Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 4 Dhu al-Hijjah 1444 | Na: 1444 H / 041 |
M. Alhamisi, 22 Juni 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uhuru wa Vyombo vya Habari chini ya Demokrasia Unaonekana Kuwa Hatari Zaidi kuliko Ule ulio chini ya Udikteta!
(Imetafsiriwa)
Mnamo tarehe 10 Mei 2023, majukwaa fulani ya habari, yakiwemo magazeti na televisheni, yaliripoti kuzuiliwa kwa hadi Waislamu 16 katika miji miwili - Bhopal na Hyderabad. Madai hayo ya kashfa yaliishambulia Hizb ut Tahrir kama shirika la 'kigaidi' linalokusudia kufanya 'Jihad' dhidi ya India. Maregeleo yalifanywa kwa vyanzo ‘visivyojulikana’ kutoka kwa mashirika tofauti ya kijasusi (serikali na muungano) ikijumuisha baadhi ya mashirika ya ‘kigeni’. Umiliki wa vitabu na maandiko ya Hizb ut Tahrir na wale waliowekwa kizuizini yalifanywa kuwa ndio msingi wa madai hayo. Tangu wakati huo riwaya tofauti za madai hayo zimekuwa zikienea mitandaoni, ikiwa ni pamoja na kuwahusisha Waislamu 16 waliokamatwa na kesi inayoendelea ya wanachama wa Hizb ut Tahrir katika jimbo la Tamil Nadu. Hata majukwaa mashuhuri ya habari kama vile ‘India Today’ au ‘Economic Times of India’ hayakuweza kufuata kanuni rahisi ya maadili, ambapo wanachapisha kwa ujasiri kwenye tovuti zao, na kuvuta kwa urahisi 'simulizi' waliyopewa bila kuangalia ukweli wa kimsingi kuhusu Hizb ut Tahrir! Kama wangefanya hivyo wangegundua kwamba Hizb ut Tahrir (Chama cha Ukombozi) ni chama cha kisiasa kinachofanya kazi ya kusimamisha tena Khilafah - mfumo wa utawala wa Kiislamu - kwa njia ya Utume, katika ulimwengu wa Kiislamu kupitia mvutano wa kifikra na kisiasa na hakitabanni hatua za kisilaha, kwa kuiga mfano wa Mtume (saw) na njia yake katika kusimamisha dola ya kwanza ya Kiislamu.
Baada ya kuanguka kwa USSR, Marekani iliunda adui mpya wa kifikra wa ulimwengu wa Kiislamu, ili kuweka umma wake upande wa wale wanaoendesha serikali ya Marekani. Hili liliunda taswira ya simulizi za vyombo vya habari vya kimataifa ambazo zinaonyesha vitendo vya uhalifu kama "ugaidi wa Kiislamu", wakati nyingi kati yao ni operesheni zilizopangwa na Marekani na washirika wake. Tangu vita vya kikatili dhidi ya Uislamu ambavyo Marekani iliendesha kwa upande mmoja tangu 2001, simulizi hizi zimesafirishwa nje na kukumbatiwa na washirika wake wenye tamaa na watawala vibaraka. Na kwa hivyo, kutoka kwa "Demokrasia Tukufu zaidi" hadi "Demokrasia Kubwa", kuna wingi wa vyombo vya habari vya Amerika na India ambavyo vinaficha ukweli na kueneza uwongo, haswa linapokuja suala la kuripoti habari za Waislamu na Uislamu.
Kwa tamaa ya umaarufu katika soko la vyombo vya habari, utata wa kuwafurahisha wale walio mamlakani, na tamaa ya malipo kutoka kwa matajiri, maovu haya yote yanajumuisha dhamana kwamba "manufaa" yanakuwa ndio kipimo cha vitendo miongoni mwa wanahabari, badala ya maadili murua na kutafuta ukweli.
Uhuru wa Vyombo vya Habari unatamaniwa na kupigia debe katika demokrasia kama miongoni mwa taasisi msingi taasisi za kuwajibisha taasisi nyingine ndani ya serikali. Vinachukuliwa kuwa mojawapo ya vipimo vikuu ambavyo kwavyo taasisi za Magharibi hupima "afya na ustawi" wa mataifa mengine.
Kwa hivyo ni nini cha kusema kuhusu taasisi maarufu za vyombo vya habari, nchini India - demokrasia kubwa zaidi, kushindwa kuzingatia kanuni za maadili zilizochapishwa kwenye tovuti zao wenyewe!? Kanuni za maadili kama vile kufanya ukaguzi rahisi wa ukweli au kufanya usawa kwa kuwasilisha maoni ya upande wa pili au kutopotosha watu au kudanganya.
Mara nyingi sana mtu anaweza kuona marejeleo ya vyombo vya habari kama vile ‘chanzo cha kuaminika’ au ‘chanzo kisichofichuliwa’ anapokusudia watu walio serikalini kama chanzo. Watu kama hao ambao mara chache wanaweza kuwajibika mbele ya sheria kwa kupanda uwongo katika nyanja ya umma.
Ni nini kinachopaswa kufanywa kwa vyombo vya habari vinavyotetea kulinda ‘uhuru wa kujieleza’, huku kikizuia barua pepe bila kujali kujua ‘mtazamo mwingine’?
Je, tunaweza kusema nini kuhusu vyombo vya habari ambavyo vimelemazwa na udhibiti unaowazuia kuingia kwenye tovuti, kutoka kwa serikali inayojaribu kuwawajibisha?
Nini kifanyike kwa "Baraza la Vyombo vya Habari la India", ambao wameshindwa kuingiza maadili ya "kutosema uwongo" kwa wanachama wake, na ambao wameweka kanuni za maadili ambazo mara kwa mara zinafanywa kuwa hazina maana na wanachama wake wa baraza?!
Je, ni nini cha kusema kuhusu vyombo vya habari, katika demokrasia kubwa zaidi, ambavyo vimeshindwa kuihisabu serikali yake inayochukulia umiliki wa “Vitabu na Vipeperushi” kama kumiliki “Silaha” zinazopaswa kuadhibiwa chini ya sheria mbovu za UAPA?!
Kutetea uwongo kwa namna ya kupotosha au kwa makusudi kuficha “Ukweli”, kama inavyoshuhudiwa katika serikali za demokrasia, ni hatari zaidi kuliko ukimya kuhusu “Ukweli”, kama ilivyo katika udikteta.
Kama inavyojulikana vyema, ili kuficha uwongo, uwongo mwingine lazima uzuliwe. Kwa hiyo, katika serikali za demokrasia, na kwa kuwepo kile kinachoitwa uwingi wa taasisi kama utaratibu unaodaiwa wa kudhibiti na kuzuia ukiritimba wa mamlaka, imekuwa ni wajibu kutunga urongo unaotosheleza taasisi zote hizi kuficha uongo mmoja, na hili ndilo linalofisidi na kupotosha umma.
Uislamu unaweka thamani kubwa kwa yule anayemhisabu mtawala kwa ajili ya Haki. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «سَيِّدُ الشُّهَدَاءِ حَمْزَةُ بْنُ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، وَرَجُلٌ قَامَ إلَى إمَامٍ جَائِرٍ فَأَمَرَهُ وَنَهَاهُ، فَقَتَلَهُ» “Bwana wa Mashahidi wote ni Hamza bin Abdul Muttalib na mtu aliyesimama kwa mtawala jeuri akamwamrisha mema na akamkataza maovu, kisha akauwawa na mtawala huyo.”
Kwa hivyo, kwa wale walio na jukumu la kufikisha habari kwa umma na bado wanabeba maadili ya kusema "Ukweli", ulizeni tu swali rahisi kwenye majukwaa yoyote ya habari ya mtandao kama vile ChatGPT, Wikipedia, Google, n.k. na mtapata maelezo ya msingi kuhusu Hizb ut Tahrir ambayo yanapaswa kufuta uwongo wote uliozushwa.
Ama vyombo vya habari ambavyo kwa aibu vimeamua kusahau misheni yao ya kufikisha “Ukweli” tunawakumbusha juu ya ahadi yao ya taaluma hiyo kwa kutumia maneno ya Mtume Mohammad (saw), «أَلَا أُخْبِرُكُمْ بِأَكْبَرِ الْكَبَائِرِ؟» “Je, siwapeni habari juu ya dhambi kubwa zaidi ya madhambi makubwa?” Wakasema, "Bila shaka, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu." Mtume akasema, «الْإِشْرَاكُ بِاللهِ وَعُقُوقُ الْوَالِدَيْنِ» “Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kuwaasi wazazi wawili.” Na alikuwa anapumzika, kisha akakaa na kusema, «أَلَا وَقَوْلُ الزُّورِ» “Na kusema ushahidi wa uongo.” Na akarudia rudia hili hadi akanyamaza.
Mhandisi Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |