarehe 16/1/2021 mabadiliko ya baraza la mawaziri lililojumuisha vitengo 11 vya mawaziri kati ya 25. Rais wa Tunisia alikataa marekebisho ya vitengo hivyo vya mawaziri, pamoja na kufutwa kazi kwa mawaziri wengine wa karibu naye. Saied alisema mnamo 25/1/2021: "Mabadiliko ya mawaziri yaliyofanywa hivi karibuni na Waziri Mkuu Hisham Al-Mashishi kwa serikali hayakuheshimu taratibu zilizoainishwa kwenye katiba, hasa ile iliyoainishwa katika Sura ya 92, ambayo ni umuhimu wa majadaliano katika Baraza la Mawaziri ikiwa inahusu kuanzisha marekebisho ya muundo wa serikali, pamoja na ukiukaji mwingine (hakuutaja)." Alisema, "Baadhi ya wale waliopendekezwa katika mabadiliko ya katiba wana kesi dhidi yao au wana faili za mgongano wa kimaslahi. Yeyote anayehusika katika kesi hawezi kula kiapo, na kula kiapo sio utaratibu rasmi, lakini ni utaratibu wa kimsingi. Na alielezea kutoridhishwa kwake na "kutokuwepo kwa wanawake kutoka orodha ya mawaziri waliopendekezwa ..." (AFP, 25/1/2021). Maamuzi ya Rais yalikuja wakati Tunisia inateseka na shida ya uchumi, iliyozidishwa zaidi na athari za janga la virusi vya Korona, linalokabili nchi vibaya sana, na tishio la anguko la karibu la mfumo wa afya, ambao ulilazimisha kupokea msaada wa haraka wa kimatibabu kutoka nchi nyingine siku zilizopita. Taasisi ya Takwimu ya Tunisia imechapisha kuwa uchumi wa Tunisia umeshuka kwa asilimia 8.8 mnamo 2020, (Takwimu kutoka kwa "serikali" Taasisi ya Takwimu ya Tunisia ilionyesha, mnamo Jumatatu, kwamba uchumi wa nchi hiyo ulirekodi kushuka kwa rekodi ya asilimia 8.8 mnamo 2020. Uchumi wa Tunisia, ambao unategemea sana utalii, uliathiriwa sana na athari za janga la virusi vya Korona ... Taasisi ya Takwimu ilisema kwamba kiwango cha ukosefu wa ajira kiliongezeka hadi asilimia 17.4 katika robo ya nne ya 2020, ikilinganishwa na asilimia 16.2 iliyorekodiwa katika robo ya tatu ya mwaka huo huo .. (Anadolu Agency, 15/2/2021).

2- Mnamo tarehe 25/7/2021, Afisi ya rais wa Tunisia ilichapisha taarifa kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook, ambayo ilisema: "Baada ya kushauriana na Waziri Mkuu na Spika wa Bunge la Wawakilishi wa Watu, na kwa mujibu wa kifungu cha 80 cha Katiba, Rais wa Jamhuri, Kais Saied, amechukua maamuzi yafuatayo, leo, 25/7/2021 ili kuhifadhi uadilifu wa nchi na usalama wa nchi na uhuru, na kuhakikisha utendaji kazi wa kawaida wa taasisi za serikali: “Waziri Mkuu, Mheshimiwa Hisham Al-Mashishi, ameng’olewa, kusitisha kazi na mamlaka ya Bunge kwa muda wa siku 30; kuondoa kinga ya bunge ya wabunge wote wa Bunge la Wawakilishi wa Watu. Rais wa Jamhuri anachukua mamlaka ya utendaji akisaidiwa na serikali inayoongozwa na Waziri Mkuu aliyeteuliwa na Rais wa Jamhuri.” Aliongeza: "Na katika saa zijazo, agizo litatolewa kudhibiti hatua hizi za kipekee ambazo zililazimishwa na hali, na ambalo litaondolewa wakati sababu zao zitapotea ... Afisi ya rais inatoa wito kwa watu wa Tunisia kutofuata wanaoendeleza machafuko." (Dubai CNN, 26/7/2021). Saied alikuwa amesisitiza kuwa maamuzi yake ni ("sio kusitishwa kwa katiba, na sio kuondoka kwa uhalali wa kikatiba" (Al Jazeera Net, 26/7/2021). Na Rais wa Tunisia Kais Saied alitangaza mnamo Ijumaa kuwa hatageuka kuwa dikteta, kwa kuzingatia kwamba ("Anajua vizuri maandishi ya katiba, anaheshimu na ameyasoma."). Mapema, shirika rasmi la habari lilionyesha kwamba mahakama ilikuwa imefungua uchunguzi wa wanachama wanne wa chama cha Ennahda, pamoja na mlinzi wa kibinafsi wa Ghannouchi, kwa madai ya kujaribu kutekeleza vitendo vya vurugu mbele ya Bunge, na mwakilishi katika Bunge la Tunisia, Yassin Al-Ayari.” (FRANCE 24 - AFP - Reuters, 30/7/2021).

3- Kwenye ukurasa wake rasmi wa Facebook mnamo 26/7/2021, Spika wa Bunge la Tunisia, Rached Ghannouchi, alikanusha kuwa Rais wa Jamhuri alishauriana naye. Aliandika: "Spika wa Bunge la Wawakilishi wa Wananchi anakanusha kwamba alishauriwa ili kutekelezwa Sura ya 80 ya Katiba. Hajawahi kushauriwa na Kais Saied, Rais wa Jamhuri kuhusu kutekelezwa Kifungu cha 80 cha Katiba. Chochote kingine ni madai ya uwongo.” Mnamo Jumatatu asubuhi, jeshi lilimzuia Spika na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuingia katika makao makuu ya bunge na kuwajulisha kuwa walikuwa na maagizo ya kufunga Bunge. Ghannouchi alisema, ("Mimi ndiye Spika wa Baraza nimesimama mbele ya taasisi ambayo ninaiongoza na jeshi linanizuia kuingia ndani." Alimshtaki Kais Saied kwa kufanya "mapinduzi dhidi ya mageuzi." (Al-Jazeera, 27/7/2021), lakini Saied alisema: (Maamuzi yake ya hivi karibuni sio jaribio la mapinduzi dhidi ya katiba na kwamba hana nia ya kufanya mapinduzi dhidi ya katiba na uhalali nchini, na kwamba maamuzi ya hivi karibuni ni ya kisheria kabisa na yataisha mara tu hatari inayokabili nchi itaondolewa.” (Ukurasa wa Facebook wa Afisi ya rais wa Tunisia, 27/7/2021). Halafu, mnamo 30/7/2021, Reda Gharslawi alitoa kiapo cha kikatiba mbele ya Rais Kais Saied kuendesha Wizara ya Mambo ya Ndani, baada ya kuwa mshauri, kama Al-Jazeera ilivyochapisha mnamo 30/7/2021.

4- Kuhusu athari za nchi kuu zinazohusika katika Tunisia, zilikuwa kama ifuatavyo:

a- Amerika: Amerika haina ushawishi thabiti wa kisiasa nchini Tunisia. Jamii ya kisiasa iliyopo hapo asili ina uhusiano na Uingereza, kisha Ufaransa iliweza kuingia na ushawishi wake pia, na kwa hivyo wanasiasa wako ndani ya ushawishi wa Uropa; yaani Uingereza na Ufaransa. Amerika imejaribu kuingilia kati kwa kiwango fulani kupitia msaada wa kijeshi na misaada ya asasi za kiraia. Kuhusu msaada wa kijeshi, Amerika imejaribu njia hii kupata ushawishi nchini Tunisia. Kwa miongo kadhaa, kwa kisingizio cha ugaidi, Amerika imekuwa ikiwapa silaha, ikifanya mazoezi na kufanya kazi na jeshi la Tunisia. Amerika ilifadhili jeshi la Tunisia chini ya mfumo wa Kimataifa wa Elimu na Mafunzo ya Kijeshi (IMET) na kupitia Mpango wa Ushirika wa Kupambana na Ugaidi, usaidizi wa Amerika ulifikia takriban dolari bilioni 2.7 kati ya 2012 na 2016. Wakati huo Tunisia iliteuliwa kuwa mshirika asiye mwanachama wa NATO mnamo 2015. 1/10/2020, Waziri wa Ulinzi wa Amerika Mark Esper alisaini makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi wa miaka 10 na Tunisia. Esper alielezea katika hotuba yake baada ya mkutano wake na Rais Kais Saied, ("Tunatarajia kupanua uhusiano huu ili kusaidia Tunisia kulinda bandari zake na mipaka ya ardhi, kuzuia ugaidi na kuweka juhudi za uharibifu za tawala za mabavu mbali na nchi yako." (Africa News, 1/10/2020)

Ama uhusu njia ya msaada wa asasi za kiraia, inafanywa na Ubalozi wa Amerika nchini Tunisia katika mfumo wa Utawala Bora na Mpango wa Kusaidia Kupambana na Rushwa nchini Tunisia unaofadhiliwa na Ubalozi wa Amerika wenye thamani ya $ 5.6 milioni.

"Kituo cha Kitaifa cha Korti za Serikali (NCSC) kimesaini hati ya makubaliano na Wizara ya Uhusiano na Mashirika ya Kikatiba na Jumuiya ya Kiraia ili kuunda jukwaa la elektroniki kwa asasi za kiraia. Jukwaa hili litachangia kuwezesha asasi za kiraia kujiandikisha kwa kitalifa, pamoja na kuandaa ripoti za kifedha na za kimaelezo za shirika ili kuongeza ufanisi na mifumo ya uwajibikaji...” (Ubalozi wa Amerika jijini Tunis, Disemba 20, 2020)

Lakini njia hizi zinaweza kutumika kama kiingilio cha ushawishi katika nchi ikiwa kuna ombwe la kisiasa na isio na ushawishi wa serikali kongwe kama Uingereza, pamoja na Muungano wa Ulaya, hasa Ufaransa na Ujerumani, ambazo zinaimarika kufikia Uingereza ... Kwa hivyo, vitendo hivi vya Amerika sio ukiukaji wa ushawishi wa Uingereza au Ulaya nchini Tunisia kwa sasa. Jeshi ni dogo sana na linachukua jukumu dogo katika siasa za nchi. Kwa hivyo, bado inahitaji muda zaidi kupata mawakala waaminifu kwake na kujenga uwezo wa jeshi kuchukua jukumu lenye ushawishi nchini Tunisia, na hii inaweza kuchukua muda ... ikimaanisha kuwa jukumu la Amerika halina ufanisi nchini Tunisia hadi sasa, lakini badala yake ni jukumu la jumla kwa kisingizio cha kutaka demokrasia na haki za binadamu! Lakini, Amerika haitaacha majaribio yake ya kupenya Tunisia.

b-Uingereza: Ilikuwa ikidhibiti mambo kikamilifu kabla ya mapinduzi. Iliendesha nchi nyuma ya pazia kupitia wakala wake Zine El Abidine na mtangulizi wake Bourguiba kikamilifu, na haikuwa na mshindani wa kimataifa kwa maana halisi kwenye eneo la Tunisia, lakini ilifadhili vyama vya upinzani waziwazi, kama vile kukaribisha Rached Ghannouchi, kiongozi wa harakati ya Ennahda, kumeza upinzani wa "Kiislamu" na kutumia kadi hii muhimu wakati inahitajika ... Uingereza ilikuwa ikitangatanga nchini Tunisia. Mnamo mwaka wa 2015, Ubalozi wa Uingereza nchini Tunisia ulialika Kampuni ya Ushauri ya Kimataifa ya Adam Smith kutoa ushauri kwa serikali nchini Tunisia, kutoa mafunzo kwa maafisa wakuu na kuunda sera na kuanzishwa kwa sheria mpya. Vivyo hivyo, Aktis Strategy Ltd ililetwa Tunisia, mkandarasi wa maendeleo anayesimamia mikataba ya mamilioni ya pesa kwa Afisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza na Jumuiya ya Madola. Kwa kuongezea, Uingereza ilikuwa ikidhibiti tabaka la kisiasa kutoka Habib Bourguiba hadi Ben Ali hadi Beji Essebsi, ambaye alianzisha chama cha Nidaa Tounes mnamo 2012. Alikuwa mmoja wa marafiki wa Habib Bourguiba na mshirika wa Ben Ali, kwa hivyo alikusanya vikosi vya zamani vya kisekula, vikosi ambavyo Waingereza walikuwa wakishirikiana navyo, na kwa hivyo Uingereza ilidumisha ushawishi nchini kwa kudhibiti tabaka la kisiasa. Lakini, kunga’atuka kwa Zine El Abidine kutoka urais nchini Tunisia, Uingereza imepoteza wakala wake mwenye nguvu lakini haikupoteza utawala, kwa sababu ina mawakala wengi ndani ya dola nchini Tunisia na pia nje ya dola hiyo.

Lakini ushawishi wake wa kisiasa umekuwa dhaifu kuliko hapo awali, haikuimarishwa na kurudi kwa Ghannouchi kutoka Uingereza, ambaye ni mwaminifu kwake, kwa sababu wanachama na viongozi wa Chama cha Ennahda hawajaungana juu ya uongozi wa Ghannouchi, hasa kwa kuwa amekuwa msekula. Huko Ennahda kuna wanyofu ambao wana imani na Uturuki na rais wake Erdogan, hii ilileta kikwazo kwa Uingereza katika kuunganisha safu ya wafuasi wake, na hata ilifungua njia kwa Amerika iliyounganishwa na Uturuki kushawishi chama cha Ennahda kutoka ndani na kutishia uongozi wa Ghannouchi wa harakati kutoka ndani. Ili kumaliza suala hili, harakati ya Ennahda ilianza kupunguza "Uislamu" wake ili kuongeza kukubalika kwa wasekula ndani yake, kwa hivyo ilitenganisha "Dawah" kutoka "kisiasa" na ikaungana na Nidaa Tounes mnamo 2014 kuunda mwamko mpana wa kibunge kumuunga mkono wakala wa Uingereza Beji Essebsi, lakini chama chake hakikuendelea na nguvu zake kikavunjika. Kwa kuchunguza msimamo wa Uingereza, inakuwa wazi kuwa matukio nchini Tunisia yameishtua.

Gazeti la Uingereza la The Guardian lilichapisha, kulingana na Al Jazeera Net, mnamo tarehe 27/7/2021, nakala iliyoitwa "Maoni ya Guardian juu ya mapinduzi nchini Tunisia: Masika kugeuka kuwa kipupwe" na ikasema kwamba Tunisia inashuhudia mapinduzi ya mageuzi, ikizingatiwa kwamba, ("Vikosi vya usalama kuvamia vituo vya televisheni sio ishara nzuri kabisa" na akasema kwamba "raia kufanya matendo bila kujali na kukubali dhana zisizo za kawaida kwa sababu uhuru na demokrasia haikufanikisha utulivu wa kisiasa na uchumi ulioendelea. Badala yake, ufisadi, mfumko wa bei na ukosefu wa ajira uliendelea , theluthi moja ya familia nchini Tunisia zilihofia kwamba ziliishiwa na chakula mwaka jana baada ya kuzuka kwa janga la virusi vya Korona, na kwamba serikali, kulingana na nyaraka zilizovuja, ilikuwa tayari kufuta ruzuku ya mkate katika mazungumzo ya mkopo wa dolari bilioni 4 kutoka kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF), ambao ni wa nne katika miaka 10, na chuki dhidi ya serikali katika kushughulikia janga hilo ilizidi kuwa mbaya kutokana na kiwango cha deni la kitaifa, ambapo ulipaji mkopo sasa umekuwa mara sita ya bajeti ya afya ya nchi kwa ukubwa zaidi.” Hivyo, utawala ulikuwa chini ya shinikizo la Amerika kupitia Mfuko wa Fedha wa Kimataifa. Amerika inafanya kazi kuimarisha uwepo wake nchini Tunisia kupitia shinikizo hizi. ”).

Kwa haya yote, ni wazi kwamba ushawishi wa Uingereza nchini Tunisia umepungua, na kwa hali zinazoendelea kuudhoofisha, Ufaransa imepata mlango wa kuingia kwa nguvu Tunisia. Uingereza ilidhani kuwa ushawishi wa Ufaransa haukuwa hatari kwa sababu imekuwa ikiratibu Ufaransa, haswa dhidi ya ushawishi wa Amerika, nchi hizi mbili zilikubaliana juu ya hili. Lakini, swala la Brexit limesababisha mpasuko mkubwa kati yao, na hakuna hata mmoja wao aliyefanya juhudi yoyote kuukarabati. Kwa kweli, nchi kadhaa za Jumuiya ya Ulaya, hasa Ujerumani, zimekuwa na msimamo sawa na ule wa Ufaransa, kwani hawakuelezea kile kilichotokea Tunisia kama mapinduzi kama vyombo vya habari vya Uingereza, (Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani Maria Adebahr alisema leo, Jumatatu, kwamba Berlin ina wasiwasi juu ya kuongezeka kwa machafuko ya kisiasa nchini Tunisia na inataka nchi hiyo irudishwe katika hali ya sheria ya kikatiba, hata hivyo, inaamini kuwa kile kilichotokea sio "mapinduzi" ...) (Sputnik, 7/26/2021).

c-Ufaransa: Kuhusu msimamo wa Ufaransa, ndio wa kushangaza zaidi:

- Rais mpya, Kais Saied, alikuwa mpingaji mkuu wa wakoloni, na mapendekezo yake ya mapinduzi yalikubaliwa kwa Watunisia ambao walimchagua kwa matumaini ya kuondoa walinzi wa zamani ambao walikuwa wakiongoza serikali katika kipindi cha baada ya mapinduzi kwa njia moja au nyingine. Wakati Rais Saied alipoingia madarakani mnamo Novemba 2019, rais huyo wa Tunisia alijitegemea, mwanzoni, lakini kwa kuwa mawazo yake na silika yake ilikuwa imewekwa kwa sababu ya kutegemea nguvu ya kimataifa, alipata mikono ya Ufaransa ikiwa wazi kwake na Ufaransa iliota kurudi Tunisia kama mwanachama hai wa mfumo wake wa Francophone. Miongoni mwa ushahidi kwamba Ufaransa imefanikiwa kumfanya Kais Saied kuwa wakala wake ni huu ufuatao:

- Pamoja na bunge la Tunisia kugawanywa katika sehemu mbili; wafuasi wa Rais Kais Saied, na wale ambao wanampinga, ambao ni sehemu kubwa zaidi. Muungano wa Heshima (Karama) uliungana na harakati ya Ennahda ndani ya sehemu ya bunge dhidi ya Rais Kais Saied na uadui zaidi kwa Ufaransa ndani ya Bunge la Tunisia umeanza kufanya kazi ya kuvuruga uhusiano wa Ufaransa na Tunisia, kwa hivyo ilipendekeza wazo la "Ufaransa kuomba msamaha" kwa ukoloni wake wa Tunisia kwa kura ya bunge, na hii haikuibuliwa wakati wa urais wa Essebsi au Marzouki, ambayo inaonyesha kwamba wapinzani wa Rais Saied wanataka kumuaibisha rais na kuiaibisha Ufaransa katika uhusiano wake na Tunisia, na kukumbusha uadui wa kikoloni. Lakini rais wa Tunisia amechukua msimamo ambao yuko karibu kutetea Ufaransa kinyume na kampeni zake za Uchaguzi, Saied alisema: ("Anayeomba msamaha anajihukumu mwenyewe," na kuongeza, "Wacha tuangalie siku za usoni." Ufaransa ilitenda uhalifu nchini Tunisia, lakini chini ya mfumo wa ulinzi, sio ukoloni wa moja kwa moja, kama ilivyo kwa Algeria. Aliongeza kuwa Watunisia walilipa sana gharama ya uhuru wao na wanastahili kuombwa msamaha, lakini kutangaza msamaha haitoshi. Aliendelea, "Labda kuombwa msamaha pamoja na miradi na pengine ushirikiano mpya," ikizingatiwa kwamba orodha ya msamaha haikukosa hatia, na la kushangaza, "Kwa nini baada ya miaka 60 tunaomba kuombwa msamaha?" (Tovuti ya UltraTunisia, 23/6/2020).

- "Mnamo Juni 2020, Saied alichagua Ufaransa kama mashukio yake ya kwanza barani Ulaya baada ya kuchukua majukumu yake, na hivyo kuimarisha uthabiti wa uhusiano na Paris." (Anatolia, 4/6/2021), na kabla ya ziara ya Rais wa Tunisia jijini Paris na karibu yake, Maafisa wakuu wa Ufaransa walimiminika Tunisia katika kile kinachoonyesha uhusiano maalum baada ya Kais Saied kuchukua madaraka (kwa upande huu, mwaliko wa rais kwenda Ufaransa unaweza kuwa utangulizi wa miradi ya ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizi mbili, hasa wakati ziara hii ilitangulia ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa kwenda Tunisia mnamo Mei 2020 na kabla ya hapo ziara ya Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu la Ufaransa, hakukuwa na uvujaji wa habari yoyote juu ya yaliyomo katika ziara hizo mbili isipokuwa taarifa za kawaida juu ya maswala ya maslahi ya kawaida (Al -Jazeera, 18/6/2020).

- Ufaransa iliendelea kutuma maafisa wake wakuu kwenda Tunisia kila wakati migogoro nchini Tunisia ilipo ongezeka na hitaji la kuiunga mkono Ufaransa lilipo ongezeka pamoja nayo (Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex aliwasili nchini Tunisia mnamo Jumatano jioni kwenye ziara akifuatana na mawaziri sita na itaendelea hadi Alhamisi, ikiwa na lengo la kuimarisha uhusiano na nchi hiyo ya Kiafrika, ambayo inashuhudia shida kadhaa na kukumbwa na janga la virusi vya Korona… mazungumzo hayo yatashughulikia faili za "ushirikiano wa kiuchumi", "msaada" na "shida ya kiafya", na ziara hiyo itajumuisha kutiwa saini kwa makubaliano, ziara ya semina ya kujenga mtandao wa treni za mwendo kasi nchini Tunisia, na mkutano kwenye uwanja wa kidijitali ulioandaliwa na wafanyabiashara wa Tunisia na Ufaransa. (Ufaransa 24, 2/6/2021).

- Rais wa Tunisia alishiriki Mkutano wa Kiuchumi wa Afrika ulioandaliwa na Ufaransa jijini Paris (Russian Sputnik, 22/5/2021) na hakutangaza matokeo yoyote ya nje kwa Tunisia, isipokuwa kwa ahadi ya chanjo za Korona, na hii inaonyesha kuwa ziara hiyo ilikuwa na lengo la kujadili hali ya ndani ya Tunisia na Rais Macron, ambapo Saied alizungumza kwa muda mrefu juu ya hali ya ndani nchini Tunisia katika vyombo vya habari vya Ufaransa. Labda ziara hiyo ilikuwa kujibu ziara ya Ghannouchi jijini Qatar, ambayo aliiita "diplomasia ya bunge", ikimaanisha kuwa kila mmoja wao anaimarishwa na mabwana zake na mawakala wenza.

- Ufaransa iliahidi euro bilioni 1.7 kusaidia Tunisia kwa njia ya misaada na mikopo hadi 2022, kufadhili miradi katika sekta ya afya na kuunda fursa za kazi. Rais wa Ufaransa Macron alitangaza mkopo wa euro milioni 350 wakati wa ziara ya Rais wa Tunisia Kais Saied jijini Paris katikati ya mwaka wa 2020 ... (The New Arab, 2/11/2020).

- Idhaa ya Al-Jazeera iliripoti tarehe 28/7/2021, katika taarifa rasmi iliyo wazi iliyotolewa na Ufaransa, kile Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Le Drian alichosema: "Ufaransa inafuatilia yanayojiri nchini Tunisia kwa hamu kubwa zaidi." Alinukuliwa na RT mnamo 28/7/2021: (na kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa, katika taarifa iliyotolewa mnamo Jumatano, kwamba Le Drian alizungumza kwa simu leo ​​na mwenzake wa Tunisia, Othman Al-Jarandi. Le Drian alisisitiza, kulingana na taarifa hiyo, "umuhimu wa kuteua, haraka iwezekanavyo, Waziri Wakuu, na kuunda serikali ambayo inaweza kukidhi matakwa ya watu wa Tunisia kwa kuzingatia mgogoro unaopitia nchi hiyo."

Kwa kumalizia: Dalili zote za mzozo mkali wa kimataifa nchini Tunisia zinaonyesha kuwa ni mzozo kati ya Uingereza, ilio na ushawishi wa zamani na mkubwa nchini Tunisia, na Ufaransa, ushawishi mpya na usio na msimamo ndani yake, na kwamba Amerika bado iko mbali na kituo kikuu katika mzozo huu, licha ya kwamba Ufaransa na mawakala wake wanataka kuimarishwa na Amerika na mawakala wake katika eneo hilo, dhidi ya mawakala wa Uingereza nchini Tunisia. Kwa hivyo, inasukuma mawakala wake nchini Tunisia kwa wakala wa Amerika nchini Misri, lakini ushawishi wa Misri nchini Tunisia ni kidogo sana kuliko ushawishi wa mawakala wa Uingereza nchini Algeria, ambayo iko karibu moja kwa moja na Tunisia. Rais wa Algeria aligusia Tunisia na uhusiano wake na Ufaransa aliposema: (Tebboune alisema kuwa Ufaransa inaichukua Algeria kwa uzito, akielekeza maneno yake kwa mwandishi wa habari, ambaye alimwuliza ikiwa Ufaransa bado inaiona Algeria kama mkoa wa Ufaransa, akisahihisha hili kwa kusema, "Hapana, hapana” Na akaendelea: "Unamaanisha nchi nyingine ambayo wanaipa maagizo, na kukaa kimya juu ya hilo na kuyatekeleza." Wengine walielewa kuwa maneno ya rais wa Algeria yanakusudia Tunisia, hasa baada ya matamko ya Rais wa Jamhuri, Kais Saied, wakati wa ziara yake nchini       Ufaransa, ambapo alisema kuwa Tunisia haikuwa chini ya ukoloni lakini ilikuwa chini ya ulinzi ... (Tovuti ya El-Hosary, 8/7/2021).

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu