Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  3 Safar 1445 Na: Afg. 1445 H / 03
M.  Jumamosi, 19 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vyama vya Kiislamu na Visivyokuwa vya Kiislamu ni Hali Halisi Mbili Tofauti Zinazohitaji Hukmu Tofauti za Sharia!

(Imetafsiriwa)

Wakati wa uwajibikaji wa Serikali kwa Kongamano la Taifa, Waziri wa Sheria wa Imirati ya Kiislamu ya Afghanistan alisema kuwa uasisiwaji wa vyama vya kisiasa ni 'dhidi ya Sharia na mapenzi ya watu' na kwamba uendeshwaji wao ‘umekatazwa katakata’ nchini. "Uzoefu wetu unaonyesha kuwa vyama vya kisiasa vimekuwa sababu kuu ambayo imesababisha taifa kuelekea majanga," alisema. Kwa hivyo, "hatutatoa idhini kwa [vyama vya kisiasa] kufanya kazi nchini," aliongeza.

Afisi ya habari ya Hizb ut Tahrir/ Wilayah Afghanistan inataja nukta zifuatazo kuhusiana na maelezo ya hivi karibuni ya Waziri wa Sheria:

1. Vyama ambavyo maagizo yake yamejengwa juu ya Jamhuri, Utaifa, Demokrasia na itikadi nyenginezo zisizo za Kiislamu - vile vinazofuata malengo kinyume na yale ya Uislamu kwa kuhakikisha maslahi ya dola za Mashariki na Magharibi au kukuuza maadili ya kidemokrasia; Vile ambavyo vimewezesha njia kwa uvamizi na wakoloni na vimekuwa ndio chanzo cha aibu katika historia ya Ummah wa Kiislamu, haswa Afghanistan, sio tu viko dhidi ya Sharia na mapenzi ya watu, lakini ni jukumu la Dola ya Kiisilamu kupiga marufuku uendeshwaji wao katika jamii.

2. Vyama ambavyo vinafanya kazi kwa kuzingatia imani na malengo ya Kiislamu sio tu vinatilia nguvu ukuuzaji maadili ya Kiislamu katika jamii lakini pia huimarisha Dola ya Kiislamu. Hivyo basi, kupiga marufuku vyama kama hivyo husababisha jamii kunyimwa kheri kubwa ambayo huenezwa kwa watu kupitia vyama kama hivyo. Kwa kweli, ni kutokana na mapambano ya vyama vya Kiislamu ambapo ilipelekea Jihad dhidi ya uvamizi wa Kisoviet - kwani viongozi wengi wa Imirati ya Kiislamu walikuwa wanachama wa vyama hivi. Vivyo hivyo, harakati ya Kiislamu ya Taliban ilitokea kama chama cha kijihad, katika wakati nyeti mno, wakati jamii ya Afghanistan ilikuwa ikiteseka na vita vibaya sana vya wenyewe kwa wenyewe na walitenda kwa mujibu wa jukumu lao la kidini - matokeo yake ni serikali ya sasa.

3. Neno Hizb (chama) ni neno la Quran ambalo hutumika katika hisia chanya na hasi (Hizb-u-llah) dhidi ya (Hizb-u-Shaitan) kwenye maandiko, kwa hivyo kuvua maana hasi pakee kutoka kwake ni dhidi ya Quran Tukufu. Mwenyezi Mungu (swt) amewaita maswahaba wote wa Nabii Mohammad (saw) kama 'Hizb-u-llah' (chama cha Mwenyezi Mungu). Neno 'chama', sio kwa maana yake ya sasa (ambayo hufafanuliwa kupitia macho ya mifumo ya Kidemokrasia ya Magharibi na Mifumo ya Kikomunisti ya Mashariki), linajumuisha uhalisia wa kiasili wa wanadamu kwa maana yake halisi. Kutoka kwa mtazamo wa Kiislamu, uwepo wa vyama vya Kiislamu sio tu kwa mujibu wa Sharia lakini ni faradhi. Na kuwepo na kikundi (ummah) miongoni  mwa Waislamu ambao watalingania kheri (Uislamu wote), wataamrisha mema na kukataza maovu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika kuhusiana na hili:

[وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ]

“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.” [Aali Imran:104].

Kutokana na hili, tangu mwanzo kabisa mwa uenezaji Uislamu, mtu angepata Maswahaba wa Nabii Mohammad (saw) wako kama Chama cha Kisiasa cha Mtume (saw). Mtu angeweza pia kugundua kuwa baada ya kufariki kwa Nabii Mohammad (saw), Maanswari na Muhajirina waliwasilisha wagombea wao wanaotaka kuteuliwa kama khalifa wa Mtume (saw), mithili tu ya vyama viwili vya kisiasa. Wakati wa fitna (uchochezi) wa mauaji ya Sayyidna Uthman, kikundi (chama) kilichoongozwa na Talha, Zubair na Aisha (Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote) kiliundwa ili kuhakikisha haki inayolenga kutekeleza Qisas (kisasi). Pia, ili kuilinda Khilafah kutokana na kuwa Udikteka, Imam Hussain (Mwenyezi Mungu awe radhi naye) na wafuasi wake waliendelea kutaka uwajibikaji wa Yazid na walijitahidi hadi tone la mwisho la damu yao. Hali kama hiyo pia imeonekana katika historia ya wanazuoni (Ulama) wakubwa wa Ummah na wafuasi wao, mfano wake mkubwa ni mapambano ya Imam Ahmad bin Hanbal dhidi ya fitna ya wakati wake (imani kwamba Quran ilikuwa ni kiumbe).

Kwa hivyo, tunatarajia kwa matumaini mema kwa viongozi wa Imirati ya Kiislamu katika kutofautisha dhahiri kati ya vyama vya Kiislamu na visivyokuwa vya Kiislamu, na pia tunadhani kwamba marufuku hiyo inapaswa kutumika tu kwa vyama ambavyo vinafanya kazi kwa msingi wa itikadi zisizo za Kiislamu na kufuata Malengo yasiyokuwa ya Kiislamu katika jamii, kama vile kukuuza maadili ya kitaifa na ya kidemokrasia chini ya mwavuli wa mashirika ya kiraia na mashirika mengine ya kigeni (UNAMA) ambayo yanafanya kazi kwa pamoja kwa njia iliyoandaliwa kwa malengo ya Magharibi nchini Afghanistan. Kwa hivyo, nukta zilizoorodheshwa hapo juu ni ukumbusho ambao utawafaidisha tu waumini na ni ushauri wa dhati wa kusambazwa miongoni mwa viongozi wa jamii. Kwa mujibu wa aya iliyotajwa hapo juu ya Quran, Mtume Mohammad (saw) ameamuru kama ifuatavyo:

«وَالَّذِی نَفْسِـی بـِيدِهِ لَـتَـأْمُـرُنَّ بـِالْمَعْرُوفِ وَلَـتَـنْـهَوُنَّ عَنِ الْمُنْكَرِ أو لَيوشِكَنَّ اللَّهُ أَنْ يبْعَثَ عَلَيكُمْ عِقَاباً من عِنْدِهِم لَتَدْعُـنَّهُ فَلاَ يسْـتَجِيبُ لَكُمْ»

“Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hamtaacha kuamrisha na hamtaacha kukataza maovu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atakaribia kutuma adhabu juu yenu kutoka kwake. Kisha mtamuomba na wala hatakujibuni.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu