Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali

Gumzo za Kisiasa

[Majibu ya maswali yaliyopokelewa kutoka kwa baadhi ya wanachama]

(Imetafsiriwa)

1- Muulizaji anauliza: Je, inawezekana kuhitimisha makubaliano kama makubaliano ya Kennedy na Khrushchev mnamo 1961, ambayo Amerika inahitimisha moja na China? Je, tunaweza kusema hivi? Hasa kwa vile China kama nchi yenye nguvu ya kiuchumi duniani imekuwa tishio namba moja kwa nguvu za Marekani? Pia, tishio la Amerika kwa China huko Taiwan lina uhusiano gani na hilo?

Jibu: Kuhitimisha makubaliano kama haya haiwezekani. Badala yake, Amerika inajitahidi kuihusisha China katika vita na Taiwan ili iweze kuidhibiti na kuifanya iwe chini ya utashi wake. Pamoja na kuizuia kuiunga mkono Urusi nchini Ukraine. Inatekeleza vitendo vinavyoikasirisha China na inaunda ushirikiano kuizunguka ili kufanya kazi dhidi yake na kuiwekea vikwazo. Ilianzisha vita vya kiuchumi dhidi yake, na kwa hivyo inaonekana kwamba itaendelea na hatua hizi hadi suala la Taiwan litakapomalizika, kwa sababu China inasisitiza kushikilia Taiwan hata kwa nguvu, kama ilivyosemwa na  rais wake, Xi Jinping, ambaye amepata urais upya wa tatu kwa muda wa miaka mitano; alisema: "China inahifadhi haki ya kutumia nguvu juu ya Taiwan kama njia ya mwisho katika hali ya kulazimisha," (Al-Jazeera 16/10/2022). China inaangalia kile kinachotokea nchini Ukraine na jinsi mambo yatakavyoendelea, ili janga hilo lisijirudie ndani yake ikiwa Urusi itashindwa vibaya huko Ukraine. Tuliona kwamba imejizuia kuiunga mkono Urusi nchini Ukraine, bali ilijiondoa baada ya awali kutangaza uungaji mkono wa Urusi kwa ukamilifu na kutia saini makubaliano nayo katika suala hili na kisha ikachukua msimamo wa kutoegemea upande wowote. Msimamo huu uliidhuru Urusi, ambayo Putin aliitaja kuwa na msimamo sawia, akieleza kuelewa msimamo wa China ili asiupoteze iwapo angeikemea au kuikosoa. Kwa hivyo, inawezekana kwamba Amerika haitahitimisha makubaliano ya kimataifa ya ushirikiano kama ilivyofanya na Muungano wa Kisovieti wa zamani hadi itakapomaliza vitendo vyote hivi. Pia, haitahitimisha makubaliano nayo ya kuanzisha eneo la ushawishi katika Bahari ya Kusini na Mashariki ya China, kwa kuwa inahamasisha nchi dhidi yake na inajitahidi kuizuia kudhibiti maeneo haya mawili.

2- Muulizaji anasema: (Urusi ingeweza kujibu “mithili ya mgogoro wa makombora wa Cuba” kwa kutishia Marekani kwa ukaribu nayo, kama ilivyokuwa Muungano wa Sovieti... kwa nini haikufanya hivyo?)

Jibu: Kauli hii haina uhalisia kwa Urusi, ambayo inahisi na kutambua kwamba Amerika ina nguvu kuishinda. Hii ni tofauti na Muungano wa Kisovieti, ambao mamlaka yake yalikuwa sambamba na yale ya Marekani. Ili kuzama zaidi katika maana hizi, nguvu za nyuklia za nchi zote mbili leo ni sawa, lakini Amerika ina ngao ya kombora ambayo inailinda kutoka kwa makombora ya Urusi, Urusi haina ngao kama hiyo. Kile ambacho Urusi imetangaza kutengeneza makombora mapya yenye uwezo wa kupita ngao ya kombora bado kiko katika hatua zake za awali, ikimaanisha kuwa idadi ya makombora ya nyuklia ya Urusi ambayo yanaweza kufika katika ardhi ya Marekani na kupita ngao ya kombora ni chache zinazofanya kazi kikamilifu, na kinyume chake, makombora yote ya zamani ya Amerika yaliyowekwa kufikia ardhi ya Urusi bado yanaweza kufanya hivyo.

Hii ni pamoja na maendeleo makubwa katika silaha za kawaida za Marekani kama vile ndege zisizo na rubani, ndege za siri na makombora mahiri ambayo Urusi haina mwenzake wa kulinganishwa nayo, kwani vita vya Ukraine vilithibitisha kuwa jeshi la anga la Urusi ni dhaifu na haliwezi hata kudhibiti anga ya nchi kama Ukraine, na droni zake ziko nyuma. Ripoti zinazungumzia matumizi yao ya droni za Iran katika vita vya Ukraine. Mbali na udhaifu mwingine mkubwa wa majeshi ya Urusi ya kawaida, ambao vita vya Ukraine vimeweka wazi, na kuweka wazi udanganyifu wake wa ukuu. Ni dola gani kuu ambayo haiwezi, kwa takriban miezi minane, kuishinda nchi ndogo kama Ukraine, hata ikiwa inapokea msaada wa Magharibi? Ni ukuu gani kwa Urusi, ambayo iliharakisha kujiondoa karibu na mji mkuu Kiev mwanzoni mwa vita, kabla ya msaada wa Magharibi kwa Ukraine kuongezeka?! Hiyo ni, wakati Ukraine ilikuwa na nguvu ndogo! Kwa hivyo, kama nilivyo sema hapo awali; msemo huu (kwamba Urusi inaweza kujibu "mithili ya mgogoro wa makombora wa Cuba" kwa kutishia Marekani kwa ukaribu sana) hauwezekani, kwa sababu Urusi leo si kama Muungano wa Kisovyeti katika siku hizo wakati mgogoro wa makombora wa Cuba ulipotokea.

3- Ama kuhusu suala la ushirikiano wa kimataifa lililotajwa katika swali, ina maana kwa Wamarekani kwamba nchi kubwa hutumikia maslahi ya Marekani kwa malipo ya makubaliano ya Marekani ya kuipatia kitu kutokana na ngawira za kimataifa ambazo Amerika inaamua. Kwa mfano, Urusi ilikubali kutumikia maslahi ya Amerika nchini Syria, kwa hivyo ilifanya uvamizi wake wa kijeshi mnamo 2015, na Urusi ikaibuka kuwa nchi kubwa na sifa ya "veto" ya Urusi katika Baraza la Usalama ikajulikana, hii ni ngawira ya kimataifa isiyofaa kudharauliwa. Amerika ilitaka kuhamisha huduma za Urusi hadi Amerika kwenye bonde la China dhidi ya Korea Kaskazini na dhidi ya China. Walakini, Urusi ilikataa, na wakati Amerika ilikuwa na uhakika wa kukataa kwa Urusi, Amerika ilianza kupunguza dori ya Urusi, ambayo ilionekana kuwa na nguvu nchini Syria, na kuiudhi katika maswala mengi kama vile vita vya Azerbaijan na Armenia na mengine mengi.

Haya ni mawazo ya Marekani, kwani Washington haifikirii kugawanya ushawishi na mtu yeyote, bali inafikiria kushirikisha nchi nyingine ambazo zinaitwa nchi kubwa ili kusaidia kufikia maslahi ya Marekani duniani kote kwa malipo ya baadhi ya ngawira za kimataifa ambazo Marekani inakubali kuipa nchi hii au ile. Huu ni mstari wa kufikiri wa Marekani na China, na Urusi na nchi za Ulaya. Leo, hii ni pamoja na upanuzi wa Amerika wa dori ya Ujerumani katika Ulaya mashariki mbele ya Urusi, lakini yote haya ni chini ya usimamizi na mipango ya uongozi wa Amerika. Na kama Ujerumani itaamua kujiondoa katika uongozi wa Marekani na kutoka katika mipango yake na kutenda peke yake, basi Marekani itaisumbua. Hii ndio mantiki inayotawala fikra za Wamarekani.

4-Kuhusu kauli katika swali, "Kwa nini Marekani haikuiwekea India vikwazo ilipokubali kuagiza mafuta kutoka Urusi?"

Jibu kwa hili ni kwamba Amerika haikuiwekea India vikwazo kwa sababu hii inatishia hatima ya vibaraka wake nchini India wakiongozwa na Modi na Chama chake cha Bharatiya Janata. Kwa hivyo, haikupinga ununuzi wake wa gesi na mafuta kutoka Urusi kwa sababu haikuweza kuipatia njia mbadala. Ikiwa India itasimamisha ununuzi wake wa rasilimali za nishati kutoka Urusi, kama ilivyotokea Ujerumani, bei ingeongezeka maradufu nchini India, ambayo watu wa India hawawezi kumudu. Ingeathiri serikali inayounga mkono Marekani ya Modi, na hivyo kuishusha, fursa inayosubiriwa na vibaraka wa Uingereza wenye nguvu bado wa chama cha Indian Congress nchini India. Hata pia inairuhusu kuendelea kununua silaha kutoka Urusi, kama ilivyozoeleka tangu enzi za chama cha Congress, kilichotawala India kwa muda mwingi tangu kuanzishwa kwake 1947 hadi 1998. Chama cha Bharatiya Janata (BJP) kilikuja kwa mara ya kwanza na kutawala hadi 2004, na kisha chama cha Congress kilirudi kutawala India hadi 2014. Baada ya hapo, BJP iliregea madarakani hadi leo, na mafanikio yake yalitokana na makubaliano na watawala vibaraka wa Pakistan.

Kisha Amerika ikawaamuru, haswa huko Kashmir, ambayo iliongeza umaarufu wa chama hiki. Ndio maana India iliponunua makombora ya S-400 kutoka Urusi, Amerika haikuiwekea vikwazo kama ilivyoiwekea Uturuki. Badala yake, iliiondoa India dhidi ya vikwazo ndani ya mfumo wa kupambana na maadui wa Amerika kupitia Sheria ya Vikwazo, inayojulikana kwa kifupi CAATSA, ambapo Baraza la Wawakilishi la Marekani liliidhinisha msamaha huo kama sehemu ya idhini yake ya bajeti ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani kwa mwaka  wa 2023 mnamo 14/7/2022, wakidai kwamba "kuondolewa kwa vikwazo kutaimarisha uhusiano wa ulinzi kati ya Amerika na India" (Anatolia 16/7/2022). Hiki kilionekana kuwa ni kiwango cha unafiki kama kiliwekwa kwa Uturuki kwa madhumuni haya ndani ya mfumo wa sheria hii wakati hakikuwekwa kwa India, ambayo inaonyesha kwamba Amerika inaogopa kupoteza ushawishi wake nchini India na kuanguka kwa vibaraka wake katika Chama cha Bharatiya Janata ikiwa vikwazo kama hivyo vitawekwa juu yake na kuzuia kununua rasilimali za nishati kutoka Urusi. Ingawa hii haimuathiri Erdogan na serikali yake, ambayo inazunguka katika mzunguko wake, lakini inaongeza umaarufu wake na kufinika uhusiano wake na Amerika.

5- Kuhusu hoja nyingine zilizotajwa katika maswali kuhusu mafuta na gesi, majibu ni kama ifuatavyo:

a- Ulaya ni mwathiriwa namba moja / kuhuzunishwa na kukatizwa kwa silsila za usambazaji wa kawi ya Urusi, kwa sababu Ulaya inaona hatari ya upanuzi wa Urusi karibu nayo, kwa hivyo inataka, kwa makubaliano na Amerika, kuwa na uwezo zaidi wa kukabiliana na Urusi wakati sio tegemezi kwa gesi na mafuta yake, na iko tayari kubeba matokeo. Kwa hivyo, haisemwi kwamba Amerika inaelekeza Ulaya kuondoa utegemezi wa kawi ya Urusi, ingawa mwelekeo huu wa Amerika ni mkakati wa zamani wa Amerika tena. Badala yake, inaweza kusemwa kwamba Amerika ilifanikiwa kwa kuimarisha misimamo ya Ukraine, kuiunga mkono na kuiburuta kuelekea Magharibi kwa kuihusisha Urusi nchini Ukraine, yaani, imefanikiwa kwa miongo kadhaa ya kuingilia Ukraine kwa kuisukuma Urusi kwenye kona hii ambayo inaweza kueleweka tu kama tishio kwa Ulaya nzima. Wakati tishio la Urusi kwa Ulaya lilipotokea na halisi, nchi za Ulaya ziliambatana kwa hiari na mkakati wa Amerika na kisha kukata rasilimali za kawi ya Urusi kutoka Ulaya. Hii ilifuatiwa na kupanda kwa bei ya gesi asilia kwani ndiyo gesi iliyokuja kwa njia ya mabomba mengi na sio kupitia meli za majini zinazosafirisha gesi majimaji, hivyo bei yake ilikuwa nafuu. Wakati mabomba hayo "yalipokatwa", ikawa muhimu kwao kuagiza zaidi kupitia meli za baharini, na hii ni ghali kwa sababu ya viwanda vya kuyeyusha gesi katika nchi zinazouza nje na kisha kuirudisha katika hali ya gesi katika nchi zinazoagiza barani Ulaya.

b-Kuhusu mafuta, bei yake ilipanda duniani kote, si tu Ulaya, tofauti na gesi. Amerika pia iliathiriwa na kupanda kwa bei ya mafuta, na hiyo inaweza kusemwa kuhusu vyanzo vya nafaka, za Urusi na Ukraine, ambazo zilivurugwa, ikimaanisha kuwa kupanda kwa bei ya nafaka pia kulikuwa duniani kote na sio Ulaya pekee. Barani Ulaya, kama ilivyo katika mataifa mengine, suala la uhaba wa nafaka na mafuta ni suala la bei ya juu kutokana na uwezekano wa kusafirisha kutoka sehemu tofauti na Urusi na Ukraine. Kuhusu gesi asilia sio sawa kwa sababu ya usasa wa tasnia ya uyeyushaji wa gesi na uhaba wa meli za gesi, pia ilochangia hili ni kuongezeka kwa utegemezi wa ulimwengu wa gesi asilia kwa sababu ambazo zimekuzwa kwa miongo kadhaa kuhusiana na mazingira na tabianchi, yaani, haina uchafuzi wa mazingira na hatari ndogo kuliko nyinginezo kama vile makaa ya mawe na nishati ya nyuklia.

c- Kuhusu Amerika inayoota kupanga kwa bei ya gesi asilia kimataifa kwa dolari, hii ni hakika, lakini kuna vizuizi vikubwa. Urusi inakubaliana na China na nchi nyingine juu ya kubadilishana biashara katika sarafu za ndani, na hii ni mbinu ya Urusi ambayo imepata njia yake tangu 2014. Nchi nyingi zimekuwa zikifikiria sawa tangu mgogoro wa kifedha wa 2009, wakati nchi za dunia ziligundua utegemezi wao mkubwa kwa dolari ya Marekani. Inaweza kusemwa kuwa mbinu ya kubadilishana biashara isiyo ya dolari kwa kweli imefungua njia yake duniani, ingawa bado ina kikomo. Labda kwa viwango vya riba vilivyopandishwa vya Amerika na sera mpya dhabiti ya dolari ambayo ilipitisha mnamo 2022, inataka kuregesha imani katika dolari na kudhoofisha mbinu hiyo ya kubadilishana biashara katika sarafu zingine za ndani. Kwa muda mrefu, sera za tabianchi husababisha utegemezi zaidi wa gesi asilia kimataifa, na kuongezeka kwa umuhimu wa chanzo hiki cha kawi, na kwa hivyo suala la kuipangilia bei kwa dolari litakuwa na faida kubwa kwa Amerika.

d- Inaweza kuwa muhimu zaidi kuzingatia mafanikio ya juhudi za Amerika za kukata silsila za usambazaji wa gesi kati ya Urusi na Ulaya kupitia bomba kama vile laini za Nord Stream kama kukata njia za umeme ambazo hazidhibitiwi na Amerika, na hii inaonyesha kuwa Amerika haikufanya kazi kuishinikiza Uturuki kukata njia za gesi na Urusi kwa kuzingatia kuwa Uturuki ina uhusiano na Amerika. Rais Putin wa Urusi alitangaza nia ya kuanzisha kituo cha Uturuki cha kusambaza gesi ya Urusi kwa Ulaya, kumaanisha kwamba Marekani inataka biashara ya gesi ya Urusi kwenda Ulaya katika siku zijazo kupitia njia zinazodhibitiwa na Washington.

6 Rabii’ Al-Akhir 1444 H

31/10/2022 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu