Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Baraza la Usalama liko “Mfukoni mwa Marekani” Likiendeshwa na Maslahi yake na Maslahi ya Mayahudi na Wakoloni wa Makafiri
(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 11/6/2024, Baraza la Usalama lilitoa azimio la kuunga mkono mradi wa Biden kwa ajili uvamizi wa kikatili wa Kiyahudi dhidi ya Gaza, bali Palestina yote! Maandishi ya azimio hilo, kama yalivyochapishwa na CNN, mnamo tarehe 11 Juni 2024, yalisema yafuatayo: (Baraza la Usalama “linakaribisha pendekezo jipya la kusitisha mapigano lililotangazwa mnamo Mei 31, ambalo lilikubaliwa na ‘Israel,’ na kutoa wito kwa Hamas pia kulikubali, na kuzitaka pande husika zikubali kutekeleza masharti yake kikamilifu bila kuchelewa na bila masharti.”

Ama kuhusu pendekezo la kusitisha mapigano ambalo azimio hilo linakusudia, ni yale ambayo Rais wa Marekani Biden alikuwa ametangaza mnamo 31/5/2024 katika Ikulu ya White House, ilisema, kama ilivyotajwa na tovuti ya arabic.rt.com mnamo 1/6/2024:

[(...Sasa, baada ya diplomasia ya kina, iliyofanywa na timu yangu, mazungumzo yangu mengi na viongozi wa 'Israel', Qatar na Misri, na nchi nyingine za Mashariki ya Kati, 'Israel' sasa imetoa pendekezo kubwa jipya ... Pendekezo hili jipya lina awamu tatu:

1-Awamu ya kwanza itadumu kwa wiki sita ambayo ingejumuisha: Usitishaji kamili wa mapigano, uondoaji wa vikosi vya 'Israel' kutoka maeneo yote ya Gaza yenye wakaazi … Wakati wa wiki sita za awamu ya kwanza, 'Israel' na Hamas watajadiliana kuhusu mipango muhimu kufikia awamu ya pili, ambayo ni kumalizwa kwa kudumu kwa uhasama. Lakini… ikiwa mazungumzo yatachukua muda wa zaidi ya wiki sita kutoka awamu ya kwanza, usitishaji vita bado utaendelea maadamu mazungumzo yanaendelea…Marekani, Misri na Qatar zitafanya kazi kuhakikisha mazungumzo yanaendelea, hadi makubaliano yote yafikiwe.

2- Awamu ya pili, ambayo itajumuisha: Kuachiliwa huru kwa mateka wote waliobaki hai, wakiwemo wanajeshi wa kiume... Na maadamu Hamas itatimiza ahadi zake, usitishaji wa muda wa mapigano utakuwa, kwa maneno ya pendekezo la ‘Israel’, “kumalizwa kwa uhasama daima” ikiwa Hamas itashindwa kutimiza ahadi chini ya makubaliano hayo, 'Israel' inaweza kuregelea tena operesheni za kijeshi.

3- Hatua ya tatu ambapo mpango mkubwa wa ujenzi mpya wa Gaza ungeanza.)

Biden anamalizia kwa kusema: (- “Hivyo, nimehimiza uongozi nchini ‘Israel’ kusimama nyuma ya makubaliano haya, licha ya shinikizo lolote linalokuja.

- Na kwa watu wa ‘Israel’, acha niseme hivi. Kama mtu ambaye amekuwa na ahadi ya maisha yote kwa 'Israel,' kama rais pekee wa Marekani ambaye amewahi kwenda 'Israel' wakati wa vita, kama mtu ambaye ametuma Vikosi vya Marekani kuilinda moja kwa moja 'Israel' iliposhambuliwa na Iran, nakuombeni murudi nyuma na mufikirie kitakachotokea ikiwa wakati huu utapotezwa”.

- Na kwa mkataba huu, 'Israel' inaweza kuoanishwa kwa kina zaidi ndani ya eneo hilo, ikiwa ni pamoja na -- haishangazi kabisa, ikiwa ni pamoja na wanaojua makubaliano ya kihistoria ya uhalalishaji mahusiano na Saudi Arabia ...)]

Kinachoonekana wazi kutokana na tangazo hili ni kwamba limejaa mabomu yanayosubiri muda kulepuka ili kurefusha muda wa uvamizi. Hatoi wito wa kujiondoa kabisa, bali wa “kuondolewa kwa majeshi ya 'Israel' kutoka maeneo yote yenye wakaazi ya Gaza...”, na anacheza na maneno ya kudanganya na kukwepa, akisema, “Usitishaji vita kamili na wa kina... kumaliza kwa kudumu kwa uhasama...”, kisha anasema, ‘Ikiwa Hamas itashindwa kutimiza ahadi zake chini ya makubaliano hayo, 'Israel' inaweza kuanzisha tena operesheni za kijeshi” na anamalizia kwa kutangaza kwamba yeye na Mayahudi wanaoikalia kwa mabavu Palestina ni wawili katika karne isiyoweza kutenganishwa. Anasema, “Kama mtu aliye na ahadi ya maisha yote kwa 'Israeli',” na anawatangazia juu ya uhalalishaji mahusiano wa kihistoria! “'Israel' itaweza kupata uoanishwaji zaidi katika eneo hili na mpango huu, ikiwa ni pamoja na kupitia makubaliano ya kihistoria ya uhalalisha mahusiano na Ufalme wa Saudi Arabia.” Kisha anajingonganisha mwenyewe katika uamuzi huo na kusema: “'Israel' imewasilisha pendekezo jipya,” yaani, kana kwamba ni pendekezo la 'Waisrael', kisha anarudi na kusema, “Nimeuhimiza uongozi wa 'Israel' kuunga mkono mkataba huu...” kana kwamba sio pendekezo la 'Israeli'! Hatimaye, licha ya umbile baya la tangazo la Biden, anasisitiza kwamba Misri na Qatar zitadhamini utekelezwaji wake pamoja na Marekani! “Marekani, Misri na Qatar zitafanya kazi kuhakikisha mazungumzo yanaendelea hadi makubaliano yote yafikiwe.

Uamuzi huu unajiri kufuatia mauaji ya kutisha yaliyofanywa na umbile halifu la Kiyahudi mnamo tarehe 9 Juni 2024 katika kambi ya Nuseirat, ambapo Wapalestina 274 waliuawa shahidi na wengine 698 kujeruhiwa, ambayo inawakilisha moja ya siku za umwagaji damu zaidi kwa miezi kwa watu mjini Gaza.

Enyi Waislamu: Si ajabu kwamba Marekani, makafiri wa kikoloni na miundo yao, dola ya Kiyahudi, wanatushambulia. Ni maadui wa Uislamu na Waislamu, sio kuanzia leo bali wa miaka mingi iliyopita. Wala si ajabu kwamba makafiri wakoloni kwa kuegemea sheria za kimataifa wanaweza kuzishambulia nchi za Kiislamu kwa sababu sheria hii ilianzishwa kwa mara ya kwanza dhidi ya Waislamu na dola yao (Dola ya Uthmani) kwenye Mkutano wa Westphalia mwaka 1648, ambao baadaye uligeuka na kuwa Ligi ya Mataifa na kisha Umoja wa Mataifa. Hayo yote si maajabu, lakini cha ajabu ni kwamba watawala wa nchi za Kiislamu jirani na Palestina wanatazama jinai na mauaji yanayoendelea huko huku wakiwa wamenyamaza kimya na kuyazuia majeshi kunusuru (nusrah) Gaza, na kwa hakika Palestina yote. Bali, mbora wao ni yule anayehesabu mashahidi na kuwaita “wafu” na kuwahesabu waliojeruhiwa kana kwamba ni kundi lisilofungamana na upande wowote, bali liko karibu zaidi na Mayahudi, kana kwamba kinachotokea ni katika nchi ya mbali na sio katika Ardhi iliyobarikiwa ambayo Mwenyezi Mungu ameibariki na viunga vyake! Uvamizi wa kikatili wa Mayahudi dhidi ya Gaza haukufanyika siku moja au mbili zilizopita, lakini takriban miezi tisa iliyopita, na watawala wa Kiislamu wamesalia kimya, badala yake, wamehakikisha utekelezwaji wa maazimio ya kimataifa ambayo yalikuwa ni mabaya kwa Waislamu, Mwenyezi Mungu awaangamize, wadanganyika kiasi gani!

Enyi Majeshi katika Ardhi za Kiislamu: Je, wakati haujawadia wa damu yenu kuchemka katika mishipa yenu mnapoona na kusikia jinai na mauaji yanayotokea dhidi ya ndugu zenu wa Gaza, na kwa hakika Palestina yote, yanayoathiri watu, miti na mawe?! Je, vilio vya watoto, miito ya wanawake, na maombi ya wazee hayakusukumeni kuwanusuru?

[وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Al-Anfal: 72] Je, Aya za Mwenyezi Mungu Al-Qawi Al-Jabbar (Mwenye nguvu na Mwenye uwezo), hazikusukumini musimame kama waanaume dhidi ya umbile la Kiyahudi?

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ]

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini.” [At-Tawbah: 14] Je, kumtii Mwenyezi Mungu ni bora au ni kuwatii watawala wenu? Wanaofanya usalama wao wa kitaifa kuwa huru na Gaza na watu wake, ilhali ni umbali wa pua na mdomo tu kutoka kwao, au hata chini ya hapo? Hawa ndio watawala wanaowaunga mkono wakoloni makafiri, na wasiwasi wao pekee ni kubakia kwenye viti vyao vya utawala vilivyopinda. Mkiwafuata wao hawatokufaeni duniani wala Akhera, na hoja yenu ya kuwatii itakuwa batili Siku ya Kiyama.

[إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ * وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا مِنَّا كَذَلِكَ يُرِيهِمُ اللهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ وَمَا هُمْ بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ]

“Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata, na hali ya kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano yao * Na watasema wale walio fuata: Laiti tungeweza kurudi tukawakataa wao kama wanavyo tukataa sisi! Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyo waonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni.” [Al-Baqara: 166-7]

Enyi Askari katika Majeshi ya Waislamu: Watu wa umbile la Kiyahudi si watu wa vita au mapigano. Ni waoga na wamekumbwa na udhalilifu na umasikini. Mnashuhudia wanaume waumini kutoka miongoni mwa kaka zenu wakiwa na silaha ambazo hazilinganishwi na silaha za Mayahudi, lakini wanawapiga kwa nguvu, na wale wanaokimbia mbele yao wanakimbilia ndege ili kuwalinda.

[لَنْ يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ]

Maadui hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa. [Aal-i-Imran: 111] Bila shaka munajua kwamba Palestina ni ardhi iliyobarikiwa... ardhi ya Kiislamu ambayo Mayahudi hawana haki ya kuwa na mamlaka nayo. Hakuna nafasi ya suluhisho la dola mbili ndani yake. Bali itarudi kama vile Al-Farouq alivyoifungua, Makhalifa Waongofu wakailinda, Salah ud-Din akaikomboa, na Abdul Hamid akaihifadhi kutokana na Mayahudi. Itarejea kwa juhudi za askari wakweli wa Mwenyezi Mungu, wale watakaotimiza Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), «لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ...» “Mtapigana na Mayahudi na mtawaua” [Imesimuliwa na Muslim kutoka kwa Ibn Umar].

[وَلَتَعْلَمُنَّ نَبَأَهُ بَعْدَ حِينٍ]

“Na bila ya shaka mtajua khabari zake baada ya muda.” [Sad: 88]

H. 6 Dhu al-Hijjah 1445
M. : Jumatano, 12 Juni 2024

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu