Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 11 Dhu al-Hijjah 1445 | Na: H 1445 / 043 |
M. Jumatatu, 17 Juni 2024 |
Kuwekwa Kizuizini kwa Sababu ya Majadiliano Tu ya Hadhara kuhusu Kanuni za Shariah ya Kiislamu katika Demokrasia Kubwa Zaidi Duniani
(Imetafsiriwa)
Mamlaka za polisi kutoka jimbo la Tamil Nadu nchini India zimeripoti kuzuiliwa kwa Waislamu sita kwa kufanya amali za Hizb ut Tahrir (HT). Watu hao waliokamatwa ni pamoja na Dkt Hameed Hussain, ambaye ana shahada ya uzamifu ya Uhandisi Mitambo, Baba yake Hussain Ahmed Mansoor na kaka yake Abdul Rehman ambaye ni Msomi wa Kiislamu na wengine watatu, Mohammed Maurice, Khader Nawaz Sherif na Ahmed Ali. Wanaume wote sita ni wenyeji wa Chennai. Ripoti hiyo ilielezea mijadala na harakati za kisiasa za kuunga mkono mfumo wa utawala wa Khilafah, miongoni mwa watu na mitandao ya kijamii, kuwa ni jambo lisilokubalika kiasi cha kuibua mashtaka ya vitendo vya uhalifu na uharamu dhidi ya watu hao sita. (Chanzo: Deccan Herald)
Katika tukio jengine tena nchini India, inayodaiwa kuwa demokrasia kubwa zaidi duniani, mtu anaweza kushuhudia kwamba mjadala kuhusu kanuni za Sharia kuhusiana na nyanja ya maisha ya kisiasa, inashughulikiwa kama uhalifu. Hii ni hivyo licha ya kwamba hakuna uhalifu unaotendwa, au hata kuchochewa, na watu hao sita husika. Vitendo vya serikali ya Modi wakati wa uchaguzi vinaonyesha wazi dhamira ya mala fide na kutapatapa kwa viongozi wa India kuzuia fikra za kisiasa za Uislamu. Mamlaka zinatafuta kuwatisha Waislamu, ili kuzichafua fikra hizi na kuwaweka mbali Waislamu na fikra hizi. Mamlaka zinataka kuwaoanisha Waislamu katika fikra potovu, zisizo za Kiislamu. Sera ya India inaambatana na, na ni sehemu ya kampeni ya kimataifa ya dola zenye nguvu duniani dhidi ya kurudi kwa Uislamu katika nyanja ya kisiasa. Ulimwengu kwa jumla unajua sana kuhusu kutochukua hatua kwa matawi ya utendaji na mahakama ya demokrasia hii kubwa zaidi. Kitengo chake cha utunzi wa sheria kinatoa taarifa za chuki dhidi ya wageni, kinachukua hatua zisizo za kisheria. Kinatukuza vitendo vya ugaidi na ghasia za makundi dhidi ya Waislamu.
Ubaguzi wa kimadhehebu ulidhihirika pindi Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, alipofanya kampeni za uchaguzi wa 2024 huko Rajasthan.
Alichochea hasira ya umma kwa kutoa madai ya kashfa kwamba bunge la Congress litakabidhi utajiri wa taifa kwa Waislamu. Alipindisha manifesto ya Bunge la Congress inayotaka usambazaji wa mali kwa maskini. Ubaguzi wa kimadhehebu unadhihirika wakati Waziri Mkuu wa Uttar Pradesh Yogi Adityanath anapotoa wito wa 'kuweka risasi' kwenye vichwa vya wahalifu, au kuadhibu familia za wahalifu kwa kubomoa nyumba zao, kwa njia zisizo za kisheria. Ubaguzi wa kimadhehebu ulidhihirika wakati Waziri wa Mambo ya Ndani wa India Amit Shah 'alipokiri mwenyewe' kushiriki katika Mauaji ya Gujarat ya 2002, akiashiria kile ambacho BJP inaweza kufanya. Kushindwa kwa demokrasia kushikamana na sheria ambayo wao wenyewe hutunga ni dhahiri sana sio tu katika demokrasia kubwa zaidi lakini katika demokrasia zote, iwe Marekani, Uingereza, Ulaya, Asia na umbile haramu la Kizayuni. Ari yao ya kuzuia ukosoaji wenye utambuzi wa kufeli huku huifanya kuwa potovu zaidi. Demokrasia huwaadhibu ‘walinganiaji wa mabadiliko’ kwa kuwapotezea muda wao gerezani na mchakato wa polepole wa sheria, wakijificha katika vazi la uhalali. Hii ni huku udikteta ukiwaadhibu 'walinganiaji mabadiliko' waziwazi tu.
Hizb ut Tahrir (HT) haitachoka kuwasilisha haki na kulingania mfumo wa Khilafah kwa njia ya Utume licha ya vitisho inavyovikabili chini ya mifumo iliyobuniwa na mwanadamu kama vile demokrasia na udikteta.
Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa cha Kiislamu kilichoanzishwa kwa lengo la kusimamisha Khilafah ya Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu. Hizb ut Tahrir inaifunga kazi yake kwenye njia ya Mtume (saw) ya mvutano ya kifikra, kimfumo na kisiasa kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah katika ulimwengu wa Kiislamu. Katika nchi ambazo Waislamu wanaishi wachache, Hizb ut Tahrir inafanya kazi ndani ya umma wa Kiislamu, ikiwakumbusha juu ya wajibu wa kusimamisha Khilafah na kuwaalika kuwezesha upatikanaji wake katika ardhi za Kiislamu. Kwa zaidi ya miongo saba ya kuwepo kwake, Hizb ut Tahrir haijawahi kukengeuka kutokana na njia yake ya kifikra na kisiasa. Licha ya upinzani, propaganda na athari za uwongo, Hizb ut Tahrir itaendelea kufanya kazi ya kusimamisha tena Khilafah ya Kiislamu ambapo Waislamu na wasiokuwa Waislamu wanaweza kuishi kwa amani na maelewano chini ya mfumo uliofafanuliwa na Mwenyezi Mungu, Muweza wa yote, wa Milele, Asiyezuilika.
[قُلْ هُوَ الرَّحْمَنُ آمَنَّا بِهِ وَعَلَيْهِ تَوَكَّلْنَا فَسَتَعْلَمُونَ مَنْ هُوَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ]
“Sema: Yeye ndiye Mwingi wa Rehema; tunamuamini Yeye, na juu yake tunategemea. Mtakuja jua ni nani aliye katika upotovu ulio dhaahiri.” [Surah Al Mulk - 29]
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |