Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  30 Dhu al-Hijjah 1445 Na: H 1445 / 046
M.  Jumamosi, 06 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uchaguzi nchini Marekani na Uingereza Unashindana katika Kulenga Uislamu na Waislamu
(Imetafsiriwa)

Katikati ya uungaji mkono wa Marekani na Uingereza kwa mauaji yanayofanywa na umbile la Kiyahudi, ambalo liliasisiwa na Himaya ya Uingereza yenyewe, na baada ya zaidi ya miezi tisa ya uungaji mkono wao kwa umwagaji damu wa Waislamu mjini Gaza, kampeni za uchaguzi wa rais na chama zinaendelea hivi sasa nchini Marekani na Uingereza. Katika kampeni hizi, wale wanaojiona wanastahili zaidi kuongoza dola hizi mbili za kikoloni, ambazo zimesababisha njaa na udhalilifu kwa mataifa, zikifanya juhudi zao kubwa kupata tonge ya chakula, tama la maji, na muangaza ambao sasa unazima zaidi kuliko kumulika katika miji mikuu na miji mikuu ya nchi za Kiislamu, kama vile Cairo na Karachi.

Leo, nchini Marekani, wanasiasa wenye mikono inayochuruzika damu ya Waislamu wanashindana, bila haya kutangaza uungaji mkono wao kwa dola ya kihalifu, umbile la Kiyahudi, na hata kushindana katika kutuma msaada zaidi kwa umbile hili. Wanalaumiana wao kwa wao kwa mapungufu ya kuwapa mabomu na silaha zinazoua watoto na wanawake wasio na hatia katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Licha ya Biden kuendeleza aina zote za uungaji mkono wa kijeshi, kifedha, kisiasa na vyombo vya habari kwa umbile la Kiyahudi, mpinzani wake Trump alimdhihaki, akimwita “Mpalestina” akimaanisha kushindwa kwake kuunga mkono mauaji ya halaiki huko Gaza! Alidokeza kwamba ataongeza uungaji mkono kwa umbile la Kiyahudi ili kufikia ndoto yake ya ubwana juu ya Umma wa Kiislamu katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina na kuiangamiza.

Ama Uingereza, pande zote mbili (Conservatives and Labour) zinashindana kwa kutumia suala la wahamiaji ambao wengi wao wanatoka katika nchi za Kiislamu wanaoteswa na serikali zao ambazo ni Vibaraka wa Uingereza na Marekani. Wanaahidi kuwafukuza wakimbizi na wanyonge au kupunguza utitiri wao, na kuwaacha wakabiliane na hatima yao katika bahari. Mkruseda wa Kibaniani Sunak, Waziri Mkuu wa Uingereza, alikwenda kwa umbile la Kiyahudi kwa ndege ya kijeshi iliyobeba vifaru na silaha, akijisifu juu ya kuongoza vita vya kikruseda  vya Ulaya ili kuivamia ardhi iliyobarikiwa kwa mara nyingine tena!

Hizi ni kampeni za uchaguzi katika dola kubwa za Kikruseda, kampeni zinazotoa wito wa kuuawa kwa Waislamu na kuungwa mkono kwa wauaji wao, na kuteswa wanyonge na wakimbizi miongoni mwao. Je, kuna manufaa yoyote kwa Waislamu katika chaguzi hizi? Je, wanaweza kupata haki kati ya hawa walaghai? Ni dhahiri shahiri kwamba Waislamu hawana hisa katika chaguzi hizi; wao ni wahanga na kafara. Tofauti kati ya Conservatives na Labour na kati ya Republicans na Democrats iko kwenye utaratibu na chombo cha kuchinja, hivyo ni jambo lisilowezekana kuwa mtu anayetaka kutuua kwa mizinga na vifaru ni bora kuliko anayetaka kutuua kwa njaa, kuzama majini, au njia nyenginezo!

Kumchagua yeyote kati ya washindani hawa hairuhusiwi kabisa, bila kujali tafsiri za wanazuoni wa sultan na waabudu pauni na dolari. Hakuna ikhtilafu kwamba kumchagua yeyote kati yao ni leseni kwao kuwaua Waislamu zaidi na kuongeza mateso yao duniani kote, hasa katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina. Yeyote anayetaka kuwa mshirika wa wahalifu hawa ateue mtu wa kumpigia kura. Kwa kufanya hivyo atajidhulumu nafsi yake na hatakuwa na nafasi ya kuwa kipenzi cha Mwenyezi Mungu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ مِنْكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Surat Al-Ma’ida:51]

Waislamu wanaoishi katika nchi za Magharibi, zikiwemo Marekani na Uingereza, wana wajibu wa kutetea matukufu ya Waislamu kutokana na ukiukaji wa wahalifu hao. Hili haliwezi kufikiwa kwa kujihusisha na njama zinazosukwa na wagombea hao kwa kumpigia kura yeyote kati yao, kwani wote ni sura za sarafu moja ya riba. Badala yake, inapaswa kufanywa kwa kuwashutumu kupitia njia na mbinu zote halali, kama inavyoruhusiwa na sheria za nchi hizo zenyewe. Dori hii, pamoja na kuwa ni wajibu kwa taifa lao na watu wanaodhulumiwa duniani, wakiwemo watu wa ardhi iliyobarikiwa na Gaza, pia ni kitendo adhimu kisichopingwa na watu wowote wenye nia ya haki na wale wenye maadili miongoni mwa wanafikra huru katika nchi za Magharibi.

Siku hizi sauti zao zimekuwa kubwa kutokana na kufichuliwa kwa wanasiasa na vyama vyao vya kisiasa na kufichuliwa kwa kauli mbiu potofu walizokuwa wakitoa kwa muda mrefu kama vile uhuru, haki za binadamu na demokrasia. Hata hivyo, wako katika haja kubwa ya Waislamu wanaoishi miongoni mwao ili kuwaongoza kwenye njia iliyo sawa na kuuwasilisha kwao Uislamu kama hadhara badali ya kuchukua nafasi ya mfumo wa kibepari ambao umesababisha wanadamu na watu wa Magharibi kuteseka.

Hii ndio dori ya Waislamu katika nchi za Magharibi: dori ya wabebaji wa ujumbe wa haki kwa watu wote, ambao kwao wanafanya wema kwa watu wenye nia ya haki katika nchi hizo. Kuwepo kwao Magharibi kwa hivyo kunakuwa chanya kwa viwango bora vinavyomridhisha Mwenyezi Mungu, na kunawatoa watu wa nchi hizo kutoka kwenye giza la ubepari na dhulma zake hadi kwenye nuru ya Uislamu na uadilifu wake. Kwa njia hii wanatekeleza wajibu wao wa kufikisha ujumbe badala ya kujihusisha na mchezo mchafu wa kisiasa wa Kimagharibi ambao msingi wake ni mafuvu ya Waislamu na kuwanyima watu haki zao. Hao ni walinganizi kwa Mwenyezi Mungu ili kuwaokoa watu, na sio kuyumba katika jamii zilizo potea na kupotoka. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[وَلْتَكُنْ مِنْكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ]

“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.” [Surat Aal-i-Imran:104].

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu