Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  24 Rabi' I 1444 Na: 1444 H / 014
M.  Alhamisi, 20 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

"Uvumilivu" wa Watawala wa Ghuba Unajumuisha Vipengee na Sheria zote Isipokuwa Uislamu na Waislamu!
(Imetafsiriwa)

Chini ya kichwa cha urongo cha "Uvumilivu", watawala wa Imarati walizindua hekalu jipya la moja ya dini za kikafiri katika eneo la Jebel Ali. Hapo awali walitotora hisia za Waislamu walipofungua makanisa kadhaa kwa ajili ya Wakristo, na pia sinagogi la Mayahudi. Yalikuwa yameundwa na wizara iitwayo Wizara ya Uvumilivu mnamo 2016 ili kupigia upatu ufunguzi wa mahekalu ya ziada ya makafiri chini ya kichwa cha “Uvumilivu.” Lakini wakati huu utotoraji wao ni mkubwa na mkali zaidi, wamefungua hekalu la Kibaniani! kwa gharama ya dolari milioni 16; huku Mabaniani wenye msimamo mkali wakiwakabili Waislamu wa Bara Hindi kwa aina za dhulma na mateso mbele ya macho na masikio ya watawala wa Imarati na dunia kwa jumla. Kuanzia kuigeuza misikiti kuwa mahekalu ya kibaniani, hadi kuwashambulia wanawake wa Kiislamu mabarabarani, hadi kuwapiga marufuku kuvaa hijabu katika vyuo vikuu, hadi kuwafukuza Waislamu kutoka majumbani mwao huko Assam, hadi miongo kadhaa ya kuwatesa na kuwaua Waislamu wa Kashmir na kuwaweka chini ya utawala wa moja kwa moja wa kijeshi, hadi kwenye kampeni ya kuondoa uraia kutoka kwa Waislamu wa India na kuwanyima haki zao za kiraia, hadi kuzusha mashtaka ya ugaidi dhidi ya vijana wa Kiislamu na kukamatwa kwa visingizio hafifu ambavyo havina mantiki, hadi kwenye uvamizi wa magenge ya Kibaniani dhidi ya Waislamu mabarabarani na masokoni, kuwaburuta na kuwaua...

Ama watawala wa Imarati wanafumbia macho jinai zote hizo dhidi ya Waislamu nchini India na kisha kujenga hekalu kubwa la Mabaniani kwa gharama ya dolari milioni 16!

Vipi wasiweze na ilhali wamefumbia macho jinai za umbile la Kiyahudi dhidi ya Ardhi Iliyobarikiwa na Msikiti wa Al-Aqsa kisha wakachapisha pamoja nao licha ya hasira na kukataliwa na watu wa Umma wa Kiislamu. Watawala wa Imarati wamesahau

(إِنَّمَا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَن تَوَلَّوْهُمْ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَأُولَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ)

“Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Al-Mumtahanah: 9].

Lau watawala wa Imarati wangetaka kunusuru Uislamu na Waislamu nchini India, wangeweza kufanya hivyo.

Wana karata nyingi mikononi mwao za kushinikiza maslahi ya India; Ya kwanza kati ya hizi ni uwepo wa jamii ya Wahindi ya watu milioni 3.5 na hii inamaanisha nini kwa mtiririko wa kifedha ambao India inapokea kutoka kwa uchumi wa UAE. Hii ni pamoja na umiliki wao wa jumba kubwa la vyombo vya habari, ambalo linajumuisha vyombo vya habari vya kimataifa na kikanda, pamoja na majeshi yao ya kielektroniki. Hii ni bila kuhesabu uwezo wao wa kushawishi kupitia mitandao mahusiano ya kikanda na kimataifa ambayo wanamiliki.

Ndio, watawala wa Imarati wana zana na uwezo wote huu, lakini hawana moyo ulio na ghera kwa Uislamu na Waislamu, wala kwa matukufu yao.

Walikuwa miongoni mwa waanzilishi wa kuwapokea wahalifu wauaji kutoka kwa Chama cha Baath, kwa pande zao za kiusalama na za kisiasa, licha ya kujua kwao vitendo vya kihalifu walivyofanya dhidi ya watu wa Ash-Sham, ikiwemo kuwaua, kuwahamisha, kuvunja heshima na kutumia silaha za kemikali. Je, “uvumilivu” ambao watawala wa Imarati wanaulingani ni kwa ajili ya maadui wa Uislamu na Waislamu pekee, na wao ndio wanaopiga vita hukmu za Uislamu na kuziweka mbali na utawala na maisha ya watu?!

Wakati watawala wa Imarati wakiwa mbioni kufungua mahekalu ya ziada kwa ajili ya Makafiri, watawala wa Bahrain wanakusudia kumkaribisha Papa wa Kanisa Katoliki kuanzia tarehe 3/11/2022 hadi 6/11/2022, ambapo imepangwa kuwa Papa wa Kanisa Katoliki atakutana na Sheikh wa Al-Azhar Ahmed Al-Tayeb na taasisi za makanisa huko Bahrain. Pamoja na wajumbe wa "Baraza la Wazee wa Kiislamu" linaloongozwa na Sheikh wa Al-Azhar. Mnamo tarehe 4/2/2019, watawala wa Imarati hapo awali walikuwa wamemkaribisha Papa Mkatoliki na Sheikh wa Al-Azhar chini ya majina yayo hayo, na wakati huo pande hizo mbili zilitia saini hati ya Udugu wa Kibinadamu.

Inaonekana kutokana na matukio haya kwamba Dola za Ghuba zinaharakisha kujaribu kuhalalisha kuwepo kwa mahekalu mapya kwa ajili ya Makafiri katika Bara Arabu, na kumdandia Sheikh wa Al-Azhar kwa ajili hiyo. Na iwapo Sheikh wa Al-Azhar hatarekebisha jambo hilo, atajikuta katika uhalisia mpya hatari, hasa ikiwa watawala wa Nyumba ya Saud watamkaribisha kupitia kufanya kongamano liitwalo “Uvumilivu” ili kupitisha mradi wa ujenzi wa mahekalu ya Makafiri katika ardhi ya Misikiti Miwili Mitakatifu.

Enyi Waislamu:

Dini ya Uislamu imepangilia mahusiano yote, yakiwemo mahusiano na wasiokuwa Waislamu, kwa njia ya kina isiyomuacha mwanadamu katika hali ya kuchanganyikiwa. Umechora mfumo wa mahusiano chini ya utawala wa dola na katika jamii. Hivyo basi, baada ya haya, je Waislamu wanahitaji kujenga mahekalu kwa ajili ya Makafiri katika Bara Arabu, ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ameharamisha kwa dini nzima ya ukafiri, kama Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivyosema:

«أَخْرِجُوا الْمُشْرِكِينَ مِنْ جَزِيرَةِ الْعَرَبِ» “Wafukuzeni washirikina kutoka bara Arabu!” Na vipi kuhusu mkataba wa Umar kwamba washirikina wasijenge mahekalu yao mapya katika nchi za Waislamu?

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاء بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللَّهَ لاَ يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ * فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَى أَن تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ فَعَسَى اللَّهُ أَن يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِ فَيُصْبِحُواْ عَلَى مَا أَسَرُّواْ فِي أَنفُسِهِمْ نَادِمِينَ)

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. * Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo kwake wakawa wenye kujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao.” [Al-Ma‘idah: 51-52].

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu