Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  18 Safar 1444 Na: 1444 H / 007
M.  Jumatano, 14 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kati ya Kibaraka Msaliti na Mnafiki Mrongo

Watawala wa Waislamu Watoa Rambirambi kwa Mvunjaji wa Khilafah, Uingereza, kwa Kifo cha Malkia Wake
(Imetafsiriwa)

Mnamo Novemba 20,1922, katika Kongamano la Lausanne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza George Curzon aliweka masharti manne kwa nchi yake kukubali kuutambuliwa uhuru wa Uturuki, nayo nii: kuondolewa kabisa kwa Khilafah, kufukuzwa khalifa nje ya mipaka, kunyang'anywa pesa zake, na tangazo kwa dola ya kisekula! Hadi leo, haya bado ni masharti ya kafiri mkoloni Magharibi kukubali mfumo wowote wa serikali katika nchi za Kiislamu; jambo ambalo linaonyesha ushahidi wa maana zaidi kwamba nchi za Kiislamu bado ziko chini ya ukoloni wa Magharibi, lakini mikononi mwa watawala vibaraka, ambao huzifungua ardhi kwa Magharibi kila inapotaka kuzipora, na endapo Waislamu watainuka, wanawauwa kwa chuma na moto!

Ndiyo maana, tangu Malkia Elizabeth II wa Uingereza alipofariki dunia Alhamisi iliyopita, watawala wa Waislamu wanaonyesha masikitiko na huzuni yao kubwa kutokana na kifo chake! Wamemsifu kwa sifa mbalimbali za utukufu, heshima na uongozi, kana kwamba aliyekufa ni mama yao aliyewazaa! Baadhi yao hata walitangaza kuomboleza na kupeperusha bendera nusu mlingoti! Wakati pindi Waziri Mkuu wake wa zamani Boris Johnson alipomuomboleza katika Bunge la Uingereza la House of Commons, hakusahau kuifanya hadhira icheke alipowatajia jinsi yeye na malkia wake walivyokejeli mnamo mwaka wa 2012 upumbavu wa mmoja wa watawala wa Kiarabu aliye karibu na Uingereza!

Enyi Waislamu: Watawala hawa si viongozi wala hawana ubwana wa mamlaka, bali ni vibaraka waovu waliochaguliwa kimakusudi na Magharibi mkoloni kafiri. Mmoja wao amelala mfukoni mwa bwana wake kama panya anayefugwa, na anaamini ndani ya kina cha dhamiri yake potofu kwamba madhumuni ya utawala wake ni kuziweka wazi nchi za Kiislamu kwa maslahi ya Magharibi, na kuwakandamiza watu endapo watajaribu kufanya kuregesha utawala wa Kiislamu. Mikono hii iliyopanuliwa ya ushawishi wa kikoloni hautang'olewa kutoka katika nchi yetu isipokuwa Khilafah iregee tena, na kwayo mamlaka yatarudi kwenu, na kuipa heshima Dini yenu na kuihifadhi nchi yenu. Jambo hili linategemea mwitikio wa watu wenye nguvu na ulinzi, hususan majeshi, kwa wito wa kuiregesha Khilafah. Kwa hiyo, wazuieni na wasukumeni wasimamishe Khilafah, kwani wao ndio nguzo halisi za utawala katika nchi.

Enyi Watu Wenye Nguvu na Ulinzi: Katika hotuba yake akichukua kiti cha enzi, Mfalme mpya wa Uingereza aliapa kuwa mtetezi wa imani, aliahidi kuihifadhi na kuilinda dini ya Kikristo ya Kiprotestanti. Ama nyinyi, mumesalia kimya juu ya watawala ambao wamethibitisha bila shaka yoyote kwamba walitoa ahadi kwa Magharibi kuupiga vita Uislamu na watu wake! Je, msimamo wenu kwa hili ni upi?! Ni upi udhuru wenu wa kuchelewesha kuwang'oa wasaliti hawa, na kutangaza kiapo chenu na ahadi yenu ya kuihifadhi Dini ya Uislamu, kuuhifadhi ubwana wake, na kuwachunga Waislamu na maslahi yao?

Je, mnamsubiri Mwenyezi Mungu (swt) akubadilisheni na watu walio bora kuliko nyinyi, kisha muwe mumepoteza maisha yenu kwa kuwatumikia vibaraka wasaliti wanaompiga vita Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw)?!

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَإِن تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ ثُمَّ لا يَكُونُوا أَمْثَالَكُمْ]

Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi. [Muhammad: 38].

Mhandisi Salah Eddine Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu