Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Al-Waqiyah TV: Silsila "Kutoka kwa Thaqafa Yetu"

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inafurahi kuwasilisha kwa wafuasi na wageni wa kurasa za Afisi Kuu ya Habari silsila ya video mpya katika vipindi vya Al-Waqiyah TV kwa anwani "Kutoka kwa Thaqafa Yetu", ambayo ni sehemu dondoo kutoka kwa thaqafa ya Hizb ut Tahrir inayoangazia hazina za fikra za Kiisilamu ambazo ziko kwenye vitabu vyetu katika uwasilishaji wa sauti na wa kuhamasisha.

Basi kuweni pamoja nasi…

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 1 -

Kufaulu kwa Harakati za Mageuzi!

... na kuelewa harakati za pamoja ambazo zina nguvu ya ushawishi katika zama zao, inatuonyesha kuwa hazitokei wakati ustawi unapopatikana, haki za asili za mwanadamu zinapatikana, ustawi unapatikana, na wakati ambapo utoshelevu wa kibinafsi ndio kigezo cha kuchukua mambo muhimu. Ufahamu huu wa harakati za pamoja hufanya iwe rahisi kwetu kupima kila harakati za kikundi na usawa wake sahihi, kwa kusoma mazingira ambayo harakati hiyo iliishi au inaishi ndani yake, na dhurufu ambazo ilikuwa imezivaa au inazivaa, na kiwango cha kazi ya watu wenye kujua mwenendo wa shughuli zake, na kusahilisha mambo muhimu yake katika kuondoa yale yanayokwamisha mafanikio yake au yanakwamisha maendeleo yake.

Mafanikio yake hupimwa kwa uwezo wake wa kuongeza roho ya kutoridhika kwa watu, na kuwasihi kuonyesha kutoridhika kwao kila mamlaka inayotawala au mfumo uliopo unapoathiri mfumo huu au kuhukumu kulingana na maslahi na matakwa ya mamlaka.

Chimbuko: Kitabu cha Muundo wa Chama - Ukurasa wa 27

Jumanne, 01 Ramadhan 1442 H sawia na 13 Aprili 2021 M

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 2 -

Uwiano kati ya Aqeeda na Mfumo!

... Na ni katika mporomoko wa kufikiri kwamba tuweke badali ya mfumo wetu kwa mfumo mwengine wowote, na ni katika fikra duni tudhani kwamba umma unapotabikisha mfumo pekee bila ya aqeeda utauokoa. Bali hakuna budi kwanza umma uiamini aqeeda, kisha uutabikishe mfumo unaotokana na aqeeda hii, hapo ndipo utabikisha wa mfumo na kuiamini aqeeda itakuwa ni yenye kuokoa. Hii ni kuhusiana na umma ambao umejengwa juu ya mfumo, na dola yake inasimama juu msingi huu. Ama kuhusu watu wengine na mataifa mengine, hakuna dharura ya watu hao na mataifa hayo kuuamini mfumo ili utabikishwe juu yao. Badala yake, umma unaouamini na kuubeba mfumo huo huutabikisha kwa watu wowote au taifa, hata kama hawauamini mfumo huo kwa sababu huwaamsha wao pia, na huwavutia kwenye kuuamini, na kuuamini mfumo sio sharti kwa wale wanaotabikishiwa juu yao, lakini kuuamini mfumo ni sharti msingi kwa yeyote mwenye kuutabikisha

Chimbuko: Kitabu cha Nidhamu ya Uislamu

Jumatano, 02 Ramadhan 1442 H sawia na 14 Aprili 2021 M

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 3 -

Fungamano baina ya Wanachama wa Chama!

... aqeeda thabiti, na thaqafa iliyokomaa ya chama, inapaswa kuwa ndio fungamano kati ya wanachama wa chama, na inapaswa kuwa ndio kanuni inayoongoza kikundi cha chama, sio kanuni ya kiidara iliyoandikwa kwenye karatasi. Na njia ya kuimarisha aqeeda na thaqafa hii ni kusoma na kutafakari, ili akili iwe umbo maalum, na ili kupatikane muungano wa fikra na hisia, na hapana budi mazingira ya imani yabaki ndani ya kambi moja juu ya muungano wa chama, mpaka vitu viwili viunganishwe ndani ya chama navyo ni: moyo na akili. Kwa hivyo, hapana budi kuuamini mfumo ili moyo uanze kuunganisha baina ya wanachama wa chama, kisha kuusoma mfumo kwa undani.

Chimbuko: Kitabu cha Muundo wa Chama

Alhamisi, 03 Ramadhan 1442 H sawia na 15 Aprili 2021 M

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 4 -

Njia ya Mwamko Wetu!

... njia ya mwamko wetu ni njia moja, nayo ni kurudisha tena maisha ya Kiislamu. Hakuna njia ya kurudisha tena maisha ya Kiislamu isipokuwa kupitia Dola ya Kiislamu, na hakuna njia ya kufanya hivyo isipokuwa tunapouchukua Uislamu kikamilifu: tunauchukua kama Aqeeds inayotatua fundo kubwa, na yenye kuangazia juu yake kwa mweleko wa mtazamo wa maisha, na nidhamu zinazochipuza kutokamana na Aqeeda hii, ambayo msingi wake ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume Wake, na utajiri wake wa kithaqafa ni thaqafa ya Kiislamu inayojumuisha fiqh, hadith, tafsiri, lugha, na mengineo, na hakuna njia ya kufanya hivyo isipokuwa kwa kubeba uongozi wa kifikra wa Kiislamu ubebaji kamilifu kupitia ulinganizi wa Uislamu, na kwa kuwepo Uislamu kamili kila mahali, hadi utakapohamishwa ubebaji uongozi wa kifikra kwenda kwa umma kwa ujumla na kwa dola ya Kiislamu, tutasimama kuubeba uongozi huu wa kifikra kwa ulimwengu.

Chimbuko: Kitabu cha Nidhamu ya Uislamu

Ijumaa, 04 Ramadhan 1442 H sawia na 16 Aprili 2021 M

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 5 -

Mbebaji Ulinganizi Hapaki Watu Mafuta!

... Na ubebaji ulinganizi wa Kiislamu unahitaji kuwa ubwana kamilifu uwe kwa mfumo wa Kiislamu, bila kujali kama unaafikiana na watu wengi au unakhalifiana nao, unalingana na ada za watu au unapingana nazo, na watu wanaukubali au kuukataa na kuupinga. Mbebaji ulinganizi hawabembelezi au kuwapaka mafuta watu, wala hajipendekezi au kuwapaka mafuta watu walio mamlakani. Haizingatii mila na desturi za watu, wala kutilia maanani kukubaliwa na watu au kukataliwa kwa namna yoyote. Badala yake, anazingatia mfumo peke yake, na anakuwa wazi kupitia mfumo peke yake, bila kuingia kwenye hesabu chochote isipokuwa mfumo. Haisemwi kwamba watu wa mifumo mingine washikamane na mifumo yao, lakini badala yake wanalinganiwa bila kulazimishwa kwa mfumo huu ili kuukumbatia, kwa sababu da'wah inahitaji kwamba kusiwe na mfumo mwingine isipokuwa huu, na kwamba ubwana uwe kwake pekee:

((هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ))

 Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia. [At-Tawbah: 33]

Chimbuko: Kitabu cha Nidhamu ya Uislamu

Jumamosi, 05 Ramadhan 1442 H sawia na 17 Aprili 2021 M

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 6 -

Wabebaji Ulinganizi na Hamu ya Kufikia Ukamilifu!

... Na haiwezekani kwa wabebaji ulinganizi huu kubeba jukumu na kutekeleza matokeo, isipokuwa watakapoingiza ndani ya nafsi zao hamu ya kufikia ukamilifu, na daima wanatafuta ukweli, na kila wakati wanakigeukia kila kitu wanachokijua, mpaka wasafishe kutoka kwake kila kitu kilichoambatanishwa na kitu kigeni, na kujiweka mbali na kila kitu kilicho karibu nacho kutokana na uwezekano wa kushikamana nacho, ili fikra wanazobeba zibakie takatifu na safi, na usafi na utakatifu wa fikra ndio dhamana pekee ya mafanikio, na mwendelezo wa mafanikio. Halafu ni lazima wabebaji ulinganizi huu watimize wajibu wao kama wajibu waliokalifishwa na Mwenyezi Mungu, na waukubali kwa furaha na kwa bishara njema ya radhi za Mwenyezi Mungu, na kwamba hawatafuti tuzo kutokana na kazi yao, wala hawasubiri shukrani za watu, na wasitambue chochote isipokuwa kutafuta radhi ya Mwenyezi Mungu.

Chimbuko: Kitabu cha Nidhamu ya Uislamu

Jumapili, 06 Ramadhan 1442 H sawia na 18 Aprili 2021 M

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 7 -

Tofauti Baina ya Thaqafa ya Chama na ya Shule!

... Ama utambuzi kwamba kuna tofauti kati ya shule na chama katika thaqafa, hilo ni ili thaqafa ya chama isibadilike kuwa thaqafa ya shule, halafu chama kikapoteza ufanisi wake. Kwa hivyo, kizuizi kizito lazima kiwekwe kati ya yaliyo ya chama na upande wa kielimu wa thaqafa ya chama, na ikumbukwe kwamba thaqafa ya chama ni kwa ajili ya kubadilisha fikra, kufanya kazi katika uwanja wa maisha, na kubeba uongozi wa kifikra katika Umma. Hairuhusiwi kwa mmiliki wake kukimbilia katika upande wa kielimu. Ikiwa haja yake ni ya kielimu, basi mahali pake ni shule, sio chama. Ni katika hatari ni kukimbilia thaqafa kwa upande wa kielimu kwa sababu huiba sifa ya kazi na huchelewesha mabadiliko ya hatua ya pili ya hatua zake.

Chimbuko: Kitabu cha Muundo wa Chama

Jumatatu, 07 Ramadhan 1442 H sawia na 19 Aprili 2021 M

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 8 -

Ukomavu wa Kithaqafa katika Chama!

... Mwanachama wa chama haondoki kutoka katika dori ya kithaqafa na kwenda katika dori ya mwingiliano isipokuwa baada ya kukomaa kithaqafa, ukomavu ambao unamfanya kuwa na shakhsiya ya Kiisilamu, kwa kuitikia nafsiya yake pamoja na aqliya yake. Amesema (saw): "Hatoamini mmoja wenu mpaka matakwa yake yalingane na yale niliyokuja nayo," na watu wajue juu yake kwamba anabeba ulinganizi wa Kiislamu, na kwamba mwegemeo wa umma uimarike ndani yake na kudhihirika juu yake, kwa kuwepo kwake kwenye halaqa na maingiliano yake na jamii, ili kujitenga kuondoke kutoka kwake. Kwa sababu kujitenga ni mchanganyiko wa uoga na kukata tamaa, lazima kung'olewe kutoka kwa watu binafsi na jamii.

Chimbuko: Kitabu cha Muundo wa Chama

Jumanne, 08 Ramadhan 1442 H sawia na 20 Aprili 2021 M

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 9 -

Aqeeda ni Mizani ya Fikra!

... Uislamu umemshughulika na mwanadamu kikamilifu ili apate shakhsiya maalum ya yeye kutofautishwa na wengine. Amemshughulikia kupitia Aqeeda yake na fikra zake, kwani ulimjaaliya kwayo msingi wa kifikra ambao hujenga juu yake fikra zake, na huunda juu ya msingi wake fahamu zake. Basi yeye hutofautisha fikra sahihi na fikra potofu pindi anapoipima fikra hii kwa Aqeeda ya Kiislamu, na kujenga juu yake kama msingi wa kifikra. Kwa hivyo mawazo yake yanajengwa kutokana na Aqeeda hii, na kwa hivyo anakuwa na mawazo yaliyotofautishwa na msingi huu wa kifikra, na anakuwa na kipimo sahihi cha fikra, kwa hivyo anasalimika kwayo kutokana na kuteleza kwa fikra, na anakanusha fikra fisidifu, na anabaki mwenye fikra ya kweli utambuzi uliosalimika.

Chimbuko: Kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu - Juzuu ya Kwanza

Jumatano, 09 Ramadhan 1442 H sawia na 21 Aprili 2021 M

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 10 -

Mzunguko wa Da'wah!

Moja ya shida ambazo zinasimama mbele ya ulinganizi ni kushikamana kwa watu na maslahi yao. Hii ni kwa sababu mwanadamu amefungamanishwa na maslahi yake ya kibinafsi na shughuli zake za kila siku, na wakati huo huo amefungamanishwa na mfumo. Maslahi haya yanaweza kuonekana kupingana na ulinganizi wa mfumo. Kwa hivyo, anajaribu kuyapatanisha kati yao. Ili kushinda ugumu huu, kila mtu anayeukubali mfumo lazima afanye da'wah na chama kuwa ni kituo cha duara ambalo maslahi yake ya kibinafsi yanazunguka, kwa hivyo hairuhusiwi kushiriki katika kazi yoyote inayokinzana na da'wah, au kazi yoyote ambayo anamsahaulisha na da'wah na kumzuia kutoka kwayo. Kwa njia hii, atakuwa ameihamisha da'wah kutoka kuwa inazungukwa na maslahi yake hadi maslahi yake kuwa yanazungukwa na da'wah.

Chimbuko: Kitabu cha Muundo wa Chama

Alhamisi, 10 Ramadhan 1442 H sawia na 22 Aprili 2021 M

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 11 -

Sifa za Muislamu wa Kweli!

... Na wakati Muislamu anapokuwa na fikra za Kiislamu na aqliya ya Kiislamu, anakuwa na sifa ya uanajeshi na uongozi wakati huo huo, akichanganya rehema na ukali, kujinyima na neema, na anayaelewa maisha kwa ufahamu sahihi, kwa hivyo anayaendesha maisha ya dunia kwa haki yake na huipata Akhera kwa kuiendea mbio. Kwa hivyo, hazongwi na mojawapo ya sifa za wenye kuiabudu, wala harengwi na mpagao wa kidini wa kujinyima kwa kibaniani, na wakati huo yeye ni shujaa wa jihad, anakuwa mshirika wa wanapiganaji, na wakati anapokuwa faragha ni mnyenyekevu. Na anajumuisha baina ya uongozi na fiqhi, na baina ya biashara na siasa. Na sifa kubwa kabisa miongoni mwa sifa zake ni kwamba yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu (swt), Muumba wake na Mwanzilishi wake. Kwa hivyo, unamkuta akiwa mnyenyekevu katika swala yake, akiacha mazungumzo ya kipuuzi, akilipa zakat yake, akifunga macho yake, akihifadhi amana yake, akitimiza ahadi yake, akitekeleza miadi yake, akipigana Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu. Huyu ndiye Muislamu, huyu ndiye muumini, na hii ndiyo shakhsiya ya Kiislamu ambayo Uislamu huunda na kumfanya kwayo kuwa mtu bora zaidi wa wanadamu.

Chimbuko: Kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu - Juzuu ya Kwanza

Ijumaa, 11 Ramadhan 1442 H sawia na 23 Aprili 2021 M

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 12 -

Dalili ya Usahihi wa Aqeeda!

... Walakini, sio maana ya kwamba fikra jumla, yaani aqeeda ya kiakili, ndio pekee inayofaa kuwa msingi jumla kamilifu wa kufikiri na mwegemeo ni kwamba huu ndio msingi sahihi, lakini maana yake ni kwamba ndio inayofaa kuwa msingi pekee, bila kujali ni kuwa ni sahihi au sio sahihi. Ama kile kinachoonyesha ikiwa msingi huu ni sahihi au sio sahihi, ni kuafikiana kwake na umbile la mwanadamu. Ikiwa aqeeda ya kiakili inaafikiana na umbile la kibinadamu, basi hiyo ni aqeeda sahihi na kwa hivyo ni msingi sahihi wa kufikiri na mwegemeo, yaani, wa kuunda shakhsiya, na ikiwa inagongana na umbile la mwanadamu, basi hiyo ni aqeeda batili na kwa hivyo ni msingi batili. Kinachomaanishwa na kuafikiana kwa aqeeda na umbile la mwanadamu ni kutambua kwamba mwanadamu ana mapungufu na anamhitaji Muumba mwenye kumpangia. Kwa maana nyengine, ni kuafikiana kwake na ghariza ya kuabudu.

Chimbuko: Kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu - Juzuu ya Kwanza

Jumamosi, 12 Ramadhan 1442 H sawia na 24 Aprili 2021 M

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 13 -

Siri ya Nguvu ya Imani ya Watu wa Mwanzo!

... Waislamu waliuamini Uislamu kwa imani ambayo haikuwa na shaka, na imani yao ilikuwa na nguvu sana kwamba hakuna maswali yoyote ambayo yangeulizwa, ambayo yalikuwa na tashwishi na shaka, ambayo yangewaathiri na hawakutafuta katika aya za Qur'ani isipokuwa katika utafutaji ambao unawatambulisha maana zake, utambuzi wa kiuhalisia katika fikra. Hawakushughulika na dhana zinazotokana na hili, wala natija za kimantiki ambazo zinaweza kutolewa kutoka kwake. Nao walitoka kwenda ulimwenguni huku wakibeba ulinganizi huu wa Kiislamu kwa watu wote, na wakipigana katika njia yake, na wakafungua miji, na watu wakawakumbatia.

Chimbuko: Kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu - Juzuu ya Kwanza

Jumapili, 13 Ramadhan 1442 H sawia na 25 Aprili 2021 M

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 14 -

Sunnah ni Dalili kama Qur'an!

... Qur’an na hadithi katika upande wa wajibu wa kufuata yaliyokuja ndani yake ni dalili mbili za kisharie, na Hadith ni kama Qur’an katika maudhui haya. Ndio sababu haijuzu kusema kwamba sisi tuna Kitabu cha Mungu tunachochukua kwake, kwa sababu linalofahamika kutoka kwake ni kuachana na Sunnah. Badala yake, ni lazima Sunnah iunganishwe na Kitabu, kwa hivyo hadith ichukuliwe kama ushahidi wa kisheria kama inavyo chukuliwa Qur'an, na hairuhusiwi kwa Muislamu kuhisi kuwa ameridhika na Qur'an bila ya hadith. Mtume (saw) alionya juu ya hilo. Imeripotiwa kuwa Mtume (saw) amesema: "Mtu miongoni mwenu atakaribia kuketi katika kochi lake, akiongea juu ya hadith yangu na kusema: Kati yangu na nyinyi kuna Kitabu cha Mwenyezi Mungu, tutakachokipata cha halali ndani yake tutakihalalisha, na tutakachokipata ndani yake cha haramu tutakiharamisha. Na hakika alichoharamisha Mtume ni kama alichoharamisha Mwenyezi Mungu." Imepokewa na Al-Hakim na Al-Bayhaqi. Na akasema katika riwaya kutoka Jaber hadi kwa Mtume: "Yeyote itakayemfikia hadithi kutoka kwangu na akasema uwongo juu yake, amewazulia uwongo watatu: Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na yule aliyeisimulia." Majma 'Al-Zawaid kutoka kwa Jaber. Kwa hivyo, hapa ni makosa kusemwa kwamba tunaipima Quran kwa Hadith, na ikiwa hailingani nayo tutaiacha, kwa sababu hiyo inapelekea kuachana na hadith ikiwa imekuja makhsusi kwa Qur'an au imefungwa kwayo, au inatoa ufafanuzi wa ujumla wake. Ambapo itaonekana kwamba kile kilicholetwa na hadith hakitabikishi Quran.

Chimbuko: Kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu - Juzuu ya Kwanza

Jumatatu, 14 Ramadhan 1442 H sawia na 26 Aprili 2021 M

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 15 -

Thaqafa ya Kiislamu!

Thaqafa ya Kiislamu ni ujuzi ambao aqeeda ya Kiislamu ndio sababu ya utafiti wake, sawa iwe ujuzi huu unajumuisha aqeeda ya Kiislamu na kuitafiti, kama vile elimu ya imani ya Mungu mmoja (Tawhid), au iwe imejengwa juu ya aqeeda ya Kiislamu kama vile fiqh, tafsiri na hadith, au iwe inahitajika katika kufahamu kile kilichochipuza kutokana na aqeeda ya Kiislamu katika hukmu kama vile Ujuzi unaohitajika katika ijtihad katika Uislamu, kama vile elimu ya lugha ya Kiarabu, istilahi ya hadith, na elimu ya usuli. Haya yote ni thaqafa ya Kiislamu kwa sababu aqeeda ya Kiislamu ndio sababu katika utafiti wake.

Chimbuko: Kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu - Juzuu ya Kwanza

Jumanne, 15 Ramadhan 1442 H sawia na 27 Aprili 2021 M

[Kutoka kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 16 -

Thaqafa ya Kiislamu ndio Msingi katika Kuchukua Thaqafa Nyenginezo!

... Maana ya kuhimiza thaqafa ya Kiislamu sio kumfunga Muislamu kwake, bali maana yake ni kuifanya iwe ndio msingi katika kujenga thaqafa na elimu, na kuruhusu thaqafa na elimu nyenginezo. Ni kwa Muislamu kujielimisha kwa thaqafa na elimu yoyote aipendayo. Isipokuwa, Shakhsiya ya Kiislamu lazima iwe ndio kituo msingi ambacho anazunguka pambizoni mwake katika kuchukua thaqafa yoyote. Waislamu walikuwa na hamu ya kuwafundisha watoto wao kwanza juu ya thaqafa ya Kiislamu, kisha baada ya kuridhishwa na umakinifu wa thaqafa hii, walikuwa wakifungua milango yao kwa thaqafa nyenginezo tofauti tofauti. Njia hii ya elimu hubakisha shakhsiya ya Kiislamu kuwa ni shakhsiya ya Kiislamu sio nyengine, yenye sifa maalum ambazo zinaitofautisha na shaksiya nyenginezo za wanadamu.

Chimbuko: Kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu - Juzuu ya Kwanza

Jumatano, 16 Ramadhan 1442 H sawia na 28 Aprili 2021 M

[Kutoka Kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 17 -

Kuchunga Usafi wa Thaqafa ya Kiislamu!

... Jambo lililoko ni kwamba inapaswa uchungaji wa hali ya juu kwa Aqeeda ya Kiislamu wakati wa kupata thaqafa na sayansi, katika kuifanya shakhsiya ya Kiislamu kuwa ndio kituo kikuu cha kuchuma thaqafa yoyote, na kuzingatia kuwa sayansi hizo hazipingani nayo katika kuchuma sayansi. Ni uchungaji huu ndio ambao unadumisha uwepo wa shakhsiya ya Kiislamu kwa Mwislamu, na huifanya thaqafa ya Kiislamu kuziathiri thaqafa nyenginezo, na kuhifadhi uhai wake kama thaqafa ya Kiislamu tofauti na thaqafa zengine zote za ulimwengu. Na ikiwa uchungaji huu unapo ondoka na Waislamu wakalichukulia sahali hilo, na wanachuma thaqafa zengine kwa msingi mwingine isiokuwa Uislamu, na wasizingatie aqeeda ya Kiislamu wakati wa kuchukua sayansi, basi hili litapelekea kwenye hatari halisi kwa shakhsiya ya Kiislamu, bali kwa Umma wa Kiislamu ikiwa mwenendo huu utarefuka na kuendelea kwa kizazi au vizazi.

Chimbuko: Kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu - Juzuu ya Kwanza

Alhamisi, 17 Ramadhan 1442 H sawia na 29 Aprili 2021 M

[Kutoka Kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 18 -

Udharura wa Kuhakiki Historia ya Kiislamu!

... Mukhtasari ni kwamba Waislamu hawakutilia maanani katika historia, sio historia ya Kiislamu, wala historia ya mataifa mengine, ingawa njia yao ya kuandika historia ni njia sahihi, na ni riwaya ya habari kutoka kwa wale walioshuhudia. Au riwaya ya kitabu kutoka kwa yule aliyesimulia habari kutoka kwa yule aliyeziona. Lakini katika historia ya mataifa mengine, walitegemea riwaya dhaifu, zilizojazwa hadithi na visa. Katika historia ya Uislamu, hawakuwachunguza wasimulizi kama walivyofanya katika seera na hadithi, na walijikita katika habari za makhalifa na watawala, na hawakujali habari za jamii na hali za watu. Kwa hivyo, historia ya Kiislamu haitoi sura kamili ya jamii au dola. Badala yake, hii inaweza kuchukuliwa kutoka kwa vitabu vya seera baada ya uhakiki wake, na kutoka kwa vitabu vya hadithi ambavyo habari za Maswahaba na taabiina zimesimuliwa. Ukweli ni kwamba historia ya Kiislamu inahitaji kuangaliwa katika kuhakiki matukio yaliyoripotiwa katika vitabu vya historia kupitia njia ya kuwahakiki wasimulizi ambao waliwasimulia na silsila yao ya upokezi, na matukio yenyewe, na kuyahukumu kwa kuzingatia uhalisia na masimulizi ...

Chimbuko: Kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu - Juzuu ya Kwanza

Ijumaa, 18 Ramadhan 1442 H sawia na 30 Aprili 2021 M

[Kutoka Kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 19 -

Historia Sio Msingi wa Mwamko!

... Miongoni mwa makosa yaliyo enea ni yale ambayo wengi wanadai kuwa historia ina umuhimu mkubwa katika mwamko wa Umma, na kwamba kuwa na maarifa ya zama za nyuma kunatoa mwanga kwa zama za sasa na kufungua njia ya siku zijazo, na huu ni udanganyifu na mkanganyiko, na ni mlinganisho wa zama za sasa zenye kuhisika kwa zama zilizopita zisizojulikana, na mlinganisho wa uhakika dhahiri ambao tunauona kwa dhana ambayo tulihadithiwa. Inaweza kuwa sahihi au inaweza kuwa ya makosa, inaweza kuwa kweli au inaweza kuwa uwongo. Ukweli ni kwamba haijuzu kuchukua historia kama msingi wa mwamko wowote, au hata kwa utafiti wowote, lakini badala yake uhalisi ambao tunataka kufanya utafiti kwake ndio hufanywa kuwa msingi kwa sababu una hisia yenye kujulikana, kwa hivyo husomwa mpaka ukafahamika, na kisha hupewa tiba kwake ima kutoka kwa Sharia ikiwa inahusiana na hukmu za kisheria, au kutoka kwa muktadha wa uhalisia matibabu ikiwa ni katika mbinu na njia ...

Chimbuko: Kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu - Juzuu ya Kwanza

Jumamosi, 19 Ramadhan 1442 H sawia na 01 Mei 2021 M

[Kutoka Kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 20 -

Khilafah na Imamah!

... Khilafah ni uongozi wa jumla kwa Waislamu wote katika ulimwenguni, ili kusimamisha hukmu za sheria za Kiislamu, na kubeba ulinganizi wa Kiislamu ulimwenguni. Dhati yake ni sawa na Imamah, kwa hivyo Imamah na Khilafah yana maana moja. Hadith Sahih zimepokea maneno haya mawili kwa maana moja. Hakuna kati yao iliyo na maana ambayo inapingana na maana ya nyingine katika andiko lolote la kisheria, yaani, si katika Kitabu wala katika Sunnah, kwa sababu hizi peke yake ndio maandiko (nusus) ya kisheria.

Chimbuko: Kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu - Juzuu ya Pili

Jumapili, 20 Ramadhan 1442 H sawia na 02 Mei 2021 M

[Kutoka Kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 21 -

Sababu ya Jihad ni Ukafiri wa Makafiri!

... Sababu ya Jihad sio kodi ya Jizyah, hata kama kwa kukubali kwao jizyah huachiliwa. Hakika sababu ya Jihad ni kule kwamba wale tunaowapiga vita ni makafiri waliokataa kuikubali da'wah. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 (قَاتِلُوا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حَتَّىٰ يُعْطُوا الْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ)

"Piganeni na wasio muamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharimishi alivyo harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa walio pewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa khiari yao, hali wamet'ii." [Tawba: 29]

Amri ya kupigana nao ni kwa sifa ya ukafiri, yaani, piganeni nao kwa sababu hawamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho ... nk. Kwa hivyo sifa hii imefungwa na vita, na hivyo basi sababu ya vita inakuwa ni ukafiri.

Chimbuko: Kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu - Juzuu ya Pili

Jumatatu, 21 Ramadhan 1442 H sawia na 03 Mei 2021 M

[Kutoka Kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 22 -

Faradhi ya Jihad Haisimami kwa Kuwepo Khilafah!

... ... Jihad ni faradhi ya kikamilifu, haikufungwa na kitu chochote, wala haikuwekewa sharti ya kitu chochote, kwani aya juu yake ni kamilifu:

(كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ)

"Mmeandikiwa kupigana vita" [Baqara: 216]. Uwepo wa khalifa hauhusiani na ufaradhi wa jihad, badala yake jihad ni faradhi ikiwa kuna khalifa wa Waislamu au la. Isipokuwa, wakati Waislamu wanapokuwa na khalifa ambaye ukhalifa wake umewekwa kisheria, na hakuondoka kwa sababu ya moja ya sababu za kuondoka, basi suala la jihad huwakilishwa khalifa na ijtihad yake maadamu yeye ni khalifa, hata ikiwa ni mtu mbaya, maadamu yuko katika Khilafah, na huwalazimu raia kumtii kwa kile anachokiona kuhusiana nayo, Na ikiwa angeamuru yeyote kati yao apigane na amiri muovu, hangepokea Abu Dawud kwa isnad yake kutoka kwa Abu Hurairah, aliyesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

 «الجهاد واجب عليكم مع كل أمير براً كان أو فاجراً»

"Jihad ni wajib juu yenu pamoja na kila amiri awe mwema awe muovu"

Chimbuko: Kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu - Juzuu ya Pili

Jumanne, 22 Ramadhan 1442 H sawia na 04 Mei 2021 M

[Kutoka Kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 23 -

Basi Waandalieni Nguvu kama Muwezavyo!

... Kuundwa kwa nguvu za kijeshi za Dola ya Kiislamu sio tu mujarrab wa kujihami pekee, lakini ni jambo lisiloepukika ambalo ni muhimu kwa Khalifa kufanya kile ambacho Waislamu waliahidi utiifu kwake. Yaani, kwa serikali kufanya kile ambacho Mwenyezi Mungu amefaradhisha juu yake, ambalo ni kubeba da'wah, au kwa maneno mengine, kwa serikali kutekeleza sera yake ya kigeni kwa njia ambayo Mwenyezi Mungu ameifaradhishia, na kudumisha mwenendo sahihi na wenye tija wa sera hii. Kwa hivyo, kuunda nguvu za kijeshi zaidi ya kuwa ngao pekee ambayo Umma unaimiliki dhidi ya vitisho vya makafiri kama vita na uwezekano wa uvamizi wao, ilikuwa njia pekee ya kuifanya sera ya kigeni ya serikali kuwa ya Kiislamu.

Chimbuko: Kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu - Juzuu ya Pili

Jumatano, 23 Ramadhan 1442 H sawia na 05 Mei 2021 M

[Kutoka Kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 24 -

Aqeeda Ndio Msingi wa Kila Fikra!

... Na mtazamo wa kina wa ulimwengu, mwanadamu na maisha ambao unatoa fikra kuu juu yake, na ndio inayomtatulia mwanadamu fundo kuu, na ndio ambayo inakuwa ni aqeeda kwa mwanadamu, na ndio inayomwekea mwanadamu kusudi la maisha, na kusudi la vitendo anavyofanya maishani, kwa sababu mwanadamu anaishi katika ulimwengu, na ikiwa fundo hili kuu halijatatuliwa katika nafsi yake, na juu ya maisha ambayo yumo ndani yake, na juu ya ulimwengu ambao ndio mahali pa maisha yake na uwepo wake, haimkiniki kwake kujua suluki ambayo anapaswa kuwa nayo. Na kwa hivyo, msingi wa kila kitu ni Aqeeda.

Chimbuko: Kitabu cha Mafahim ya Hizb ut Tahrir

Alhamisi, 24 Ramadhan 1442 H sawia na 06 Mei 2021 M

[Kutoka Kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 25 -

Tabia (Akhlaq) Haifai Kufungwa na Manufaa!

... Ama kukosa kwa mwanadamu kusifika na tabia kwa sababu ya manufaa yaliyo ndani yake, ni kwa sababu ya ukweli kwamba manufaa sio kusudio la akhlaq. Na hairuhusiwi kuwa kukusudio, ili yasije yakamfisidi au kumfanya azunguke nayo popote yanapozunguka. Akhlaq ni sifa ambazo mtu hana budi kusifika kwazo kwa hiari, akichochewa na ucha Mungu. Muislamu hafanyi vitendo vya kiakhlaqi kwa sababu vinanufaisha au kudhuru maishani, bali anavifanya kwa kuitikia amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu. Hii ndio inafanya sifa ya tabia nzuri kudumu na kuwa thabiti daima: haizunguki kwa kuzunguka manufaa.

Chimbuko: Kitabu cha Mafahim ya Hizb ut Tahrir

Ijumaa, 25 Ramadhan 1442 H sawia na 07 Mei 2021 M

[Kutoka Kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 26 -

Maslahi Hayana Mafungano na Hukmu!

...  Isipokuwa kwamba, kuondoka kwa hukmu kwa sababu ya kutokuwepo kwa sababu (Illa) yake haimaanishi kabisa kwamba hukmu hiyo imebadilika, badala yake hukmu ya kisheria juu ya suala ni ile ile haijabadilika, isipokuwa tu hukmu imeondoka kwa kukosekana sababu yake na hukmu huregea kwa kuregea sababu yake.

Na kule kwamba hukmu inazunguka pamoja na sababu, kuwepo na kutokuwepo, haimaanishi kubadilika kwa hukmu hizi kwa kubadilika wakati na mahali, ili kudai kuwa kuleta maslahi na kukwepa uovu ndio sababu (illa) ya hukmu za Sharia, na hii hubadilika kwa kubadilika wakati na mahali, kwa hivyo hukmu inabadilika kwa mabadiliko yake, kwa sababu kuleta maslahi na kuiepusha uovu sio sababu (illa) ya hukmu ya Sharia hata kidogo. Kwani halijapatika andiko lolote linaloonyesha kuwa kuleta maslahi na kuzuia maovu ni sababu ya hukmu za kisheria, na hakuna andiko lolote linaloonyesha kuwa ni sababu (illa) ya hukmu maalum, kwa hivyo haiwezi kuwa ni sababu (illa) ya kisheria.

Chimbuko: Kitabu cha Mafahim ya Hizb ut Tahrir

Jumamosi, 26 Ramadhan 1442 H sawia na 08 Mei 2021 M

[Kutoka Kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 27 -

Siasa ni Uchungaji wa Mambo ya Umma!

... Siasa ni uchungaji wa mambo ya Umma ndani na nje, na hufanywa na dola na Umma, ama dola ndio ambayo hufanya uchungaji huu kivitendo, na Umma ndio ambao huhisabu dola kwa hilo.

Uchungaji wa mambo ya Umma ndani na nje kwa upande wa dola hufanywa kupitia kutekeleza mfumo ndani, na hii ndio sera ya ndani. Ama kuhusu kuchunga mambo ya Umma nje kwa upande wa dola, ni uhusiano wake na dola, watu na mataifa mengine, na kueneza mfumo huo kwa ulimwengu, na hii ndio sera ya kigeni. Kuelewa sera ya kigeni ni jambo muhimu ili kuhifadhi umbile la dola na Umma, na ni jambo msingi ili kuweza kumakinisha ubebaji da'wah kwa ulimwengu, na ni kazi ambayo haina budi kwake ili kupangilia uhusiano wa Umma na wengine kwa sura sahihi.

Chimbuko: Kitabu cha Fahamu za Kisiasa za Hizb ut Tahrir

Jumapili, 27 Ramadhan 1442 H sawia na 09 Mei 2021 M

[Kutoka Kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 28 -

Mipango na mbinu!

... Hakika Mipango ya kisiasa, na njia ambazo mipango hii inatekelezwa, hubadilika kulingana na mahitaji ya maslahi, japokuwa mipango hubadilika kwa uchache kuliko njia, na tofauti kati ya mpango na njia, kama inavyoonekana na wale wanaofuatilia siasa za kimataifa, ni kwamba mpango ni sera ya jumla, iliyoundwa ili kufikia moja ya malengo yanayotakiwa na kueneza mfumo au njia ya uenezaji wake,  ama mbinu ni sera ya maalum katika sehemu miongoni mwa sehemu ambazo husaidia kufanikisha na kudhibitisha mpango.

Chimbuko: Kitabu cha Fahamu za Kisiasa za Hizb ut Tahrir

Jumatatu, 28 Ramadhan 1442 H sawia na 10 Mei 2021 M

[Kutoka Kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 29 -

Uhakika wa Chama cha Kiislamu!

... Chama cha Kiisilamu ndicho ambacho kinasimamisha Aqeeda ya Kiisilamu, kinatabanni fikra, hukmu na masuluhisho ya Kiislamu, na njia kinayotembea kwayo ni njia ya Mtume (saw).

Kwa sababu hii, hairuhusiwi kwa Waislamu kukusanyika pamoja kwa misingi isiyokuwa Uislamu kama fikra na njia. Kwa sababu Mwenyezi Mungu amewaamuru hivyo, na kwa sababu Uislamu ndio mfumo pekee mzuri katika uwepo huu, ni mfumo wa kiulimwengu unaoafikiana na maumbile, na unamtatulia mwanadamu matatizo yake kama mwanadamu, humtatulia haja zake muhimu katika ghariza na mahitaji ya viungo, na huyapangilia na kupangilia ushibishaji wake kwa njia sahihi, bila kukandamiza au kuyaachilia huru. Na bila ghariza moja kufinika na ghariza nyengine, ni mfumo kamili unaopangilia mambo yote ya maisha.

Chimbuko: Kijitabu cha Ufafanuzi wa Hizb ut Tahrir

Jumanne, 29 Ramadhan 1442 H sawia na 11 Mei 2021 M

[Kutoka Kwa Thaqafa Yetu]

- Halaqa 30 -

Kusimamisha Khilafah ni Wajib Usioepukika!

... Na Waislamu, tangu dola ya Khilafah kuondolewa katika Vita vya Kwanza vya Dunia, wamekuwa wakiishi bila ya dola ya Kiislamu, na bila kutawala na Uislamu, kwa hivyo kazi ya kurudisha Khilafah, na kuregesha tena uwepo wa hukmu kwa yale yote yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu, ni wajibu uliowekwa na Uislamu, na ni wajib usioweza kuepukika, ambao hakuna khiyari ndani yake, wala kukata tamaa katika suala hilo. Kuzembea katika kuifanya ni moja ya maasi makubwa, Mwenyezi Mungu atamwadhibu kwa adhabu kali zaidi, amesema (saw):

«وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ في عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً»

"Na yeyote atakayekufa bila kiapo cha utiifu (bay'ah) shingoni mwake amekufa kifo cha Jahiliyyah" [Imepokewa na Muslim], na kwa sababu kuachana nayo ni kuachana na utekelezaji faradhi muhimu zaidi miongoni mwa faradhi za Uislamu kwani hupelekea kukoma utekelezaji wa hukmu za Uislamu, badala yake hupelekea kukosekana Uislamu katika nyanja za maisha, na (chochote ambacho wajibu hautekelezwi bila hicho basi hicho pia ni wajibu).

Chimbuko: Kijitabu cha Ufafanuzi wa Hizb ut Tahrir

Jumatano, 30 Ramadhan 1442 H sawia na 12 Mei 2021 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu