Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali
Viwango vya Kampeni ya Haftar Kusini mwa Libya

(Imetafsiriwa)

Swali:

Kwa nini Haftar, kibaraka wa Amerika nchini Libya, anapeleka majeshi yake katika eneo kubwa mno la Libya kusini na wala hatulizii makini juhudi zake dhidi ya eneo tiifu kwa Uingereza la Libya magharibi na kuichukua Libya yote kwa manufaa yake? Ushawishi na uzito uko kaskazini na magharibi na mashariki, na wala sio kusini, au kuna malengo mengine ya kampeni yake eneo la kusini?

Jibu:

Tunatathmini yafuatayo ili kufafanua jibu hili:

Kwanza: Baada ya kibaraka wa Amerika, Haftar, kuichukua Benghazi, aliingia katika udhibiti wa Libya mashariki, na kupitia kutatua mzozo kwa manufaa yake katika mji wa Dernah katikati mwa 2018, Haftar alikazanisha kikamilifu mshiko wake juu ya Libya mashariki. Kupitia kugurisha vita hadi eneo la ukanda wa mafuta, ameongeza joto la mzozo nchini Libya kati ya vibaraka wa Amerika, wanao ongozwa na Haftar na vibaraka wa Uingereza wanao ongozwa na Al-Sarraj jijini Tripoli. Kupitia kuweza kupanua udhibiti wa ukanda wa mafuta, nguvu zake za kijeshi sasa zimetawala juu ya serikali ya Al-Sarraj.  

Lakini nguvu zake za kijeshi, anazo saidiwa na kibaraka wa Amerika, Sisi, sio zote ni muhimu katika kumwezesha kuichukua Libya magharibi, ambako nchi za Ulaya zenyewe zinamsukuma nje, vile vile kutoka karibu na eneo tiifu kwa Uingereza nchini Algeria. Hofu hii ya Algeria na kuingilia kati kwake iko wazi katika taarifa za Haftar: “Waziri wa Kigeni wa Libya Tahir Saila alipinga mnamo Jumatatu “taarifa za kizembe” za Jenerali Khalifa Haftar, ambazo kwazo ametishia “kugurisha vita vya Libya hadi Algeria kwa sekunde…” Haftar alitangaza mwanzoni kuwa Algeria “inapatiliza hali ya usalama nchini Libya” na kwamba “wanajeshi wa Algeria wamevuka mpaka wa Libya.” (France 24, 10/9/2018)   

Pili, uhalisia huu ni kwa sababu ya usaidizi wa Sisi wa Misri na nyuma yake Amerika kwa ajili ya Haftar, uliomsaidia kudhibiti Libya mashariki na eneo la ukanda wa mafuta. Uhalisia unaoafikiana una wakilishwa na serikali ya Al-Sarraj na kuwa tayari kwa Algeria kuihami kutokana na ukaribu wake wa kijografia, na Wazungu/ulaya wanaosimama nyuma yake. Uhakika huu na uhakika unaokinzana unaunda hali sare, ingawa mkono wa juu wa kijeshi unaegemea upande wa Haftar kwa sababu ya usaidizi mkubwa wa Amerika unaokubaliana na maono yake ya suluhisho nchini Libya; yaani, ufunguzi wa majadiliano baada ya hali ya Haftar kuwa muhimu au nusu muhimu. Lakini kwa mwangalio wa kitovu cha kisiasa, mizani ingali imeinama kwa manufaa ya Al-Sarraj. Ushawishi wa Ulaya unamdhamini yeye udhibiti wa Tripoli, mji mkuu, na uzito wa kitovu cha kisiasa cha Ulaya. Hivyo basi, Haftar hawezi kuendelea na kuuchukua mji mkuu huo na hawezi kufungua majadiliano ya makini pamoja na serikali ya Al-Sarraj ili aonekane kuwa pande sawa.  

Matatizo haya mawili ya pande hizo mbili za mgogoro nchini Libya yamesababisha hali ya kukwama ambayo hakuna upande wowote ulioweza kutatua. Hivyo basi, hatua ya kuelekea Libya kusini ilikuwa ni fursa kwa Haftar ili aweze kuongeza udhibiti wake wa kijeshi na kisha tatizo hilo litakuwa limetatulika kwa ushawishi mkubwa zaidi wa Amerika kuliko ule wa Ulaya. Na hivi ndivyo ilivyotokea: “majeshi ya Jenerali Khalifa Haftar yalianzisha oparesheni kubwa ya kijeshi kusini mwa nchi hiyo mnamo Jumatano ili “kuitakasa” kutokana na makundi ya kisilaha, ikiwemo chembe chembe za misimamo mikali za ISIS, na magenge ya wahalifu, kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Kitaifa la Libya.” (France 24, 17/1/2019). Chini ya vichwa vya habari “ugaidi na magenge ya uhalifu”, Amerika inamsukuma kibaraka wake Haftar kusini mwa Libya ili kupata malengo mengi ya kindani na kieneo ili kuimarisha ushawishi wake na kupunguza ushawishi wa nchi za Ulaya.         

Tatu, baada ya uchunguzi, inafichuka kuwa kampeni ya Haftar kusini mwa Libya imepata kwake yeye na ushawishi wa Amerika malengo mawili kuhusiana na mzozo ndani ya Libya, na Amerika pia ilipata malengo mawili mengine dhidi ya Ulaya na dhidi ya ushawishi wake barani Afrika, na maelezo yake ni kama ifuatavyo:

1- Malengo katika kiwango cha mzozo ndani ya Libya ni:

a- Udhibiti wa eneo kubwa, na endapo Haftar ataweza kupanua udhibiti wake wa kijeshi juu ya maeneo haya makubwa kusini mwa Libya, hii itampatia yeye mkono wa juu katika majadiliano vile vile. Kwa kuongezea umuhimu wa kindani wa kijeshi wa kudhibiti miji, kama vile Sabha na miji mingine ya kusini, itampa yeye “uhalali” kama upande unaoshikilia sehemu kubwa ya eneo la Libya, na athari za masuluhisho ya kisiasa, ingawa kuwa karibu na mpaka wa Algeria kusini ni tishio kwake, lakini huenda akalenga kumakinisha hilo huku Algeria ikishughulishwa na uchaguzi wa uraisi.

b- Udhibiti wa uchumi wa Libya; baada ya kwenda mbele na nyuma, majeshi ya Haftar yalikazanisha mashiko yake juu ya Ukanda wa Mafuta katikati ya mwaka wa 2018, na kugurisha mapato yake hadi tawi la Shirika la Kitaifa la Mafuta mjini Benghazi badala ya Tripoli, hivyo kuinyima serikali ya Sarraj Ukanda wa Mafuta upande mmoja, na Haftar alikuwa akijitayarisha kuyasafirisha kwa manufaa yake upande mwengine. Vita hivyo kisha vikaenda katika bandari za mafuta ili kumzuia Haftar kuyasafirisha. Wanamgambo wa Al-Jidran walidhibiti bandari za Sidra na Ras Lanuf, na serikali ya Sarraj jijini Tripoli inaichukulia Jidran kuwa mamlaka halali ya ulinzi wa vifaa vya mafuta. Lakini hili halikuthibitishwa na serikali ya Sarraj. “Kisha ghasia kali zilizuka pamoja na Majeshi ya Libya na hatimaye Kitengo Kikuu cha utoaji amri za kijeshi cha majeshi ya Libya kilitangaza mnamo Juni 21 udhibiti kamili wa eneo la Ras Lanuf na Sidra.” (Russian Sputnik, 7/7/2018).

Haftar alidhibiti Ukanda wa Mafuta ikiwemo bandari za usafirishaji. Kuanzia tarehe hiyo, juhudi za serikali ya Makubaliano inayoongozwa na Al-Sarraj zimekuwa na zinaendelea kuangazia juu ya kuzizuia nchi kutokana na uingizaji mafuta ya Libya kutoka eneo la mafuta linalodhibitiwa na majeshi ya Haftar. Nguvu ya usafirishaji ya Libya imepungua pakubwa. Serikali ya Sarraj imekuwa ikisafirisha mafuta yaliyo chimbwa katika Jangwa la Marzouk, hususan viwanja vya Ash-Sharara; mapipa elfu 300 kwa siku, na El-Feel mapipa elfu 125 … Kwa kugurishwa vita vyepesi hadi kusini, na kuyadhibiti majeshi ya Haftar juu ya kiwanja cha mafuta karibu na mji wa Sabha. “Msemaji wa majeshi Mashariki mwa Libya alisema mnamo Jumatatu katika mtandao wa Twitter: “Majeshi yamekamilisha udhibiti kamili wa kiwanja cha Ash-Sharara pamoja na asasi zake kuu kwa amani bila ya ghasia zozote na sasa yanakilinda kwa maelekezo ya Idara ya kiwanja hicho” (Al-Youm As-Sabi’ 11/2/2019)

Hii inaongezea katika ushawishi wa kiuchumi wa Haftar. Kiwanja hiki kikubwa cha mafuta, ambacho kingezalisha mapipa 400,000 kwa siku na kinamilikiwa na kampuni ya Uhispania, ndio mada ya mzozo mkubwa kati ya kibaraka wa Amerika Haftar na vibaraka wa Uingereza jijini Tripoli. Na kwa haya yanayojiri, yaani udhibiti wa Haftar, unaomruhusu kudhibiti kirahisi viwanja hivyo nyuma yake, hadi kusini ya mbali, hususan kiwanja cha El-Feel, serikali ya Sarraj ingepoteza mshipa wake wa kiuchumi na kutegemea mwavuli wa kimataifa wa Ulaya ili kumzuia Haftar kutokana na kusafirisha mafuta na kumlazimisha kuyasafirisha kupitia taasisi za mafuta za Tripoli. Lakini, anayadhibiti machimbuko na kuiacha kadhia ya usafirishaji kupitia bandari na mabomba ambayo hayadhibiti kwa majadiliano, ambayo kwayo anapata malengo yake ya kifedha ili aweze kuingiza pesa mishipani mwa majeshi yake.  

2- Malengo hayo mawili dhidi ya Ulaya na dhidi ya ushawishi wake barani Afrika ni:

a- Kuufanya uhamiaji kutoka Afrika kuwapasua kichwa Ulaya … Hili ni lengo la Amerika dhidi ya Ulaya; kuizuia kutokana na kuasisi kambi za kijeshi nchini Libya kwa kisingizo cha kukomesha uhamiaji wa Kiafrika hadi Ulaya. Udhibiti wa kibaraka wa Amerika, Haftar, wa asasi za kijeshi ndani zaidi ya Libya, ambazo nyingi yazo ni viwanja vya ndege na barabara za kurukia ndege ambazo anazizuia nchi za Ulaya kutokana na kuzitumia, ima kwa ajili ya ushawishi wao nchi Libya au kwa malengo ya kieneo barani Afrika. Kwa kutumia kisingizo cha kukomesha uhamiaji wa Kiafrika hadi Ulaya, nchi za Ulaya zinajenga ngome katika asasi hizo, ambayo inakataliwa na Amerika na kibaraka wake Haftar. “Jenerali Mstaafu wa Libya Khalifa Haftar ameonya kuhusu juhudi za pande za kimataifa za kuanzisha uwepo wa kijeshi katika baadhi ya maeneo kusini mwa Libya. Alisema hayo wakati ambapo Kitengo Kikuu kiko makini kuanzisha mahusiano mazuri na ushirikiano sambamba wa kimikakati kwa pande zote za kimataifa, kuna habari kuhusu matakwa ya baadhi ya pande za kimataifa kuanzisha uwepo wa kijeshi kusini mwa Libya … Duru kutoka Libya zimeripoti kuwa ujumbe wa usalama na kijeshi kutoka Italy umezuru mji wa Gatt (katika eneo la mbali la Kusini Magharibi mwa Libya) mnamo Alhamisi, kwa lengo la kuanzisha kambi ya kijeshi na kiraia ya Italy, kwa ufadhili wa Ulaya, ili kudhibiti uhamiaji haramu.” (Al-Jazeera Net, 29/6/2018).   

Kupitia udhibiti wa Haftar juu ya maeneo muhimu katika eneo la kusini, anawanyima Wazungu/ulaya kumakinisha na kuunda kambi za kijeshi kusini mwa Libya. “Chumba cha oparesheni za anga cha Kitengo Kikuu cha utoaji amri za kijeshi cha jeshi la Libya kimetangaza marufuku ya kutua na kuruka katika viwanja vya ndege na eneo la kusini isipokuwa kwa idhini yake, kikionya kutotua kwa ndege yoyote katika sehemu ya eneo hilo, endapo itaruka pasi na idhini kutoka kwa uongozi wa jeshi la Libya.” (Al-Youm As-Sabi’ 8/2/2019). Hivyo basi, Amerika kupitia kumsukuma Haftar kusini ingewazuia Wazungu/ulaya kutokana na kuingia kusini mwa Libya, na tatizo la uhamiaji wa Waafrika liwekwe kama kigongo kinachoumisha kichwa Ulaya.  

b- Hatua dhidi ya ushawishi wa Ulaya katika eneo la Sahara, malengo ya kampeni ya Haftar kusini mwa Libya hayakufungika na kupatikana kwa malengo hayo ya juu. Amerika inapanga, na inatabikisha kwa njia ya moja kwa moja, lengo la kieneo ili kudhoofisha ushawishi wa Ufaransa eneo hilo la Sahara. Nafasi iliyoko kusini mwa Libya imesababisha mazingira mwanana kwa amali ya kijeshi ya makundi ya upinzani ya Kiafrika eneo la kusini mwa Libya. Makundi ya upinzani ya Chad, Nigeria na Sudan yamekuwa na hata kuwa chembe chembe ya mizani ya nguvu za kindani nchini Libya, ambayo ni nguvu ya kuzingatiwa na sio ya kupuuzwa.     

“Gazeti la Chad, Unity kwa lugha ya Kifaransa lilisema mnamo Jumatano kuwa takriban chembe chembe 11,000 za upinzani wa Chad kwa sasa zimepelekwa kusini mwa Libya.” (Bawabat Al-Wasat, 4/4/2018). Na kwa kuwepo kisingizio cha “ugaidi”, ambacho kinatumiwa kwa uingiliaji kati wa Amerika, na kuelekeza vibaraka wake kudandia wimbi lake, Amerika inajitokeza hadharani kuingilia kati nchini Libya. “Afisa mmoja wa Libya alisema kuwa majeshi ya Amerika na Libya yalifanya mashambulizi ya pamoja katika eneo la katikati lililokuwa na idadi kadhaa ya wafuasi wa al-Qaeda pambizoni mwa mji wa Aubarey mnamo Jumatano.” (EURO News Arabic 14/01/2019). Kisingizio cha Amerika cha ugaidi ndicho kile kile kilichotumiwa na Haftar “ili kulisafisha eneo hilo kutokana na makundi ya kigaidi na kijeshi.”    

Nguvu za kijeshi eneo la kusini mwa Libya ni harakati za Chad. “Jeshi la Kitaifa la Libya likiongozwa na Afisa wa Kijeshi Khalifa Haftar, Januari iliyopita lilianzisha kampeni ya kijeshi kusini magharibi mwa nchi hiyo dhidi ya makundi makubwa zaidi pinzani ya kijeshi ya Chad.” (RT 12/2/2019) Jeshi la Kitaifa la Libya lilisema katika taarifa fupi iliyotangazwa na Haftar, kuwa “Ndege za kivita za jeshi la Kiarabu la Angani la Libya zililipua kwa zamu mijumuiko mitatu ya magenge ya Chad na washirika wao katika eneo letu tunalolipenda la Kusini” (Arabiya Net, 8/2/2019)

c- Ni wazi kutokana na hili kuwa kampeni ya Haftar eneo la kusini mwa Libya inatekeleza oparesheni ya ufurushaji wa makundi haya kutoka Libya, yaani kuyasukuma ng’ambo ili kuwa na misheni nyengine nchini Chad, ambayo ni kusababisha mzozo katika ushawishi wa Ufaransa, ambayo ilitokea mara moja na bila ya kuchelewa. “Waziri wa Kigeni wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian alisema mnamo Jumanne, vikosi vya Ufaransa vimeupiga bomu msafara wa waasi nchini Chad ili kuzuia mapinduzi dhidi ya Raisi Idriss Deby, na kumjibu Raisi Idriss Deby, ndege za kijeshi za Ufaransa ziliulipua msafara wa waasi wenye silaha uliokuwa ukivuka wiki iliyopita kutoka Libya na kupenya eneo la Chad. Le Drian aliwaambia wabunge: “Kundi moja la waasi kutoka kusini mwa Libya lilianzisha shambulizi … ili kuchukua utawala kwa nguvu jijini N'Djamena, Raisi Deby alituomba kwa maandishi kuingilia kati ili kuzuia mapinduzi na kulinda nchi yake.” (Reuters, 12/2/2019) Kwa kuwa hatari anazoleta kibaraka wa Amerika, Haftar, kwa Chad ni za kihakika, Ufaransa ilipeleka jeshi kubwa katika mji mkuu wa Chad ili kumhami kibaraka wake Idriss Deby. “Ufaransa inapeleka vikosi 4,500 katika mji mkuu wa Chad N'Djamena kama sehemu ya mchakato unaojulikana kama nguvu ya kupambana na ugaidi ya Burgan.” (Chanzo kilichotangulia)

d- Kutokana na yote haya, imegeuka kuwa Amerika na uingiliaji kati wake nchini Libya, na licha ya kukosa uwezo kwa kibaraka wake kutatua hali hiyo katika maeneo ya magharibi mwa Libya kwa manufaa yake kwa sababu ya usaidizi wa Ulaya kwa serikali ya Sarraj, Amerika imechukua hatua ya kudhoofisha ushawishi wa Ufaransa nchini Chad, na maendeleo ya wapinzani wa Idriss Deby ndani ya eneo la Chad kutoka upande wa kusini mwa Libya yaweza kuwa ni utangulizi wa kile kinacho kuja: mapigano nchini Chad, na pengine baada ya hapo, Niger dhidi ya ushawishi wa Ufaransa, na dhidi ya utawala wa kampuni za Kifaransa, hususan juu ya migodi ya uranium ndani ya eneo hilo.

Nne: Kwa kutamatisha, Haftar kwa usaidizi mkubwa wa kijeshi unaotolewa kwake na Amerika, hususan kupitia Misri, ameweza kuigawanya Libya katika sehemu mbili. Ameidhibiti kikamilifu sehemu ya mashariki, na kuudhibiti Ukanda wa Mafuta, kitovu cha uchumi wa Libya, na ameweza kupenya sehemu ya magharibi. Amerika inamuelekeza kusini ili kuendeleza zaidi udhibiti wake wa kijeshi na kiuchumi. Hivyo basi, yuko katika njia panda na hawezi kupenya magharibi mwa Libya, kwa sababu ya hofu ya Algeria na usaidizi mkubwa wa Ulaya kwa serikali ya Sarraj.

Amerika inamsukuma Haftar ili kupata malengo yake mengine, ambayo yanaongeza mzigo kwa nchi za Ulaya juu ya kadhia ya uhamiaji, na kushambulia kutoka upande mwengine ushawishi wa Ufaransa katika nchi jirani ikianza na Chad.

Hivi ndivyo viwango vya kampeni ya Haftar kusini mwa Libya, na ni wazi kuwa nchi za kikafiri zinaingilia mambo nchini Libya kwa ajili ya maslahi na ushawishi wao, na Waislamu ni makundi yanayopigana wenyewe kwa wenyewe, pasi na kujali lolote kuhusu utukufu wa Mwenyezi Mungu katika mauwaji ya ndugu zao na kuharibu mafuta ya nchi yao. Vibaraka hao na nyuma yao nchi za kikafiri hawataondolewa, wala uovu wauenezao katika ardhi ya Uislamu isipokuwa Waislamu wasimame kidete na kikweli kweli, na kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu na kutangaza Khilafah yao itakayo regesha mambo pale yanapostahiki, na kuyafanya matumaini ya makafiri katika biladi za Kiislamu kuwa jinamizi kwao.

 (إِنَّ فِي هَذَا لَبَلَاغاً لِقَوْمٍ عَابِدِينَ)

“Hakika, katika hii (Qur’an) yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada” [Al-Anbiya: 106]

15 Jumada II 1440 H
Jumatano, 20/2/2019 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 02 Aprili 2020 20:59

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu