Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mabadiliko Yanayohitajiwa na Pakistan ni Siasa Mpya na Dola Mpya kwa Msingi wa Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt); Khilafah kwa Njia ya Utume

(Imetafsiriwa)

Katika miaka michache iliyopita mateso ya Waislamu wa Pakistan yameongezeka mara kwa mara, kutokana na matatizo ya kiuchumi. Zaidi ya hayo, kipindi hicho hicho kimeshuhudia kuongezeka kwa machafuko ya kisiasa na ukosefu wa utulivu, na kushindwa kwa utawala nchini Pakistan. Serikali na taasisi zake hazipo, hazina hamu wala hazijali, katika kutatua matatizo yanayowakabili wananchi, na kusababisha maafa zaidi kwa wananchi.

Kupooza kisiasa na ukosefu wa utulivu ambao Pakistan inashuhudia leo, ni matokeo ya moja kwa moja ya siasa zilizofeli, ambazo tabaka tawala la kisiasa inazifanya. Kwa kuchochewa na fahamu ya Magharibi ya siasa, siasa zilizotabanniwa na PTI, PML-N, PPP, na vyama vingine vya kisiasa, zinazunguka pambizoni mwa kutafuta madaraka, kwa gharama yoyote, na pia kupata maslahi ya wanasiasa tawala, majenerali na idara ya juu ya mahakama. Kwa jina la kauli mbiu kama vile ukuu wa kiraia, utawala wa sheria na utawala wa watu, siasa hizi zimejikita pambizoni mwa wanasiasa, majenerali na majaji kupigana wao kwa wao kwa ajili ya mamlaka zaidi, na mgao wa rasilimali, ambayo wanaweza kujitengea wenyewe. Hii ni siasa ya kufanya mapatano, kutumikia maslahi ya Magharibi na taasisi za kimataifa, kupitisha sheria zinazowaongezea muda majenerali, wanasiasa na majaji na kuwatuza wafuasi waaminifu wa kisiasa na wafadhili wa vyama vya kisiasa. Hakuna chengine isipokuwa kukataliwa kikamilifu kwa siasa za sasa, ambazo msingi wake ni kutafuta madaraka, na kutabanni siasa mpya zilizojengwa juu ya msingi wa Uislamu, kutamaliza masaibu ya Waislamu wa Pakistan.

Pakistan inahitaji siasa mpya ambayo inalenga kuchunga mambo ya watu. Siasa ambayo imeegemezwa katika kutabikisha Shariah ya Kiislamu, ambapo watawala hutabikisha hukmu zilizovuliwa kutoka katika Qur'an Tukufu na Sunnah za Mtume, na ambapo Umma unamhisabu mtawala kwa uzembe wake katika kutabikisha Uislamu. Siasa inayoona maslahi ya Ummah kama yalivyofafanuliwa na Shariah ya Kiislamu, na ambayo inaulinda Ummah kutokana na hila na mipango ya wakoloni makafiri. Siasa ambayo imejikita katika kuunganisha rasilimali za kiuchumi za Ummah, zitumike kwa Waislamu wote. Siasa mpya inayotaka kuunganisha nguvu za kijeshi za Ummah, kuikomboa Palestina na Kashmir zinazokaliwa kwa mabavu. Siasa ambayo inalenga katika kubeba Ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu mzima. Siasa inayozalisha watawala ambao ni walinzi wanaojali wa Ummah.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«كُلُّكُمْ رَاعٍ، وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، وَالأَمِيرُ رَاعٍ، وَالرَّجُلُ رَاعٍ عَلَى أَهْلِ بَيْتِهِ،وَالْمَرْأَةُ رَاعِيَةٌ عَلَى بَيْتِ زَوْجِهَا وَوَلَدِهِ، فَكُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»‏

“Nyote ni wachungaji na nyote mutaulizwa kuhusu mulivyovichunga. Mtawala ni mchungaji na mwanamume ni mchungaji wa familia yake; mwanamke ni mchungaji kwa nyumba ya mumewe na watoto wake; hivyo basi nyinyi nyote ni wachungaji na nyote mutaulizwa kuhusu mulivyovichunga.” (Bukhari)

Pamoja na siasa mpya, Pakistan inahitaji dola mpya. Kutabanni mfumo wa kisiasa wa Kimagharibi wa utawala, demokrasia, dola ya sasa inaruhusu wanasiasa kutunga sheria ili kulinda maslahi yao wenyewe, pamoja na maslahi ya mabwana zao wa Magharibi. Maslahi yenye nguvu ya kibiashara hushawishi mchakato wa kutunga sheria, na idara za serikali, kutabanni sheria na sera, ambazo zinafadhili mabepari. Muundo wa serikali ya kifederali yenye ngazi tatu hulemaza uamuzi na uundaji wa sera. Mikoa na serikali za mitaa zinazoshikiliwa na vyama tofauti vya kisiasa hutafuta kuhujumiana wao kwa wao na serikali ya shirikisho. Mgawanyiko huu wa madaraka pia unawaruhusu watawala, katika ngazi zote za serikali, kujiondolea jukumu la kusimamia mambo ya Ummah.

Rasilimali za Punjab hazipelekwi kwa wakimbizi wa mafuriko wa Sindh, ilhali serikali ya kifederali haiwasaidii wakimbizi wa mafuriko wa Sindh, Balochistan na KPK kwa sababu chama tawala cha PML-N hakiwaoni kama wapiga kura wake wakuu. Uchaguzi kila baada ya miaka mitano, na haki ya kuvunja serikali na mabunge, imezua hali ya kutokuwa na utulivu wa kisiasa nchini Pakistan, ambayo inalemaza serikali. Kwa upande wa nje, dola ya Pakistan inategemea mara kwa mara mikopo kutoka kwa dola za kigeni na taasisi za fedha za kimataifa, ambazo zinaweka masharti magumu ya kiuchumi na kisiasa na kuifanya sera ya kiuchumi na sera nje ya Pakistan kuwa chini ya unyenyekevu wa dola za kigeni.

Katika dola mpya, Khilafah Rashida ya Pili juu ya Njia ya Utume, Ummah humchagua Khalifa kwa maisha yote na kumpa Bayah, kwa sharti kwamba atatabikisha Shariah ya Kiislamu, na kutekeleza Jihad, kwa badali ya utiifu wa Ummah. Khalifa huondolewa ikiwa Kufr Buwah (Ukafiri wa Wazi) utadhihirika katika utabikishaji wake. Hili huleta utulivu wa kisiasa na kumruhusu Khalifa kutabanni sera za muda mrefu kwa ajili ya kuboresha Ummah. Khalifa ndiye anayeteua Magavana wa majimbo na Aammil (meya) wa miji. Wanaripoti kwa Khalifa na Khalifa anawajibika kwa Ummah kwa utendakazi wao. Raia wote wa dola ya Khilafah wamehakikishiwa haki kwa mujibu wa Shariah ya Kiislamu na si kwa misingi ya rangi, kabila au uwezo wao wa kisiasa. Khalifa hawezi kutunga sheria. Amefungwa na Shariah ya Kiislamu na ni lazima atabikishe sheria zinazotokana na Quran Tukufu na Sunnah za Mtume. Uislamu unawaharamisha Waislamu kujisalimisha kwa mamlaka ya Kikafiri. Hairuhusiwi kwa dola ya Khilafah kuwa sehemu ya taasisi za kimataifa, ziwe za kisiasa au za kifedha, ambapo makafiri wana mamlaka juu ya Waislamu. Na Uislamu umeharamisha kabisa Waislamu kuchukua msaada kutoka kwa makafiri katika mambo ya vita. Hivyo dola mpya, Khilafah Rashida ya Pili, itatutawala kwa msingi wa Wahyi, na kutabikisha sheria na sera zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt) ndani ya Quran Tukufu na Sunnah za Mtume. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(وَأَنِ احكُم بَينَهُم بِما أَنزَلَ اللَّهُ وَلا تَتَّبِع أَهواءَهُم وَاحذَرهُم أَن يَفتِنوكَ عَن بَعضِ ما أَنزَلَ اللَّهُ إِلَيكَ)

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Surah Al-Ma’idah 5:49].

Khilafah ni muundo wa kisiasa wa Uislamu. Hairuhusiwi kwa Ummah kuwa bila ya Khalifa, kwa zaidi ya michana tatu na masiku matatu. Ni faradhi kwa Waislamu kumteua Khalifah, kumpa Bayah ya utiifu kwake, na kumsaidia katika utabikishaji wa Shariah ya Kiislamu na kutekeleza Jihad ili kueneza Ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu mzima. Mtume (saw) amesema,

«كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمُ الأَنْبِيَاءُ، كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لاَ نَبِيَّ بَعْدِي، وَسَيَكُونُ خُلَفَاءُ فَيَكْثُرُونَ‏.‏ قَالُوا فَمَا تَأْمُرُنَا قَالَ فُوا بِبَيْعَةِ الأَوَّلِ فَالأَوَّلِ، أَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ، فَإِنَّ اللَّهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ»‏

‘“Walikuwa Banu Israil siasa zao zikiendeshwa na Mitume; Kila Mtume anapokufa, mwengine alichukua nafasi yake. Na hakika yake hakutakuwa na Mtume baada yangu, lakini kutakuwa na Makhalifa ambao watakuwa wengi. Watu wakauliza, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Unatuamuru (tufanye) nini?” Akasema, “Mpeni ahadi ya utiifu (bay’ah) yule ambaye atapewa ahadi ya utii kwanza. Wapeni haki zao, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza juu ya usimamizi wao.”’‏ (Bukhari)

Enyi Maafisa wa Vikosi vya Wanajeshi vya Pakistan!

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alileta ruwaza mpya kwa wanadamu, inayotokana na Wahyi kutoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. Yeye (saw) alianzisha siasa mpya, dola mpya na mujtamaa mpya, ambao uling'aa kama mwanga wa nuru kwa ulimwengu wote. Hata hivyo, yeye (saw) alisaidiwa katika utume wake na watu wenye nguvu, silaha na chuma, watu waliobarikiwa wa Answar (ra), ambao walitumia uwezo wao kutoa Nusrah kwa ajili ya kusimamishwa kwa Dola ya kwanza ya Kiislamu.

Leo, jukumu hili la Kisharia liko juu ya mabega yenu. Jitokezeni na Usaidizi wako wa Nguvu (Nusrah), kwa ajili ya ruwaza mpya kwa Ulimwengu wa Kiislamu. Toeni Bay’ah yenu ya Nusrah ya kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume (saw), na mupate radhi za Mola wenu Mlezi, na kufaulu katika dunia hii na Akhera.

H. 29 Jumada I 1444
M. : Ijumaa, 23 Disemba 2022

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu