Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuanza na Kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan Kunaamuliwa tu na Muandamo wa Kisharia Pekee wa Hilal (mwezi mwandamo)
(Imetafsiriwa)

Kwa fadhila na neema za Mwenyezi Mungu, tunakaribia kuwasili kwa mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan kwa mwaka wa Hijri 1445. Kwa mara nyingine tena, mijadala inazuka baina ya Waislamu kuhusu iwapo mwanzo wa Ramadhan unaweza kuamuliwa kabla kwa kutumia hesabu za kifalaki na ni ipi njia sahihi ya kukabiliana na suala hili. Baadhi ya vituo vya Kiislamu nchini Denmark vimechagua kufuata hesabu za kifalaki kwa kuzingatia mambo fulani, huku vyengine vikikataa jambo hilo na kusisitiza kwamba mwanzo wa mwezi lazima uthibitishwe kwa kuiona hilal (mwezi mwandamo) kwa macho kwa mujibu wa njia ya Kiislamu.

Swali hili ni muhimu kwa Waislamu duniani kote.

Sehemu ya mjadala unaoendelea inahusu tafsiri na utekelezaji sahihi wa hukmu za Kiislamu, hasa kwa Waislamu wanaoishi Magharibi. Kwa hiyo, Hizb ut Tahrir nchini Denmark inaona ni muhimu kufafanua nukta zifuatazo:

Kuanza kwa saumu ya mwezi wa Ramadhan kunategemea kuona hilal kwa dalili za kidini, ikiwemo Hadith ambayo Mtume Muhammad (saw) alisema... صُومُوا لِرُؤْيَتِهِ وَأَفْطِرُوا لِرُؤْيَتِهِ فَإِنْ غُبِّيَ عَلَيْكُمْ فَأَكْمِلُوا عِدَّةَ شَعْبَانَ ثَلَاثِينَ» “Fungeni (saumu) kwa kuuona (mwezi mwandamo) na fungueni kwa kuuona (mwezi muandamo), lakini ikiwa mutagubikwa na mawingu musiweze kuuona, basi kamilisheni idadi ya siku thalathini za Sha’aban.” [Al-Bukhari]

Swali hili ni suala la kidini linalohusiana moja kwa moja na nususi za kidini na linachukua kutoka kwazo hali ya ulazima.

Waislamu lazima wachukue misimamo yao juu ya masuala kama hayo ya kidini kwa kuzingatia yale ambayo nususi za Quran na Sunnah za Mtume (saw) yanaashiria, bila ya kuathiriwa na mazingira yaliyopo au mazingatio ya kivitendo. Kudai kuwa kupambanua mwanzo wa Ramadhan ni kwa kuiona Al-hilal kunahusiana na "kasoro ya kisheria" na kwamba sio lazima kuona mwezi mwandamo lakini inatosha kujua uwepo wake ni madai yasiyo sahihi na hakuna dalili ya kuunga mkono. Ikiwa haiwezekani kuona mwezi mwandamo katika mwisho wa mwezi, basi Hadith ya Mtume (saw) imetoa suluhisho. «... فَإِنْ غُبِّيَ عَلَيْكُمْ فَأَكْمِلُوا عِدَّةَ شَعْبَانَ ثَلَاثِينَ» “lakini ikiwa mutagubikwa na mawingu musiweze kuuona, basi kamilisheni idadi ya siku thalathini za Sha’aban.”

Hata kama hesabu za falaki zilikuwa sahihi, suala hilo halihusiani na kuthibitisha hali ya kianga katika maana ya kisayansi.

Kuamua mwanzo au mwisho wa Ramadhan hakuhitaji "dhamana ya kisayansi" ya kuzaliwa kwa mwezi mwandamo. Hakuna dalili ya kidini kwamba kuanza kwa saumu lazima kutegemee kuzaliwa kifalaki kwa hilal (mwezi mwandamo), lakini lazima iwe juu ya kuuona, kama Mtume (saw) alivyoamuru katika Hadith iliyotangulia.

Kwa hivyo, ikiwa mwezi mwandamo wa Ramadhan upo lakini umefichwa na mawingu kiasi kwamba hauwezi kuonekana kwa macho, katika hali hii, ni lazima tutimize Sha’aban kwa muda wa siku thelathini.

Sisi, Hizb ut Tahrir Denmark, tukiongozwa na mapenzi yetu kwa Dini yetu na kujitolea kwa Sharia yake, tunataka kufafanua kwamba mwanzo wa mwezi wa Ramadhan unapaswa kuamuliwa tu kwa njia iliyowekwa kwenye nususi za kidini, yaani kupitia mwandamo, na sio kupitia hesabu ya kifalaki.

Kuna kipengee chengine muhimu ambacho Waislamu wapendwa wanapaswa kukifahamu.

Hiki ni kipengee cha kina zaidi katika mjadala wa sasa wa jinsi ya kuamua kuanza kwa mwezi wa Ramadhan ambacho kinapita zaidi ya kipengee cha kisheria. Kwa kweli, ni suala zito zaidi ambalo linaathiri ufahamu wetu wa Uislamu kisheria na jinsi tunavyoamiliana dalili za kidini. Kwa Waislamu wanaochagua kutegemea hesabu za falaki badala ya kuona, miongoni mwa hoja zao ni kwamba tunaishi katika jamii isiyokuwa ya Kiislamu ambapo taratibu za Kiislamu zinapokea ufahamu mdogo na zinakaribu kutokuwepo. Kwa hivyo, kulingana na wao, kutegemea hesabu za falaki kunafaa zaidi kwa Waislamu wa Magharibi kwa sababu za kivitendo na kusahilisha mambo. Kisha, taawili dhaifu sana za nususi au maoni ya baadhi ya wasomi hutumiwa kuhalalisha msimamo ambao tayari umechukuliwa kuhusu kutegemea hesabu za falaki. Zaidi ya hayo, maoni yasiyofaa, kama vile kutokuwepo kwa mzozo kati ya Uislamu na sayansi, yanaongezwa.

Hapa tumelazimika kutahadharisha kwamba hii ni njia yenye matatizo kwa sheria ya Kiislamu pindi maslahi yanayodhaniwa au yanayofikiriwa yanakuwa ndio vigezo vinavyoamua, ikiwemo dhurufu zilizopo, ikiwa ni pamoja na serikali inayotawala, katika kuchagua baina ya rai, hata katika masuala ya ibada.

Kwa njia hii, mtu anaweza kuteleza kwa hatari kuelekea kuurekebisha Uislamu kwendana na mfumo wa kijamii ambao hauheshimu Uislamu lakini badala yake unaupinga na unalenga kuwaoanisha na kuwaingiza Waislamu ndani yake.

Enyi Waislamu: Kwa pamoja tunautazamia kwa hamu mwezi ujao wa Ramadhan unaowakusanya Waislamu duniani kote mara tu mwandamo wa hilal (mwezi mwandamo) utakapothibitishwa popote pale juu ya uso wa ardhi, kuanzia tarehe 29 Sha’aban, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atuwezeshe kuupitia tena mwezi mtukufu wa Ramadhan na kuleta faraja na ushindi kwa Umma wa Kiislamu. Vile vile tunaomba mwezi huu uwe Ramadhan ya mwisho bila ya Khilafah Rashida.

Mwisho, tunawakumbusha Waislamu wapendwa kuwa mkanganyiko unaojitokeza mara kwa mara kuhusu kuanza na kumalizika kwa Ramadhan na kusherehekea sikukuu ya Idd unatokana na kutokuwepo utawala wa Kiislamu kwa karne nyingi na hivyo kutokuwepo mamlaka halali ya Kiislamu ya kusimamia mambo ya Waislamu, ikiwemo ibada zao za kawaida, na kufanya maamuzi ya lazima kwa Waislamu wote kote duniani.

H. 20 Sha'aban 1445
M. : Ijumaa, 01 Machi 2024

Hizb-ut-Tahrir
Denmark

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu