Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vitisho vya Usalama na Amani ya Kudumu

Pamoja na mivutano yote inayozunguka kung'atuliwa kwa Trump na kuapishwa kwa Biden kama rais mpya wa Amerika, haipaswi kupotea kwa mujtamaa, kwa jamii za kikabila na haswa, jamii yetu tishio la usalama linalosababishwa na wazalendo weupe wa mrengo wa kulia.

Matangazo yametolewa na afisi za eneo za FBI kuwashauri Waislamu kuwa macho juu ya vitisho na mashambulizi yoyote yanayoweza kutokea kwa Misikiti yetu. Kusudi la ujumbe wetu sio kutisha. Tunahitaji kuchukua tahadhari zinazohitajika lakini tuelewe uhalisia wa hali ya Waislamu.

Huenda ikawa rahisi kwa Waislamu kulinganisha na maisha ya wahamiaji Waislamu waliokimbia mateso kutoka Makka kwenda Uhabeshi na kupewa usalama na Najashi. Tunaweza kuwa na maoni kwamba kinachohitajika leo ni Najashi wa kisasa. Tuweni wazi kabisa, hakuna Najashi wa kisasa kwani Najashi alikuwa ni mfumo.

Fauka ya hayo, tunaweza hata kulinganisha kirongo kwa Obama na wengine na hata kuwa na maoni mazuri juu ya ujuzi wa Biden dhidi ya Trump. Mara kwa mara, tumeshuhudia marais wa Amerika wakitabikisha mfumo uliopo wa kisekula ambao ubaguzi wake wa rangi , ubaguzi wa kidini, na chuki dhidi ya wageni yako kitaasisi.

Usekula huzaa na kuendekeza wabaguzi weupe na mfano wao.

Usekula huzaa mazingira ya vitisho na majungu wanayokabiliana nayo Waislamu.

Usekula huzaa urahisi ambao vyombo vya habari hupewa leseni ya uhuru wa kufanya wapendavyo kuudhalilisha Uislamu na kuunasibisha kwa njia ya kupotosha na maneno ya kihemko kama ugaidi, msimamo mkali, siasa kali n.k.

Tunapaswa kulichukulia onyo la tishio la usalama linalokuja kwa uzito bali kwa kutambua wazi kwamba hili haliepukiki na litaendelea.

Wakati wa matatizo na shida, tunapaswa kukumbuka kuwa Mwenyezi Mungu (swt) anatukumbusha juu ya haja ya kuwa na subira, uvumilivu, na kushikamana Haki.

Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Surah Al-'Ankabut Ayah 2:

]أَحَسِبَ النَّاسُ أَن يُتْرَكُوا أَن يَقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يُفْتَنُونَ]

Je! Wanadhani watu wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe?” [TMQ 29:2].

Yeye Mwenyezi Mungu (swt) atukumbusha katika Surah Yusuf Ayah 110:

[حَتَّى إِذَا اسْتَيْأَسَ الرُّسُلُ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ قَدْ كُذِبُوا جَاءَهُمْ نَصْرُنَا فَنُجِّيَ مَنْ نَشَاءُ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُنَا عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ]

Hata Mitume walipo kata tamaa na wakaona kuwa wamekadhibishwa, hapo ikawajia nusura yetu, wakaokolewa tuwatakao. Na adhabu yetu haitowawacha kaumu ya wakosefu.” [TMQ 12:110].

Yeye (swt) asema katika Surah Al-Baqarah Ayah 214:

[أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِكُم ۖ مَّسَّتْهُمُ الْبَأْسَاءُ وَالضَّرَّاءُ وَزُلْزِلُوا حَتَّىٰ يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ مَتَىٰ نَصْرُ اللَّهِ ۗ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّهِ قَرِيبٌ]

Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale walio pita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.” [TMQ 2:214].

Mwenyezi Mungu (swt) anatuonyesha waziwazi kuwa njia yake ya kuwaruzuku waumini ushindi ni kwanza kuwatia katika mitihani kadha wa kadha ili kuona namna gani walivyo shikamana na Dini yake. Na hakika, Yeye (swt) ametuahidi ushindi kwa wale wanaovumilia.

Mtume Muhammad (saw) amesema:

عن سعد بن أبي وقاص رضي الله عنه قال: سئل النبي ﷺ: أيُّ الناس أشد بلاءً؟ قال:

«الْأَنْبِيَاءُ، ثُمَّ الْأَمْثَلُ فَالْأَمْثَلُ، يُبْتَلَى الرَّجُلُ عَلَى حَسَبِ دِينِهِ، فَإِنْ كَانَ فِي دِينِهِ صَلَابَةٌ زِيدَ صَلَابَةً، وَإِنْ كَانَ فِي دِينِهِ رِقَّةٌ خُفِّفَ عَنْهُ، وَلَا يَزَالُ الْبَلَاءُ بِالْعَبْدِ حَتَّى يَمْشِيَ عَلَى الْأَرْضِ مَا لَهُ خَطِيئَةٌ»

Sa’d ibn Abi Waqqas (ra) amesimulia: Mtume Muhammad (saw) aliulizwa, ni watu gani ambao wanapatikana na mitihani mikali? Yeye (saw) akasema: "Mitume, kisha mfano wao kwa mfano wao, mtu hupewa mtihani kulingana na kiwango cha Dini yake, basi ikiwa yuko imara katika Dini yake huzidishiwa mitihani, na ikiwa katika Dini yake kuna udhaifu huhafifishiwa mitihani, na mitihani haitawacha kumwandama mja mpaka atatembea juu ya ardhi akiwa hana dhambi." [Ahmad]

Tunapaswa kusimama pamoja na Uislamu kwa fahari, nyakati za raha na shida – kwani hii ndio amri, matarajio, na mfano kwa kizazi chetu kijacho.

Tuchukueni funzo kutoka kwa mfano wa uliotangulia uliotaja kuhusu wahamiaji ambao walitafuta himaya huko Uhabeshi. Ingawa wahamiaji hao walipata usalama na amani, bado walikuwa hawajatulia au kuridhika kwani walikuwa wakitamani kila mara kurudi kuwa na Mtume (saw) na kuwa naye chini ya mamlaka ya Kiislamu.

Kinyume chake, popote ulimwenguni, kama jamii, hatuna usalama tunaouhitaji kulinda na kutabikisha Dini yetu - kwa hivyo, hamu yetu ya mamlaka ya Kiislamu inapaswa kuwa kubwa zaidi.

Kwani Mtume (saw) amesema,

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Hakika Imam ni ngao watu hupigana nyuma yake na kujihami kwayo.”

Insha’Allah, ni lazima tutazame mbele na kufanya kazi kwa ajili ya siku ile ambayo mamlaka ya Kiislamu yataasisiwa.

Hizb ut Tahrir

Amerika

H. 4 Jumada II 1442
M. : Jumapili, 17 Januari 2021

Hizb-ut-Tahrir
Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu