Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Leo Hii Imarati Na Bahrain Zinatia Saini ya Mkataba Pamoja na Dola ya Kiyahudi, Mkataba wa Uhaini Mkuu kwa Palestina Ambayo Ndipo Alipofikia Mtume (saw) Katika Safari Ya Isra Na Miiraj Yake. … Wanafanya Hivyo Hata Bila ya Kumhofu Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Waumini!

France 24 jana 14/9/2020 M ilichapisha: (Mashariki ya kati, Jumanne itaingia kwenye mkondo mpya, wakati ambapo dola ya Imarati na Ufalme wa Bahrain zitatia saini mkataba wa makubaliano pamoja na (Israel) huko Washington… na yatarajiwa kusimamiwa na rais wa Amerika Donald Trump, katika sherehe ya saini hiyo itakayofanyika ikulu ya White House … na wajumbe wawili wa Kiarabu, wataongoza mawaziri wa mambo ya nje wa dola mbili hizo za Ghuba…) yaani, ni kwamba Imarati na Bahrain leo Jumanne huko katika mji Mkuu mweusi wa Washington watatia saini makubaliano ya khiyana kuu kwa mahali ilipokuwa Isra ya Mtume (saw) na Miraj yake, pasi na kumuogopa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake (saw), na wala waumini! Nao kwa kufanya hivyo, watakuwa wamefuata mwenendo wa mfano wao kabla yao: Serikali ya Misri, katika mkataba wa Camp David, na uliopangwa huko Oslo, na serikali ya Jordan katika waadi Araba! Hakika, watawala katika miji ya Waislamu, kabla ya mikataba hii na baada yake walikuwa wakiamiliana na dola ya Kiyahudi lakini wakifanya hivyo nyuma ya pazia, huku wakizingatia katika hilo haya japo kidogo, bali hata aibu. Na kilipoondoka hicho kizibo, kutangaza waziwazi wa usawazishaji mahusiano imekuwa sasa ni jambo (la kifahari) kwao. Wanatangaza wazi hili bila ya kuhisi unyonge au hata angalau aibu kidogo au haya! Na unyonge huu hakuna budi utawafika tu! Wakubali hilo au wakatae, huo ndio mwisho wa mhalifu yeyote katika haki ya dini yake au Ummah wake)

سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ

"Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya" [Al-An'aam: 124].

Kwa hakika, ni moja kati ya makubwa, kutokea hili linalotokea! Ambapo usawazishaji mahusiano unaendelea kwa kasi hii, huku Ummah na majeshi yake wakiangalia na kusikia, bila ya majeshi ya Waislamu kutikisika na kuwapindulia dunia juu yao na kuwaondoa! Kisha, na wale ambao bado hawajatia saini mikataba ya wazi hawana tofauti yoyote na waliotia saini. Kwani Oman hukaribisha na kukaribishwa na dola ya kiyahudi. Nayo Qatar ni ya kati na kati (iso na mapendeleo) kati ya Mayahudi na Gaza! Na utawala wa Saudi katika nchi iliyo na misikiti miwili mitukufu, anga zake ziko wazi kwa ndege za dola bandia na iliokalia kimabavu Al-qudsi tukufu ya Waislamu!! Kisha, nao utawala wa Uturuki, ungali unaitambua dola ya Kiyahudi ilioikalia kimabavu Palestina! Ama kiukweli, ni moja ya makubwa kutokea hili linalotokea, kana kwamba ni jambo la kawaida kati ya ndugu wa tumbo moja! Na kana kwamba sio zaidi ya tofauti ndogo tu ya kimtazamo kuhusu mipaka!.

Enyi Waislamu!

Hakika Ardhi Iliyo barikiwa ya Palestina, ardhi iliyokuwa mafikio ya Safari ya Israa na Miraj, imo ndani ya nyoyo za Waislamu. Hata kama wameonjwa kwa watawala Ruwaibidhwa (wenye akili ndogo) wanaowatii makafiri wakoloni, zaidi ya kumtii Mola wa viumbe! Hakika Palestina na Qudsi yake ni Palestina ya Waislamu wala Palestina sio ya hao watawala wasaliti, wala Qudsi si yao! Na kusawazisha mahusiano kati yao na dola ya kiyahudi iliyoinyakua Palestina kimabavu, wote watahitimishwa na udhalili na aibu mpaka siku yao walioahidiwa. Kwani hakika, Palestina itarudi kwa wenyewe baada ya kupigana na Mayahudi wanyakuzi wa Ardhi Iliobarikiwa, katika siku ambayo itakayoshuhudiwa, itakayofunikwa na sauti za takbira zitokazo kwa majeshi ya Waislamu. Na hiyo ni ahadi isiyo ya uongo, iliyosemwa na mkweli msadikiwa (saw) aliposema:   

لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ، فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ حَتَّى يَقُولَ الْحَجَرُ: يَا مُسْلِمُ هَذَا يَهُودِيٌّ، فَتَعَالَ فَاقْتُلْهُ

"Mtapigana Na Mayahudi Na Mtawaua Kweli Kweli, Hadi Jiwe Liseme: Ewe Muislamu Huyu Hapa Myahudi Njoo Umuue" [Imepokewa na Muslim].

Enyi Waislamu!

Hakika wanajeshi katika miji ya Waislamu ni watoto wenu, ni ndugu zenu, ni watu wenu wenyewe, na miongoni mwao wapo wenye ikhlasi. hivyo basi, waangazieni nyoyo zao kwa haki na muwasukume kwake, ili waikomboe Palestina kutoka kwa umbile ovu la Kiyahudi ambalo limeinyakua na kueneza humo uharibifu na ufisadi, kwa msaada wa viongozi katika nchi za Waislamu, ambao badala ya kupigana na umbile hilo, wamekuwa wakichunga usalama wake! Na lau si hivyo, umbile hilo lisingebakia mpaka leo hii. Kwani hakika Mayahudi huwa hawanusuriwi katika vita vya kikweli pamoja na Waislamu.

لَنْ يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ

"Hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa" [Al-Baqara: 111].

Na huu ndio uhalisia wao, na hivi ndivyo walivyo. Lakini badala ya kupigana nao viongozi hawa wanafanya nao muamala wa mapatano nao! Na badala ya kuwatoa katika miji yetu kama alivyosema Allah mshindi  mwenye hikma:

وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُمْ مِنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ

"Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni" [Al-Baqara: 191].

Mara twaona hawa matwaghut wanathibitsha humo!

قَاتَلَهُمُ اللَّهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ

"Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?" [Al-Munafiqun: 4].

Enyi Waislamu!

Hakika mambo yalivyo, hili jambo haliwezi kutengenea ila kwa yale yaliyotengenea mwanzo wake: Nayo ni: Kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt), na wanajeshi watakao watikisa maadui wa Mwenyezi Mungu (swt). Na hayo hayatokuwa ila kwa kurudi upya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ili ing’oe umbile la Kiyahudi lilochafua Palestina twahara kwa miaka zaidi ya sabini, na kisha kuirudisha Palestina kikamilifu katika makaazi ya Uislamu, ikiwa ni mji wa Izza ndani ya dola yenye Izza, ambayo ni Khilafah kwa njia ya Utume… na hilo litakuwa tu kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na hili latiliwa nguvu na mambo manne yenye maana ya kukatikiwa:

Kwanza: Ni kuwa Ummah wa Kiislamu ni Ummah bora zaidi uliotolewa kwa ajili ya watu.

كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ

"Nyinyi mmekuwa bora ya Umma walio tolewa watu" [Al-i-Imran: 110].

Na Ummah ambao hii ndio hali yake, hautavumilia unyonge. Hautoisahau Qudsi yake, haijalishi watakavyofanya matwaghut, bali utawakanyaga kwa miguu yake kisawasawa hasa.

Pili: Ahadi itokayo kwa Mwenyezi Mungu (swt) ya kuwafanya makhalifa katika ardhi.

وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ

"Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao" [An-Nur: 55].

Na bishara njema ya Mtume Wake (saw) ya kurudi tena kwa Khilafah kwa njia ya Utume.

ثم تكون خلافة على منهاج النبوة

"Kisha itarudi Khilafah kwa njia ya Utume" [Imepokewa na Ahmad].

Tatu: Hadithi ya mkweli msadikiwa (saw) aliposema kuhusu kupigana na Mayahudi Na Kuwaua:

لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ، فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ حَتَّى يَقُولَ الْحَجَرُ: يَا مُسْلِمُ هَذَا يَهُودِيٌّ، فَتَعَالَ فَاقْتُلْهُ

"Mtapigana na Mayahudi na mtawaua kweli kweli, hadi jiwe liseme: Ewe Muislamu huyu hapa Myahudi njoo umuue" [Imepokewa na Muslim].

Nne: Chama cha ukweli na chenye ikhlasi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt), kinachofanya kazi kuhakikisha ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na bishara njema ya Mtume wake (saw). Chama ambacho ni kiongozi asiyewadanganya watu wake, chenye uoni na moyo, kinacho waongoza Ummah kwenye kheri ambayo itawafufua kwa Izza na ushindi na kufaulu duniani na akhera. Na wape habari njema waumini.

Hivyo, Ummah ambao ndani yake kuna hii mihimili ya ushindi, basi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (SWT) utasimamisha tu Khilafah yake na kukomboa Qudsi yake, na utakata mikono ya madhalimu na mabwana wao na wasaidizi wao.

وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ

"Na siku hiyo Waumini watafurahi, Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu".

H. 27 Muharram 1442
M. : Jumanne, 15 Septemba 2020

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu