Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ujumbe kwa Waislamu nchini Tanzania katika Siku Kuu ya Idd Al-Fitr
(Imetafsiriwa)

Mwezi mtukufu wa Ramadhan umepita, na hapa tumefika katika siku iliyobarikiwa ya Idd Al-Fitr, na sisi katika Hizb ut Tahrir / Tanzania tunawapongeza Waislamu wa Tanzania na Ummah mzima wa Kiislamu kwa ujio wa Idd Al-Fitr, tukimuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba iwe ni Idd njema na ya furaha.

Saumu yetu ya mwezi wa Ramadhan imeambatana na uhalisia wa kutisha na wa giza, kwani umasikini na njaa vimeongezeka, na maovu yameenea, na pamoja na hayo, Ummah wa Kiislamu umeanza kufunga kwa shauku, taqwa, subira na yakini, huu ni ushahidi mzuri, na tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atukubalie saumu yetu na swala yetu ya qiyam, na atusamehe mapungufu na makosa yetu.

Enyi Waislamu: Ramadhan imepita kwa mara nyengine tena, na Waislamu hawana Khalifa wa kusimamia mambo yao, kuhifadhi ibada zao, kulinda ardhi zao, kutetea heshima zao, na kunusuru matukufu yao. Mayahudi waliushambulia Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa na watu wa Palestina, na hakuna mwokozi. China iliwakamata Waislamu Turkistan Mashariki, kuwatesa na kuwaweka kizuizini, na kuwalazimisha kula wakati wa Ramadhan, na hakuna msaidizi. Misiba ni mingi katika nchi za Waislamu, na hakuna njia ya kutokea.

Enyi Waislamu: Mumesifiwa katika mwezi wa Ramadhan kwa sifa kubwa ya sifa za Waislamu, ambayo ni kushikamana na Halali na Haramu. Mumetupa matamanio yenu nyuma ya migongo yenu, na mumekimbilia kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa kutaka radhi zake. Jueni kwamba haya munatakikana kwenu katika Ramadhan na katika miezi isiyokuwa Ramadhan, na ni lazima katika swala na saumu, katika bayah (kiapo) kwa Khalifa kusimamisha adhabu za Shariah (hudud), na katika hukmu za Shariah, kwa sababu yote yametoka kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka mwenye kusema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً]  

Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu [Al-Baqara: 208].

Kuingia katika Uislamu kikamilifu kunamaanisha kuutabikisha Uislamu katika nyanja zote za maisha. Haya ni kwa kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah ya Kiislamu katika nchi ya Kiislamu, ili kwamba Dola ya Khilafah ipate kupanuka na kuijumuisha dunia nzima, ikijaza mashariki na magharibi ya ardhi uadilifu na nuru. Mwenyezi Mungu akipenda, Al-Aziz Al-Hakim.

Enyi Waislamu: Hizb ut Tahrir / Tanzania inawasihi msikose fursa hii na inawaalika kufanya kazi pamoja na Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah ya Kiislamu, mlinzi na mhifadhi wa Waislamu. Vile vile inavuta mazingatio yenu kwenye ulazima wa kushikamana na hukmu za sharia siku ya Idd na kutozivunja kwa kuvuka mipaka ya Mwenyezi Mungu (swt), kwa kisingizio cha kusherehekea Idd, na kuchunga familia zenu na watoto wenu na kuwalea kwa mujibu wa sheria za Uislamu mtukufu. Kwa kumalizia, tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atukubalie sisi na nyinyi na aifanye Idd hii kuwa siku ya kheri na baraka kwa Umma wa Kiislamu popote pale.

H. 1 Shawwal 1444
M. : Ijumaa, 21 Aprili 2023

Hizb-ut-Tahrir
Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu