Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Katika Kumbukumbu ya Ukombozi wa Kostantinopoli

Hizb ut Tahrir / Amerika Imefanya Kongamano kwa Anwani “Nusra ya Mwenyezi Mungu ipo Karibu”

(Imetafsiriwa)

Kama nyongeza ya kampeni ya kiulimwengu iliyo zinduliwa na Hizb ut Tahrir chini ya muongozo wa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amuhifadhi, “Ukombozi wa Kostantinopili Bishara Njema ili ikatimia … Ikifuatiwa na Bishara Njema!”, Hizb ut Tahrir / Amerika imefanya kongamano kwa anwani “Nusra ya Mwenyezi Mungu ipo karibu”, mnamo Jumapili, 24 Jumada al-Awwal 1441 H sawia na 19 Januari 2020 M.

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir imezindua kampeni hii ya kiulimwengu kuadhimisha Ukombozi wa Konstantinopoli iliyo zingirwa kuanzia 26 ya Rabii’ al-Awwal mpaka 20 Jumada al-Awwal 857 H sawia na 5 Aprili hadi 29 Mei 1453 M.

Kongamano lilianza kwa aya kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuanzia mwishoni mwa Surat Al-Imran, kisha Dkt. Abdur Rafay akazungumzia majanga ya Waislamu kwa jumla na hususan kwa Waislamu nchini India. Alionesha kwamba majanga ya Waislamu nchini India ni matokeo ya wao tu kuwa Waislamu. Alizungumzia namna India ambayo inaitwa nchi kuu ya demokrasia inaonesha watu ukweli wa uongo wa demokrasia ambayo kamwe haiwakingi watu dhidi ya unyanyasaji wa watu, hususan unyanyasaji dhidi ya Waislamu.

Kisha hotuba ikatolewa na Ustaadh Taiseer Hussein, aliye ongelea kuhusu ukombozi wa Kostantinopoli, nao ulikuwa ni kutimia kwa bishara njema ya kwanza iliyo patikana baada ya kukombolewa Waajeni na Warumi na itafuatiwa na kusimamishwa kwa Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume na ufunguzi wa Roma, na ukombozi wa Ardhi iliyo Barikiwa – Palestina.

Ndugu Taiseer alisisitiza kwamba bishara njema hizi hazimaanishi kwamba tukae chini na kusubiri, bali atulingania na kutuhimiza kufanya kazi kwa bidii ili kusimamisha Khilafah.

Kisha ukawadia muda wa maswali na majibu, na Kongamano likahitimishwa kwa dua ya kumuomba Mwenyezi Mungu ushindi na nusra, na kusimamisha Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa Walimwengu.

#Constantinople

#ConquestofIstanbul

H. 24 Jumada I 1441
M. : Jumapili, 19 Januari 2020

Hizb-ut-Tahrir
Amerika

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: Demokrasia, Kufeli kwa Jengo Capitol! »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu