Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Wale Wote Wanaotaka Uhuru kutokana na Marekani, Lazima Wafanye Kazi ya Kusimamisha Tena Khilafah kwa Njia ya Utume

(Imetafsiriwa)

Mjadala wa nchi nzima, kutoka kwa raia hadi kwa watu walio mamlakani, umepanuka kutoka kwa kuanguka kwa Rupia mbele ya dolari ya Kimarekani, na utumiaji wa anga ya Pakistan kwa droni za Amerika, hadi jinsi Pakistan inaweza kuwa huru kikweli, wakati tunabeba hasara kubwa kwa uchumi wetu, elimu, afya na usalama. Visingizio vya muda mrefu na madai ya uongozi wa sasa wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan, unaotawala kinyume na Uislamu, sasa yamefichuliwa. Umesema kwa miongo kadhaa kwamba lazima tuwatii Waamerika, kwa sababu hatuwezi kuishi, bila dolari zao. Kwa hivyo uliunga mkono uvamizi wa Amerika kuanzia 2001, kisha ukaitelekeza Kashmir Iliyokaliwa kimabavu kutoka 2003, na kufikia kilele cha kuisalimisha Kashmir Iliyokaliwa kimabavu kwa Modi, mnamo Agosti 2019. Kwa miaka mingi, hadi sasa, umetoa nafasi ya anga ya Amerika, juu ya mitambo yetu nyeti ya kijeshi, huku wanachochea ukosefu wa utulivu kwenye Mstari wa Durand. Kwa hivyo umeungana na Waamerika kwa miongo kadhaa, ukituchoma na maridhiano kwa usalama wetu na uchumi wetu. Hali yetu imekuwa mbaya zaidi mfululizo, huku uongozi huu ukisisitiza kwamba hatuna chaguo jengine.

Hata hivyo, kiuhalisia, ni uongozi wa Pakistan ambao wenyewe ndio kwanza unahusika kwa utegemezi wa dolari. Hauanzishi viwanda vizito, ili tuweze kutengeneza mashini na injini zetu wenyewe, na hivyo kumaliza haja ya uagizaji wa gharama kubwa. Hausimamishi Khilafah, kuunganisha ardhi za Waislamu zenye utajiri wa nishati, ili tusihitaji uagizaji wa mafuta ghali kutoka nje. Unaifungamanisha sarafu na biashara yetu na dolari, badala ya sarafu ya dhahabu na fedha ya Uislamu. Kwa hiyo, inatuangushia nyundo miguuni mwetu na kisha kusema kwamba kuchechemea ni lazima kwetu! Je, si wakati haujawadia wa sisi kusonga, au angalau kufikiria kwa kina, kuweka uongozi mpya unaotawala kwa mujibu wa Quran Tukufu na Sunnah za Mtume? Kwa hakika, inajulikana kwetu sote kwamba Pakistan, kama Ulimwengu wote wa Kiislamu, imebarikiwa na Mwenyezi Mungu (swt) kwa kila aina ya hazina, ikiwemo nishati, madini, ardhi ya kilimo na idadi ya vijana. Yote ambayo itachukua ili kuboresha hali yetu ni uongozi ambao ni wa kweli kwetu na Dini yetu tukufu. Hata hivyo, bila hili, tunaweza tu kutarajia maangamivu.

Kwa hakika, baada ya miongo kadhaa ya mikopo ya kiuchumi kutoka, na makubaliano na, taasisi za kikoloni, IMF na Benki ya Dunia, ni nini uongozi wa Pakistan umeleta kwa ajili yetu? Umegeuza uchumi wetu kuwa kitega uchumi, kwa wale wanao amiliana na riba. Mapato mengi ya kodi ya Pakistan sasa yanatumika kwa riba, huku deni la Pakistan likipanda, kutokana na dhulma ya riba. Mnamo 1971, deni la Pakistan lilikuwa rupia bilioni 30, lakini kutoka 2021 limeongezeka zaidi ya bilioni 40,000. Hivyo, wanaokopesha kwa riba, haswa taasisi za kimataifa za kikoloni, wanatukamua damu, kupitia uovu wa riba. Ilhali, uongozi wa sasa si chochote ila ni vibaraka wa Marekani, wanaojali tu msaada wake kwa viti vyao vya enzi, huku wakitangaza vita na Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw), kupitia kudumu katika dhambi kubwa la riba.

Zaidi ya hayo, kuongezeka kwa deni kunakuja na matakwa ya wakoloni yanayolemaza, ambayo uongozi wa Pakistan huyatekeleza, bila kujali mateso yetu. Unabinafsisha rasilimali zetu za nishati na madini, na kuelekeza mapato makubwa kutoka kwa hazina ya serikali hadi kwenye mifuko ya kampuni za kibinafsi. Inaongeza ushuru, na kufyeka ruzuku, unalemaza viwanda vyetu na kilimo. Unasimamia kudhoofika kwa mara kwa mara kwa Rupia, ambayo inatuzamisha katika dhoruba isiyopungua ya mfumko wa bei. Kiuchumi, kwa uwazi kabisa, kuna mgogoro wa uongozi, ambao utatatuliwa tu na mfumo wa uchumi wa Kiislamu, unaopaswa kutabikishwa na Khilafah Rashida.

Kuhusu muungano wa kijeshi na Marekani, umekuwa janga kwa Pakistan. Silaha za Pakistan zina utegemezi hatari kwa usambazaji wa Amerika. Vibaraka wa Marekani wanatambuliwa na kuajiriwa kupitia mafunzo ya kijeshi ya kigeni. Siri za kijeshi zinafichuliwa kupitia mawasiliano ya karibu ya kijeshi. Muungano mzima umeegemea upande wa dola kuu ya kikoloni, Marekani, na kusababisha unyonyaji wa jeshi, ujasusi na anga ya Pakistan, kwa malengo ya kieneo ya Marekani. Haitoshi kuibadilisha Marekani, dola kuu ya kikoloni, kwa dola nyengine kuu ya kikoloni, Urusi au China, kwa maana muumini hapaswi kung’atwa katika tundu moja mara mbili! Pia haitoshi kulalamikia usaliti wa mara kwa mara wa Marekani katika vita vya 1965, vita vya 1971 na sasa, inapoinyanyua India kama kiongozi wa kanda.

Huku Uislamu ukitoa ruwaza pana ya kijeshi ya kuzikomboa ardhi zetu zinazokaliwa kwa mabavu na kufungua ardhi mpya kwa rehema na uadilifu wa Uislamu, uongozi wa sasa umehakikisha utengano wetu na kudhoofika mbele ya maadui zetu, kwa kushikamana na utaifa, dola ya kitaifa na mfumo wa kimataifa wa Kimagharibi. Jeshi letu na ujasusi zimenyimwa dori yake ya kweli, zimepunguzwa kuwa chombo cha kudhibiti viti vya enzi vinavyotikisika vya uongozi fisadi, mbele ya hasira yetu inayoongezeka. Kwa hakika, ni Khilafah pekee ndiyo itakayokuwa na sera huru ya mambo ya nje na ya ndani, yenye msingi wa Uislamu, na kukomesha udhibiti wa Waamerika, milele. Ni Khilafah ndiyo itakayouimarisha Ulimwengu wa Kiislamu, kwa kuunganisha kama dola moja. Itamaliza muungano na dola za maadui, kama vile Marekani, na kuamiliana nao kwa misingi ya vita. Itajenga viwanda vizito, ili kukomesha utegemezi wa silaha za kigeni. Khilafah itamaliza ushirikiano na mawasiliano nyeti na maadui waliothibitishwa wa Uislamu na Waislamu.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Hebu na tufanye kazi pamoja na Hizb ut Tahrir, kuanzia sasa, kusimamisha tena Khilafah Rashida, ili hatimaye tupate watawala wanaotutawala, kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) ameahidi,

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الأَرْضِ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi.” [Surah an-Noor 24:55]. Hakika kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume kutakuja tu kupitia Nusra ya Mwenyezi Mungu (swt), ambayo itapewa wale walioamini na kuifanyia kazi Dini yake. Hivyo basi, fanyeni kazi na Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Dini ya Mwenyezi Mungu (swt), kama katiba na dola. Kwa yakini, hakutakuwa na mabadiliko mpaka Khilafah kwa Njia ya Utume isimamishwe tena, kupitia harakati inayoongozwa na Hizb ut Tahrir.

Enyi Waislamu wa Majeshi ya Pakistan! Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kibinafsi alitaka Nusra kwa ajili ya Dini hii kutoka watu wa vita, akiomba, «فَهَلْ عِنْدَ قَوْمِكَ مِنْ مَنَعَةٍ؟»  “Je, watu wako wana nguvu?” Kwa hiyo, baada ya kiapo (Bay’ah) cha Pili cha Aqabah cha Nusrah, Yathrib iliyokuwa na matatizo ikawa Al-Madinah Al-Munawwarah yenye nguvu, dola ambayo kisha ikaeneza Dawah ya Uislamu hadi kwa dola kuu za ulimwengu za wakati huo, kama utangulizi wa Jihad, kuondoa vikwazo vya kimada katika njia ya halaiki ya watu, ambao kwa hiari yao walisilimu. Toeni Nusrah yenu sasa kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Nusrah ni jukumu lenu la Kishariah, enyi wanajeshi wa Mwenyezi Mungu (swt), hivyo itoeni sasa kwa Hizb ut Tahrir.

H. 14 Muharram 1444
M. : Ijumaa, 12 Agosti 2022

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu