Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Jibu la Swali

Matukio nchini Syria na Kuanguka kwa Utawala wa Assad
(Imetafsiriwa)

Swali:

Asharq Al-Awsat ilichapishwa mnamo tarehe 8 Disemba 2024: (Utawala wa Assad umeanguka: Upinzani wa Syria umetangaza leo, Jumapili, kwamba umeikomboa Damascus na kuupindua utawala wa miaka 24 wa Rais Bashar al-Assad. Taarifa ya upinzani kwenye televisheni ya taifa ilisomeka: “Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu, mji wa Damascus umekombolewa na dhalimu Bashar al-Assad amepinduliwa.” Upinzani uliongeza kuwa wafungwa wote wameachiliwa huru.)

Hay'at Tahrir al-Sham (HTS) ilikuwa ameanzisha mashambulizi kaskazini mwa Syria chini ya jina la “Kuzuia Uchokozi” mnamo tarehe 27/11/2024, na kufuatiwa na shambulizi la Jeshi la Kitaifa la Syria chini ya jina la “Alfajiri ya Uhuru” mnamo tarehe 30/11/2024. Aleppo ilichukuliwa, pamoja na udhibiti kamili wa maeneo yote ya Idlib, kisha Hama, Homs ... na leo Damascus ... na yote haya ni karibu siku kumi. Hivyo ni kipi kilicho nyuma ya yale yanayotokea Syria? Shukran

Jibu:

Ili kufafanua mambo, ukweli ufuatao lazima uzingatiwe:

Kwanza: Makundi yaliyoanzisha shambulizi hilo: Kulingana na BBC, 28/11/2024, makundi yaliyoshiriki katika shambulizi hilo ni “Chumba cha Operesheni za Al-Fath Al-Mubin,” ambacho kinaongozwa na Hay'at Tahrir Al-Sham. (HTS) na inajumuisha Upinzani wa Kitaifa wa Ukombozi (National Liberation Front) unaoungwa mkono na Uturuki, na kundi la Jaysh Al-Izza... pamoja na Jeshi la Kitaifa la Syria, ambalo linawakilisha muungano wa mirengo ya upinzani inayoungwa mkono na Uturuki na haihusiki katika Chumba cha Operesheni za Al-Fath Al-Mubin. Kwa hivyo, vikundi vingi vinavyoshiriki katika shambulizi hilo ni vikundi vilivyo na uhusiano na Uturuki na watiifu kwake, kwani Jeshi la Kitaifa ndio uundaji wake, na HTS iko chini ya macho na masikio ya Uturuki; maelewano kati ya shirika hilo na Uturuki ni ya kushangaza kwa mtu yeyote mwenye macho.

Pili: Hatua hizi, ambazo mwanzoni zilikuwa kama ujumbe wa kinidhamu kwa Bashar kwa sababu hakujibu maombi ya Erdogan, kama alivyomwomba Rais wa Urusi Putin: [kufanya kazi kuendeleza mazungumzo ya kuhalalisha mahusiano kati ya Ankara na Damascus na kwa Bashar kukubali mwaliko aliompa wa kukutana naye... (Reuters, 25/10/2024)], lakini Bashar hakujibu, badala yake aliomba kuondolewa kwa majeshi ya Uturuki na alikuwa ameweka masharti na kuahirisha. Lavrov, mpatanishi wa Urusi, alithibitisha hili na kuliambia gazeti la Uturuki la Hurriyet mnamo tarehe 1/11/2024 kwamba Bashar anaomba kuondolewa kwa vikosi vya Uturuki “...kwamba kikwazo kikuu kwa hili ni uwepo wa vikosi vya Uturuki kaskazini mwa Syria.” Erdogan alikasirika na kutoa idhini kwa shirika hilo na Jeshi la Kitaifa kuhama: “Vyanzo vya upinzani vilivyowasiliana na ujasusi wa Uturuki vilisema Uturuki ilikuwa imetoa idhini kwa kukerwa.” (AFP; Deutsche Welle, 30/11/2024).

Tatu: Ingawa vuguvugu hili mwanzoni lilikuwa ni la kukomboa maeneo yaliyoko karibu na Idlib, likisukumwa na Bashar kushindwa kujibu mapendekezo ya Uturuki ya kujadili suluhisho la kisiasa kati yake na upinzani, sekta kubwa za watu wanaoteseka kutokana na dhulma ya Bashar zilichukua fursa ya hilo na kutoka katika pande zote. Hawakuishia katika kile kilichopangwa awali katika maeneo ya kupunguza kasi ya Idlib, bali walikwenda zaidi ya hapo katika mikoa mbalimbali ya Syria. Kwa sababu jeshi la Syria pia lilikuwa likiteseka kutokana na dhulma ya Bashar na halikuwa na ukinaifu wa kumtetea, kwa hiyo, kujiondoa kwake kuliendelea. Kisha, sekta zinazotembea za watu zikaingia Aleppo, Hama, kisha Homs, na hatimaye mienendo ya watu wa Syria ikafika Damascus. Haya yote yametokea kwa kasi ndani ya siku kumi tangu harakati zianze tarehe 27/11/2024.

Nne: Misimamo ya pande za kikanda na kimataifa:

1- Ama Iran na Urusi: Zilishangazwa na yale yaliyokuwa yakitokea. Kwa hivyo, Urusi iliimarisha usalama katika Kambi ya Anga ya Hmeimim na Kambi ya Wanamaji ya Tartus, na nchi hizo mbili ziliwasiliana, “Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Araghchi alijadili maendeleo ya Syria na mwenzake wa Urusi Lavrov,” (Shirika la Anadolu, 30/11/2024).

Kufuatia shambulizi hili, Iran ilifanya harakati za kidiplomasia kulisimamisha na kutatua matatizo na Uturuki, hivyo Waziri wake wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi aliwasili Ankara mnamo tarehe 2/12/2024, na kukutana na mwenzake wa Uturuki Hakan Fidan; ambaye alizungumza na mwenzake wa Marekani Blinken na kusema: [“Mchakato wa kisiasa kati ya utawala na upinzani lazima ulete matokeo chanya kwa ajili ya amani na utulivu nchini Syria” (Shirika Anadolu, 1/12/2024)].

2- Ama kuhusu Uturuki: Ilitaka suluhisho la kisiasa na Bashar kupitia mazungumzo ya amani, kama ilivyofanya Marekani, lakini Bashar alifikiri kwamba angeweza kupata faida kwa kutojibu haraka, hivyo majibu yake kwa ofa ya Erdogan yalikawia, akifikiri kwamba hilo halingeikasirisha Marekani. Inaonekana kwamba Erdogan alikasirishwa na hili, kwa hiyo alichukua idhini ya Amerika kumfundisha Bashar somo, hivyo suluhisho la mazungumzo lingekuwa katika mazingira ya mapigano ambayo yalionekana kuwa ushindi kwa Erdogan dhidi ya Bashar. Kutokana na hayo, aliyasukuma makundi ya upinzani kushambulia, akiyaunga mkono kwa silaha muhimu na habari za kijasusi:

a- Mnamo tarehe 25/10/2024, Erdogan aliwaambia waandishi wa habari baada ya kukutana na Putin kando ya Mkutano wa BRICS huko Kazan kwamba yeye [“alimwomba Rais Putin wa Urusi kufanya kazi ya kuendeleza mazungumzo ya kusawazisha mahusiano kati ya Ankara na Damascus na ili Bashar kukubali mwaliko huo ilimwalika kukutana naye.” (Reuters 25/10/2024)].

b- Wapatanishi wa Urusi walimjibu Erdogan zaidi ya mara moja kwamba kuna masharti kwa Bashar al-Assad kukutana naye na kusawazisha mahusiano naye, ikiwa ni pamoja na kuondoa vikosi vya Uturuki kutoka Syria. Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, alilithibitishia gazeti la Uturuki, Hurriyet mnamo tarehe 1/11/2024 kwamba “Uturuki na Syria zinaonyesha nia ya dhati ya kuanzisha tena mazungumzo ili kusawazisha mahusiano, na kwamba kikwazo kikuu kwa hili ni uwepo wa Wanajeshi wa Uturuki kaskazini mwa Syria. Hii inaashiria ukaidi wa Bashar ambaye alitumia nafasi mbaya ya Erdogan juu ya usawazishaji mahusiano, na pia alitumia vibaya uungaji mkono wa nchi za Kiarabu kwake, kwa hivyo aliona kuwa Amerika ingali inamtaka kwa sababu haijapata badali yake!

c- Wakati serikali ya Uturuki ilipokata tamaa ya kupata suluhisho la mazungumzo pamoja na Bashar chini ya mazingira haya, ilipata kibali cha Amerika kwa suluhisho la mazungumzo kutekelezwa kwa utangulizi wa kijeshi kumshinikiza Bashar. Kwa hivyo, Erdogan alihamasisha makundi yaliyojihami tangu 27/11/2024. Hili linathibitishwa na ukweli kwamba utawala wa Uturuki ndio uliowaruhusu kuanza kushinikiza utawala wa Bashar, yaani kwa idhini kutoka Uturuki [“vyanzo vya upinzani vilivyowasiliana na ujasusi wa Uturuki vinasema kwamba Ankara ilitoa idhini kwa shambulizi hilo.” (Deutsche Welle, 30/11/2024)]; hii ilikuwa ni ili Bashar akubali kukaa na Erdogan, kurekebisha mahusiano na Uturuki, na kupatana na upinzani... kisha kufikia suluhisho la kisiasa kulingana na vipimo vya Marekani! Hiyo ni, “awamu mpya” kwa Syria, kama Erdogan alivyosema wakati wa maongezi ya simu na Katibu Mkuu wa UN Guterres, “Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan alisisitiza mnamo Alhamisi kwamba Syria inaingia katika awamu mpya ambayo inasimamiwa kwa utulivu.” (Arabi21, 5/12/2024).

3- Ama kuhusu Marekani: Haikushangazwa na mashambulizi ya wapinzani wa Syria. Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan alisema: “Haikuwa jambo la kushangaza kwamba wapiganaji wa upinzani wenye silaha walijaribu kuchukua fursa ya hali hiyo...” (Al-Arabiya ya Kiingereza; Al Jazeera Net, 1/12/2024), na haikuonyesha wasiwasi wowote, kama Al Jazeera Net ilivyoripoti mnamo tarehe 1/12/2024 kutoka Ikulu ya White House ikisema: “Tunafuatilia kwa karibu hali ya Syria na tumekuwa tukiwasiliana kwa muda wa saa 48 zilizopita na miji mikuu.” Msemaji wa Baraza la Usalama wa Kitaifa la Marekani Sean Savett alisema (Marekani, pamoja na washirika wake, wanahimiza kupunguzwa kasi ya ghasia, ulinzi wa raia na makundi ya walio wachache, na mchakato mzito na wa kuaminika wa kisiasa ambao unaweza kumaliza vita hivi vya wenyewe kwa wenyewe mara moja na milele kwa suluhisho la kisiasa linaloendana na UNSCR 2254.” (White House, 30/11/2024; RT, 1/12/2024).

Al Jazeera iliripoti kwenye tovuti yake mnamo tarehe 2/12/2024:

(Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitoa taarifa ikisema, “Kuongezeka kwa ghasia kwa sasa kunasisitiza tu hitaji la dharura la suluhisho la kisiasa linaloongozwa na Syria kwa mzozo, kulingana na UNSCR 2254.” ikiregelea azimio la UN la 2015 lililoidhinisha mchakato wa amani nchini Syria na ambalo halijatekelezwa hadi sasa. Linaeleza kuwa mazungumzo ya amani nchini Syria yanapaswa kuanza Januari 2016. Huku likisisitiza kuwa watu wa Syria ndio wanaoamua mustakabali wa nchi hiyo, lilitoa wito wa kuundwa kwa serikali ya mpito na kufanya uchaguzi chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, na kutaka kusitishwa mara moja kwa mashambulizi yoyote dhidi ya raia yaliyochapishwa kwenye tovuti yake mnamo tarehe 4/12/2024: (Blinken aliona kuwa jambo muhimu zaidi kwa sasa ni kusukuma mbele mchakato wa kisiasa unaozingatia azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, katika jaribio la kutatua na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria). Shirika la Habari la Khabar lilichapishwa kwenye tovuti yake mnamo 7/12/2024: (Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilisema: Tulimfahamisha Blinken kuhusu haja ya serikali ya Syria kufanya mazungumzo na upinzani).

4- Ama uhusu umbile la Kiyahudi: Euro News Arabia iliripoti mnamo tarehe 30/11/2024 yafuatayo: (Waziri Mkuu wa 'Israel' Benjamin Netanyahu, alijitokeza Jumanne iliyopita jioni kuwatangazia 'Waisraeli' kukubali kwake kusitisha mapigano na Hezbollah. Katika hotuba yake, Netanyahu hakusahau kumregelea Rais wa Syria, Bashar al-Assad, na kusema katika hotuba yake, “Assad anacheza na moto.” Saa chache baada ya hotuba hiyo, makundi ya Syria yalianzisha mashambulizi yaliyoratibiwa dhidi ya vikosi vya Assad kaskazini mwa Syria, ambayo yalizua maswali mengi kuhusu hali ya kaskazini mwa Syria, ambayo si ya kawaida kwa suala kama hilo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya 'Israel'). Kisha Al Jazeera Net ikaripoti mnamo tarehe 1/12/2024 kwamba gazeti la Yedioth Ahronoth lilisema: (Jeshi la 'Israel' liliizuia ndege ya Iran kutua Syria kwa tuhuma kwamba ilikuwa imebeba silaha kwa ajili ya Hezbollah ya Lebanon), kana kwamba ni umbile la Kiyahudi linataka kuizuia Iran kuregea kwa nguvu kwenye uwanja wa Syria kwa kisingizio cha kubeba silaha kwa ajili ya chama hicho nchini Lebanon, na kwa hivyo haitaki mwelekeo wa kijeshi kwa Iran au Chama cha Iran nchini Syria na Lebanon.

Tano: Kwa kuhitimisha, kwa kuzingatia yale tuliyoeleza hapo juu, ni kama ifuatavyo:

1- Upande uliodhibiti kuanza kwa mashambulizi kuelekea maeneo ya kupunguza kasi ya ghasia nchini Syria ni Uturuki na Amerika iko nyuma yake.

2- Wanataka kutokana na hili “kuanzisha mchakato wa kisiasa unaoaminika” ... “awamu mpya” ... ili kupanga utawala mpya nchini Syria, na ninarudia baadhi ya kauli za maafisa wa Marekani na Uturuki katika suala hili:

Msemaji wa Baraza la Usalama wa Kitaifa la Marekani, Sean Savett, alisema: [“Marekani, pamoja na washirika wake, wanahimiza kupunguzwa kasi ya ghasia, ulinzi wa raia na makundi ya walio wachache, na mchakato mzito na wa kuaminika wa kisiasa ambao unaweza kukomesha vita hivi vya wenyewe kwa wenyewe mara moja na kabisa na suluhisho la kisiasa linaloambatana na UNSCR 2254”. (White House, 30/11/2024; RT,1/12/2024)]. Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan alisisitiza, mnamo Alhamisi, kwamba Syria inaingia ‘awamu mpya’ ambayo inasimamiwa kwa utulivu. (Arabi21, 5/12/2024).

3- Ijapokuwa hawakufafanua walichomaanisha na suluhisho la kisiasa ambalo mashambulizi haya yangepelekea, uhalisia wa wingi wa vikosi vinavyopigana hivi sasa kwenye mipaka unaweza kuashiria kwamba kile ambacho Amerika na wafuasi wake wanapanga ni serikali ya muungano ya Syria kati ya majeshi haya ambayo yangeurithi utawala wa dhalimu ambao umeondolewa, na ambamo kungekuwa na majimbo yenye kujitawala wenyewe sawa na jimbo la Wakurdi linalojitawala wenyewe nchini Iraq.

4- Amerika, ambayo inadhibiti suluhisho hilo, itaruhusu maslahi ya Mayahudi kupatikana, kwani Amerika iliwahakikishia hilo katika makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Mayahudi na Lebanon alfajiri ya tarehe 27/11/2024, ambayo ni siku hiyo hiyo makabiliano ya kijeshi yalianza nchini Syria. Na kuizuia Iran isirudi kwa kasi ya kijeshi katika uwanja wa Syria kwa kuunga mkono chama chake nchini Lebanon, yaani kukata uhusiano wa kijeshi ulioko uwanjani kati ya Iran na chama chake nchini Lebanon.

Haya ndiyo mambo ambayo kauli za maafisa wa Marekani na Uturuki hapo juu zinaashiria kuanzisha mashambulizi nchini Syria.

Sita: Hatimaye, yale yaliyotokea na yanayoendelea nchini Syria leo, kutokana na umwagaji damu, majumba kuharibiwa, na familia kuhamishwa, ni jambo la uchungu, hasa kwa vile ni kutafuta suluhisho la kisiasa na awamu mpya ambayo haiko mbali na mifumo ya kiraia ya kisekula iliyoko katika nchi za Waislamu baada ya wakoloni makafiri na vibaraka wao kuweza kuondosha mfumo wa utawala katika Uislamu (Khilafah) miaka mia moja iliyopita... na kisha mataifa yakakusanyika dhidi yetu mithili ya wanyama wanaowinda mawindo yao, Ummah utaregea, ukiwa na heshima na utukufu kama ulivyokuwa, na Khilafah Rashida itaregeshwa tena, Mwenyezi Mungu akipenda. Lakini sheria ya Mwenyezi Mungu inataka kwamba Malaika wasitushukie kutoka mbinguni kutusimamishia Khilafah huku tukiwa sisi tumekaa, badala yake inapaswa kusimamishwa kwa mikono ya watu wanaomuamini Mola wao ambaye Yeye (swt) amewazidishia uongofu. Hatuwakosi watu wa aina hiyo wawe jeshini au upinzani, hata kama ni wachache, hasa kwa vile mfuatiliaji wa matukio yaliyoanza siku kumi zilizopita, anaona wanaopinga utawala huo si wale pekee walioanzisha makabiliano haya na serikali, kama wafuasi wa Uturuki na nyuma yake Amerika, kufikia mabadiliko ya kisekula kwa kuihamisha kutoka bega hadi bega ... lakini pia wengine walijiunga katika makabiliano, waliunguzwa na dhulma ya utawala huo na kutaka kuubadilisha ili kutimiza matamanio ya Waislamu wa Syria.

Kwao tunawahutubia wito: kufanya kila wawezalo kuzuia masuluhisho potovu ya kisiasa ya kisekula ambayo wakoloni makafiri na vibaraka wao wanayataka. Na kutoruhusu mihanga yao katika matukio haya kupotea bure na kuwa athari iliyosahaulika! Na kuwaunga mkono wale wanaofanya kazi ya kusimamisha utawala wa Uislamu, Khilafah Rashida, ili wapate malipo makubwa na ushindi mkubwa. Na kisha wao watakuwa miongoni mwa wanaostahiki bishara njema:

نَصْرٌ مِنَ اللهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ “…nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!” [As-Saf: 13].

6 Jumada Al-Akhir 1446 H

8/12/2024 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu