Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hatimaye, Viziba Uso Vimeanguka kutoka Nyusoni mwa Vibaraka wa Marekani, Erdogan, Rouhani na Putin. Wameshughulishwa na uwakala wa kuhakikisha wanamhifadhi kibaraka wa Marekani ndani ya Syria, ili Marekani imakinike kutatua Janga la Korea na China
(Imetafsiriwa)

Siku ya Jumatano 04/04/2018, maraisi wa Urusi, Iran na Uturuki walikutana mjini Ankara, na kutoa kauli yao ya mwisho. Ilikuwa wazi kutokana na kauli hiyo, ima kupitia kauli ya maandishi au kwa yaliyofichika…kwamba wao watatu wameamua kuhakikisha wanaudhibitisha utawala wa kibaraka wa Marekani ndani ya Syria, na kusitisha muamko wa watu wa Syria wa kutaka kusimamisha utawala wa Kiislamu.
Ama kwa Erdogan, alitumia khiyana na kuendelea kufanya hivyo, ndani ya Oparesheni ya Euphrates Shield, na kuunganisha wapiganaji kuelekea ngao yake, ambapo Aleppo ilianguka na kukabidhiwa utawala. Kisha ikaja Oparesheni Olive Branch, ambapo aliwaunganisha wapiganaji kwenda Afrin na kusini mwa Idlib kukaanguka, ikafuatiwa na mashariki mwa Ghouta…Bado ana “Ngao” na “Matawi” aliyoyaficha mpaka amalize kuwaunganisha wapiganaji ndani ya Idlib, na kisha awaunganishe katika eneo jengine, mwishowe Idlib itaanguka!
Ama kwa Rouhani-Khamenei, wanamgambo wake nchini Syria wamezagaa katika milima na majangwa, kuanzia kitengo cha ulinzi cha mapinduzi na chama chake cha Lebanon, mpaka wanagambo wake wa angani. Wote wanatoa kila juhudi kuuwa watu ili kumdhibiti dhalimu wa Ash-Sham.
Ama kwa Putin, uhalifu wake ndani ya Syria uko wazi kwa kila mmoja kuona, na hauhitaji khiyana kuuonyesha, kama wanavyofanya Erdogan au Rouhani-Khamenei. Wanatumia khiyana, kwa sababu wanapiga kelele za juu kwamba ni Waislamu! Putin hahitaji kufanya hivyo, anajulikana kama adui wa Uislamu na Waislamu.
Hawa watatu wameshughulishwa na kudhibiti utawala wa kisekula wa kibaraka wa Marekani ndani ya Syria na wanatekeleza uhalifu, uuaji na ukatili ndani ya Syria, walioko katika mamlaka yao na hata zaidi ya nguvu zao! Wanajua kwamba serikali hii inaendeshwa kwa msukumo wa Marekani, na kwamba kuimakinisha kiwakala ni kuiruhusu Marekani kuweza kupambana na majanga ya Mashariki ya Asia ndani ya Korea Kaskazini na China… Lau wangelikuwa na busara wangelifuata mtizamo mwengine kuliko huu, lakini Shetani anawadhibiti wafuasi wake.
Hata hivyo, wahalifu hawa, ima wamekuwa watatu au Marekani ipo nyuma yao, wasingeliweza kuwa na msimamo kwa uhalifu wao lau isingelikuwa kwa idadi ya makundi yanayowafuata, kwa mujibu wa sera ya kurambisha ya kupeana karoti na nifuate, iliyofungamanishwa na pesa chafu, vitisho na kuogofya, ingelikuwa si hivyo wahalifu hao wangelifeli.
Japo Hizb ut Tahrir imemaliza kila juhudi katika kujaribu kuleta muamko ndani ya makundi haya, kutokana na yanayoendelea, bado wanakimbilia njia hiyo kwa kisingizio cha kupata pesa na silaha, na kwamba Hizb ut Tahrir haiwezi kufanya hivyo bali wanawaunga mkono kwa ushauri… Wakaongezea kuwa ushauri hautoshi katika vita vya silaha! Hawakujua kwamba upanga wao una pande mbili, ni ngao katika mkono wa aliye na muamko na wenye utambuzi kutoka katika uovu wa adui wake, na zana yenye nguvu kumshinda adui wake…Lakini ngao hii ina makali wakati imo mkononi mwa aliye danganywa, akikimbilia msaada wa wahalifu, pande zake zilizovunjika zinawaua wafuasi wake mbele ya adui!
Twayaambia makundi haya yaliyopinga ushauri wetu na muamko; walisema kuwa haya hayato wasaidia katika vita, na wakachagua msaada wa pesa na silaha kutoka kwa wasaliti wa Waislamu, Waarabu, Waturuki na Wafursi, wengine wakaongezea kuwa watachukua hata kutoka kwa wahalifu wa Kimarekani na Kirusi. Wakifikiria kuwa kuchukua kwao pesa chafu kutawafanya kutositisha mapigano kwa ajili ya Ash-Sham… Twawaambia wote: Sasa mwaona matokeo ya vitendo vyenu na maneno yenu, mumetenganishwa na kufurushwa kutoka majumbani mwenu na watoto!
Hata hivyo, Ummah huu hautoshindwa, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mambo yatabadilika. Ummah huu umefikwa na majanga na zaidi ya hayo ni kutoka kwa vita vya Msalaba na Tatar, na ulinyanyuka na kuwang’oa na kuwa kileleni mwa dunia tena. Ni kweli utawala wa Uislamu ulikuwa umesimamishwa nyakati hizo, na kwamba Khilafah ilikuwepo licha ya udhaifu wake, bado Ummah ulikuwa na kiongozi aliyewaunganisha katika kupigana na adui, na kusimamisha ukweli na kuangamiza uongo, na kisha ukamshinda adui na kuinuka tena… Leo hakuna utawala wa Uislamu, hakuna Khilafah, hivyo basi, nani atakayewaunganisha Waislamu kupigana?
Hakika mtu anaweza kusema hivi, ni upi uchanganuzi wa hali halisi, lakini kazi ya kuregesha Khilafah inaendelea kwa nguvu, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Imekuwa hitajio kubwa kwa Waislamu ndani ya nchi zao, na wanatamani kwa maneno na vitendo, na wanafanya kazi kubadilisha siku nyeusi za 26, 27 na 28 za Rajab 1342H, ambazo zilikuwa jukwaa la ukhaini na uhalifu katika kuvunja Khilafah. Wanawania kuziondosha siku hizo nyeusi, na kuweka badala yake Khilafah tena, katika siku iliyochaguliwa na Mwenyezi Mungu, na ni jambo jepesi kwa Mwenyezi Mungu kulitekeleza hili, na kisha wale waliokosa, waliosaliti na kufanya uhalifu watajua hatima yao.
Enyi Waislamu: Hao watatu waliotekeleza uhalifu dhidi ya Syria, Makafir na wanafiq miongoni mwao hawatofurahi katika uhalifu na mauaji yao dhidi ya watu wa Ash-Sham na watu wake, lakini adhabu yao itakuja kutoka wasiko kutarajia. Ash-Sham imejaa mfano wao lakini bado imesimama, na wameangamia. Na hivi ndivyo itakavyokuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu (swt)

إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا “Hakika, Mwenyezi Mungu anatimiza amri yake. Mwenyezi Mungu kajaalia kila kitu na kipimo chake” [At-Talaq: 3].

Mwisho, huu ni ujumbe kwa majeshi ya Waislamu yaliyomo ndani ya kambi… Hali yenu inashangaza, mkitumwa na watawala mkawaue Waislamu munatwii, na Waislamu wanapowalilia kutaka msaada wenu, mnasita na kuwaangusha na kubakia kimya mfano wa kimya cha kaburi. Na mnatoa hoja kuwa mnatwii wakuu wenu, ilhali hii ndiyo barabara inayowapelekea katika hizaya duniani na adhabu chungu Yaumul Qiyama, na hao (watawala) hawatowasaidia siku hiyo, lau mtazungumza mkijitetea:

(يَوْمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ يَقُولُونَ يَا لَيْتَنَا أَطَعْنَا اللَّهَ وَأَطَعْنَا الرَّسُولَا * وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا) “Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto. Watasema: Laiti tungeli mtii Mwenyezi Mungu na tungeli mtii Mtume! Na watasema: Mola wetu Mlezi: Hakika sisi tuliwatii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia.” [Al-Ahzab: 66-67]

Hata hivyo, bado munao muda wakuweza kuyabadili muliyo yafanya, kwa kuinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu, kuurudisha utawala wa Uislamu katika ardhi, na kukata mahusiano na wadhalilishaji na wanafiki, na Makafiri wakoloni. Hili liwe kafara kwa madhambi yenu, na Mwenyezi Mungu ni mkweli alisema:

وَإِنِّي لَغَفَّارٌ لِمَنْ تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا ثُمَّ اهْتَدَى “Na hakika Mimi ni Mwingi wa Kusamehe kwa anaye tubia, na akaamini, na akatenda mema, tena akaongoka.” [Ta-Ha: 82].

Kwa kuongezea, twataka kusema kwa Waislamu jumla, musikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu, Ash-Sham itabakia kuwa Ash-Sham, nyumba tukufu ya Uislamu. Ahmad katika simulizi yake alieleza kutoka kwa Jubair Bin Nafir, kwamba Salma bin Nufail, aliwaambia kuwa alikwenda kwa Mtume (saw), na Mtume (saw) akamwambia

«أَلَا إِنَّ عُقْرَ دَارِ الْمُؤْمِنِينَ الشَّامُ» “Hakika nyumba ya waumini ni Ash-Sham”

Katika simulizi nyingine ya Na’im Bin Hammad kuhusiana na mzozo, kutoka kwa Katheer Bin Murrah, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema:

«عُقْرُ دَارِ الْإِسْلَامِ بِالشَّامِ» “Ash-Sham ni nyumba ya Uislamu.”

Tukimalizia, Hizb ut Tahrir, muongozaji asiyedanganya watu wake, inaendelea na kazi yake pamoja na kupitia Ummah, na iko imara katika ukweli, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Hayakubadilika na haitobadilisha mawazo na njia yake, maanake ni ya ukweli.

فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَال “Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu?” [Yunus: 32]

Chama kina nguvu kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na Dini, kinamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mwenye Hekima, kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu itimizwe kwa mikono yake.

وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ “Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa kabla yao," [An-Nur: 55].

Na bishara ya Mtume (saw) itatimizwa na chama na watu wake, na Waislamu wote. Abu Daoud At-Tialsi asimulia kutoka kwa Hudhayfah kwamba alisema kwamba: Mtume (saw) alisema:

«... ثُمَّ تَكُونُ جَبْرِيَّةً، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»، ثُمَّ سَكَتَ “kisha kutakuwepo na ukandamizaji kwa muda atakao Mwenyezi Mungu, kisha atauondosha Atakapotaka, na kisha kutakuwepo na Khilafah kwa njia ya Utume” na kisha akabakia kimya” Na Ahmad akatoa kutoka katika mfano huo: Mtume (saw) alisema:

«... ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ نُبُوَّةٍ» ثُمَّ سَكَتَ “kisha kutakuwepo ufalme wa ukandamizaji kwa muda atakao Mwenyezi Mungu, kisha atauondosha Atakapotaka, na kisha kutakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume” na kisha akabakia kimya”

Hizb ina uhakika wa ushindi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, si tu kwa mitume na manabii, bali pia kwa waumini wa kweli, si tu Akhera, bali pia hapa duniani,


إِنَّا لَنَنْصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watakapo simama Mashahidi,” [Ghafir: 51]. Siku hiyo, waumini watafurahi kwa ushindi wa Mwenyezi Mungu, na wahalifu watapata hizaya hapa duniani, na adhabu chungu Akhera. Mwenyezi Mungu ni muweza katika kulipiza [Al-Muntaqim], Ni Mwenye Nguvu na Hekima


H. 18 Rajab 1439
M. : Alhamisi, 05 Aprili 2018

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu