Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  28 Rajab 1445 Na: 1445 H / 08
M.  Ijumaa, 09 Februari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mnamo Tarehe 28 Rajab, ni Mwaka wa 103 Tangu Kuondolewa Khilafah ya Kiislamu
(Imetafsiriwa)

Wakati kama huu mwezi wa Rajab (katika kalenda ya mwandamo wa mwezi) umekaribia tena huku Umma wa Kiislamu ukiwa bado unateseka sana kwa kukosekana Khilafah ya Kiislamu. Hivi sasa miaka mia moja na tatu kamili iliyopita mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H, Khilafah ya Kiislamu iliondolewa mikononi mwa dikteta mhalifu, Mustafa Kamal. Ni zaidi ya karne moja tu ambapo Umma wa Kiislamu umekuwa ukiteseka kutokana na mitetemeko ya baada ya tukio hilo la kusikitisha na kuhisi kila kukicha hadi leo. Kwa vile Khilafah ya Kiislamu ilishuhudia kuporomoka kwa hujma za kisiasa, kijeshi na kithaqafa za Dola ya Kikoloni ya Uingereza, ilikuwa ni baada ya kuanguka kwa mwavuli huo wa ulinzi wa Waislamu ambapo maeneo yao yalikoloniwa, dola za taifa zikapandikizwa juu yetu, hukmu ya Kiislamu ilisitishwa na damu yetu, mali, na heshima pamoja na ibada na matukufu yetu yalikiukwa. Unyama unaoendelea kufanywa na umbile la Kizayuni huko Gaza, ukandamizwaji wa Waislamu wa India na utawala wa Hindutva, jinai inayoendelea ya Serikali ya China dhidi ya Waislamu wa Uighur na mambo mengine yanayofanana na hayo yanatokea kwa kukosekana Ngao ya Waislamu (Khalifa).

Mtume Muhammad (saw) amesema:

«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ یقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَیتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam (kiongozi, Khalifa) ni ngao watu hupigana nyuma yake na kujihami kwaye.”

Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan imezindua kampeni kwa mnasaba huo kote Afghanistan. Amali hizi zimetekelezwa kupitia majukwaa ya mtandaoni na pia maingiliano ya ana kwa ana kwa mara nyingine tena kuwakumbusha Waislamu kuhusu kusimamisha Khilafah – wajibu wa Kiislamu ambao unalenga hasa kuwataka watu wenye nguvu Kusimamisha Khilafah Rashida ya pili na kuwanusuru Waislamu waliodhulumiwa ni Faradhi juu yao.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan inazikaribisha rasmi jamii zote za Afghanistan, vyombo vya habari na waandishi wa habari, hasa wale ambao wana hisia za dhati juu ya Uislamu na maadili yake ili kupanua uungaji mkono wao katika kueneza ujumbe wa haki kwa kupigia debe na / au kuangazia amali za kampeni hii ya dhati, kuwa sehemu muhimu ya juhudi kama hizo zenye lengo la kurudisha Khilafah Rashida ya Pili.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu