Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Demokrasia, Kufeli kwa Jengo Capitol!

(Imetafsiriwa)

Kile ambacho ulimwengu umeshuhudia leo ni kuvunjika kimsingi kwa uongozi na serikali iliyofeli ambayo inajali zaidi faida ya kisiasa kuliko kuchunga mambo ya watu.

Tukio hili linafichua kufeli kwa taasisi za serikali ya Amerika katika ngazi zote:

Ubaguzi wa rangi wa kitaasisi

Mauwaji ya kitaasisi ya watu wanaotoka nchi nyengine

Ukosefu wa usawa wa mali wa kitaasisi

Maslahi ya kikampuni ya kitaasisi

Utofauti wa kitaasisi wa upataji huduma za afya

Lazima tugundue kuwa Trump ni Amerika - yeye sio mkengeukaji wa ada iliyoko. Trump ni matokeo ya nidhamu fisidifu ya Kiamerika ya demokrasia, usekula na urasilimali ambazo zinaendelea kunyima haki na kusaliti jukumu lake la kuchunga mambo ya watu wake.

Miongo kadhaa ya tofauti za kisiasa sasa imelipuka kwa kutoiamini nidhamu hii na kuvunjika kwa jamii iliyogawanyika. Amerika ni taifa lililogawanyika katika mistari ya kisiasa, kiuchumi, kirangi na kitamaduni na hii hapa inagawanyika vipande vipande.

Demokrasia ya Kiamerika imeharibika mbele ya macho ya watu wake na ulimwengu. Ni 'jamhuri ya ndizi' katika kutengeneza mengi kama yale ambayo imeunda katika sehemu tofauti za ulimwengu. Kama wasemavyo, "kuku wamerudi nyumbani kupumzika."

Ni wakati sasa dunia kukumbatia mfumo mbadala. Uislamu unatoa badali hiyo. Hadhara ya Kiisilamu iliyotabikishwa na Dola ya Khilafah ilikuwa na rekodi ya kipekee, kiasi ya kutokuweko nyengine, katika kuwaunganisha watu kutoka kwa jamii na makabila mengi, kuwainua kutoka kwa umaskini, kuwapa heshima, huduma ya afya, amani, usalama na juu ya yote uadilifu. Mabilioni ya watu kote ulimwenguni wanahitaji mfumo ambao una jukumu la Kimungu la kushughulikia mambo yao.

Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Surah Al-Fath:

[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَكَفَى بِاللَّهِ شَهِيداً]

Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki, ili aitukuze juu ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi. [TMQ Al-Fath: 28]

H. 22 Jumada I 1442
M. : Jumatano, 06 Januari 2021

Hizb-ut-Tahrir
Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu