Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Waislamu wa Dearborn, Michigan Wasimama Imara kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto Wetu

Uislamu dhidi ya Ajenda ya Kisekula ya LGBTQ

(Imetafsiriwa)

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَاراً وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَا يَعْصُونَ اللَّهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ)

“Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa.” [At-Tahrim 66:6]

Macho yote yako kwa Dearborn, Michigan - nyumbani kwa mkusanyiko wa idadi kubwa zaidi ya Waarabu-Waamerika nchini - kama wazazi, haswa na wazazi Waislamu, kwa ujumla wakipinga usambazaji wa vitabu viovu vya LGBTQ katika mfumo wa shule za umma wa jiji hilo. Maandamano ambayo yalisonga na kufunga kumbi za bodi ya shule yalichemka huku jumuiya na bodi ya shule zikitofautiana, bodi ya shule ikilazimisha mamlaka ya Dola ya Kisekula dhidi ya jamii iliyohisi sauti zao, wasiwasi na mamlaka yao juu ya watoto wao yamenyakuliwa. Huu ni mvutano wa kawaida unaopasua mishipa ya nchi, huku makundi yanayoonekana kuwa ya wachache kama vile la ushawishi wa LGBTQ yakifurahia kuungwa mkono na mfumo huo dhidi ya jamii nyingi za kitamaduni zinazoonekana kuwa kimya—hata hivyo, ya kwanza inayoonekana nchini Marekani ni jamii ya Waislamu. Ishara moja iliyoshikiliwa katika maandamano hayo, haswa, ilinasa mfadhaiko uliopo, ikisema kwamba “Ikiwa Demokrasia Ni Muhimu, Sisi ndio Wengi.”

Uhalisia ulio nyuma ya mfadhaiko huu – ni haki za nani, sauti ya nani, na mfumo wa nani wa maisha ambao kikweli ndio unao stahiki - yanaingia ndani zaidi kuliko mfululizo wa matukio yanayotokea huko Dearborn, Michigan, na yanazungumzia mfumo usiofungamana, unaogongana, na wenye upendeleo wa Demokrasia ya Kisekula yenyewe. Katika kuondolewa kwa Mungu kutoka kwa nyanja ya maisha ya umma na ya kijamii, hakuna chanzo cha maadili yenye malengo, sahihi au batili, na badala yake hushindana vyama mbalimbali kwa maslahi yao binafsi - mara nyingi kwa gharama ya wale walio dhaifu kinguvu au kiidadi. Pasi na majibu sahihi, jibu pekee lililobaki ni kwamba linaweza kufanya sawa! Si ajabu kwamba Dola ya Kisekula inaposonga mbele, badala ya utulivu na mshikamano, kinachozuka ni sauti zinazopingana, siasa za upendeleo, kuchanganyikiwa, na vurugu. Leo watoto wanaweza kutafuta tiba ya kuzuia homoni na upasuaji usioweza kutenduliwa bila hata idhini ya wazazi wao, muundo wa kawaida wa familia una changamoto, na daima kuna alfabeti inayoongezeka kila wakati ya kitambulisho kipya cha kijinsia na uhalisia unaolazimishwa juu ya watu.

Uislamu, kinyume chake, ni mfumo kamili wa maisha, nidhamu, na muundo ambao uko wazi kabisa, bila mgongano, na ndio tiba pekee ya hali ya Kijahiliyah (ujinga, dhulma, kuchanganyikiwa, hali kupotea) leo. Uislamu ni sahali, uliofupishwa katika uthibitisho wake wa imani: kwamba hapana Mungu wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad (saw) ndiye Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu – na kwamba kila kinachotokana na hayo ni haki, sahihi kimaadili, na msingi ambao kwao mujtamaa hujengwa. Uhalisia hivi leo ni kwamba mifumo mingine yote ya maisha imeinama, imefungana, au imelegea kuhusiana na Mfumo wa Kilimwengu wa Kisekula - yaani, isipokuwa Uislamu! Kwa hiyo, kama Waislamu, tuna wajibu wa kushikamana, kusimama kidete, na kuwalingania wengine kwa yale ambayo ni bora kwao katika maisha haya na yajayo. Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw) wametangaza yale yanayostahiki na yasiyostahiki katika suala la muundo wa familia, mahusiano ya kijinsia, sahihi na makosa – na jibu la Muislamu aliyeukubali msingi huo ni kusema tu kwa kujibu kwamba tunasikia, na tunatii - bila kujali shinikizo, siasa ndogo ndogo za upendeleo, au bodi ya shule!

(وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا)

“Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.” [Al-Ahzab 33:36]

Kwa kumalizia, ni jambo la kutia moyo sana kuona jamii ya Waislamu huko Dearborn ikisimama kulinda usafi wa watoto wetu. Waislamu kote nchini tunatakiwa kuwaunga mkono wazazi na watoto wenzetu. Kwa kufanya hivyo lazima tufanye yafuatayo:

1. Wazazi wanapaswa kupambana na maadili ya kiliberali ya Kisekula kuanzia umri mdogo sana na kuwashajiisha watoto kufikiri kwa kina juu ya kile wanachofundishwa na kupinga fikra hizi kwa fikra wazi za Kiislamu.

2. Tambua kwamba shule na jamii kwa jumla huwafunza watoto fikra na maadili ya kiliberali ya kisekula. Kwa hivyo, ni muhimu sana kueleza msimamo wa Kiislamu juu ya uhusiano wa mwanamume na mwanamke, ndoa, uhusiano wa kimwili, familia, mujtamaa na serikali. Ni lazima tuwafahamishe watoto mfumo wa kijamii wa Uislamu. Kwa kuongeza, hii inamaanisha kuelezea mfumo mbadala wa maisha kinyume na mfumo wa kiliberali wa kisekula.

3. Jamii ya Kiislamu lazima idai mashirika, viongozi na wanaharakati wa Kiislamu kujitenga na ajenda za Kiliberali (Democrat) au za mrengo wa Kulia (Republican). Lazima tupange mustakabali wetu wenyewe kulingana na Aqidah yetu ya kipekee, mawazo msingi na maadili bora.

4. Hatimaye, kujivunia Uislamu na maadili yetu na kuwalinda watoto wetu bila kujali ni majina gani ambayo wale wanaochukia haki wanaweza kutupa.

Familia zetu, majirani zetu, ardhi, na Ulimwengu wa leo wanahitaji sana rehma, utulivu, uadilifu na haki ya Uislamu—na kwa hiyo, umefika wakati sasa wa sisi kama jamii na Umma tufanye kazi na kuendesha harakati zetu kipekee chini ya bendera ya Uislamu na kwamba turegeshe tena sifa yetu kama Umma bora uliotolewa kwa ajili ya Wanadamu!

(كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللّهِ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ)

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu”. [Aal-i-Imran 3:110]

H. 21 Rabi' I 1444
M. : Jumatatu, 17 Oktoba 2022

Hizb-ut-Tahrir
Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu