Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  24 Muharram 1446 Na: H 1446 / 008
M.  Jumanne, 30 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali ya Jordan Kuanzisha Afisi ya NATO ni Uhalifu dhidi ya Palestina na Gaza na Usaliti kwa Umma wa Kiislamu
(Imetafsiriwa)

Baada ya NATO kutangaza uamuzi wake wa kufungua afisi ya kwanza ya mawasiliano katika eneo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika katika mji mkuu wa Jordan, Amman, uamuzi ambao ulikuja wakati wa mkutano wa hivi karibuni wa NATO jijini Washington, taarifa imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Jordan na Washirika kutoka nje, ambao walisema, “Washirika walipitisha katika mkutano wa kilele wa NATO wa 2024 jijini Washington mpango wa utekelezaji wa kuimarisha mbinu ya ushirikiano katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini ili kuendana na maendeleo katika mandhari ya usalama, kieneo na kimataifa. Mpango huu ulikuwa makini kuonyesha dhamira ya muungano katika kuimarisha ushirikiano na nchi jirani za kusini kwa kuanzisha afisi ya uhusiano wa muungano katika Ufalme wa Hashemiya wa Jordan, ambayo ni afisi ya kwanza ya mawasiliano katika kanda hiyo”.

Kwa kuzingatia hili, tunafafanua mambo yafuatayo:

Kwanza: Matukio ya tarehe 7 Oktoba 2023 M, na matokeo ya tishio la kweli la uwepo wa umbile la Kiyahudi, yalijaza nyoyo za viongozi wa Marekani na Magharibi hofu na kuogopa na kuwakumbusha juu ya majeshi ya Kiislamu yasiyoweza kushindwa wakati yalipokuwa wakivunja milango ya miji mikuu ya Ulaya. Hofu hii iliwapelekea kupepesuka na kuchukua hatua na vitendo vinavyoashiria yale ambayo nyoyo zao zinayaficha ya chuki kali dhidi ya Uislamu na Waislamu, hivyo wakakusanya meli na ndege zao katika bahari za Waislamu, wakafanya mizunguko ya kijeshi huko, wakaimarisha kambi zao za kijeshi huko kwa silaha mbalimbali za hali ya juu, na kulipa umbile la Kiyahudi tani za silaha za hali ya juu na risasi za maangamizi. Kufungua afisi ya mawasiliano ya NATO nchini Jordan sio mwisho wa hatua hizo; wanadhani kwamba matendo yao yatawalinda na Waislamu, au yatawazuia Waislamu kusimamisha Khilafah yao, au kuliangamiza umbile la Kiyahudi, na kuikomboa Palestina.

Pili: Serikali tendaji nchini Jordan, ambayo iliasisiwa kwa ajili ya kulinda umbile la Kiyahudi na kuzuia Waislamu kuikomboa Palestina, inaendeleza uadui wake kwa Uislamu na Waislamu. Bali, haioni aibu kutangaza uadui huu hadharani. Serikali hii ya kihalifu sio tu kwamba inaridhiki na kuasisiwa kwa umbile la Kiyahudi nchini Palestina, kulinda umbile hili la pariah, kuzuia Ummah wa Kiislamu kutekeleza wajibu wake wa kuikomboa Palestina, kukaa kimya kuhusu vita vya uharibifu ambavyo umbile hili la pariah linaendesha huko Gaza, na kulipa umbile la Kiyahudi mboga, matunda, maji, na njia za uhai. Serikali hii tendaji ya kihalifu hairidhiki na yote yaliyo hapo juu; badala yake, inafungua afisi ya mawasiliano katika eneo lake kwa ajili ya muungano wa kijeshi wa Magharibi unaochukia Uislamu na Waislamu (NATO), na hivyo kupambana na hisia kali za Waislamu nchini Jordan na nchi nyingine za Kiislamu dhidi ya watu wao huko Gaza na Palestina, ikitangaza kujifungamanisha kwake na maadui wa Ummah bila haya wala vibaya.

Tatu: Madhumuni ya kuanzishwa kwa afisi hii nchini Jordan sio siri tena kwa mtu yeyote, kama ilivyoonekana wazi katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Wahamiaji ya Jordan katika ibara “ili kwenda sambamba na maendeleo katika mandhari ya usalama, kieneo na kimataifa.” Je, kuna yeyote aliye na shaka yoyote kwamba mandhari ya usalama inayozungumziwa ni Gaza na uharibifu, mauaji, uhamisho na njaa yanayotokea huko? Licha ya kila kitu ambacho umbile la Kiyahudi inafanya huko Gaza, imeshindwa vibaya kufikia malengo yake yoyote mjini Gaza, na imeshindwa kupata ushindi wowote, haijalishi ni mdogo jinsi gani - kama viongozi wa umbile la Kiyahudi wenyewe wanavyokiri - na kwa kuzingatia vuguvugu la wananchi wanaokataa uvamizi wa Kiyahudi dhidi ya Gaza duniani kwa jumla na hasa nchi za Kiislamu, na hofu ya Wamagharibi kuhusu harakati pana ya Umma wa Kiislamu, huku Wamagharibi wakikata tamaa ya uwezo wa tawala vibaraka katika nchi za Kiislamu kuendelea kudhibiti na kutawala mambo, na uhakika wake kwamba Ummah unakaribia kuzifagilia mbali tawala hizi na kuziondoa, na hivyo kuondoa uwepo wao katika nchi zetu; kwa kuzingatia haya yote, hatua hii ilitoka kwa NATO, ili wao wenyewe waweze kusimamia utekelezaji wa mipango yao na kulinda maslahi yao katika ardhi zetu, na kulinda umbile la Kiyahudi.

Nne: Uislamu umeharamisha Waislamu kuanzisha miungano ya kijeshi na kufunga mapatano ya kijeshi na nchi nyengine, basi itakuwaje iwapo itafunga na maadui wa Mwenyezi Mungu, Mtume wake na maadui wa Ummah? Aidha, kilichofanyika si muungano wa kijeshi kati ya NATO na Jordan, bali ni njia ya kikoloni ya nchi za Magharibi kufikia malengo yao na kutekeleza mipango yao katika ardhi zetu. Kanuni msingi ya Waislamu ni kwamba ni lazima wasiwaruhusu kufikia hilo, lakini watawala Ruwaibidah (wajinga duni) katika ardhi zetu wanasisitiza kumuasi Mwenyezi Mungu (swt) na kuusaliti Ummah.

Tano: Ni wajibu wa lazima kwa Waislamu kukomesha vitendo hivyo vya kipumbavu vinavyofanywa na watawala wao wapumbavu wanaong'ang'ania viti vyao vibovu (vya utawala) katika kuwatumikia wakoloni makafiri, na Waislamu watekeleze wajibu wao katika kukemea maovu, na mazingatio yaelekezwe moja kwa moja kwa wale walio na nguvu wenye uwezo wa kubadili uovu huu, nao ni majeshi katika ardhi za Kiislamu. Hivyo juu yenu - enyi maafisa na wanajeshi - ni matumaini ya Ummah uliobanwa ili kuuongoza kuelekea kuwabadilisha watawala hao kwa nguvu, na kuelekea kuzikomboa ardhi za Kiislamu zinazokaliwa kwa mabavu, kuliondoa umbile la Kiyahudi la pariah kutoka kwa uwepo, na kuondoa dhulma, ukandamizaji na uvamizi kutoka kwa watu wenu nchini Palestina na Gaza, na kutibua mipango ya Magharibi na NATO, na nyinyi mnaweza kufanya hivyo kwa msaada wa Mwenyezi Mungu (swt) ikiwa mutadhamiria, na kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa ikhlasi na kusimamia na kupanga vyema, na Ummah uko pamoja nanyi na nyuma yenu, na Mwenyezi Mungu ndiye msaidizi wenu.

[وَلَيَنصُرَنَّ اللهُ مَن يَنصُرُهُ إِنَّ اللهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ]

“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.” [Al-Hajj: 40]

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu