Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Tangazo la Trump Huku Watawala Wakikosa Kuchukua Hatua Yoyote Mbele Yake Ni Kofi Zito Migongoni Mwao Amewavua Hata Sitara iliyo Wafinika Uchi Wao

(Imetafsiriwa)

Usiku wa leo tarehe 6-7/12/2017 Trump ametangaza Al-Quds (Jerusalem) kuwa mji mkuu wa dola ya Kiyahudi: “Katika barua kutoka ikulu ya White House mnamo Jumatano, raisi wa Amerika Donald Trump aliitambua Jerusalem kama mji mkuu wa “Israel” na kuamuru Wizara ya Kigeni ya Amerika kufanya matayarisho ya kuhamisha ubalozi wake kutoka mji wa Tel Aviv mpaka Jerusalem, na kuanza kandarasi na wajenzi… Trump akaongezea: “Mimi naitimiza ahadi ya kuitambua Al-Quds kuwa mji mkuu wa “Israel”…” (al-Arabiya.net 6/12/2017)… Cha kustaajabisha zaidi, kabla ya tangazo hili, watawala wengi katika biladi za Kiislamu, waliokuwa wakitoa vitisho juu ya Al-Quds na Msikiti wa al-Aqsa, mfano wa Salman, Abbas, Abdullah, as-Sisi, na (Muhammad) VI, walijulishwa na Trump kuwa atatangaza utambuzi wake huu katika hotuba yake baada ya masaa kadhaa… ilhali wote hawa, walibakia kimya cha mtungi mithili ya wafu kuzimu, au hata zaidi ya hivyo!

Hakika, Trump katili/dhalimu mjinga ametekeleza, adui wa Uislamu na Waislamu; ametimiza ahadi yake kwa Mayahudi. Hakika ukafiri ni mila (dini) moja, na haishangazi kwa makafiri kusimama kwa umoja.
Lakini, cha kustaajabisha ni kuwa watawala katika biladi za Waislamu watawafuata pasi na kujali kuwa miongoni mwao. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ مِنْكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ)
“Enyi mulio amini! Musiwafanye Mayahudi na Manasara kuwa vipenzi. Wao ni vipenzi wao kwa wao. Na yeyote atakaye wafanya vipenzi miongoni mwenu, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu” [Al-Ma’ida: 51]

Enyi Waislamu:
Amerika iliitambua dola ya Kiyahudi tangu mnamo 1948 na kuiunga mkono baada ya hapo, watawala hawa wakanyamazia kimya, na hata kujenga urafiki na Amerika! Walifedheheshwa na kugubikwa na udhalilifu.
Dola hii ya Kiyahudi iliendelea na uvamizi wake wa Palestina yote na Al-Quds yote iliyosalia mnamo 1967, kwa uvamizi huu waliungwa mkono vilevile na Amerika, huku watawala hawa wakinyamazia kimya, na hata kuichukulia Amerika kama rafiki muaminifu na kuifanya mpatanishi wa suluhu na serikali ya Kiyahudi. Walifedheheshwa na kugubikwa na udhalilifu.

Walikuwa wanapotosha na kuhadaa kuwa Amerika ingeishinikiza dola ya Kiyahudi kuwapatia kitu ili kuasisi dola kwacho, hata kama itanyimwa nguvu za kijeshi, na Jerusalem Mashariki ingekuwa mji mkuu wake… Hivyo basi walidunishwa kwa udanganyifu huu. Hakika, hawakumuhadaa yeyote ila nafsi zao, kwa kukosa macho ya kuona mbele… Walifedheheshwa na kugubikwa na udhalilifu.
Na sasa Amerika, kwa ulimi wa Trump inatangaza utambuzi wake kuwa Jerusalem, ambayo ni ardhi ya Isra na Mi’raj, Qibla cha kwanza cha Waislamu, na ambako msikiti wa tatu kati ya misikiti mitatu ambayo Muislamu hufunga safari kuizuru, inatangazwa mashariki yake na magharibi yake kuwa mji mkuu wa serikali ya Kiyahudi… Trump aliwasiliana na watawala hawa kabla ya tangazo hili pasi na kuupa uzito wala kuutilia maanani usemi wao tasa kuwa wanaithamini Jerusalem. Aliwapigia simu kabla ya tangazo lake, na kuongezea katika fedheha na idhlali, katika hotuba ya utambuzi wake alotangaza kuwa atamtuma makamu wa raisi kwenda kubadilishana tabasamu na watawala hao. “Trump ametangaza kuwa makamu wake wa raisi, Mike Pence, atawasili eneo la Mashariki ya Kati siku zijazo,,,” (alarabiya.net 6/12/2017). Na kwa hivyo ni kweli ule msemo usemao kuwa: “Yeyote ambaye ni rahisi kumdhalilisha… jeraha litakuwa na uchungu gani ikiwa uchungu wenyewe umekufa.”

Enyi Waislamu: Je, wapo watu wawili wenye akili timamu watakao hitilafiana juu ya vipi kuiokoa Palestina kutoka katika makucha ya magengi ya Kiyahudi? Je, wapo watu wawili wenye akili timamu watakao hitilafiana juu ya vipi kupambana na Amerika na wengine mfano wake, nchi zinazounga Mayahudi? Je uokovu wa Palestina haupo katika kuharakisha majeshi kupigana na serikali hiyo na kuivunja mgongo wake kwa mikono yenu, kwani Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ) “Piganeni nao, Mwenyezi Mungu atawaadhibu kwa mikono yenu, na awafedhehi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini” [At-Tawba: 14]

Je, uokovu wa Palestina haupo katika kutabanni hali halisi ya kivita na dola zinazounga mkono serikali ya Kiyahudi? Je, si katika maamrisho ya Mwenyezi Mungu Ta’ala, Wenye hekima, kuwafurusha wavamizi katika ardhi ya Kiislamu waliowafurusha watu wake?

(وَأَخْرِجُوهُمْ مِنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ) “…na muwatoe popote walipo kutoeni” [Al-Baqara: 191].

Je, hii si amri ya Mwenyezi Mungu dhidi ya nchi zinazounga mkono Mayahudi walioivamia ardhi ya Kiislamu na kuwafurusha watu wake?

(إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ) “Hakika Mwenyezi Mungu anawakataza kuwafanya vipenzi wale wanaowapiga vita katika dini, na wakawatoa katika majumba yenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na anaye wafanya hao kuwa vipenzi basi hao ndio madhalimu” [Al-Mumtahina: 9]

Je, huu sio ukweli unaohisiwa na kila mwenye moyo au mwenye kusikia na kushuhudia?
Enyi Waislamu, Enyi Majeshi katika biladi za Waislamu: Kimya cha watawala hawa juu ya uvamizi wa Kiyahudi kwa sehemu kubwa ya Palestina mnamo 1948 na kutoharakisha majeshi kuikomboa Palestina yote kutoka katika makucha ya Mayahudi, ni kosa kubwa na ovu zaidi… Na kunyamzia kwa hawa watawala juu ya unyakuzi wa sehemu iliobaki ya Palestina mwaja 1967 na kutoharakisha majeshi kuikomboa Palestina yote kutoka kwa magengi ya kiyahudi ni kosa na ovu kubwa zaidi… Na kufeli kuifanya hali halisi ya kivita dhidi ya nchi zinazounga mkono serikali hii ya Kiyahudi ni uhalifu vilevile… Urafiki na utiifu kwa nchi hizo ni khiana kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini.

Trump amewafichua watawala hawa; amewapokonya sitara ya mwisho iliyokuwa ikiwafinika uchi wao kwa kimya chao juu ya hotuba yake ovu. Sasa vipi basi mamlaka ya biladi za Waislamu yatabakia mikononi mwao? Ni jukumu la wanajeshi kuharakisha na kuwang’oa watawala hawa Ruwaybidha (wazembe) kwa miguu yao ikiwa hawatapigana dhidi ya maadui wavamizi wa ardhi hii tukufu na hawatatabanni hali halisi ya kivita dhidi ya zile nchi zinazounga mkono serikali hiyo… Kipaumbele cha Waislamu na majeshi yao inapaswa iwe kuwapindua watawala hawa na kuasisi dola ya Kiislamu: Khilafah Rashidah. Hivyo basi dola kuu za makafiri wakoloni hawatasubutu tena kutia mguu wao katika sehemu yoyote ya ardhi za Waislamu wala kuwadhuru, wacha serikali hii katili ya Kiyahudi ambayo imepigwa na idhlali na fedheha, kwani Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ) “Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na kisha hawatanusuriwa” [Al-i-Imran: 111].

Enyi Waislamu, Enyi Majeshi katika biladi za Waislamu:
Hizb ut Tahrir, kiongozi muadilifu asiye wadanganya watu wake inawaonya kutonyamaza kimya juu ya uhalifu wa watawala hawa na khiana zao, na inawaonya kutohadaiwa na upotofu wao na urongo wao baada ya siku hii. Na jueni kwamba matokeo ya kimya hiki hayatakoma tu kwa Palestina bali mbele zaidi ya Palestina.

Hakuna udhuru uliobakia, au hata mithili ya udhuru kwa wale wenye kutii amri za watawala hawa makhaini duni thamani, wanaowazuia kuiondoa serikali ya Kiyahudi na kuiregesha Ardhi Takatifu katika boma la Uislamu. Utiifu kwao katika hali hii utawaletea fedheha hapa duniani na adhabu kali kesho Akhera. Na wala hakutawanufaisha kusema baadhi ya wenzenu kuwa walikuwa tu wakiwatii waheshimiwa wao, kwani matokeo ya maneno hayo yaliyopotoka yatakuwa ni matokeo maovu pekee, kwani Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا) “Na watasema: Mola wetu! Hakika sisi tuliwatii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia” [Al-Ahzab: 67].

Hakika, kuwatii watawala hawa masafihi kunapelekea kwenye upotofu na fedheha hapa duniani na adahbu uchungu kesho Akhera. Hawa ni watawala waliojitolea katika urongo, khiana, upotevu na upotofu. Kutoka kwa Jabir ibn ‘AbdMwenyezi Mungu, Mtume (saw) alimwambia Ka’ab ibn ‘Ujrah,

«أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ لِكَعْبِ بْنِ عُجْرَةَ: أَعَاذَكَ اللَّهُ مِنْ إِمَارَةِ السُّفَهَاءِ. قَالَ: وَمَا إِمَارَةُ السُّفَهَاءِ؟ قَالَ: أُمَرَاءُ يَكُونُونَ بَعْدِي لَا يَقْتَدُونَ بِهَدْيِي وَلَا يَسْتَنُّونَ بِسُنَّتِي، فَمَنْ صَدَّقَهُمْ بِكَذِبِهِمْ وَأَعَانَنَهُمْ عَلَى ظُلْمِهِمْ فَأُولَئِكَ لَيْسُوا مِنِّي وَلَسْتُ مِنْهُمْ وَلَا يَرِدُوا عَلَيَّ حَوْضِي، وَمَنْ لَمْ يُصَدِّقْهُمْ بِكَذِبِهِمْ وَلَمْ يُعِنْهُمْ عَلَى ظُلْمِهِمْ فَأُولَئِكَ مِنِّي وَأَنَا مِنْهُمْ وَسَيَرِدُوا عَلَيَّ حَوْضِي» “Hakika Mtume (saw) alimwambia Ka’b bin ‘Ujrah: “Namuomba Mwenyezi Mungu akulinde kutokana na utawala wa masafihi).” Akauliza: na ni upi utawala wa masafihi? Akasema: ni watawala watakaokuja baada yangu wasiofuata uongofu wangu wala Sunnah zangu, yeyote atakaye wasadikisha urongo wao na kuwasaidia katika dhulma zao basi hao si katika mimi wala mimi si katika hao, wala hawatokunywa katika birika langu peponi. Na yeyote ambaye hatawasadikisha urongo wao na hatawasaidia katika dhulma zao basi hao ni katika mimi na mimi ni katika hao na watakunywa katika birika langu peponi.” (Ahmad)

Hivyo basi, Enyi Waislamu fanyeni bidi katika kung’oa utawala wao, na kusimamisha utawala wa Uislamu, mutapata ushindi wa maisha yote mawili, maisha haya ya duniani na maisha ya kesho Akhera, kwani Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ) “Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusra ya Mwenyezi Mungu, humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

H. 19 Rabi' I 1439
M. : Alhamisi, 07 Disemba 2017

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu