Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 29 Sha'aban 1444 | Na: 1444 H / 033 |
M. Jumanne, 21 Machi 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tangazo la Matokeo ya Uchunguzi wa Mwezi Mwandamo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa mwaka 1444 Hijria
(Imetafsiriwa)
Bismillah Ar-Rahman Ar-Raheem na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, Aliyetufaradhishia kufunga mwezi wa Ramadhan na kuifanya kuwa ni miongoni mwa nguzo za Uislamu, na rehma na amani zimshukie yule aliye teremshiwa Qur’an Tukufu katika mwezi mtukufu, kama uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi, bwana wetu Muhammad na jamaa zake na maswahaba wake wote.
Imepokewa kutoka kwa Bukhari katika Sahih yake kutoka kwa Muhammad bin Ziyad kwamba amesema: “Nilimsikia Abu Hurairah (radhi za Allah ziwe juu yake) akisema: Amesema Mtume (saw) au amesema Abu Al-Qasim (saw) :
«صُومُوا لِرُؤْيَتِهِ وَأَفْطِرُوا لِرُؤْيَتِهِ فَإِنْ غُبِّيَ عَلَيْكُمْ فَأَكْمِلُوا عِدَّةَ شَعْبَانَ ثَلَاثِينَ»
“Fungeni kwa kuuona [mwezi mwandamo wa Ramadhan], na fungueni kwa [kuuona mwezi mwandamo wa Shawwal], na ikiwa mbingu zimejaaa mawingu (na hamuwezi kuuona), timize siku thalathini za Sha’aban.”
Baada ya kuchunguza mwandamo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan katika usiku huu wa kuamkia Jumatano, muandamo wa mwezi mpya haujathibitishwa kwa mujibu wa matakwa ya muandamo wa Shariah, hivyo basi kesho, Jumatano ni tamati ya Sha’aban, na hivyo kesho kutwa, Alhamisi, ndio siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa mwaka 1444 Hijria.
Kwa mnasaba huu, nafikisha salamu na pongezi zangu za Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na wote wanaofanya kazi humo, kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, nikimuomba Mwenyezi Mungu amsaidie na aharakishe ushindi na tamkini kwetu kupitia mikono yake.
Ramadhan inakuja mwaka huu, huku dunia ikikumbwa na mgogoro wa kifedha unaozidi kuwa mbaya siku hadi siku, hadi nchi nyingi duniani zinakabiliwa na mzigo huo, wakiwemo watu binafsi, taasisi za kibinafsi na hata serikali hazijaepushwa na hilo. Mfumo wa kibepari umewachosha watu kwa riba, ukiritimba, uvamizi wa kiuchumi na uporaji wa mali kwa maslahi ya makampuni ya ukiritimba ya kibepari na nchi zinazoyafuata, zikiongozwa na Marekani.
Katika miongo kadhaa iliyopita, utandawazi umekuwa ni mashini iliyoundwa na Marekani ili kutekeleza sera hii ya uhalifu dhidi ya watu. Lakini baada ya hadhi ya China kukua, sauti ya Urusi iliongezeka, na uasi wa Ulaya uliongezeka, Marekani inarudisha utandawazi kwa mara nyingine tena, na kuleta uchumi wa nchi hizi "chini" ya uchumi wake, ambayo iliifanya kuchukua fursa ya vita kati ya Urusi na Ukraine kuidhoofisha Urusi na kuzihusisha Ulaya na China ndani yake. Haijalishi maafa ambayo vita hivi vilisababishia watu wa Ukraine, na mapigo ya kiuchumi ambayo yalitishia usalama wa chakula wa nchi nyingi za ulimwengu, kwa sababu Marekani inaona vita hivi kama kufikia maslahi yake, haijalishi vina madhara kiasi gani kwa wengine!
Ama kuhusu hali ya Waislamu, haiko mbali na mandhari hii. Ndio watu wa kwanza kuathiriwa na uchawi wa kiuchumi, kisiasa na usalama wa nchi za Magharibi. Nchi za Kiislamu ni miongoni mwa nchi tajiri zaidi, na eneo lao ni mojawapo ya maeneo muhimu zaidi. Hata hivyo, watawala wao hawako sambamba nao, kwani wao ni vibaraka wa nchi kuu za kibepari za Magharibi, na walengwa wa hesabu zake za kijiografia. Njia za nchi za Magharibi za kukazanisha mshiko wao kwa nchi za Kiislamu zilikuwa kwa kuzingatia mambo matatu: kukabidhi madaraka kwa vibaraka, kuanzisha sera ya kutenganisha Dini na maisha, na kuwa makini katika kuifisidi idara ya mahakama na wale wanaotekeleza amri zake. Hivyo, Ummah unakuwa mfungwa wa maslahi yake.
Hata hivyo, hali hizi na mashambulizi yaliyofuata ya Wamagharibi dhidi ya Uislamu na ardhi za Kiislamu yalizidisha imani ya Waislamu kwamba mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu ndio njia bora zaidi ya maisha, na kwamba bado wako katika hali ya ukoloni na udhalilifu tangu Khilafah ulipovunjwa na ardhi zake zikachanwa chanwa. Kwa hiyo, Khilafah leo hii ni rai jumla miongoni mwa Waislamu. Badala yake, wanaona kwamba umoja wa nchi yao ndani ya dola moja ndio maslahi muhimu zaidi ya maslahi yao leo.
Lakini pamoja na kuwa Ummah unazidi kukaribia zaidi wazo la kutabikisha Shariah, bado ungali unajikwaa katika kutafuta njia inayoelekea kwenye lengo hili. Watu wake bado hawajaongozwa kwenye haja ya kusimama kidete katika kushikamana na njia ya Utume ya kuiregesha Khilafah. Jambo hili halitatambuliwa na watu wa kawaida kipeke yao isipokuwa waelimishwe katika thaqafa jumla.
Enyi Wamiliki wa Majukwaa... Enyi Muliochukua Jukumu la Kuifahamisha Rai Jumla:
Hii hapa dori yenu, Enyi waundaji wa rai jumla, na hasa miongoni mwenu ambao mnalinda sana maslahi ya Umma wa Kiislamu. Hivyo basi, nyinyi nyote, wanahabari, wanazuoni, washawishi, wamiliki wa tovuti na majukwaa, na wasimamizi wa vikundi na miundo, muliokubali jukumu la "kuufahamisha Ummah kuhusu masuala ya kipaumbele." Makundi ya Umma wa Kiislamu yanakufuateni mchana na usiku, ili kuchukua mawazo kutoka kwenu kuhusu masuala ambayo lazima yatahadharishwe kwa wakati ufaao. Hakuna kipaumbele leo ambacho ni muhimu zaidi kwa Umma wa Kiislamu kuliko suala la kuiregesha Khilafah kwani ndio mama wa masuala yote. Bali, ni kadhia nyeti ambayo hatua ya uhai au kifo lazima ichukuliwe.
Enyi Waislamu Mlio na Uwezo wa Mabadiliko... Enyi Watu Wenye Nguvu na Ulinzi!
Kwa nini mnashindwa kuinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu, je mnawaogopa watawala wenu?! Je, hamuwaoni wanatembea kama ng'ombe wa kufugwa kila wanapomtembelea mmoja wa watawala wa nchi za kikoloni za makafiri?! Basi je, inafaa kwenu kutawaliwa na hawa Ruwaibidah (watawala wajinga), hali nyinyi ndio Umma bora uliotolewa kwa watu?! Au je munaiogopa Magharibi kafiri mkoloni?! Je, hamuoni jinsi inavyoyumba kila mgogoro unapoikumba? Kutoka kwa janga la virusi vya Korona hadi kukaliwa kwa Capitol Hill ya Amerika hadi vita vya Ukraine hadi kufilisika kwa benki za Marekani. Kila Magharibi inapokabiliwa na mgogoro, udhaifu wake hufichuka, na jamii zake huanza kuingiwa na wasiwasi wa machafuko, kutokana na ukali wa ubinafsi wao. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[بَأْسُهُمْ بَيْنَهُمْ شَدِيدٌ تَحْسَبُهُمْ جَمِيعاً وَقُلُوبُهُمْ شَتَّى ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لّا يَعْقِلُونَ]
“Wao kwa wao vita vyao ni vikali. Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasio na akili.” [Al-Hashr: 14].
Enyi Waislamu Mlio na Uwezo wa Mabadiliko... Enyi Watu Wenye Nguvu na Ulinzi!
Tunakusihini musiuache mwezi wa Ramadhan kupita mwaka huu bila ya kutoa Nusra (msaada wa kimaada) kwa mradi wa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Ili, furaha ya Waislamu siku ya Idd Al-Fitr iwe sherehe ya Eid na sherehe ya ushindi ulioahidiwa. Hadhi yako miongoni mwa Waislamu itakuwa kama ile ya Ansari wakubwa kutoka kwa watu wa Al-Madinah Al-Munawwarah, Mwenyezi Mungu awe radhi nao. Ummah uko tayari kujitoa muhanga kwa ajili ya Uislamu. Mradi wa kuanzishwa Khilafah umebainishwa na Hizb ut Tahrir kuwa ni ramani ya kina ya kuanzishwa kwake na kujenga dola yake, kwa hivyo kilichobakia kwenu ni kuitikia kile tunachokuitieni. Mcheni Mwenyezi Mungu, enyi Watu wenye Nguvu na Ulinzi... Mcheni Mwenyezi Mungu katika Uislamu na Waislamu.
Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[فَالَّذِينَ آمَنُواْ بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُواْ النُّورَ الَّذِيَ أُنزِلَ مَعَهُ أُوْلَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ]
“Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuata nuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenye kufanikiwa.” [Al-A’raf: 157]
Nawaombea mwezi wenu uwe wenye kubarikiwa, Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh.
Mkesha wa Jumatano ndio siku ya kwanza ya mwezi uliobarikiwa wa Ramadan wa mwaka 1444 H.
Mhandisi Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |