Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ramadhan Imepita na Idd imefika, na Umma wa Kiislamu Bado Unaishi Katika Dhiki na Umekumbwa na Misiba kutoka Pande zote!
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Tanzania itoa, kwa Umma wa Kiislamu kuanzia mashariki yake mpaka Magharibi, pongezi zake kwa mnasaba wa Idd ul Fitr iliyobarikiwa, ikimwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atukubalie saumu, swala, usomaji wa Qur'an na amali njema kutoka kwetu na kwenu na kuziweka katika mizani ya matendo yetu mema Siku ya Kiyama. Siku ambayo haitofaa kitu mali wala watoto ila wale watakaomjia Mwenyezi Mungu na nyoyo safi.

Enyi Waislamu: Tumefunga Ramadhan na kusherehekea Idd iliyobarikiwa. Miaka 103 imepita tangu Ummah upoteze ngao yake, ambayo ni Khilafah, baada ya hapo Ummah wetu haukujua furaha, raha, au utulivu.

Ramadhan imepita na Ummah wetu katika Ukanda wa Gaza haupati kifuturu wala kula daku (suhur), bali hufunga na kufungua saumu ya kupigwa mabomu ya umbile la Kiyahudi kwa njia ya anga, nchi kavu na baharini, katika jinai mbaya kabisa na mauaji ya halaiki mashuhuri yanayoambatana na uvunjaji majumba salama, misikiti, hospitali na vyuo vikuu, bila kusahau njaa ya kimakusudi. Mayahudi hawakuridhika na jinai hizo, bali walishambulia kwa mabomu misafara ya misaada ya chakula, yote chini ya macho ya watawala wasaliti, hasa katika nchi za Misri, Jordan, Saudi Arabia na Uturuki, ambao waliendelea kulipatia umbile la Kiyahudi mafuta na chakula linalohitaji badala ya kulipiga vita katika kuwanusuru watu wetu wa Palestina na Gaza.

Ramadhan imepita na Idd imefika, na jela za madhalimu katika nchi za Kiislamu bado zimejaa watu waliodhulumiwa, hasa wale wanaobeba ujumbe (wabebaji wa dawah) na kutafuta haki.

Ramadhani imepita na Idd imefika, na Ummah wetu unatawaliwa na umasikini na nyama yake inatafunwa na njaa, licha ya kuwa nchi za Kiislamu ni nchi tajiri zaidi duniani kwa utajiri, ardhi zenye rutuba na malisho.

Ramadhan imepita na Idd imefika, na Umma bado umegawanyika katika nyanja mbali mbali, kiasi kwamba bado haujaweza kuungana katika kufunga na kufungua kwake!

Msimamo wa wanachuoni wa Ummah kuhusu hitilafu hii haukuwa katika kiwango kinachotakiwa, kwani walikubaliana na watawala katika kutawanyika kwao badala ya kufanya kazi na wafanyikazi waaminifu kusimamisha Khilafah mpaka tumpe kiapo cha utiifu Khalifa ambaye mamlaka yake yatasuluhisha tofauti hii.

Hatimaye, tunamuomba Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa Walimwengu wote, aharakishe nusra Yake ili tusimamishe Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ambapo Ummah wetu utaokolewa na mabalaa yanayousibu, na ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu itatimia na bishara njema za Mtume wake (saw) zitatimia.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum 30:4 – 5]

H. 1 Shawwal 1445
M. : Jumatano, 10 Aprili 2024

Hizb-ut-Tahrir
Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu