Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  30 Shawwal 1444 Na: Afg. 1444 H / 08
M.  Jumamosi, 20 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Marekani Inasisitiza Kuikalia Anga ya Afghanistan, Sisi Tunasisitiza Kusimamishwa Khilafah!
(Imetafsiriwa)

Kamanda wa Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM), Jenerali Michael Kurilla aliwasilisha ripoti kwa Bunge la Congress kuhusu operesheni yao ya kijasusi kuanzia robo ya kwanza ya mwaka huku akisema kuwa Taliban wana dhamira kubwa ya kuiangamiza Dola ya Kiislamu-Khorasan (IS-K) nchini humo, lakini kulingana na yeye, Taliban hawana uwezo wa kuzuia mashambulizi ya kigaidi ya mustakbali ya kundi hilo lililotajwa. Hivyo basi, Marekani inaongeza juhudi za uchunguzi juu ya anga ya Afghanistan. Ili kufanya hivyo, wanafanya majaribio kwenye zana za uchunguzi ambazo zinaweza kubaki hewani kwa muda mrefu.

Hili ni tukio jengine tena la Marekani kuangazia wasiwasi wake juu ya kudhibiti anga ya Afghanistan kufuatia kuibuka kwa Imarati ya Kiislamu ya Afghanistan mnamo Agosti 2021. Wakati ilipokabiliwa na kushindwa kijeshi ardhini nchini Afghanistan, Marekani imekuwa ikijitahidi kurudisha ushawishi wake kupitia njia mbalimbali za kujipenyeza katika eneo la Afghanistan.

Pamoja na kuanguka kwa Jamhuri ya Afghanistan, karibu mali zote za kijasusi za Marekani, ikiwemo serikali ya kijamhuri, Ubalozi wa Marekani, taasisi za usalama/kijeshi, mashirika yasiyo ya kiserikali...nk., zilivunjwa nchini humu. Haya yote yanaratibiwa na majasusi rasmi wa CIA, ambao wanafanya shughuli za kijasusi kwa ajili ya Marekani. Hata hivyo, kushindwa kijeshi kwa Marekani kulisambaratisha mitandao hii, na kusababisha wasiwasi ndani ya Marekani. Kudumisha udhibiti wa anga ya Afghanistan kunamaanisha kuendelea kuwafuatilia na kuwalenga watu ambao hawaipendelei Marekani, huku wakati huo huo wakitoa shinikizo kwa Imarati ya Kiislamu. Kwa upande mmoja, wanatafuta ushirikiano wa kijasusi na Marekani, wakilenga kuondoa mapengo yao ya kijasusi mashinani. Kwa upande mwingine, mara kwa mara wanawaonya wazee wa Imarati kwamba kujifungamanisha kwa aina yoyote na Uislamu na kushindwa kuambatana na maslahi ya Marekani na/au maadili ya kisekula kutawafanya kuwa shabaha.

Marekani inaendelea na sera yake ya upanuzi, ikijipenyeza popote inapopata ombwe la mamlaka na kupuuza mipaka, huku ikijionyesha kama mtetezi wa kanuni fulani zinazoonekana kuwa za kibinadamu. Kuhusiana na hili, nchi za kieneo pia zinaendelea na usaliti wao, kuruhusu anga yao kutumika kwa ndege za kijasusi za Marekani kutekeleza malengo yao ya kijeshi na kijasusi katika eneo hilo na kuwaondoa. Kuuawa kwa Ayman Al Zawahiri ni ushahidi wa jinsi nchi jirani zilivyosaidia CIA kufikia lengo. Marekani inajitahidi kutekeleza malengo haya chini ya pazia la 'vita dhidi ya ugaidi' huku ikitumia kauli mbiu hii kupigana kikatili dhidi ya Uislamu na Waislamu katika ardhi za Kiislamu kwa muda wa miaka 20 iliyopita.

Hivyo basi, mabadiliko ya kimsingi nchini Afghanistan yanategemea mabadiliko ya kimsingi katika eneo hilo. Ikiwa Asia ya Kati na Pakistan hazitaungana chini ya mwavuli wa Afghanistan; na ikiwa mipaka bandia na ya kikoloni haitavunjwa, ni dhahiri kwamba khiyana ya viongozi wa kieneo dhidi ya Afghanistan na Waislamu wengine haitakoma - ushirikiano wao na Marekani utaendelea. Kwa upande mwingine, mabadiliko haya lazima yazingatie Uislamu. Iwapo jografia hii itaunganishwa chini ya Uislamu na fahamu ya Umma wa Mmoja, na ikiwa Khilafah itasimamishwa katika jografia hii, wasaliti wataondolewa kwenye uso wa ardhi. Mbali na Nusrah (msaada) ya Mwenyezi Mungu, wanafikra/wataalamu na rasilimali za Ummah huu watasonga mbele kuelekea jografia hii, wakisafisha ardhi na anga kutokana na kukaliwa kimabavu na hata kumtishia adui ndani ya maeneo yao wenyewe.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu