Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Serikali ya Denmark Inataka Kuzuia Uchomaji wa Quran Mbele ya Afisi za Mabalozi, Ili Kulinda Maslahi Yake, ambayo bila Shaka sio kwa Ajili ya Heshima kwa Uislamu
(Imetafsiriwa)

Ni dhahiri kwamba nia ya serikali ya Denmark ya kutoa uamuzi wa kupiga marufuku kuchomwa moto kwa Qur'an mbele ya afisi za balozi za kigeni haionyeshi kwa vyovyote vile kwamba serikali hiyo ghafla ina hamu ya kuilinda jamii ya Kiislamu nchini Denmark kutokana na mashambulizi ya chuki ya mara kwa mara yanayoilenga.

Serikali ya Denmark ndiyo mhusika mkuu katika kupambana na maadili ya Kiislamu, kupitia sera yake ya kiserikali ya kuwalenga Waislamu na majaribio yake ya kuwaoanisha katika jamii kupitia utoaji sheria za kibaguzi dhidi yao ili kulazimisha udhibiti juu yao. Ukiukaji wa kisiasa dhidi ya Uislamu na Waislamu, pamoja na vitendo vya chuki dhidi yao, vyote vilifadhiliwa na fedha za serikali, na hii imekuwa sehemu ya vita dhidi ya Uislamu nchini Denmark tangu 2005.

Maslahi ya kisiasa na kiuchumi hayabadilishi chochote katika sera ambayo serikali inaifuata kwa Uislamu na Waislamu kindani. Kinyume chake, sheria itakayoidhinishwa inathibitisha kwamba uhuru wa kujieleza ulikuwa ni kisingizio tu cha kutumiwa kwa ubaguzi na ulitumiwa na serikali mtawalia kwa lengo la kueneza matusi kwa Waislamu au pale serikali zinapoona ni kwa maslahi yao.

Muda uliotegewa wa uchomaji moto wa hivi karibuni wa Qur'an haulingani na sera ya kigeni ya serikali, ambayo inalenga kudumisha urafiki na tawala dhalimu katika nchi za Kiislamu, na hilo lilidhihirika katika ziara ya hivi karibuni ya waziri mkuu katika Mashariki ya Kati. Si ajabu kwa serikali ya Denmark kutofuata maadili yake inayodaiwa nje ya nchi, kwani inataka kwa namna isiyo na kifani kuzifungulia tawala dhalimu katika ulimwengu wa Kiislamu zinazotekeleza ukandamizaji na mateso dhidi ya watu wa nchi hii kwa ushirikiano na nchi za Magharibi, bila kuzingatia ukinzani wa miungano hii na haki za binadamu!

Wanasiasa wa vyama vinavyounda serikali wanajaribu kutafuta rai jumla yenye kuunga mkono utoaji wa sheria ambayo itazuia kuchomwa moto kwa Quran, kwa kueneza wazo la usalama na amani ya Denmark. Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark, Lars Loke Rasmussen, alionekana kufarijika baada ya Jumuiya ya Kongamano la Kiislamu kutoa taarifa yake mnamo siku ya Jumatatu, hivyo kuokoa muda kwa serikali kutatua tatizo la kuchoma nakala za Qur'an.

Hizb ut Tahrir nchini Denmark inatoa wito kwa kila mtu kutambua ukweli kuhusu suala hili na udanganyifu wa kisiasa unaofanywa. Pia tunatilia maanani ukweli kwamba Waislamu hawawezi kutulia hadi Denmark na nchi za Magharibi ziache kuingilia nchi za Kiislamu, na kabla ya sheria zisizo za haki na vitendo vya dhulma dhidi ya Waislamu katika nchi hizi kukomeshwa. Na Waislamu waruhusiwe kuishi kwa mujibu wa imani zao, na walindwe dhidi ya ubaguzi wowote dhidi yao, kama ambavyo ujio wa Khilafah Rashida utawalinda raia wake dhidi ya ubaguzi wowote bila ya kujali imani zao.

H. 15 Muharram 1445
M. : Jumatano, 02 Agosti 2023

Hizb-ut-Tahrir
Denmark

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu